UTANGULIZI
Kuwafundisha washiriki kufikiri ki- masoko na kuelewa baadhi ya mbinu za masoko kitu ambacho kitawafanya waelewwe maana ya maneno “soko na masoko” pia utafiti wa soko na kuyafanyia kazi katika biashara/miradi yao.
Soko ni nini?
Soko ni utaratibu au mtindo uliowekwa kwa mujibu wa kanuni /sheria kumwezesha mfanya biashara kuuza bidhaa zake kwa wateja/walaji. Husaidia kupanga nini uuze,nani umuuzie au jinsi gani watu wanavyoweza kujuakitu gani unauza,hivyo kukuwezesha kuzalisha kile ambacho kinahitajika katika soko sahihi.
Mafanikio katika biashara hutokana na mwonekano wa kipekee wa bidhaa au bidhaa unayozalisha kukidhi matakwa ya walaji au wateja pia, kuweza kutambua aina fulani ya watu ambao wangependa kununua bidhaa yako na kuweza kueleza bayana ni kitu gani, watu wategemee kunufaika kwa kunua bidhaa zako kati ya kundi hili la walengwa.
Kwa kifupi soko ni MTEJA Wa bidhaa na huduma uayozalisha
Soko lako ni;
Wateja wako ulionao kwasasa
Wateja uaotarajia kuwapata baadae
Wateja uliopoteza na untarajia watakurudia tena
Masoko ni nini?
Masoko ni shughuli yoyote ile anayofanya mfanyabiashara ili kuimarisha biashara yake.
Haitoshelezi tu kukaa kungojea oda.
Mfano wa shughuli hizo ni;
Kuelewa matakwa ya wateja wa bidhaa yako
Kupanga bei ambayo wateja watakuwa tayari kulipa na itakupa faida
Usambazaji wa bidhaa au huduma kwa wateja wako
Kuwavutia wateja wanaume bidhaa au huduma yako
UTAFITI WA SOKO
1. Kwa nini tujifunze kuhusu soko?
a) Mahitaji (demand)
Waswahili husema ‘unaweza kumlazimisha punda aende mtoni lakini huwezi kumlazimisha anywe maji’inamaana bidhaa zako kuwa wakati soko halihitaji bidhaa zako huwezi kulazimisha bidhaa yako inunuliwe
b) Bidhaa sahihi – usijaribu kumuuzia kitana mtu mwenye kipara bali muuzie kofia
c) Kufuata mkumbo-ni vema kutofautisha bidhaa za kuuza kwa wateja
2. Unahitaji kufahamu nini kutokana na soko lako?
Maswali yafuatayo ndio yakusaidia kufanya utafiti wa soko lako
Wateja wako ni akina nani?
Wako wapi
Mahitaji yao ni nini?
Wanapendelea nini kutokana na bidhaa zako
Ni mara ngapi na kiasi gani a wanacho nunua?
Wana nunua wakati gani?
Ni kiasi gani cha pesa wako tayari kutoa?
Ni jinsi gani bidhaa zitawafikia wateja
Washindani wako ni wapi?
Ubora wa bidhaa zao na bei zao vikoje
NB; kutafuta majibu ya maswali haya kunaitwa utafiti wa masoko
3. Jinsi ya kufanya utafiti a soko
Mbinu zifuatazo zinaeza kutumika kufanya utafiti wa soko la bidhaa au huduma unazozalisha:-
Kupitia Kwa wateja (kusikiliza maoni yao, kuachunguza na kuwauliza maswali).
Kuwauliza maswali watumiaji mbali mbali wa bidhaa zako ( nini wanachohitaji na wasicho kihitaji, mapendekezo na nini kiongezwe)
Kwa marafiki na ndugu
Kusoma kwenye vitabu, magazeti, kusikiliza radio na kuangalia televisheni
Kupeleka bidhaa zako katika maonesho ya biashara
Kuangalia biashara za washindani wako: bei, ubora, tofauti za bidhaa,, kuonesha bidhaa, na huduma zinazoambatana na bidhaa zako
Onesha sampuli ya bidhaaa au tembezasampuli ya bidhaa na waulize watu maoni juu ya bidhaa zako
4. Jumuisho la masuala ya masoko
B-Nne katika masoko
Bidhaa
Bei
Banda
Bango
a) BIDHAA- Bidhaa ni kitu chochote kinachozalishwa kwa ajili ya kuuza au kutumia.
Sifa za bidhaa
Bidhaa nzuri ni ile inayoridhisha na inakidhi matakwa ya soko. Kwa mfano:-
Ubora(muda, malighafi nzuri, iliyotengenezwa vizuri)
Yenye kuvutia ( rangi,mapambo,usafi, utengenezaji mzuri)
Mtindo (umbile zuri, inahusiana na thamani,saizi)
Ya kisasa (Inayoendana matumizi ya mtindo uliopo- fassion)
Tofauti na bidhaa za ashindani
b) BEI- Bei nithamani ya bidhaa au huduma ambayo mteja yuko tayari kumudu au kulipia. Kwa hiyo bei hujumuisha Gharama zote na faida au Bei huiumuisha gharama za ununuzi, gharama za uendeshaji na faida.
Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kupanga bei.
Ghrama zote ka jumla (gharama halisi)
Bei za wapinzani
Mahali ulipo 9 kiasi ambacho wwateja wwako radhi kulipia kwa kutegemea uezo wao kifedha)
Msimu (kwa mfano bei kubwa za vinyago msimu wa watalii au bei ndogo za feniture wakati wa mvua )
Kupata faida ya kutosha kuendesha shughuli bila matatizo
c) Banda au mahali pa kufanyia biashara
Banda ni mahali muhimu sana katika kuuza bidhaa au huduma. Mahali pa kufanyia biashara panatakiwa pae na sifa zifuatazo:-
Rahisi kufikiwa na wateja
Usalama, usafi
Sehemu ya maegesho
Kuwa karibu na huduma nyingine muhimu kama vile usafiri wa daladala, sehemu za vinywaji, vyakula,umeme n.k
Yenye mwanga wa kutosha
Rahisi kuonekana
Huduma hutolewa saa zote
5. Upangaji mzuri wa bidhaa mahali pa biashara.
Bidhaa zipangwe kwa seti
Mahali pa wazi panapoonekana kiurahisi
Weka bidhaa chache katika makundi madogo madogo
Weka bidhaa za aina mbalimbali
Panga sehemu yenye mwanga wa kutosha
Sehemu safi
Tumia picha au katalogi
6. BANGO AU UVUMISHAJI
Uvumishaji unajumuisha shughuli kadhaa ikiwa ni pamoja na uvumishaji wa mauzo,utangazaji,uhusiano wa jumuia na mbinu za kuuza. Shughuli hizo zinasaidia kuwavitia wateja, lakini hasahasa zinawapa wateja imani na bidhaa zako kuhakikisha kuwa hawanunui kwa mtu mwingine.Jambo muhimu la kuzingatia katika uvumishaji wa bidhaa ni lazima uwe mchangamfu na kuwa macho kuvutia wateja.
Kuvumisha mauzo (sales promotion)
Punguza bei yako kidogo ili wateja waone kuwa ni ndogo. Mfano:- shs 999.00 badala ya 1000.00
Weka bei maalum wakati wa sikukuu mbalimbali
Panga bidhaa madirishani ilizionekane kwa nje (display)
Uza bidhaa zinazoendana. Mfano muuza maandazi anaweza kuuza chai au muuza sukari anaweza kuuza majani ya chai
Utangazaji
Radio, magazeti,tv,sinema,mabango,kadi za biashara za mwenye biashara9business card)na sifa zinazotolewa kwa njia yam domo na watu watu waliokwisha kutumia bidhaa hizo.
Mahusiano
Kuchangia huduma za jamii Kama vile elimu, afya mazingira n.k
Mbinu za uuzaji
Jinsi ya kutambulisha bidhaa, eleza faida za bidhaa na ubora ake
Kumthamini mteja
Eleza faida ya bidhaa yako kabla hujataja bei
Jaribu kuuliza juu ya mahitaji ya mteja ili uweze kumwelekeza kwenye bidhaa itakayomfaa.
Kama mteja akiuliza bidhaa ambayo huuzi , unamwekeza zinapoatikana.
MKAKATI WA MASOKO
Kuwa na mkakati wa soko utakusaidia kufiki malengo yako kupitia kuweka lengo kuu/kubuni bidhaa/huduma mchanganyiko na kuchukua SWOT ANALYSIS(maeneo tunayofanya vizuri,maeneo ambayo hatufanyi vizuri,fursa tulizonazo, na changamoto zinazotukabili) katika bidhaa /huduma.
MAELEZO YA MALENGO YAKO
Maelezo ya malengo ni nini? Ni maelezo ya jumla juu ya kila unachotarajia kufikia,au lengo kuu la shirika. Hujulikana pia kama dira ya shirika . hivyo ni vema kuwa na wazo ambalo unaweza kuliweka kama kitovu cha kukuwezesha kuona unapoelekea kibiashara. Kulingana na kukua kwa biashara yako waweza kuendeleza malengo yako kuipa nguvu dira yako
Lengo lako lazima liwe dhahiri / bayana
Ni nini unataka kutimiza?
Kwa nini/ sababu gani ya kutimiza?
Nani atafanya nini?
Ni wapi utafanyia kile unachotarajia?
Kipi kinatakiwa kufikia lengo lako?
Malengo yako lazima yaweze kupimika.
Kwa kiasi gani?
Vingapi?
Malengo yako lazimayawe ya kufikiwa.
Ya juu Sana kisi cha kushindwa kufikia malengo yako?
Ya chini Sana kisi kwamba malengo yako hayaleti maana?
Ni muhimu kuweka malengo yanayokubalika lakini yenye kutamanisha.
Malengo yako yawe na uhusiano na kile unachotaka kufanya
Tuzo nitakayoipata baada ya kufikia malengo itazidi gharama (faida)
Tuzo nitakaipata baada ya kufikia malengo itafikia maezo ya malengo yako ya awaliKufikiwa kwa malengo yako kutakusaidia kufikia mipango yako?
Malengo yako lazima yaende na wakati
Ni lini litaanza?
Itachua muda gani kufikia malengo yako?Naweza kufanya nini kila juma,Mwezi juu ya bidhaa nyingine iliyopo ambayo ina matumizi sawa na ile anayohitaji, mteja..
No comments:
Post a Comment