TOFAUTI KATI YA MJASIRIAMALI NA MFANYA BIASHARA
SIFA ZA MJASIRIAMALI Kama wewe ni mjasiriamali basi lazima utakuwa na sifa moja wapo ama sifa zote kati ya hizi zifuatazo Lazima utakuwa mtatuzi wa matatizo mbalimbali yanayoikumba jamii Lazima utakuwa mbunifu na jasiri katika mazingira yoyote aliyopo Lengo lako kuu litakuwa sio kutengeneza fedha bali fedha itakuwa ni matokeo ya kutatua changamoto Fulani Nguzo yako kuu itakuwa ni uvumilivu na kutokata tamaa Lazima utakuwa unatengeneza kiasi kikubwa cha fedha kwa kutumia nguvu kidogo na kwa muda mfupi Hutatafuta wala kubembeleza wateja bali wateja watakutafuta na kukubembeleza wewe uwapatie huduma au bidhaa unayoitoa Mwisho kabisa lazima utakuwa mdadisi na mwenye kupenda kujifunza kitu kipya kila siku. SIFA ZA MFANYABIASHARA Kama wewe lengo lako ni kuwa mfanyabiashara na si mjarisiamali basi lazima utakuwa na sifa moja wapo kati ya hizi au sifa zote hizi lazima utakuwa nazo. Lengo lako kuu litakuwa ni kutengeneza fedha na si kuwa mtatuzi wa matatizo ka...