MIRADI YA UZALISHAJI MALI
1) Maana ya
mradi
Mradi ni shughuli yeyote maalumu iliyohalali ,
inayotumia raslimali kwa lengo la kutatua tatizo katika muda maalumu.
Tatizo ni hali isiyoridhisha [mapungufu]. Ukianzisha
mradi usiotatua tatizo huo siyo mradi.
2) Sifa za mradi.
Mradi mzuri wa kuongeza kipato unasifa zifuatazo ;
(i)
Unachangia
kuboresha maisha ya mlengwa.
(ii)
Uwe wa kuingiza
faida, hivyo kufanya kuwa endelevu.
(iii)
Mlengwa awe na
uwezo wa kuuendesha na kuusimamia mwenyewe.
(iv)
Una mtaji.
(v)
Unakuwa na
kupanuka.
(vi)
Una wateja [soko]
(vii)
Unatunza
kumbukumbu zote za muhimu vizuri.
3) Wazo la
mradi. [Wazo ghafi]
Mawazo ghafi ni hatua ya mwanzo katika kuanzisha mradi
na wazo ghafi ni wazo lililo kwenye fikra na halijafanyiwa tathimini. Mtu
anakuwa na msukumo wa kuanzisha mradi wa kuongeza kipato baada ya kusongwa na
kero kubwa kama vile kushindwa kumudu gharama za maisha, gharama za kusomesha
watoto, mavazi duni wakati wa sikukuu, majirani kumtambia. Hivyo mradi wa
kuongeza kipato ni njia pekee ya kumkomboa na kero hizo. Sijui niuze mkaa?.
1)
Sijui niuze
mbao?.
2)
Sijui
nilime pamba?.
3)
Sijui
nilime bustani?.
4)
Sijui
nianzishe duka?.
5)
Sijui
nianzishe saloon?.
6)
Sijui
nifuge kuku?.
7)
Sijui
nifuge nyuki?.
8)
Sijui
nifuge samaki?.
9)
Uanzishaji wa
mradi katika hatua hii mara nyingi sana hufa.
Kutathimini
wazo la mradi
Mradi kabla ya kuanzishwa sharti utathiminiwe kwa kuzingatia
vipengele vifuatavyo ;
Mauzo - Gharama = 0
(Hakuna faida wala hasara Mauzo - Gharama = Faida
(Iwapo mauzo ni makubwa)
Mauzo
- Gharama = Hasara.(Iwapo gharama ni kubwa)
II . Kukua kwa biashara: Biashara
inaweza kufikia ukomo sehemu moja na kulazimika kufungua biashara. Hiyo hiyo
sehemu nyingine ikaendelea kukuza mtaji wako.
III.
Kupanuka kwa biashara: Kuanzisha biashara nyingine tofauti hapo hapo
au mahali pengine.
IV.
Kumunufaisha mjasiriamali: Je
mradi huu utatatua sasa kero za mjasiriamali katika muda mfupi ?. au muda
Mrefu?
·
Eleza
manufaa ya mradi kama vile kuwezesha
kiuchumi, kuongeza ajira, kuongeza lishe.
·
Eleza
manufaa ya mradi kwa kuzingatia faida za kiuchumi na kijamii, manufaa ya moja
kwa moja na yasiyo ya moja kwa moja.
V.
Uwezo wa mjasiriamali mwenyewe
Mjasiriamali
ana uwezo wa kuendesha huo mradi ?. Ana stadi katika mradi anaokusudia Mtaji
binafsi alionao wa kuanzisha mradi.
VI.
Udhaifu wa mjasiriamali
Mapungufu
katika ufahamu, stadi na mtaji.
VII.
Fursa zilizopo zinazoweza kumfanya mjasiriamali akabiliane na udhaifu na
Vikwazo.
VIII. V
ikwazo vilivyopo vinavyoweza kukwamisha mradi wa mjasiriamali – sera za nchi, kupanda na kushuka kwa mali ghafi, majanga
n.k.
H adi hapo
mjasiriamali atakuwa amepata jibu kuhusu mradi anaokusudia, Aanzishe Mradi au
la?
Aina ya miradi.
1)
Miradi ya utoaji huduma: Hii ni miradi
inayoanzishwa ambayo haina lengo la kuleta kipato kama vile ujenzi wa kisima
cha maji au barabara.
2)
Miradi ya Uzalishaji Mali. Hii ni miradi inayoanzishwa kwa lengo la kupata
kipato kama vile:
·
Kilimo
Biashara
·
Ufugaji wa
kibiashara.
·
Uvuvi
·
Mradi wa
biashara.n.k
1.2.1.Mradi wa biashara
1.2.3. Maana ya biashara
Biashara
ni mradi wa uzalishaji mali unaofanywa na mtu, kikundi, shirika au kampuni kwa
lengo la kupata faida.
1.2.4. Namna ya kuanzisha mradi wa
biashara
(i)
Kunakili biashara zilizopo (copy and paste). Biashara nyingi
zinaanzishwa kwa kunakili biashara zilizopo, mtu anangalia biashara
wanayoifanya wengine na kujaribu kufanya hivyo hivyo.
Dhana ya kuwa wengine wanatengeneza faida,
kupata faida kutokana na biashara hii “kwa nini na mimi nisifanye hivyo”
(utaratibu huu ni hatari hasa biashara ukiiweka palepale na ukinakili vibaya)
(ii)
Kujazilizia biashara zilizopo. Biashara zingine zinaanzishwa kwa
kuainisha mahitaji yasiyojitosheleza na kuzijazilia.
(iii)
Kubuni bidhaa mpya na huduma mpya.
·
Biashara
zingine zinaanzishwa kwa kubuni bidhaa mpya na huduma mpya.
·
Angalia
uwezekano wa kuibua biashara mpya kwa kutafuta matatizo ya kiuchumi na kijamii.
·
Angalia
nini mahitaji ya lazima.
1.2.5.Mambo muhimu katika biashara.
(a)
Mtaji: Mtaji ni jumla ya
rasiliamali zinazohitajika katika uzalishaji wa mali kama vile fedha
taslimu,nyumba, gari, zana mbalimbali, mali ghafi, shamba n.k.
·
Ni muhimu
kujua aina ya mtaji ulionao kama unatosheleza mahitaji ya biashara unayotarajia kuanzisha.
·
Iwapo
mahitaji hayatoshelezi ni muhimu kujua njia nyingine za kuongeza mtaji kama
vile mkopo, msaada, uchangishaji, ruzuku, ubia na mwekezaji n.k.
·
Aina mbili
za mtaji ni Mtaji Anzia na Mtaji Endeshea.
(b) Mahali pa biashara:
Mfanyabiashara yeyote sharti awe mahali sahihi pa kufanyia biashara
(biashara sharti iwekwe mahali inapo uzika)
Mahali pa biashara panaweza kuathiri biashara kwa upande wa gharama za
uendeshaji, upatikanaji wa wateja na mapato kwa ujumla.
(c)
leseni ya biashara: Ni muhimu
mjasiriamali kuwa na leseni ya biashara ili kumwezesha kupata ruhusa ya
kuendesha biashara kisheria.
(d) Soko: Soko kwa lugha nyepesi ni wateja.
·
Mjasiriamali
mzuri siku zote anajua watu wananunua
nini hasa kwake, na yeye anauza nini hasa kwao ili aweze namna ya kuboresha
mauzo na kuongeza wateja.Katika biashara kitu unachokiuza ndicho unachotakiwa
kukiboresha na kukidumisha.
·
Mjasirimali
mzuri sharti aelewe sifa za wateja wake-
kipato chao,umri wao, jinsi yao, Elimu yao, utamaduni wao.Sifa hizi
zitamwezesha mjasiriamali kujipanga vizuri ili kuwahudumia wateja wake.
·
Kutangaza
biashara, matangazo huarifu wateja kuwa bidhaa ipo ili wajue, waamue kuipenda
na kununua.Katika biashara, matangazo ni
muhimu kila mara, watu wakisahau au kuanza kubadili mwelekeo, basi matangazo
husaidia.
Matangazo huwafanya wateja WAJUE WAPENDE
WANUNUE
(e) Masoko
·
Masoko kwa
lugha nyepesi ni shughuli zote zile zinazofanyika tokea wakati wa shughuli za uzalishaji hadi kufika kwa wateja.
·
Mjasiriamali
akizifahamu shughuli za masoko anao uwezekano mkubwa sana wa kufanya vizuri
katika biashara yake kwa ubora na ufanisi na kuongeza tija.
·
Kila
mjasiriamali anahitaji kuzifahamu vyema shughuli za masoko katika biashara yake, vinginevyo maisha ya
biashara yanakuwa mafupi sana.
·
Shughuli za
masoko ni pamoja na:
(i)
U tafiti:
Utafiti wa mahitaji na matakwa ya wateja. Ni muhimu kuelewa mteja wako ni nani,
yuko wapi na anahitaji nini, lini anahitaji, kwa nini anahitaji na namna gani.
(ii)
Kununua:
Ni muhimu ununuzi ufanyike kwa makini.
(iii)
K
uzalisha: Ni lazima kuweka mfumo mzuri wa uzalishaji ili kuepuka upotevu na
uharibifu.
(iv)
K
usafirisha: Njia ya usafirishaji ni lazima ipunguze uharibifu wa bidhaa
wakati wa kusafirisha, iwe njia nyepesi na rahisi ili bidhaa na huduma ziweze
kumfikia mteja kwa wakati sahihi.
(v)
Kudhibiti
bidhaa: Kudhibiti bidhaa ni pamoja na:
·
Kuagiza
bidhaa kwa wakati unaofaa.
·
Kuzitunza
vizuri zisiharibike au kuibiwa kirahisi.
·
Kuzipanga
vizuri ili zisiharibike kwa wateja kirahisi.
·
Kuzipanga
vizuri ili zionekane kwa wateja.
·
Kuzihesabu
kila mara.
·
Kudhibiti
bidhaa ni pamoja na kutunza kumbukumbu kwani msemo S“mali bila daftari hupotea bila habari”
(vi)
K upanga bei:
Kupanga bei ni utaratibu wa kupanga mapato yatakavyokuwa ili kufidia gharama
zako zote na kupata faida unayotaka kutokana na kuuza bidhaa au huduma yako.
·
Unaweza
ukapanga bei sawa na wengine.
·
Unaweza ukapunguza bei ya soko ili mzunguko wa mauzo uwe
haraka mfano photocopy 1 shs 50 badala ya shs 100.
·
Unaweza
ukapanga bei ya juu ya soko bali ukaboresha maeneo mengine (Eleza nini
unaboresha)
(vii)
K ufunga bidhaa: Ni lazima kufunga bidhaa ili kuepuka uharibifu, kurahisisha ubebaji, uuzaji na kutangaza
bidhaa.
(viii) Kutangaza: Ili kuuza unalazimika kutangaza.
·
Kutangaza
ni kuwafahamisha wateja juu ya bidhaa au huduma utowayo, uko wapi na wanaweza
kukufikiaje.
·
Kutangaza
ni kuwavutia wateja waje kwako badala ya
kwenda kwa washindani wako kwa kuwaeleza “ kitu cha ziada ulichonacho”
·
Kutangaza
ni kuwapatia wateja ujumbe muhimu ili wanunue kwako mfano kuwapa punguzo la
bei, nyongeza na zawadi wanaponunua kwako.
·
Tangaza
ubora wa bidhaa ,matumizi yake na
faida zake kupitia
magazeti,redio,TV, ubao wa matengenezo , mtandao, vipeperushi, ufadhili na
michango n.k
(ix)
Kuwahudumia wateja:
·
Huduma kwa
wateja ni vitendo vyote vizuri unavyoweza kumfanyanyia mteja ajisikie kuwa ni
wa maana.
·
Huduma kwa
wateja katika dunia hii ya utandawazi , ndivyo imebaki silaha pekee ya
kutofautisha wewe na washindani wako.
·
Mjasiliamali
sharti awatosheleze wateja wake, na iwapo mteja utamtosheleza atanunua tena na
tena bidhaa zako na mteja huyo ataziba
masikio kwa bidhaa za watu wengine.
kimeandikwa na ombeni haule
elimu na ushauri wasiliana nasi kwa namba
0659144660/0758069046/ombenihaule@gmail.com
kitabu cha fursa za biashara kinapatikana
No comments:
Post a Comment