April 05, 2017

ANZA KUKIFUATILIA KITABU CHETU CHA UTENGENEZAJI WA BIDHAA MBALIMBALI ZA VIWANDANI.. FURSA ya UTENGENEZAJI WA BATIKI TIE NA DIE ,,SOMO LA KWANZA



 BATIKI
Ni aina ya nguo au vazi la asili  linayotengenezwa kwa mikono kwa kuweka picha michoro na urembo mbalimbali.kwaapa tanzania batiki soko lake kubwa na watu wengi wamejikita kufanya ujasiriamali huu unawaingizia kipato kikubwa na kuweza kumudu maisha yakitanzania..





Malighafi zinazotumika kutengeneza batiki:
1.      Caustic soda vijiko vitatu vya chakula
2.      Sodium hydrosuphet vijiko vya chakula
3.      Rangi vijiko viwili vya chakula.
4.      Maji ya moto lita tano koroga kwa dakika mbili.
5.      Weka maji ya baridi lita tano.
6.      Parafin wax kilo moja.
7.      Vibao au sponch za picha mbalimbali.

VIFAA VYA KUTENGENEZEA:
Meza kubwa, sufuria, kitambaa cha mpira au kapeti misumari midogo, vibao au sponchi ya urembo, jiko.

JINSI YA KUTENGENEZA : Hatua ya kwanza.
1.      Chemsha mshumaa
2.      Tandika vitambaa mezani
3.      Chovya kibao chako kwenye mshumaa, gonga kwenye kitambaa.

JINSI KUTENGENEZA: Hatua ya pili
1.      Andaa ndoo au beseni, chemsha
2.      Weka malighafi namba moja hadi tatu, weka maji ya uvuguvugu.
3.      Tumbukiza kitambaa kwa dakika kumi, anika kipoe.
4.      Chemsha maji ya moto na sabuni ya maji
5.      Tumbukiza kitambaa kuondoa mshumaa na geuza ili mshumaa utoke wote
6.      Fua anika piga pasi peleka sokoni.


















TIE AND DYE
Ni aina ya batiki ya kukunja mikunjo kwa kutumia mkono
Malighafi
1.      Coustic soda vijiko vinne vya chakula
2.      Sodium hydrosulphet vijiko vitano vya chakula
3.      Rangi vijiko vine vya chakula.

VITENDEA KAZI:
Meza, kitambaa cha pambe, kalamu, uzi, sindano, mkasi, kamba, sufuria kijiko kikubwa, ndoo au beseni, jiko, vibanio, maskinna gloves.

AINA ZA TIE AND DYE.
1.      Kushona- chora  mchoro wowote  ushone, halafu vuta na uzi kwa nguvu.
2.      Kufanya- loweka kitambaa kisha tandika kwenye mkeka au nailoni, anza kuvuta kwa kufinyanga, kisha mwagia dawa.
3.      Funga uzi na kamba-kunja mkunjo wowote funga na kamba, tumbukiza kwenye dawa.
4.      Kutumia blichi (jiki)- tandika kitambaa kwenye meza halafu mwagia blichi yako uliyoiweka kwenye chupa na kutoboa mfuniko kwa ajili ya kutoa blich yako kama urembo.

JINSI YA KUTENGENEZA.
1.      Chemsha maji ya moto
2.      Pima malighafi ya kwanza hadi ya tatu, weka vyote kwenye beseni.
3.      Weka maji ya moto lita tano, koroga kwa dakika tatu, ongeza maji ya baridi lita tano
4.      Chovya kitambaa kwenye rangi acha kwa dakika kumi hadi kumi na tano
5.      Suuza kwenye maji baridi anika kisha piga pasi, tayari kwa kwenda sokoni

KIMEANDIKWA NA OMBENI HAULE 
ELIMU na USHAURI WASILIANA NASI KWA NAMBA 
0659144660/0758069046/ombenihaule@gmail.com
kitabu cha utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani kinapatikana

4 comments:

  1. Habari za leo ..je kitambaa kama rangi haijakolea inamaanisha ni rangi ndio tatizo au kuna mahali tulikosea?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ina tegemeana lakin mara kama rangi haijakolea basi itakuwa upande wa kemilaki ulichanganya hapo ..HUkufata vipimo

      Delete
  2. unaweza kunitafuta zaidi ili tusaidiane 0718567689/ 0684-863138

    ReplyDelete
  3. naitaji kujifunza kutengeneza batiki 0655138215

    ReplyDelete