habari kwa ufupi.
wiki hii tunajifunza juu ya mbolea za asili na jinsi ya kutumia shambani lengo kubwa ni kuzalisha vyakula hai.
Leo tutajifunza kitu ambacho huwenda ukuwai kufikiria kuhusu Mkojo wa Ng'ombe.
Utangulizi.
Mbolea ya mkojo wa Ng'ombe husaidia katika kilimo cha mazao mbalimbali, Vinavyopatikana katika Mkojo wa Ng'ombe Maji (Chumvichumvi), Madini kama vile Phosphorus, Potasiamu na Nitrojeni. Pia katika vidonda inasaidia kidogo kama ( Antimicrobial Agent).
UTENGENEZAJI WA MBOLEA YA MKOJO WA NG'OMBE.
Mbolea hii hupatikana kwa kukusanya mkojo wa mnyama na kuhifadhiwa katika chombo kama vile ndoo, dumu, pipa n'k hadi uoze kwa wastani wa siku 15 zinatosha kuozeasha mkojo huo.
JINSI KUWEKA MKOJO WA NG'OMBE SHAMBANI.
Mkojo wa Ng'ombe unaweza kutumia kwa uwiano wa lita 1 ya mkojo kwa lita 10 za maji kwa mimea midogo na kwa mimea mikubwa unaweza kutumia uwiano wa lita 1 mkojo kwa lita 5 za maji.
MATUMIZI YAKE SHAMBANI
-Kwa kupulizia katika majani- lowesha mmea wako kuanzia katika majani hadi shinani.
NB. Mkojo wa Ng'ombe ukitumia kwa mfululizo shambani unapunguza kabisa matumizi ya mbolea za viwandani.
FAIDA ZA KUTUMIA.
-Mimea huwa na rangi ya kijani zaidi.
-Inasaidia kuboresha hali nzuri ya udongo ( inaboresha soil texture)
- Inaondoa rangi ya unjano katika majani.
- Inafanya kazi kama kichocheo cha ukuaji wa mmea (growth promoters)
- Udongo uliowekwa mkojo wa ng'ombe haupati tatizo la upungufu wa madini yasio makuu(micronutrients), hivyo mbolea hii huongeza madini ya ziada katika udongo.
-Inatengeneza mazingira mazuri ya ukuaji wa minyoo (earthworm) hivyo kutengeneza mazingira mazuri ya minyoo kuozesha majani ya mimea n'k na pia kuruhusu mfumo mzuri wa hewa katika udongo.
Zingatia
Matumizi ya mkojo wa Ng'ombe kila baada ya siku 10 hadi 14 unafanya kazi kama kiua wadudu kana aphidi na wengineo.
No comments:
Post a Comment