Skip to main content
ANZISHA MRADI WAKUTENGENEZA KEKI MBALIMBALI
KEKI
MALIGHAFI
Blue band ½ kg
Sukari1/4 kg
Mayai 6
Unga wa ngano nusu kilo
Backing powder vijiko vya chakura 2
Maziwa kikombe cha chai kimoja
Vanilla falovor, chocolate strawberry
kijiko cha chai 1
Ice sugar packet 1
Rangi ya chakura kijiko 1 cha chai
HATUWA
YAKWANZA 1 KUANDAA KEKI
Andaa bakuli la kioo udongo au plastic
Andaa mwiko
Chukua blue band na sukari changanya
pamoja katika bakuli lako (epuka kutumia chombo cha bati kwasababu ya kutu)
Koroga sukari na blue band pamoja kwa
kutumia mwiko mpaka vilainike vizuri na povu limetokea.
Anza kuongeza yai moja huku ukikoroga
mpaka yafike mayai 4 na mchanganyiko
wako uwe mweupe.
Chekecha unga wako wa ngano vizuri
kabisa ukiwa tayari umekwisha changanywa na banking powder.
Changanya unga wako kwenye mkorogo wa
sukari blue band na mayai kisha koroga vizuri mchanganyiko wako.
Kisha ongeza maziwa kiasi na vanilla
kijiko kidogo kimoja endelea kukoroga vizuri.
Mchanganyiko huo ukishalainika vizuri acha
utulie kidogo kama dakika 5 huku ukifanya maandalizi ya kuoka keki
HATUWA
2 KUHOKA KEKI
Andaa chombo chako trey au sufuria au
chombo chochote cha bati chenye shepu au umbo ambalo ungehitaji.
Chukua blueband pakaa pembeni ndani ya
chombo chako cha kuokea kwa kutumia karatasi.b (tishu)
Kisha weka mchanganyiko wako katika
chombo cha kuokea weka jikoni kwa muda wa dakika 5, hakikisha moto unakuwa
kidogo ukiwa umepalilia kama wali.
HATUWA
YA 3 KUPAMBA KEKI
Andaa bakuli yako, chukuwa maya mawili
yaliyobaki kisha toboa kidogo na mimina
ute mweupe wa yai katika bakuli, hakikisha ni ute mweupe tu bila kiini cha yai.
Weka ice sugar vijiko 8 vya chakura
katika ule ute mweupe kisha koroga uwe mzito baada ya apo gawa mkorogo wako
katika bakuli mbili mkorogo mmoja weka rangi na mwingine usiweke rangi, mkorogo
usio na rangi pakaa kwenye keki yako yote iwe nyeupe kisha mkorogo wenye rangi
uweke kwenye penseli ya kupambia na uanze kupamba keki yako kwakuweka picha maumbo
na michoro mbalimbali.
ü
IMEANDIKWA NA OMBENI HAULE
ELIMU NA USHAURI WASILIANA NASI KWA NAMBA
0659144660/0758069046/ombenihaule@mail.com
Comments
Post a Comment