August 04, 2018

MAGONJWA YA KUKU NA TIBA ZAKE

Kuku hushambuliwa na magonjwa mbalimbali ambayo mengine yanatibika kwa dawa na mengine hayana tiba bali kuku hupewa chanjo maalumu ambayo

huzuia magonjwa hayo.Leo nitawaeleza baadhi ya magonjwa ambayo hushambulia kuku mara

kwa mara na ambayo ni chanzo cha kuwakatisha tamaa wafugaji wa kuku.

A.) MAGONJWA YANAYOHITAJI CHANJO

1> GUMBORO

Ugonjwa huu husababishwa na virusi.

DALILI ZA UGONJWA

-Kuku kuzubaa na kulundikana, pamoja na

kusinzia

-Kuku kuharisha

-Kuwa na vifo vingi kwa kuku

TIBA

Ugonjwa huu hauna tiba,,Kuku wakipewa Dawa

za oxytetracycline hupunguza vifo.

KINGA

wakinge kuku wapo kwa kuwapa chanjo ya

gumboro (Gumboro vaccine)

*2> MAHEPE (Marecks)*

Ugonjwa huu husababishwa na virusi*

*DALILI*

-Kuku hupata ulemavu na vifo vya mara kwa

mara.

*TIBA*

Ugonjwa huu hauna tiba

KINGA

Chanjo hutolewa kwa vifaranga wenye umri wa

siku moja,vifaranga hupewa chanjo ya mahepe

(Marecks vaccine)

3>NDUI YA KUKU (Fowl Pox)

Ugonjwa huu husababishwa na virusi.

*DALILI*

-Kuku hupatwa na vidonda kichwani.

-Kuku hupata uvimbe mweupe kwenye

mdomo na kushindwa kula.

TIBA

Ugonjwa huu hauna tiba.

KINGA

Chanja kuku wako wa siku 60-90 kwa chanjo ya

Ndui ya kuku (Fowl pox vaccine).

*4>MDONDO (New castle)*

Ugonjwa huu husababishwa na virusi

*DALILI*

-Ugonjwa huu hutokea kwa ghafla na kuenea

kwa haraka

-Vifo vya kuku huwa vingi

-kuku hupumua kwa shida

-Kuku hupooza na kulemaa miguu

-Kuku hupinda shingo yake

-Kuku hupunguza kutaga mayai

-kuku huarisha

-Kuku Kuzunguka zunguka na kutembea

kinyume nyume.

TIBA

Hauna tiba

*KINGA*

Chanja vifaranga wako na kuku wako kwa

chanjo ya Mdondo (New Castlef vaccine) na

urudie chanjo hii kila baada ya miezi mitatu.

*B.)MAGONJWA* YANAYOTIBIKA KWA DAWA

1>KUHARA DAMU (coccidiosis)(Koksidiosisi

Ugonjwa huu husababishwa na virusi.

*DALILI*

-Kuku huzubaa na kujikunyata

-Kuku kuharisha LinkedI chenye damu au

kinyesi cha kahawi

-Kuku hudhoofika,manyoya huvurugika na

kulegea mabawa na kuonekana kama wawevaa

koti

-Kuku hupungukiwa homa ya kula

-Vifo huwa vingi kwa vifaranga

*TIBA*

Wape kuku wako dawa kama Esb 3, Amprolium,

au Basulfa.

KINGA

Zingatia usafi wa banda la kuku na usiruhusu

unyevuunyevu katika banda la kuku,

*2>HOMA YA MATUMBO(Fowl typhoid)*

Husababishwa na bakteria

DALILI

-Kuku hupata homa kali

-Kuku huarisha kinyesi cha kijani au njano

-Vifo huwa vingi hasa kwa vifaranga wenye

wiki 1-2

-Kuku huzubaa,kuvimba viungo vya

miguu,kuchechemea,kukosa hamu ya kula

-Kuku wanaotaga hupunguza utagaji,hutaga

mayai yenye ganda laini na hupata vifo vya

ghafla

*TIBA*

Dawa za oxytetracycline kama

Furamax,Typhoprim hutibu ugonjwa huu.

KINGA

Hakikisha usafi wa banda na vyombo vya

chakula na maji kwa kuku.

Tenganisha kuku wagonjwa na wazima

C)MINYOO

Hushambulia kuku wote wakubwa na vifaranga

DALILI

-Kuku hukonda

-Kuku huarisha

-Kuku hukohoa

-Kuku hupunguza utagaji

-Kuku hudumaa katika ukuaji/hawakui vizuri

-Kuku hupungua uzito

*TIBA*

Tumia dawa za minyoo kama piperazine

KINGA

Wapewe dawa za minyoo mara kwa mara kila

baada ya miezi mitatu

D)VIROBOTO/CHAWA/UTITIRI

Hushambulia sana vifaranga na hutokea vifo

kwa wingi kwa vifaranga Kwa kuku wakubwa

tatizo halionekani kwa sana lakini nao

huathiriwa sana.

*DALILI*

-Kuku kutochangamka

-Ukuaji mdogo wa kuku

-Kuku kutotaga na kuhatamia vizuri kutokana

na kusumbuliwa na chawa,utitiri au viroboto

-Viroboto huonekana kuganda machoni

wakinyonya damu

TIBA

Tumia dawa za unga kama sevin dust

5% ,Malathion ,akheri powder kwa kuku wote na

mabanda yao.

KINGA

Boresha usafi wa mabanda ya kuku.

E)UKOSEFU WA VITAMINI A

huathiri sana kuku wadogo.

*DALILI*

-Kuku huvimba macho na kutoa uchafu mzito

kama sabuni ya kipande iliyolowana.

-Mara nyingi ugonjwa hujitokeza baada ya

kipindi kirefu cha kiangazi

TIBA

wape kuku wote dawa za vitamini za kuku

zinazouzwa dukani.

*KINGA*

Wape kuku wako mchicha na majani mabichi

mara kwa mara.

*ZINGATIO*

Fuata ushauri wa matumizi sahihi kwa kila

dawa pindi ununuapo katika duka la dawa..

No comments:

Post a Comment