April 09, 2017

AINA ZA FURSA ZINAZOFANYWA AFRICA MASHARIKI NA KATI




1    1.Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha.
2. Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha.
3. Kutengeneza na kuuza tofali
4. Ufundi, Website updating/Database: Katika Halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya na Makampuni mbalimbali.
5.Kuanzisha kituo cha redio na televisheni
6. Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya
electroniki na mawasiliano mfano; compyuta na
vifaa vya compyuta na mawasiliano.
7.Kuuza software; mfano Antivirus, Operating
Systems, Pastel, Tally, Myob, n.k
8. Kushona na kuuza nguo.
9. Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit, socks,
batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali,
10. Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo,
Mbuzi, Ngombe, Kuku, Bata, na wengine.
11. Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na
vifaa mbalimbali ktk mashule na vyuo.
12.Kutoa ushauri mbalimbali wa Kitaalamu.
13. Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza
popcorn na kuziuza.
14. Kusajili namba za simu na kuuza vocha
15. Kuwa na mradi wa Pikipiki zisizotumia mafuta
na zinazotumia mafuta
16. Kilimo cha mazao mbalimbali kulingana na
hali ya hewa ya sehemu husika.
17. Kuuza Mitumba
18. Kusimamia miradi mbalimbali
19. Kufungua duka la kuuza mitambo mbalimbali
20. Kufungua banda la chakula na chips
21. Kukodisha turubai viti na meza
22. Kufungua Supermarket
23. Kufungua Saluni
24. Kufungua Bucha
25. Video Shooting & Editing.
26. Kufungua Internet cafe
27. Duka la kuuza matunda
28. Kufungua duka la kuuza vifaa vya simu za
mkononi na landline.
29. Kufungua duka la vifaa vya ujenzi; cement, vifaa
vya umeme, duka la mabati
30. Kutengeneza michoro mbalimbali ya majumba na
miradi ya ICT
31. Kuchapa vitabu, bronchures, n.k
32. Kuanzisha kampuni ya ujenzi (Building
contractor)
33. Kuuza Vifaa vya umeme wa nishati ya jua
(solar) ,battery, inverter na vifaa vingine vya
solar n.k
34. ** Kuuza maji kwa jumla na rejaleja.
35. Kutengeneza na kuuza Unga wa lishe bora.
36. Kukodisha Music
37. Kuanzisha Mradi wa Taxi
38. Kuanzisha mradi wa Daladala
39. Kuuza vifaa vya Kompyuta, laptops, converters,
HDDs, Monitors, Softwares, CD Copiers na vifaa
vingine.
40. Kununua magenerator na kukodisha
41. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za simu
42.Kufungua kampuni ya kutoa huduma za internet (ISP)
43. Kuuza mabati na vigae
44. Kujenga apartments
45.Kufungua Kisima cha mafuta ya taa au
mafuta ya aina zote
46. Kufungua Duka la samaki
47. Kufungua Duka la nafaka
48.Kufungua Shule za Awali, Shule za Msingi,
Sekondari na Vyuo.
49. Kujenga hostel
50. Kuuza vocha na ving’amuzi vya DStv, Zuku,
Startimes, Easy TV, TNG, Digitech, Continental.
51.Kujenga mtambo wa kuzalisha umeme na
kuuza katika viwanda na wananchi.
52. Ufundi simu
53. Kufungua Hospitali, Zahanati.
54. Maabara ya Macho, Meno
55.Kuchimba/Kuuza Madini
56. Kufungua ofisi ya kutoa huduma ya simu na fax
57. Kuuza miti na mbao
58. Kufungua Grocery, bar
59. Kufungua studio ya kupiga na kusafisha picha
60. Kucharge simu/battery
61. Duka la TV na vifaa vingine
62. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika
sherehe na tamasha mbalimbali (catering).
63. Banda la kupigisha simu
64. Kuuza na kushona Uniform za shule
65. Kuanzisha duka la kuuza vitu kwa jumla.
66. Kufungua gereji za kutengeneza bajaji, pikipiki na
magari
67. Kuuza vyuma, pembejeo, rake, jembe
68. Kuuza fanicha
69. Kufungua sehemu ya kuziba pancha za matairi
ya magari na mitambo.
70. Kujenga nyumba za kulala wageni (hotel)
71. Kuagiza na kuuza vifaa vya aluminium.
72. Kuuza vioo
73. Kushona na kukodisha nguo za harusi
74. Kufungua yard kwa ajili ya kuosha magari
75. Kuuza mashine za kuchomelea (welding
machine).
76. Kuuza vifaa vya kuvaa Site (boots, helmets etc)
77. Kununua mabasi kwa ajili ya kusafirisha
wanafunzi
78. Kufungua studio ya kutengeneza vipindi vya
redio na televisheni
79.Kuanzisha ofisi ya michezo ya televisheni (TV
Games)
80.Kufungua benki
81. Kuwa na malori ya kubeba kokoto na mchanga
82. Kuuza vifaa mfano TV, CCTV Camera, n.k
83. Kuwa dalali wa vitu mbalimbali
84. Kuanzisha mradi wa kukodisha fork lift na
winchi (crane)
85. Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza viatu.
86. Kuanzisha viwanda mbalimbali
87. Duka la vifaa vya simu na gadgets mbalimbali
zinazoendana na mawasiliano ya Vodacom,
TTCL, AIRTEL, TIGO, ZANTEL, n.k.
88.Kujenga Ukumbi wa kukodisha kwa sherehe,
mikutano mbalimbali
89. Kununua matrekta, mitambo ya ujenzi wa
barabara na kukodisha
90. Kutengeneza antenna na kuuza
91. Kufungua mradi wa Machine za kusafisha,
kutoboa na kuchana mbao
92. Kufungua mradi wa kuuza vifaa vya Umeme
wa kutumia upepo
93. Biashara ya kuagiza magari
94. Kufanya biashara za Jukebox
95. Kukodisha matenki ya maji**
96. Kufungua duka la kuuza Asali
97. Kutengeneza Mikokoteni/ matoroli na kuikodisha
98. Kufungua Duka la vinyago, batiki
99. Kuanzisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA,
TIGOPESA, EZY PESA
100.Kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi
(Gym).
101. Kununua na kuuza vifaa vya kupima ardhi.
102. Kufungua duka la kuuza dawa (pharmacy).
103. Kufungua Kampuni ya Ulinzi
104. Kufungua kampuni ya "Clearing and fowarding"
105. Kuchezesha vikaragosi
106. Kuuza spea za bajaji, magari na pikipiki
107. Kuuza baiskeli
108. Kuuza magodoro
109. Kuuza vyombo mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya nyumbani mfano bakuli, sahani, vikombe, vijiko,
110. Kuuza marumaru (limestones)
111. Kuuza kokoto
112. Kuuza mchanga
113. Kufundisha Tuisheni
114. Biashara za bima
115. Kampuni ya kusafirisha abiria kwa njia ya anga (ndege)
116. Biashara za kitalii
117. Biashara za meli na maboti.
118. Kampuni ya kuchimba visima
119. Kufungua ofisi ya wakili/mawakili wa kujitegemea
120. Kuuza mkaa
121. Kutengeneza mashine za kutengeneza tofali
122. Kampuni ya kupima ardhi
123. Kampuni ya magazeti
124. Kuchapa (printing) magazeti
125. Kuuza magazeti
126. Kuchimba mafuta
127. Kiwanda cha kutengeneza mabati
128. Kiwanda cha kutengeneza fanicha
129. Kiwanda cha kutengeneza matairi
130. Kutengeneza vitanda vya chuma
131. Kununua nyumba katika Maghorofa
(Apartments) na kuzikodisha.
132. Kukodisha makapeti
133. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe.
134. Mashine ya kusaga na kukoboa nafaka.
135. Kazi ya ususi na kusafisha kucha.
136. Kuuza Gypsum
137. Malori ya kubeba mafuta na Mizigo
138. Duka la kuuza mboga za majani
139. Duka la kuuza maua.
140. Kampuni ya kuzoa takataka
141. Kampuni ya kuuza magari
142. Kuuza viwanja
143. Uvuvi
144. Kutengeneza na kuuza nguzo za kujengea fensi
145. Uchoraji wa mabango.
146. Duka la kuuza silaha
147. Ukumbi wa kuonesha mpira
148. Biashara ya mlm (network marketing)
149. Yadi kwa ajili ya kupaki magari
150. Mradi wa trekta za kukodisha kwa ajili ya kilimo

UMASKINI NA UTAJIRI NIMAAMUZI YA MTU  MWENYEWE LAKINI NJIA YA MAFANIKIO NI NYEUPE  FURSA ZINAWATIZAMA WATU ILA WATU WANAZIPUUZIA ,,UKISHINDWA KUFANYA BIASHARA IZO HUWEZI KUFANYA BIASHARA NYINGINE UTABAKI KUILAMU KASI YA MHESHIMIWA WATANO (5)


IMETOLEW NA OMBENI HAULE
ELIMU NA USHAURI WASILIANA KWA NAMBA 0659144660/ 0758069046/ ombenihaule@gmail.com
Kitabu cha fursa za biashara kinapatikana

April 07, 2017

WAJASIRIAMALI WAPO KATIKA MAKUNDI MATATU (3),,JE WEWE UPO KATIKA KUNDI GANI,,?


ELIMU YA UJASIRIAMALI BIASHARA
.Ujasiriamali katika sekta ya biashara (Entrepreneurship)
       a)      Ujasiriamali ni uwezo wa kubuni biashara kuifanya na kupata faida nakuifanya  biashara kuwa endelevu.
       b)      Ujasiriamali ni kuanza na kuendesha na kumiliki biashara inayojitegemea
.Mjasiriamali ni nani?
       c)      Mtu yoyote mwenyeuwezo wakubuni biashara akaifanya na kupata  faida na biashara yake ikawa endelevu.
       d)      Mtu yeyote anayeamua kuchukua uamuzi hatarishi kwa kuwekeza mtaji katika kuanzisha mradi ili kuingiza kipato na kupata faida.



             . Wajasiriamalli wapo wa aina tatu (3)
1.                                  1.  Wajasiriamali wakubwa
2.                                  2.Wajasiriamali wakati
3.                                  3.Wajasiriamali wadogo

  Wajasiriamali wakubwa-hufanya biashara zao kwakutumia mtaji mkubwa na biashara zao hufanyika na kufahamika kitaifa na kimataifa,,, mfano .Mohamed MO ,Bakhresa nk.
·         
 Wajasiriamali wakati-hawa ni aina ya wajasiriamali ambao biashara zao hutumia mtaji wakati na biashara zao hufanyika na hufahamika katika ngazi ya kanda na mikoa,,,Nganga,super feo.. nk.
· 
 Wajasiriamali wadogo-Hawa pia ni wajasiriamali ambao biashara zao hutumia mtaji mdoo na biashara zao hufanyika na kufahamika katika ngazi ya wilaya,,mfano ,,Ottawa wa songea,,mtasi wa mbeya,Nandra wa moshi vijijini,Charles wa kyela nk.

Qn: WEWE UNAJIITA MJASIRIAMALI, JE! WEWE UPO KATIKA KUNDI GANI APO, JADILI

JIFUNZE JIAJIRI UMASKINI HAUKUBALIKI


April 05, 2017

ANZA KUKIFUATILIA KITABU CHETU CHA UTENGENEZAJI WA BIDHAA MBALIMBALI ZA VIWANDANI.. FURSA ya UTENGENEZAJI WA BATIKI TIE NA DIE ,,SOMO LA KWANZA



 BATIKI
Ni aina ya nguo au vazi la asili  linayotengenezwa kwa mikono kwa kuweka picha michoro na urembo mbalimbali.kwaapa tanzania batiki soko lake kubwa na watu wengi wamejikita kufanya ujasiriamali huu unawaingizia kipato kikubwa na kuweza kumudu maisha yakitanzania..





Malighafi zinazotumika kutengeneza batiki:
1.      Caustic soda vijiko vitatu vya chakula
2.      Sodium hydrosuphet vijiko vya chakula
3.      Rangi vijiko viwili vya chakula.
4.      Maji ya moto lita tano koroga kwa dakika mbili.
5.      Weka maji ya baridi lita tano.
6.      Parafin wax kilo moja.
7.      Vibao au sponch za picha mbalimbali.

VIFAA VYA KUTENGENEZEA:
Meza kubwa, sufuria, kitambaa cha mpira au kapeti misumari midogo, vibao au sponchi ya urembo, jiko.

JINSI YA KUTENGENEZA : Hatua ya kwanza.
1.      Chemsha mshumaa
2.      Tandika vitambaa mezani
3.      Chovya kibao chako kwenye mshumaa, gonga kwenye kitambaa.

JINSI KUTENGENEZA: Hatua ya pili
1.      Andaa ndoo au beseni, chemsha
2.      Weka malighafi namba moja hadi tatu, weka maji ya uvuguvugu.
3.      Tumbukiza kitambaa kwa dakika kumi, anika kipoe.
4.      Chemsha maji ya moto na sabuni ya maji
5.      Tumbukiza kitambaa kuondoa mshumaa na geuza ili mshumaa utoke wote
6.      Fua anika piga pasi peleka sokoni.


















TIE AND DYE
Ni aina ya batiki ya kukunja mikunjo kwa kutumia mkono
Malighafi
1.      Coustic soda vijiko vinne vya chakula
2.      Sodium hydrosulphet vijiko vitano vya chakula
3.      Rangi vijiko vine vya chakula.

VITENDEA KAZI:
Meza, kitambaa cha pambe, kalamu, uzi, sindano, mkasi, kamba, sufuria kijiko kikubwa, ndoo au beseni, jiko, vibanio, maskinna gloves.

AINA ZA TIE AND DYE.
1.      Kushona- chora  mchoro wowote  ushone, halafu vuta na uzi kwa nguvu.
2.      Kufanya- loweka kitambaa kisha tandika kwenye mkeka au nailoni, anza kuvuta kwa kufinyanga, kisha mwagia dawa.
3.      Funga uzi na kamba-kunja mkunjo wowote funga na kamba, tumbukiza kwenye dawa.
4.      Kutumia blichi (jiki)- tandika kitambaa kwenye meza halafu mwagia blichi yako uliyoiweka kwenye chupa na kutoboa mfuniko kwa ajili ya kutoa blich yako kama urembo.

JINSI YA KUTENGENEZA.
1.      Chemsha maji ya moto
2.      Pima malighafi ya kwanza hadi ya tatu, weka vyote kwenye beseni.
3.      Weka maji ya moto lita tano, koroga kwa dakika tatu, ongeza maji ya baridi lita tano
4.      Chovya kitambaa kwenye rangi acha kwa dakika kumi hadi kumi na tano
5.      Suuza kwenye maji baridi anika kisha piga pasi, tayari kwa kwenda sokoni

KIMEANDIKWA NA OMBENI HAULE 
ELIMU na USHAURI WASILIANA NASI KWA NAMBA 
0659144660/0758069046/ombenihaule@gmail.com
kitabu cha utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani kinapatikana

(SOMO LA KWANZA 1) ANZA KUKISOMA KITABU CHETU ,,,JIFUNZE NAMNA YA KUANDAA SHAMBA KWAAJILI YA KILIMO CHA MBOGA NA MATUNDA



KILIMO CHA MBOGAMBOGA NA BUSTANI
KUCHAGUA ENEO
1.kuandaa shamba- Katika uchaguzi wa eneo kwa ajili ya bustani zingatia yafuatayo:
  • Mwinuko- Eneo lisiwe kwenye mwinuko mkali kwa sababu sehemu kama hizo zinaweza kusababisha mmomonyoko wa udongo. Endapo sehemu itakuwa ya mwinuko tengeneza matungazi (terrace) ili kuzuia mmomonyoko.
  • Udongo- Udongo unaofaa ni wenye rutuba, mboji nyingi na unaopitisha maji kwa kirahisi. Vilevile usiwe na historia ya magonjwa na wadudu waharibifu.
  • Chanzo cha Maji -Eneo la bustani liwe karibu na maji ya kudumu. Maji yasiwe na chumvi nyingi kwani huathiri ukuaji wa mimea.
  • Kitalu -Kitalu kisiwekwe mahali palipo na kivuli kingi kwa kuwa husababisha mimea kuwa dhaifu.
  • Kuzuia Upepo Mkali-Eneo la bustani lipandwe miti mipakani ili kuzuia upepo mkali. Upepo mkali huharibu mimea kwa kuvunja vunja majani na matawi na husafirisha vimelea vya magonjwa na wadudu. Pia hufanya udongo wa juu kukauka haraka na kuleta mmomonyoko.
KUTAYARISHA MATUTA-Ni muhimu udongo utifuliwe vizuri. Mabonge makubwa yavunjwe vunjwe ili Kurahisisha upitaji wa maji na hewa katika udongo. Matuta huinuliwa kidogo toka usawa wa ardhi ili kuzuia maji yasituame. Matuta haya yasitumike wakati wa kiangazi. Wakati wa kiangazi tengeneza matuta yaliyodidimia kidogo.

KUMWAGILIA MAJI- Hakikisha udongo una unyevu wa kutosha kwa kumwagilia siku moja kabla ya kuotesha mbegu. Pia baada ya kupanda mwagilia kitalu au shamba maji ya kutosha. Maji mengi husababisha mbegu au miche kuoza.

KUPANDA-Kina cha kupanda kitategemea ukubwa wa mbegu. Mbegu ndogo hupandwa katika kina kifupi zaidi kuliko mbegu kubwa. Upandaji wa baadhi ya mbegu unaweza kufanyika kila wiki ili kuweza kupata mboga mfululizo.

KUOTESHA MBEGU KWENYE KITALU-Baadhi ya mbegu za mboga huoteshwa kwanza kwenye kitalu na baadaye miche huhamishiwa shambani. Mbegu hizini kama vile za bilinganya, kabichi, nyanya, pilipili hoho na vitunguu. Kitalu kwa ajili ya kuotesha mbegu hakina budi kitayarishwe wiki moj a kabla ya kusia mbegu. Wakati wa kutayarisha kitalu, ardhi ikatuliwe katika kina cha kutosha sentimita 30 kwenda chini. Ili kuongeza mtuba ya udongo mbolea za asili kama vile samadi, takataka na mbolea vunde zilizooza vizuri ziwekwe kabla ya kusia mbegu.

KUTUMIA MBEGU BORA-Tumia mbegu bora zilizohifadhiwa kwenye dawa. Mbegu bora ni zile ambazo zimekomaa na kukauka vizuri, hazikushambuliwa na wadudu wala magonjwa na ambazo zina uwezo wa kuota vizuri. Inashauriwa kutumia mbegu zilizothibitishwa kitaalamu.

KUWEKA KIVULI NA MATANDAZO-Utandazaji wa majani makavu na uwekaj i wa kivuli ni muhimu ili kuzuia jua linaloweza kunyausha miche. Matandazo pia husaidia kuhifadhi unyevu, joto la udongo na hupunguza palizi ya mara kwa mara. Kivuli kiruhusu mwanga wa kutosha na kiondolewe kidogo kidogo kadiri mimea inavyokua.
Uwekaji wa kivuli ni muhimu ili kuzuia jua kali

KUITAYARISHA MICHE KABLA YA KUPANDIKIZA:-Wiki mbili kabla ya kuihamisha miche toka kitaluni, unashauriwa kupunguza kumwagilia ili kuizoesha iweze kustahimili hali ya sehemu inapohamishiwa. Mwagilia kitalu siku moja kabla ya kung'oa miche ili kurahisisha ung'oaji na kuepuka kuikata mizizi. Pia shamba kwa ajili ya kuhamishia miche limwagiliwe siku moja kabla ya kupandikiza ili kuloanisha udongo.
 
 MATUMIZI YA MBOLEA
  1. Mboji, Samadi na Mbolea Vunde
    Mboga hustawi, vizuri sana katika udongo wenye mbolea hizo. Hivyo ni vema mbolea hizo ziwekwe shambani kabla ya kupanda au kupandikiza. Kiasi kinachotakiwa ni ndoo moja kwa tuta lenye upana na urefu wa mita moja.
  2. Mbolea za Viwandani
    Mbolea za viwandani zimegawanyika katika makundi makuu matatu, nayo ni mbolea za chumvichumvi, chokaa na kijivu,
Mbolea za Chumvichumvi
Mbolea hizi hujulikana kama mbolea za kukuzia na huwekwa shambani baada ya mimea kuota. Zina virutubisho vingi vya Naitrojeni ambavyo huifanya mimea kukua haraka.Pia zinahusika na utengenezaji wa kijani kibichi kwenye mmea.

Nchini Tanzania mbolea za chumvichumvi zinazotumika zaidi ni:-

- Sulphate ofAmmonia (S/A) 21% N
- Calcium Ammonium Nitrate (CAN) 26 % N
- Urea 46% N.
- Mbolea ya mchanganyiko N.P.K. 25.5.5 na 20.10.10

Mbolea za Chokaa-Hizi ni mbolea zinazotumika kupandia mbegu au miche. Husaidia uotaji mzuri wa mimea, huimarisha mizizi, na hutumika katika utengenezaji wa chakula na mbegu kwenye tunda. Vilevile huhusika na usafirishaji wa nguvu kwenye mmea na hufanya mazao kukomaa haraka. Mbolea hizi huwekwa shambani wakati wa kupanda.

Aina ya mbolea za chokaa zinazotumika hapa nchini ni Triple Super Phosphate (TSP) 46% P2O5. Vilevile unaweza kutumia N.P.K 6.20.18 kwa kupandia.

Mboleaza Kijivu (Potashi)-Potashi ni kirutubisho kinachosaidia mimea katika utengenezaji wa protini na wanga. Kadhalika huhusika na utumiaji wa madini muhimu kwa maisha ya mimea. Mbolea hii pia huwezesha matunda kukomaaa, kuiva haraka, na kutengeneza mbegu bora. Vilevile husaidia ongezeko la maji kwenye mmea na kuufanya ustahimili magonjwa, ukame, baridi na hali ya udongo wenye alkalini nyingi.

Mbolea za Potashi zinazotumika ni:-
- Muriate of Potash 48 - 60% K2O
- Sulphate of Potash 48 - 50% K2O

KUBADILISHA MAZAO SHAMBANI-Kubadilisha mazao shambani ni utaratibu wa kuachs kupanda mfululizo aina ileile ya zao katika eneo hilo hilo. Iwapo eneo ni kubwa, bustani igawanywe katika sehemn tatu au nne ili kuepuka kupanda mfolulizo aina ileile ya zao. Katika kila sehemu panda aina nyingine ya mazao na ya familia tofauti kila baada ya kuvuna.

Baada ya kuvuna; mazao ya sehemu ya kwanza yapandwe katika sehemu ya pili, ya pili katika sehemu ya tatu na ya tatu yapandwe katika sehemu ya nne na yale ya nne yapandwe katika sehemu ya kwanza.
Kubadilisha mazao shambani huzuia ongezeko la wadudu na magonjwa yanayoshambulia jamii moja ya zao. Vilevile huhifadhi rutuba ya udongo na huzuia uotaji wa magugu. Utaratibu huu pia humwezesha mkulima kuweka kiasi cha mbolea kinachotakiwa shambani. Ufuatao ni mfano wa kubadilisha mazao.

MFANO WA KUBADILISKA MAZAO
Jamii ya Nyanya
  • Bilinganya
  • Nyanya
  • Pilipili
  • Viazi Mviringo
Jamii ya Matango
  • Matango
  • Maboga
  • Matikiti Maji
Mimea ya Mizizi
  • Karoti
  • Vitunguu
MATUMIZI YA MADAWA-Ni muhimu kutumia madawa ili kukinga mimea kutokana na athari za wadudu na magonjwa. Hata hivyo madawa yatumike pale inapobidi kwani ni ghali na yana madhara kwa mazingira na watu.
Mambo yafuatayo yanatakiwa kuzingatiwa wakati wa kutumia madawa. Hakikisha unatumia dawa inayoshauriwa na wataalamu.
  1. Soma kwa uangalifu maelezo yanayoambatana na dawa toka kwa watengenezaji, kabla ya kutumia na yasikiukwe. Hii itakusaidia kujua vifaa, kiasi na jinsi ya kutumia. Madawa ni hatari kwa binadamu na wanyama kama yatatumika isivyopasa.
  2. Wakati wa kuchanganya na kunyunyizia dawa, vaa nguonavifaavyakinga. Vifaa hivi ni kofia, glovus, viatu (gumboots), kitambaa cha kufunika mdomo na pua, miwani na ovaroli.
  3. Tumia maji safi kuchanganya dawa.
  4. Epuka kuvuta hewa yenye dawa. Wakati wa kunyunyizia dawa usielekee upepo unakotoka bali elekea upepo unakoenda.
  5. Usile wala kuvuta wakati wa kuchanganya au kunyunyizia dawa.
  6. Baada ya kunyunyizia dawa osha mwili kwa sabuni na maji mengi na safi.
  7. Maji yanayotumika kusafishia bomba yasimwagwe katika maji yaliyotuama au yanayotembea kwani yanaweza kuleta madhara sehemu nyingine. Maji yamwagwe kwenye shimo na kufukiwa.
  8. Nguo na vifaa vingine vilivyotumika zifuliwe mara moja kwa sabuni na maji safi.
  9. Osha vizuri mikono kwa sabuni kabla ya kula, kunywa chochote au kuvuta sigara.
  10. Makopo au chupa zilizokuwa na dawa zisitumike bali ziharibiwe na kufukiwa.
  11. Hifadhi madawa mahali salama na pasipofikiwa na watoto kwa urahisi. Dawa ziachwe katika makasha., chupa au makopo yake zilimokuwemo. Hata siku moja madawa ya mimea yasitumike kwa kutibu binadamu.
  12. Endapo kutakuwepo na matatizo yeyote katika matumizi muone Mtaalamu kwa ushauri.
  13. Iwapo sehemu ya kutolea dawa itaziba, tumia nyasi au kijiti kuzibua. Kamwe usizibue kwa mdomo.
UTUMIAJI WA MBOGA BAADA YA KUNYUNYIZIA DAWA-Mboga zisitumike mara baada ya kunyunyizia dawa. Kila dawa ina siku zake za salama, lakini kwa madawa yaliyo mengi ni siku 14 toka kunyunyizia. Hivyo ni muhimu kusoma maelezo yanayoambatana na dawa. Ikiwa mboga zitatumika kabla ya muda huo huleta madhara kwa mlaji kama vile magonjwa ya kansa. Vilevile mbegu zilizowekwa dawa zisitumike kwa kula.
 
MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU-Ni muhimu kukinga mimea dhidi ya wadudu na magonjwa ili kupata mazao mengi na bora. Zifuatazo ni njia mbalimbali zinazoweza kutumika katika kuzuia magonjwa na wadudu waharibifu.
 
UTHIBITI SANGO
Njia hii hutumia mbinu zifuatazo
  • Kupanda mbegu bora;
  • Usafi wa bustani ambao ni pamoja na kuchoma takataka na kuondoa magugu yanayoweza kutunza wadudu na magonjwa.
  • Kuchanganya mazao
  • Kutumia samadi na mboji
  • Kupanda kwa nafasi
  • Kutumia aina ya mbegu zinazovumilia au kustahimili mashambulizi ya magonjwa na wadudu
L.UDHIBITI WA KITEKNOLOJIA
Kutumia aina mbalimbali za madawa
  • Kutumia mimea inayoua wadudu, kama vile muarobaini, pilipili kali, aina fulani ya maua, marejea, tumbaku, wadudu kama vile walawangi, manyigu na mbawakau.

2.VIFAA VYA BUSTANI
Ili kuboresha kilimo cha mboga ni muhimu kuwa na

1.       jembe,

2.       kamba,

3.       reki,

4.       uma wa bustani

5.       ndoo ya kumwagilia maji,

6.       bomba la kunyunyizia dawa,

7.       toroli, panga,

8.       kwanja, sepetu,

9.       beleshi karai

10.    gan buti nk

KIMEANDIKWA NA OMBENI HAULE 
ELIMU NA USHAURI WASILIANA NASI KWA NAMBA 
0659144660/0758069046/ombenihaule@gmail.com
KITABU CHA KILIMO CHA MBOGA NA MATUNDA KINAPATIKANA