MAHITAJI
1- Vikombe 2 kunde
2- Kitunguu 1 kikubwa
3- Pilipili kichaa 2 (nyekundu na kijani ukipenda)
4- Vijiko 3 vya chakula maji ya limao (ukipenda)
5- Kijiko 1 cha chai baking powder
6- Vijiko 1½ vya chai tangawizi
7- ¼ kikombe majani ya giligilani
8- Chumvi kwa kuonja
9- Mafuta ya kukaangia
*MAELEKEZO*
1- Osha na kuloweka kunde kwenye maji ya moto siyo chini ya masaa 8, au usiku mzima
2- Katakata kitunguu, pilipili, majani ya giligilani; twanga tangawizi. Weka pembeni
3- Chuja kunde maji
4- Weka kunde, maji ya limao na pilipili kwenye mashine ya kusagia chakula au blender ila isilainike sana.
5- Unaweza pia kutumia mashine ya mkono ukipenda au kutwanga kwenye kinu. (hakikisha mashine yako ina nguvu ya kutosha kusaga kunde)
6- Ikilainika, ongeza kitunguu na majani ya giligilani kwenye mchanganyiko, saga kwa sekunde kama 20.
7- Hakikisha vitunguu na majani ya giligilani hayasagiki kabisa.
8- Weka mchanganyiko kwenye bakuli kubwa.
9- Ongeza chumvi na bakingo powder, changanya vizuri
10- Chemsha mafuta kwenye kikaango katika moto wa wastani.
11- Yakichemka, tumia vijiko 2 au mikono kutengeneza umbo kama la yai au umbo la bagia
12- Weka kwenye mafuta. Kaanga mpaka ziwe na rangi ya kahawia
13- Toa bhajiya zilizoiva kwenye mafuta.
14- Hamishia kwenye sahani/bakuli iliyowekewa tissues, au tumia chujio la bati ili mafuta yachuje
15- Pakua za moto na inapendeza kula na chachandu ya machicha ya nazi na mtindi
No comments:
Post a Comment