MAANA YA SACCOS
SACCOS
ni Asasi ya fedha ya ushirika inayoundwa na watu waliojiunga pamoja kwa HIARI
yao wenyewe ambao wamekubaliana kuweka fedha zao pamoja na kukopeshana kwa
lengo la kujiendeleza kiuchumi na kijamii. Wanachama wa SACCOS mara nyingi huwa
na fungamano la pamoja. Fungamano hilo linaweza kuwa eneo wanaloishi, kuajiriwa
na mwajiri mmoja, kuwa na ajira zinazofanana (kama vile
walimu
katika shule binafsi na serikali), kusali katika msikiti, kanisa na au dhehebu
au dini moja n.k.
HISTORIA YA SACCOS.
·
SACCOS zilianzia Ujerumani katika jimbo
la Rhine River mwaka 1847 kutokana na tatizo
la ukameambapo Friedrick Reiffein Taylor alibadilisha duka la walaji ili kupata
mtaji wa kununulia ng’ombe na kuwakopesha wakulima ambao walikuwa wanarejesha
kwa awamu. Utaratibu huu hata sasaunatumika kwa kwa baadhi ya SACCOS kununua na
kuwakopesha wanachama wake vifaa badalaya kuwakopesha fedha Taslimu.
·
[ Mwaka 1883 SACCOS iliyojulikana kama
benki ya watu “peoples bank” ilianzishwa na Mjerumani Schutze Deltizch.
Mjerumani huyu alisisitiza sana katika SACCOS misingi ya kusaidiana na kujitosheleza
na msingi mwingine ni kupendana katika shughuli za SACCOS. Wote hawa walihusika
na watu wenye matatizo ya aina moja wale wa mjini na vijijini.
·
Mwaka 1936 SACCOS ya kwanza ilianzishwa
Tanzania na Watanzania wenye asili ya Kiasia. SACCOS hiyo illitwa Ismailia
SACCOS ilianzishwa Moshi mjini nab ado inaendelea kutoa huduma hadi leo.
·
Katika Tanzania kabla ya uhuru, SACCOS
zilienezwa na kanisa Katoliki [RC] na marehemu Kadinali Lauriana Rugambwa
amabaye aliwateua watu watatu kujifunza uendeshaji wa SACCOS Kanada.Shughuli za
kufunza wananchi zilianzia Mission ya Nyegezi baadae kuenea katika maeneo
mengine. Bwana Joseph Mutayoba ambaye alikuwa momjowapo waliopata mafunzo
alichaguliwa kuwa Mweneykiti wa Kwanza wa Muungano wa Vyama vya Ushirika wa
Akiba na Mikopo Tanganyika (SCULT)
·
Baada ya uhuru mwaka 1961, kampeni ya
uanzishwaji wa SACCOS kupelekwa nchini Kanada na Marekani kwa ajili kujifunza
uendeshaji wa SACCOS.
IMEANDIKWA NA OMBENI HAULE
KWA ELIMU NA USHAURI WASILIANA NASI KWA NAMBA
0659144660/0758069046
No comments:
Post a Comment