1. VICOBAmaana yake ninini? maana yake ninini? maana yake ninini?
Jibu. VICOBA maana yake ni Village Community Bank na iki Jibu wa na maana ya Kiswahili
ya Benki ya jamii vijijini. Mfumo huu unatekelezwa kwa kuanzishwa kikundi kutokana na
watu au wanajamii wanaoishi eneo moja na kama siyo mtaa mmoja basi kijiji kimoja na
hii husaidia sana uendeshaji wa kikundi husika.
2. Mfumo wa Mfumo wa VICOBAulianza lini Tanzania na athiri yake ni wapi? ulianza lini Tanzania na athiri yake ni wapi? ulianza lini Tanzania na athiri yake ni wapi?
Jibu. Mfumo wa VICOBA kwa mara ya kwanza ulianzishwa mwaka Jibu. 2002 mwezi wa
kumi. Mfumo huu ulianzishwa na shirika la kidini lijulikanalo kwa sasa kwa jina la IRCPT
na kwa kipindi hicho lilikuwa linajulikana kwa jina la WCRP. WCRP walianzisha mfumo
huu baada ya kwenda kujifunza Zanzibar ambako CARE International walikuwa
wanatekeleza mradi wa Jozani saving and credity association (JOSACA). Watendaji
wa WCRP baada ya kujifunza mfumo wa JOSACA kwa kina na kutokana na uzoefu
wao wa uendeshaji wa shughuli za kifedha wakaamua kubadilisha jina na kuita mfumo
wa VICOBA.
Mfumo huu kwa mara ya kwanza ulianzishwa eneo la Ukonga na kisarawe ambapo
vikundi kumi vilianzishwa na ndivyo vikundi vikongwe kuliko vikundi vyovyote hapa
Tanzania na kwa bahati nzuri vikundi hivi bado vipo hai. Mfumo huu baada ya
kuonyesha mafanikio makubwa Ukonga na Kisarawe serikali na mashirika mbalimbali
ya kimaendeleo yaliweza kutembelea Ukonga na kujifunza na kila aliyejifunza aliamua
kwenda kuanzisha vikundi katika maeneo ya mradi wake.
Asili ya Mfumo wa VICOBA ni mfumo wa MMD ambao kwa mara ya kwanza
ulianzishwa nchini Niger na kwa jina la Mata Masu Dubara (MMD). MMD ni jina la
kihausa na kwa Kiswahili inamaanisha ni akina ma akina ma akina mama katika harakati za maendeleo ma katika harakati za maendeleo ma katika harakati za maendeleo.
Mfumo huu umekuwa na majina mengi kwa kila nchi kuamua kuita majina kutokana na
miradi ya kimaendeleo wanayoitekeleza. Mfano mfumo huu Uganda unajulikana kwa
jina la JENGA, Msumbiji unajulikana kama OVAPHERA na zimbambwe KI. Hata hivyo
kila nchi ambako mfumo huu unatekelezwa kuna mamboresho mbalimbali yamefanyika
[8/1, 11:16 PM] Omben ebusol: na hapa ndipo unapo kuja kuona mfumo wa VICOBA unatofauti ya kiutekelezaji na
uendeshaji wake na mfumo wa JOSACA, VSLA, SILC, VITOVU na mifumo mingine.
Mfumo wa VICOBA wenyewe katika utekelezaji wake nao umetofautiana baina ya
wadau mbalimbali ambao wapo katika mfumo huu na hii ni changamoto kwa wadau
wote wa VICOBA ambao wanahitajika kukaa pamoja na kujadili jambo hilo.
No comments:
Post a Comment