April 04, 2017

ONGEZA KIPATO NA KILIMO CHA BAMIA

 BAMIA
Asili ya mboga hii ni Afrika ya Kati na ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili limekwisha enea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama Visiwa vya Caribbean, Malaysia na Philipines.

Urefu wa mmea huwa kati ya meta moja na mbili. Matunda yake hufikia urefu wa sentimeta 10 hadi 20, na huchumwa kabla hayajakomaa sana na hupikwa pamoja na nyama, samaki au mboga nyingine. Majani yake huchumwa yakiwa bado machanga na kutumiwa kama mboga nyingine za majani.

Aina za bamia zinazojulikana zaidi ni Clemson Spineless, Emerald Green, White Velvet, Perkins Mammoth na Dwarf Prolific.

Ustawishaji:
 Zao hili hustawi katika mite 1000 kutoka usawa wa bahari na hushindwa kuvumilia hali ya baridi kali. Hustawi katika katika aina nyingi za udongo na huhitaji mvua za wastani. Mimea yake haitumii chakula kingi kutoka ardhini. Iwapo ardhi haina rutuba ya kutosha inapendekezwa kuweka mbolea ya takataka au samadi.

Kupanda: mbegu za bamia hupandwa  katika bustani, lakini pia kwanza zinaweza kupandwa kwenye kitalu na kuhamishwa baadaye. Mbegu zimiminwe kidogo kidogo na miche ifikiapo urefu wa sentimeta 10 hadi 15, idadi yake ipunguzwe. Umbali wa unaopendekezwa ni sentimeta 40-50 kati ya mimea na sentimeta 70-80 kati ya mistari. Kilo moja hadi moja na nusu ya mbegu hutosha robo hekta ya bustani (zaidi ya nusu eka hivi).

Mbegu za bamia huota kwa shida, mara nyingi huchukua siku nane hadi 12 kutokeza. Ili kurahisisha uotaji, inapendekezwa kwanza kuweka mbegu katika chombo chenye maji ya vuguvugu kwa muda wa saa 24.

Iwapo unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji bustanini. Mimea ifikiapo urefu wa nusu meta hivi wakulima wengine huondo ncha zake kwa kuamini kwamba wingi na ubora wa matunda huongezeka. Bamia huwa tayari kuchumwa baada ya miezi 2 tangu kupandwa na huendelea kwa muda mrefu.

Magonjwa: Mosaic Virus- Huu ni ugonjwa mbaya sana, majani huwa na madoamadoa na huumbuka. Haki hii hupunguza mazao. Nyunyizia dawa za sumu kuua wadudu.

kimetolewa na Ombeni haule 
elimu na ushauri wasiliana nasi kwanamba 
0659144660/0758069046
kitabu cha kilimo cha mboga na bustani kinapatikana

No comments:

Post a Comment