August 18, 2018

JINSI YA KUOTESHA MBEGU YA PAPAI

MWONGOZO.

Ili mbegu zilizo kavu za papai zipasuke na hatimae kuota zinahitaji vitu zifuatavyo.


Mwanga wa jua wa kutosha

hali joto

unyevunyevu.


hatua za kuotesha.

1. Fungua pakti yako ya mbegu.

2. Weka maji kwenye chombo  chochote na uloweke mbegu kwa muda wa siku 3 (saa 72). hakikisha unamwaga maji na kuweka mengine kila baada ya saa 24.

3. Baada ya saa 72 kupita, chukua kitamba na weka mbegu zako zote kwenye kitamba na kuzifunika vizuri.

4. Chimba shimo dogo kwenye sehemu ya mwanga wa jua wa kutosha, kisha weka mbegu ulizofunika kwenye kitamba na kuzifukia.

5. Mwagilia maji kila siku sehemu ya juu uliyofukia mbegu. itachukua siku 8 mpaka 12 mbegu kupasuka kutegemea na halijoto.

6. Mbegu zikipasuka unazihamishia kwenye kitalu au tray ya kupandia mbegu au kwenye viriba (polythene tube). katika hatua hii tumia kijiti au kitu chenye ncha kali katika kupanda mbegu. Hii inasaidia kuepuka kuvunja maotea ya mbegu.

7. Hakikisha unaweka mbegu si kwa kufukia sana. weka mbegu juu juu na fukia kwa kiasi kidogo sana udongo. Mara nyingi mbegu za papai hazina nguvu sana za kusukuma udongo kama utazifukia sana.

8. Baada ya kuweka mbegu, chukua mfuko wa sandarusi (jute bags) na  funika juu ya kitalu tafadhari usitumie majani makavu katika hatua hii.

9. Mwagilia maji kwa siku mara moja juu ya mifuko ya sandarusi kwa muda wa siku 3-5 mbegu zitaanza kutoa majani ya awali.

10. Baada ya siku 6-7 ondoa mifuko ya sandarusi.

11. Mbegu zikifikia sm 8-10 unaweza kuhamishia kwenye mashimo na kwenda kuotesha shambani.

No comments:

Post a Comment