VICOBA (Village Community Bank) ni mfumo wa kuweka
na kukopa kwa wanachama waliojiunga kwa pamoja na kuunda kikundi kwa malengo ya
kujikwamua kiuchumi. Mfumo huu ulianza Tanzania miaka kumi iliyopita na
umeonyesha mafanikio makubwa kwa wanachama wake kuweza kukopeshana, kusaidiana
katika matatizo mbalimbali, kuanzisha miradi ya pamoja ya kiuchumi.
LENGO/MADHUMUNI YA KUUNDA VICOBA
Madhumuni ya kuunda vicoba ni kuunganisha nguvu na rasilimali za wanachama ili kuondoa umaskini na kuleta maendeleo kwa kufanya yafuatayo:-
LENGO/MADHUMUNI YA KUUNDA VICOBA
Madhumuni ya kuunda vicoba ni kuunganisha nguvu na rasilimali za wanachama ili kuondoa umaskini na kuleta maendeleo kwa kufanya yafuatayo:-
- Kuchangia/kununua hisa
- Kuchangia mfuko wa jamii
- Kuendesha mfuko wa kuweka na kukopa
- Kushiriki katika mafunzo ya kuongeza ujuzi wa biashara, uongozi na uanzishaji wa shughuli mbalimbali za pamoja za maendeleo.
- Kutafuata soko la pamoja na la uhakika kwa bidhaa za wanakikundi
Kuna tofauti gani kati ya VICOBA na SACCOS?
VICOBA na SACCOS ni vikundi vya kiuchumi vyote vina malengo sawa isipokuwa mfumo wa uendeshaji.
1.
Katika
VICOBA wanachama uweka kiwango cha hisa na mara nyingi huanzia Sh.1000 na
kuendelea, kiwango hicho ni kidogo ukilinganisha na kiwango cha hisa katika
SACCOS.
2. WanaVICOBA
umaliza mzunguko wao baada ya miezi kumi na mbili (12) na kufanya tathmini
ikiwemo kugawana makusanyo na faida.
3. Riba ya mkopo katika
VICOBA ni ndogo (mara nyingi haizidi 10%)
4. Kikundi cha VICOBA
kinaundwa na wanachama 15-30, wanaoishi eneo moja au wanaofanya kazi pamoja.
5. Gharama za
uendeshaji wa VICOBA ni ndogo kwani hakuna ofisi (wanachama huchagua mahali pa
kukutana kwa muda usiozidi saa moja), vile vile viongozi wa VICOBA hawaajiriwi
(wanafanya kazi za kujitolea)
Vicoba
ikikuwa inaweza kuunda SACCOS. Mfumo wa Vicoba ni mzuri hasa kwa falsafa ya
kuanza kidogo ili kuwa na kitu kikubwa hapo baadae. Licha ya kujihusisha na
shughuri za kuweka na kukopa, wanavicoba husaidiana katika matatizo mbalimbali
kama msiba na ugonjwa. Vile vile wanavicoba wanaweza kuanzisha mradi wa pamoja
wa kikundi kwa kuunganisha rasirimali ndogo walizonazo.
Hatua za Kuunda kikundi cha VICOBA
1.
Watu
wenye wazo la kuanzisha kikundi kukutana (watu hao wasipungue kumi na tano na
wasizidi therathini)
2. Wanachama kukusanya
fedha za kiingilio (mara nyingi ni Sh. 10,000) kwa mwanachama. Fedha hiyo
hutumika kununua vifaa kama leja,kasiki n.k. Fedha ya kiingilio vilevile
hutumika kugharamia mafunzo ya awali na gharama ya usajiri wa kikundi)
3. Wanachama kuanza
mafunzo yatakayosimamiwa na mwalimu mtaalamu wa mfumo huu wa vicoba.
4. Wanachama kutunga
katiba na sheria zitakayojumuisha kiwango cha hisa, mfuko wa jamii, siku ya
kukutana n.k
WADAU WANAOTEKELEZA MFUMO VICOBA TANZANIA
Kwa
miaka mingi sasa wadau mbalimbali wanahamashisha vikundi katika maeneo
mbalimbali
na miongoni mwa wadau hao ni pamoja na UPEO, TEC, CCT, BAKWATA, AEE,
Pathfinder
International, AFRICARE, LAMP, LIWODET, MEPP, RUMAKI, Social Economic
Development
Initiative of Tanzania, SELL, VDSA, WWF, ORGUT, FLORESTA, ELCT(ND, ECD,
Mbulu)
TCRS, TANARELA, AXIOUS Foundation, WCST, ITECCO, Frankfurt Zoological
Society,
UYACODE, YWCA, EFG na wengine wengi. Maeneo mbalimbali ya Tanzania
yameweza
kufikiwa japo siyo wadau wote wanatekeleza mfumo huu kama inavyo
takiwa.
UMADHUBUTI WA VICOBA
1.3.1.
Uanzishaji wa kikundi cha VICOBA hauhitaji mtaji. Makusanyo ya kila wiki
yanayotolewa na wanakikundi ndiyo
huanzisha mfuko wa kukopesha.
1.3.2.
Vikundi huanzishwa karibu na maeneo ya wanachama wanayoishi hivyo
hupunguza gharama ya nauli na
matumizi mabaya ya muda.
1.3.3.
Mikopo ya VICOBA haina ukiritimba kama fedha zipo, maana wanakikundi
wanajua mwenendo mzima wa fedha za
kikundi kwa sababu shughuli zote za
kikikundi hufanywa mbele ya
wanakikundi wote.
1.3.4.
Kupitia mfumo huu wanakikundi wanatumia mikutano ya kikundi kama sehemu
ya kujifunza mambo mengine kama vile elimu ya
biashara, masuala ya kisheria,
ukatili wa kijinsia, jinsi ya
kuhudumia watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi,
kuelimishana haki za kila mtu na
mambo mengine ambayo wanakikundi
wanaona ni muhimu kwao kuyajadili na
kujifunza.
1.3.5.
Mfumo wa utunzaji wa kumbukumbu ni rahisi ambao unawawezesha
wanakikundi kusimamia kumbukumbu zao
za fedha bila kuhitaji elimu ya juu ya
utunzaji wa fedha.
1.3.6.
Ziada ya mikopo inayopatikana hutolewa mgao kwa wanakikundi wote mwisho
O
idadi ya hisa zake.
Imeandikwa na Ombeni Haule
Kwa elimu na ushauri wasiliana nasi kwa simu namba
0659144660/0758069046
No comments:
Post a Comment