Mkulima ni mfanyabiashara na mfanyabiashara yeyote ni mtu anayelenga faida kubwa au hasara kidogo.
Kwa hiyo ni muhimu kwa mkulima kujua thamani ya mazao yake ili aweze kujua ni bei gani unayotakiwa kuuza zao lako hii itakusaidia faida au hasara.
Kitu unachotakiwa kufanya ili kujua thamani ya zao ni.
MALI BILA DAFTALI HUPOTEA BILA HABARI.
Waliona mbali sana walisomea maeneo haya.
Mkulima unatakiwa uwe na daftari la kutunzia kumbukumbu za shughuri zako zote za shamba.
Tunza kumbukumbu za gharama zote ulizozitumia katika Kilimo chako kama ulikodi shamba au ulinunua, ulilima kwa trekta, ukaajiri watu wa kupanda ukanunua mbolea na madawa ya kuulia magugu na wadudu.
Hakikisah kuwa unatambua ukubwa| eneo la shamba ulilolima kama ni hekta moja au mbili ama ni ekari tatu au nne.
Hii itakusaidia kupata jumla za gharama ulizotumia katika uzalishaji kwa eneo husika.
PIMA JUMLA YA KIASI CHA MAVUNO YAKO.
Kiasi cha mavumo unaweza kukipima kwa idadi ya magunia au kama matunda unaweza kupima kwa uzito (kg) au ujazo.
Pima mavumo yako kwa njia yoyote unayoitumia wewe ilimradi tu Mwisho Wa siku ujue umevuna kiasi gani.hapa utapata jumla ya mavumo kwa eneo husika.
USHAURI WANGU.
katika Kilimo chochote utakacho kufanya jitahidi sana kupunguza gharama za uzalishaji ili ujiongezee nafasi ya kupata faida kubwa zaidi. Punguza gharama zote zisizo za lazima, lakini usijisahau kiasi cha kuathiri ubora wa wingi Wa mavumo.
Nashukuru kwa kuendelea kusoma
Samahani kwa wale ninawowachosha hipo siku sitahandika nivumilie kidogo tu.
No comments:
Post a Comment