April 04, 2017

IJUE MIRADI YA UZALISHAJI MALI



MIRADI YA UZALISHAJI MALI

     Maana ya mradi
Mradi ni shughuli yeyote maalumu iliyohalali , inayotumia raslimali kwa lengo la kutatua tatizo katika muda maalumu.
Tatizo ni hali isiyoridhisha [mapungufu]. Ukianzisha mradi usiotatua tatizo huo siyo mradi.

      


Sifa za mradi.
           Mradi mzuri wa kuongeza kipato unasifa zifuatazo ;
(i)   Unachangia kuboresha maisha ya mlengwa.
(ii) Uwe wa kuingiza faida, hivyo kufanya kuwa endelevu.
(iii) Mlengwa awe na uwezo wa kuuendesha na kuusimamia mwenyewe.
(iv)  Una mtaji.
(v)    Unakuwa na kupanuka.
(vi)  Una wateja [soko]
(vii)Unatunza kumbukumbu zote za muhimu vizuri.

Wazo la mradi. [Wazo ghafi]
Mawazo ghafi ni hatua ya mwanzo katika kuanzisha mradi na wazo ghafi ni wazo lililo kwenye fikra na halijafanyiwa tathimini. Mtu anakuwa na msukumo wa kuanzisha mradi wa kuongeza kipato baada ya kusongwa na kero kubwa kama vile kushindwa kumudu gharama za maisha, gharama za kusomesha watoto, mavazi duni wakati wa sikukuu, majirani kumtambia. Hivyo mradi wa kuongeza kipato ni njia pekee ya kumkomboa na kero hizo. Sijui niuze mkaa?.
1)    Sijui niuze mbao?.
2)    Sijui nilime pamba?.
3)    Sijui nilime bustani?.
4)    Sijui nianzishe duka?.
5)    Sijui nianzishe saloon?.
6)    Sijui nifuge kuku?.
7)    Sijui nifuge nyuki?.
8)    Sijui nifuge samaki?.
9)    Uanzishaji wa mradi katika hatua hii mara nyingi sana hufa.
        
Kutathimini wazo la mradi
Mradi kabla ya kuanzishwa sharti utathiminiwe kwa kuzingatia vipengele vifuatavyo ;
Faida ipatikanayo  
 Mauzo - Gharama = 0 (Hakuna faida wala hasara)               
 Mauzo - Gharama = Faida (Iwapo mauzo ni makubwa) 
                      Mauzo - Gharama = Hasara.(Iwapo gharama ni kubwa)
 
Kukua kwa biashara: Biashara inaweza kufikia ukomo sehemu moja na kulazimika kufungua biashara. Hiyo hiyo sehemu nyingine ikaendelea kukuza mtaji wako.

Kupanuka kwa biashara: Kuanzisha biashara nyingine tofauti hapo hapo au mahali pengine

Kumunufaisha mjasiriamali: Je mradi huu utatatua sasa kero za mjasiriamali katika muda mfupi ?. au muda Mrefu?                      
·        Eleza manufaa ya mradi kama vile kuwezesha kiuchumi, kuongeza ajira, kuongeza lishe.             
·        Eleza manufaa ya mradi kwa kuzingatia faida za kiuchumi na kijamii, manufaa ya moja kwa moja na yasiyo ya moja kwa moja. 
Uwezo wa mjasiriamali mwenyewe
 Mjasiriamali ana uwezo wa kuendesha huo mradi ?. Ana stadi katika mradi anaokusudia Mtaji binafsi alionao wa kuanzisha mradi.

Udhaifu wa mjasiriamali
 Mapungufu katika ufahamu, stadi na mtaji.

Fursa zilizopo zinazoweza kumfanya mjasiriamali akabiliane na udhaifu na Vikwazo.
 Vikwazo vilivyopo vinavyoweza kukwamisha mradi wa mjasiriamali – sera za nchi, kupanda na kushuka kwa mali ghafi, majanga n.k.
 H adi hapo mjasiriamali atakuwa amepata jibu kuhusu mradi anaokusudia, Aanzishe Mradi au la?

KIMEANDIKWA NA OMBENI HAULE 
ELIMU USHAULI WASILIANA NASI KWA NAMBA 
0659144660/0758069046/ombenihaule@gmail.com
kitabu cha fursa za biashara kinapatikana

No comments:

Post a Comment