Nyumba
ya kulelea Vifaranga
Ukipenda kujenga nyumba ya vifaranga
itafaa ufi kirie yafuatayo:-
a Nyumba ya vifaranga iwe karibu na
nyumba yako mwenyewe ili uweze kuwakagua
vifaranga wako mara kwa mara.
b) Ijengwe hatua 20 au zaidi mbali na
nyumba ya kuku wakubwa, hii ni kinga mojawapo ya kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa.
c) Nyumba ya vifaranga isiruhusu
ubaridi au unyevu au wanyama waharibifu kuingia. Lakini nyumba iingize hewa na
mwanga wa kutosha kila wakati.
d) Nyumba iwe na eneo la kutosha ili
vifaranga wapate nafasi ya kutembea kutafuta chakula na maji bila kubanana.
e) Ijengwe kwenye sehemu isiyoelekea
upepo unaotoka kwenye nyumba ya kuku wakubwa. Tahadhari hii husaidia vifaranga
kuepukana na magonjwa yanayoenezwa
na upepo.
Ukubwa
wa Nyumba
Eneo: Vifaranga
hawahitaji eneo kubwa katika muda wa majuma 4 ya kwanza. Nafasi
inayohitajiwa kwa kukadiria ni meta za
eneo 1 kwa kila vifaranga 16. Kwa mfano nyumba
yenye meta 10 za mraba inatosha kulea
vifaranga 160 hadi umri wa majuma 4. Vipimo
vya nyumba yenye eneo kama hili inaweza
kuwa na hatua 5 kwa hatua 4 au hatua 3 kwa
3.25. Utajenga kutegemea na eneo
ulilonalo. Baada ya majuma 4 ya umri ongeza nafasi na
uwape vifaranga eneo la kuwatosha.
Sakafu: Sakafu nzuri katika nyumba ya vifaranga
ikiwezekana inafaa ijengwe na simenti
iliochanganywa na zege. Ili kupunguza
gharama, unaweza kutumia vifaa vya ujenzi
vinavyopatikana kirahisi katika eneo
lako vitumikavyo kusiriba sakafu kama udongo wa
kichuguu au unaweza kulainisha kinyesi
cha ng’ombe kwa maji na kusiriba eneo lote la
sakafu.
Ukuta: Ingefaa kuta za
nyumba za kulea vifaranga za matofali, udongo, mabati au debe.
Kuta za matofari na udongo zipigwe lipu
ili kurahisisha usafi shaji wa nyumba au umwagiaji
wa dawa. Urefu wa kuta uwe tangu meta
1.8 – 2.4 (futi 6-8). Sehemu ya kutoka chini ya meta
0.9 – 1.2 (futi 3 – 4) izibwe na ukuta
wa tofali au udongo na sehemu ya juu iliyobakia yenye
meta 0.9 – 1.2 (futi) 3-4) ijengwe kwa
wavu wa chuma au fi to.
Mbao: Nguzo za miti au
mbao zilowekwe dawa ya mbao kama vile “Dudu killer” au oili chafu
ili kuzuia kuoza. Ukitumia miti ni
vizuri uondoe magome ambayo yanaweza kuweka vimelea
na wadudu.
Madirisha: Unaweza kutumia
maboksi, mikeka ya magunia, mapazia ya magunia ni rahisi na
yanaweza kuwekwa kwa kupigiliwa
misumari kwenye dari na upande wa chini pazia ipigiliwe
misumari kwenye ubao ili
ininginie.Unaweza kukunja mapazia/magunia ili uingize hewa na
mwanga wa kutosha katika nyumnyumba ya
vifaranga.
Paa: Mjengo wa paa uwe
unaoweza kuwapatia vifaranga hewa ya kutosha hivyo paa liwe na
tundu la kutoa nje hewa yenye joto. Kwa
kadri utakavyoweza, unaweza kutumia madebe,
mabati, makuti au nyasi n.k. kuezeka
nyumba ya vifaranga. Sehemu ya paa ikianza kuvuja
iezekwe bila kuchelewa.
IMEANDIKWA NA OMBENI
HAULE
KWA ELIMU NA USHAURI
WASILIANA NASI KWA NAMBA
0659144660/0758069046
No comments:
Post a Comment