SIFA ZA MJASIRIAMALI
Kama wewe ni mjasiriamali basi lazima utakuwa na sifa moja wapo ama sifa zote kati ya hizi zifuatazo
- Lazima utakuwa mtatuzi wa matatizo mbalimbali yanayoikumba jamii
- Lazima utakuwa mbunifu na jasiri katika mazingira yoyote aliyopo
- Lengo lako kuu litakuwa sio kutengeneza fedha bali fedha itakuwa ni matokeo ya kutatua changamoto Fulani
- Nguzo yako kuu itakuwa ni uvumilivu na kutokata tamaa
- Lazima utakuwa unatengeneza kiasi kikubwa cha fedha kwa kutumia nguvu kidogo na kwa muda mfupi
- Hutatafuta wala kubembeleza wateja bali wateja watakutafuta na kukubembeleza wewe uwapatie huduma au bidhaa unayoitoa
- Mwisho kabisa lazima utakuwa mdadisi na mwenye kupenda kujifunza kitu kipya kila siku.
SIFA ZA MFANYABIASHARA
Kama wewe lengo lako ni kuwa mfanyabiashara na si mjarisiamali basi lazima utakuwa na sifa moja wapo kati ya hizi au sifa zote hizi lazima utakuwa nazo.
- Lengo lako kuu litakuwa ni kutengeneza fedha na si kuwa mtatuzi wa matatizo katika jamii
- Mara nyingi utakuwa unatangaza sana bidhaa au huduma unayoitoa kuliko elimu juu ya huduma au bidhaa unayoitoa
- Utakuwa unapata wateja kwa msimu kulingana na biashara unayoifanya na sio wateja wa kudumu
- Lazima utakuwa unabembeleza wateja ili uwape huduma au bidhaa badala ya wao kukubembeleza wewe
- Ushindani huwa ni mkubwa sana kwa wafanyabiashara kuliko kwa wajasiriamali
- Ni rahisi sana kwa mfanyabiashara kukata tamaa kwa kile anachokifanya kuliko mtu ambaye ni mjasiriamali
- Wafanyabiashara wengi biashara zao hazidumu hufa ndani ya muda mfupi baada ya kuanzishwa .
- Mara nyingi hutengeneza fedha kiasi kidogo kwa nguvu nyingi na kwa muda mrefu zaidi n.k
No comments:
Post a Comment