Kilimo cha uyoga ni fursa yenye tija iliyojificha na inafanywa na watanzania wachache sana lakini inafaida kubwa ukiamua kuifanya ,mtaji wake ni mdogo pia unaweza ukafanya kilimo hichi katika eneo dogo nyumbani au shambani ,kilomoja ya uyoga inauzwa tsh 5,000/= mpaka 6,000/= na soko lauhakika sana
UTANGULIZI.
Uyoga ni aina ya nyuzi kuvu (fungus)
yenye kutofautiana na mimea mingine kwa kukosa chembe chembe zinazowezesha
mimea kujitengenezea chakula yenyewe kwa kutumia hewa na mwanga.
Uyoga unaota wenyewe kwenye mashamba
hasa wakati wa mvua kwenye maeneo yenye mboji nyingi. Sasa hivi nchini tunao
utaalamu wa kuotesha uyoga au ndani ya nyumba au nje kwenye kivuli maalumu.
HISTORIA YA UYOGA.
Uyoga umefahamika na wanadamu tangu enzi
za zamani sana. Miaka elfu nne kabla ya kuzaliwa Kristo watu walijua uyoga.
Historia inatueleza kwamba watu wameanza kulima kwa utaalamu mwaka 300 baada ya
kuzaliwa Kristo.
Wadadisi wa mambo wanauelezea Uyoga
kufanana sana na chakula waisraeli walichokuwa wakila kule jangwani katika
safari yao ya kutoka utumwani Misri.
Wakati Uyoga ukilimwa katika dunia yote,
hapa Afrika na hasa kwetu Tanzania mambo yalikuwa ni tofauti kabisa. Hakuna mtu
aliyesumbuka na kilimo hicho. Ni hapo majuzi tu mwaka 1993 ndipo ukulima
ulianza Dar es salaam. Mwaka 1994 ukulima ulianza Arusha, mwaka 1995 ukulima
ulianza huko Mbeya, na mwaka 2003 ukulima ulianza huko Kilimanjaro.
AINA YA UYOGA.
Inakadiriwa kuwa kuna aina milioni moja
na laki tano (1,500,000) za nyuzi kuvu (fungus) duniani; katika hizi ni aina
64,000 ambazo zimekwisha kufanyiwa utafiti na kupatiwa maelezo ya kisayansi.
Katika hizi aina 64,000, kuna ambazo zimethibitika kuwa na Uyoga halali 12,000.
Na kati ya hizi ni aina 2,000 na ndizo zinazolimwa.
Katika aina 2,000 za uyoga zilizokwisha thtbitika, hapa Tanzania ni aina 40 tu.
Katika aina 2,000 za uyoga zilizokwisha thtbitika, hapa Tanzania ni aina 40 tu.
Uyoga Mamama (Oyster mushroom).
Aina hii ya Uyoga hustawi katika nchi za
Tropics. Utaalamu unaohitajika siyo mgumu. Baadhi ya aina zinazooteshwa ni hizi
zifuatazo;
. Pleurotus oystreotus
. Pleaurotus sajo-caju
. Pleaurotus sapidus
. Pleurotus flabel atus - (pink oyster)
. Leaurotus Pulmonerius
. H. K. n.k
. Monkey Head
. Auriclaria
. Pleurotus oystreotus
. Pleaurotus sajo-caju
. Pleaurotus sapidus
. Pleurotus flabel atus - (pink oyster)
. Leaurotus Pulmonerius
. H. K. n.k
. Monkey Head
. Auriclaria
Nyingine zinazooteshwa hapa nchini kwa
kiasi kidogo ni;
. Agaricus bitoquis (uyoga vifungu)
. Agaricus bitoquis (uyoga vifungu)
Uyoga taka ambazo ni;
. Coprinus cinereus
. Caprinus Comatus
. Lentinus edodes
. Volvoriella Volvocea
. Coprinus cinereus
. Caprinus Comatus
. Lentinus edodes
. Volvoriella Volvocea
Nyingine ni;
. Ganodema lucidum
. Ganodema lucidum
FAIDA ZA UYOGA
Uyoga una maajabu makubwa katika maisha
ya mwanadamu, Uyoga ni lishe bora kwa mwanadamu, ni dawa na tiba kwa mwanadamu,
ni zao la kuingizia watu kipato, ni rafiki wa mazingira pia.
LISHE
. Uyoga ni zao lenye viini lishe (amino
acids) zote 22 zinazohitajika na mwili wa mwanadamu.
. Protini iliyoko kwenye Uyoga inafikia
kiwango cha asilimia arobaini. Hii inalingana na protini iliyoko kwenye maziwa.
. Kuna wingi mkubwa sana wa vitamini B,C
na D.
. Uyoga hauna mafuta mengi. Una asilimia
tatu tu. Hivyo hauna Colestrol.
. Uyoga unayo madini yote muhimu kwa
mwanadamu; phosphorus, Iron, Calcium na Potash.
TIBA
Utafiti uliofanyika siku za karibuni
umethibitisha kuwepo kwa dawa nyingi ndani ya uyoga zenye uwezo wa kutibu kwa
ufanisi, magonjwa ya wanadamu na mifugo. Kwa wanadamu magonjwa yafuatayo
yanatibiwa;
. Kifua kikuu TB
. HIV/AID upungufu wa kinga mwilini
. Kisukari
. Shinikizo la damu
. Magonjwa ya moyo na uti wa mgongo
. Saratani
. Matatizo ya figo
. Vifo vya watoto wachanga
. HIV/AID upungufu wa kinga mwilini
. Kisukari
. Shinikizo la damu
. Magonjwa ya moyo na uti wa mgongo
. Saratani
. Matatizo ya figo
. Vifo vya watoto wachanga
KUSAFISHA MAZINGIRA
Kufuatana na ripoti ya wataalamu wa chuo
kikuu Kivais na Magingo ya miaka ya tisini, Tanzania inayo masalio ya kilimo na
misitu zaidi ya tani milioni kumi na saba (17,000,000). Masalio haya yameachwa
yakioza, au kuchomwa moto au kulishwa mchwa pamoja na mapanya. Ikiwa masalio
haya yatatumika kuoteshea Uyoga, Mazingira yataboreka na uchumi utakua.
Uzalishaji wa Uyoga unaanzia pale mkulima au mtumiaji wa bidhaa za kilimo na
misitu anapomalizia.
MASALIO YA TAKATAKA BAADA YA KUOTESHA
UYOGA.
Masalio ya takataka (vimeng'enywe)
hutumika kama ifuatavyo;
.
KULISHA MIFUGO
Uyoga una uwezo wa kuvunja vunja chembe
chembe za vimeng'enywe na kuviboresha kuwa protini na madini mengi, kisha
kufyonza hicho na kutengeneza matunda ya uyoga. Baada ya kuvuna uyoga
chembechembe hizi bado zina ubora mkubwa wa chakula kwa ajili ya mifugo kama
vile ng'ombe, mbuzi, nguruwe, sungura n.k. Tunao wafugaji wanaotumia
vimeng'enywe hivi kulishia mifugo nao wameendelea kupata maziwa mengi.
.
MBOLEA
Vimeng'enywe hivi hutumika kama mbolea
shambani na katika bustani. Matokeo ya kutumia vimeng'enywe hivi yameonyesha
ufanisi mkubwa.
.
METHANE GAS
Tukijenga mfumo wa kutengeneza gesi kama
kawaida, tunaweza kutumia vimeng'enywe hivi kutengeneza methane gas. Hii gesi
itatumika kupikia, kuwasha taa na mambo mengine kama hayo. Mabaki katika zoezi
hili huwa na mbolea nzuri ifaayo sana. Mazao ya shamba na bustani yaliyokuzwa
kwa mbolea hii yana bei nzuri zaidi sokoni, maana yanahesabika yamezalishwa
kiasili (organic agriculture).
. ZERI ( Zero Emmission Research Initiative).
Umoja wa Mataiga umeiteua Tanzania
pamoja na nchi nyingine katika bara la Afrika kuendeleza na kutekeleza mfumo wa
ZERI. Huu ni mfumo wa kutochafua mazingira kwa njia ya kutoa moshi. Masalia ya
kilimo ba misitu yasichomwe moto bali yageuzwe kutoka hali yake na kuwa kitu
kingine labda kilicho bora na chenye thamani zaidi. Masalia ya sokoni
hatutayaacha yaoze bure, tutayasindika ili yaweze kuzalishia uyoga. Pumba za
mpunga na kahawa hatutazichoma moto. Tutazitumia kwa kuzitengenezea chipboards,
vivyo hivyo na maranda ya mbao, takataka za katani, kahawa na n.k. zitageuzwa
kuwa kitu bora zaidi.
UTAYARISHAJI WA SHAMBA LA UYOGA.
Mambo ya muhimu ya kuzingatia:
. Ukubwa wa shamba
. Uwezekano wa upanuzi
. Usafi wa eneo
. Upatikanaji wa takataka za kulimia yaani vimeng'enywe
. Upatikanaji wa maji safi
. Umbali kutoka kwenye soko
. Ukubwa wa shamba
. Uwezekano wa upanuzi
. Usafi wa eneo
. Upatikanaji wa takataka za kulimia yaani vimeng'enywe
. Upatikanaji wa maji safi
. Umbali kutoka kwenye soko
Ndani ya ndani
. Hewa safi ya inayozunguka
. Joto linalotakiwa
. Unyevunyevu kwenye hewa unaotakiwa
. Carbondioxide na mwanga vinatakiwa
. Joto linalotakiwa
. Unyevunyevu kwenye hewa unaotakiwa
. Carbondioxide na mwanga vinatakiwa
Shamba
Shamba la uyoga linapaswa liwe na
viambatanisho vifuatavyo;
. Sehemu ya kutayarisha vimeng'enywe
. Kichanja cha kuhifadhi majani au aina yoyote nyingine ya vimeng'enywe.
. Sehemu ya kuchemshia vimeng'enywe
. Sehemu ya kupandia mbegu kwenye vimeng'enywe vilivyokwisha kuchemshwa.
. Banda kamili la kukuzia lenye sifa zilizokwisha ainishwa hapo juu
. Sehemu ya kuhifadhia uyoga uliovunwa au chumba cha baridi kutegemea na hali halisi.

KUANDAA SHAMBA LAKUOTESHEA UYO
Mkulima anashauriwa kutumia vifaa
vinavyopatikana katika eneo lenyewe. Kwa mfano mkulima mwenye shamba la
migomba, baai atumie marawa katika kuta na paa. Unaweza ukatumia nyasi za
kawaida au majani ya mpunga, ngano na mengine ya namna hiyo, unaweza kutumia
matofali mabichi, unaweza kutumia mabanzi. Ndani ya nyumba weka weupe. Hii ni
chokaa au kitambaa cheupe. Hii ni kwa sababu uyoga hukua kuelekea rangi ya
mazingira yaliyouzunguka. Lakini rangi nyeupe huchochea ukuaji na hudumisha
usafi. Nyumba ya uyoga iwe na madirisha makubwa mazuri.
MAANDALIZI YA VIMENG'ENYWE
Kama ilivyosemwa hapo mwanzo, kila jani
lililokomaa na kukauka, lafaa kuoteshea uyoga. Michanganyiko ifuatayo yafaa
sana kuoteshea uyoga.
. Majani ya mpunga au migomba yenye
unyevu 62%
. Pumba za mahindi unyevu 62%
. Sukari
. Chokaa
. Pumba za mahindi unyevu 62%
. Sukari
. Chokaa
Vimeng'enywe viko vingi, mkulima
anashauriwa awaone wataalamu kwa ushauri.
MAHITAJI MENGINE
Ifuatayo ni orodha ya mahitaji mengine;
. Jiko la kuchemshia
. Pipa tupu la lita mia mbili
. Mifuko ya plastic size 10" × 15" yenye uwezo wa kuhimili joto
. Viroba (polysacks) pvs ya kuweka ndani ya pipa
. Vibangili vya kipenyo cha 1.5
. Kamba au uzi wa kushonea viatu ili kufunga mifuko wakati wa kuchemsha.
. Vipande vya magazeti
. Rubber band size ya mpira wa ndana ya tairi ya baiskeli.

HATUA ZA KUFUATA KATIKA KUOTESHA
. Katakata majani yaliyokomaa na makavu
katika urefu usiozidi nchi nne
. Changanya majani haya na virutubisho hapo juu i.e. pumba za mahindi, sukari na chokaa.
. Changanya sawasawa kwa kutumia maji safi ndoo tatu hadi tano.
. Zilundike mahali safi ukitengeneza mlinduko wenye kimo cha mita moja hadi mita moja na nusu.
. Funika kwa polythene paper na vitambaa vya sulphate
. Majani ya migomba yalowekwe kwa siku mbili hadi tatu kabla ya kuvundikwa
. Ziache kwa muda wa masaa 24
. Weka vimeng'enywe hivi katika mifuko ya polythene
. Weka maji lita 40 katika pipa lenye kichanja cha mbao chenye kuzuia mifuko isigusane na maji
. Bandika kwenye jiko hadi mvuke unapotoka , hesabu msaa manne.
. Ipua mifuko yako na iweke mahali safi
. Sasa ni wakati wa kufanya kila kitu kwa hali usafi. Tunatumia maji yenye detol kusuzia mikono yetu
. Otesha uyoga kama mtaalamu atakavyokuonyesha
. Baada ya siku 21 ondoa vipande vya gazeti ulivyotumia kufunika mifuko
. Baada ya siku 10 nyingine utaanza kuvuna uyoga. Uta una kwa muda wa miezi 2 hadi 3
. Weka uyoga uliovuna ili kuhifadhi ubora wa uyoga.

MAGONJWA YA UYOGA
Uyoga ni viumbe hai. Hivyo hupatwa na
magonjwa kama hali ya mazingira na utendaji haitakidhi. Kuna magonjwa ya aina
kama ifutavyo;
. Bacteria
Uyoga unakuwa na rangi ya kutu. Hata
mifuniko inakuwa na rangi hiyo. Ugonjwa huu unatambulika kiurahisi., kwani
unakuwa unateleza.
. Fungus
Aina zifuatazo ndizo hasa zishajulikana;
. Blue mould
. Black mould
. Brown mould
. Blue mould
. Black mould
. Brown mould
. Virus
Uyoga uliopendeza unasinyaa mara moja.
Unaanza kutoka jasho.
MASOKO
Mpaka sasa hoteli za kitalii zinapika
uyoga wa kutoka nje uliowekwa kwenye makopo.
Ikumbukwe kuwa kwenye makopo kuna uyoga halisi kidogo sana. Pia katika supermarket za hapa nchini kuna uyoga fresh kutoka Kenya. Pia tujue kuwa majirani wetu waliotuzunguka Kenya, Uganda, Zambia na Malawi wamepiga hatua kubwa katika kilimo cha uyoga. Swali tunalopaswa tujiulize sote ni hili " Kulikoni Tanzania kuhusu Uyoga".

KIMEANDIKWA NA OMBENI HAULE
KWA ELIMU NA USHAURI WASILIANA NASI KWA NAMBA
0659144660/0758069046/ ombenihaule@mail.com
kitabu cha kilimo bora cha uyoga kinapatikana kwa PDF
No comments:
Post a Comment