August 10, 2018

MCHANGANUO WA KILIMO CHA MATIKITI

Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. 


Zao hili lina wapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. 


Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama kama matango,maboga na maskwash. 


Zao la tikiti maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi. 




Katika shamba la ukubwa wa shamba la ekali moja(1.acre) lililoandaliwa vizuri, kupandwa na kuhudumiwa vizuri mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi cha TANI 15-36, ambacho kitamsaidia kupata fedha zitakazo msaidia katika mahitaji yake mbalimbali na kuondokana na Umasikini.


Tikiti maji ni moja ya mazao ya matunda ambayo yamejipatia umaarufu mkubwa kote ulimwenguni. Zao ili ni moja ya mazao ambayo ni rahisi sana kuzalisha na lisilohitaji gharama kubwa. Gharama ya kulima ni kuweza kufahamu mazingira yanayofaa kwa ajili ya tikiti maji, uchaguzi sahihi wa mbegu, upandaji, matunzo na mambo mengine machache yasiyokuwa na gharama kwa mkulima.



Faida ni kubwa kwa mkulima, kwa kuwa zao hili huuzwa kwa kilo na ukubwa hutegemeana na matunzo shambani. Mkuu wangu kilimo cha bustani ni changamoto! Faida ipo tena nzuri ya kuridhisha kabisa. Binafsi nina uzoefu wa kutosha juu ya kilimo cha tikiti maji.


Mathalani unataka kulima ekari1 ya tikiti, huu ni mchanganuo mfupi kabisa;kawaida ekari1=sqm4000 Kwa spacing ya 1m shimo hadi shimo na 2m mstari kwa mstari na kila shimo huwa naacha miche 2 na kuruhusu matunda3. Na kama utapata mbegu ya hybrid itakuwa vizuri zaidi maana MATUNDA yake yanajiuza yenyewe, shambani ni sh1500. 

So ukishusha hesabu hapo juu: 

Jumla ya mashina ktk ekari1 ni 

Sqm4000÷(1m×2m)×2=4000 

Idadi ya MATUNDA =(4000×3)=12000 

Mauzo shambani ni 12000×1500=Tshs18,000,000/= 

Tatizo ni usimamizi, ila kilimo hiki kinalipa sana!anza kulima zao hili ili uweze kujiongezea kipato na kuondokana na umaskini wa kujitakia. Amka sasa.



AINA ZA MATIKITI MAJI

Kuna aina kuu mbili za matikiti maji, ambazo ndani yake zimegawanyika kulingana na aina ya mbegu, ilipofanyiwa utafiti na kuzalishwa. Aina hizo ni;

Matikiti yenye rangi ya kijani. Aina hii ni ya duara na huwa na umbo kubwa.

Matikiti yenye rangi ya mabaka mabaka. Aina hii ni ndefu na huwa na umbo la wastani.


Uzalishaji

Kwa kawaida ekari moja huchukua miche elfu mbili na mia tano (2,500) ya matikiti maji. Gharama ya uzalishaji wa zao hili ni ndogo sana ukilinganisha na aina nyinginezo za mazao. Tunda la tikiti maji huwa na uzito wa kati ya kilo mbili mpaka kilo kumi na tano. Kilo moja huuzwa kati ya shilingi za kitanzania 350-1000. 


Zao hili husaidia katika udhibiti wa magugu shambani, pamoja na utunzaji wa udongo kwa kuwa hutambaa na kufunika udongo.kangetakilimo



MATAYARISHO YA SHAMBA NA UPANDAJI

Baada ya kuchagua aina ya mbegu unayohitaji kupanda, inashauriwa kulima shamba na kuacha kwa muda wa kipindi kitakachoruhusu nyasi na magugu mengine kuoza kabla ya kupanda.Hii inasaidia majani na magugu kutoota upesi pindi ukipanda miche yako ya matikiti.kangetakilimo 


Hakikasha kuwa shamba lako limelimwa vizuri na udongo kulainika, udongo uwe umechimbuliwa kiasi cha inchi 8-10 kwenda chini.kangetakilimo




 Hakikisha kuwa shamba lako lina nafasi ya kutosha kwa kuwa matikiti huhitaji nafasi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kupata mwanga wa jua wa kutosha. Katika shamba la ukubwa wa hecta moja kiasi cha kilo 3-4 cha mbegu kinaweza kutumika.kangetakilimo


 Panda mbegu 2 au 3 moja kwa moja katika kila shimo. Usipande katika kitalu kwasababu miche ya mitikiti huwa ni dhaifu sana wakati wa upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 - 2 kutoka mstari hadi mstari. kangetakilimo


Zingatia kutokutumia mbegu za tikiti uliloninua kwasababu linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi na ubora wa matikiti yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)kangetakilimo


Kila shimo hakikisha umeweka mbegu tatu na uzipande kwa utaratibu wa pembe tatu au kwa lugha rahisi mafiga.

Zikishaanza kutoa matunda hakikisha kila shina unaacha matunda matatu mengine kata ili kuruhusu ukuaji mzuri wa tunda kwani yakiwa mengi yatakuwa yanagawana chakula hivyo tunda kuwa dogo ambalo ukipeleka sokoni unapata pesa kidogo.

No comments:

Post a Comment