1- Ili kuongeza matumizi ya mazao hayo na kudumisha ubora wake ni muhimu teknolojia za
kusindika nafaka zitumike. Usindikaji pia huongeza thamani ya zao.
2- Punje za mahindi hutumika kupika makande na husindikwa kupata unga unaotumika katika
matumizi mbalimbali.Vile vile bidhaa nyingine zinazotokana na mahindi ni mafuta na wanga.
KUSINDIKA MAHINDI KUPATA UNGA
- Kuna aina mbili za unga wa mahindi:-
1- Unga wa mahindi yasiyokobolewa *(Dona)*
2- Unga wamahindi yaliyokobolewa *(Sembe)*
KUSINDIKA MAHINDI KUPATA UNGA WA DONA
Vifaa
• Mashine ya kukoboa
• Mashine ya kusaga
• Ungo
• Debe
• Mifuko
• Chekeche ya nafaka
JINSI YA KUSINDIKA
1- Pepeta na pembua mahindi ili kuondoa vumbi na takataka nyingine kwa kutumia chekeche,
ungo au sinia.
2- Osha kwa mahindi yako kwa maji safi na salama
3- Anika kwenye chekeche safi ili yakauke
4- Saga mahindi kupata unga
5- Fungasha kwenye mifuko safi na kavu ya pamba, plastiki/nailoni, makaratasi yasiyopitisha
unyevu kisha hifadhi katika sehemu safi na kavu
6- Kumbuka kuwa Kusaga mahindi bila kukoboa hudumisha virutubishi vilivyomo kwenye mahindi na
kupunguza upotevu wa chakula.
UNGA WA MAHINDI YALIYOKOBOLEWA
JINSI YA KUSINDIKA
1- Pepeta na pembua mahindi ili kuondoa vumbi na takataka nyingine kwa kutumia chekeche,
ungo au sinia
2- Koboa na saga
3- Fungasha kwenye mifuko safi na kavu ya pamba, plastiki/nailoni na ya karatasi isiyopitisha
unyevu.
4- Hifadhi kwenye sehemu safi na kavu
5- Kumbuka Kusaga mahindi yaliyokobolewa hupunguza virutubishi na wingi wa chakula kwa kiasi
cha asilimia *17 hadi 33*
6- Matumizi ya unga wa mahindi
7- Hutumika kutengeneza vyakula mbalimbali kama vile ugali, uji, togwa na vyakula vya watoto.
8- Pia huchanganywa na shayiri na kutengeneza vinywaji kama vile bia.
KUSINDIKA MPUNGA
1- Mpunga husindikwa kupata mchele ambao pia husindikwa kupata unga.
2- Kusindika mpunga kupata mchele
Vifaa
• Mashine ya kukoboa
• Madebe
• Ungo
• Chekeche
• Vifungashio
JINSI YA KUSINDIKA
1- Anika mpunga juani kwa muda wa siku moja kisha uache upoe kwa usiku mmoja ndipo ukoboe.
2- Pepeta na pembua kutoa takataka kabla ya kukoboa
3- Koboa kwa kutumia mashine.
KUFUNGASHA
1- Baada ya kupanga madaraja fungasha kwenye mifuko isiyopitisha unyevu na hifadhi katika
sehemu kavu na safi.
MATUMIZI YA MCHELE
1- Mchele hutumika kutengeneza vyakula mbalimbali kama vile wali, uji, biriani, mseto, pilau, bisi,
tambi na vitafunwa. Chenga za mchele hutmika kwa kutengeneza chakula cha mifugo.
KUSINDIKA MCHELE KUPATA UNGA
*Vifaa*
• Mashine ya kusaga
• Vifungashio
*JINSI YA KUTENGENEZA*
1- Saga mchele safi kupata unga
2- Fungasha kwenye mifuko safi na kavu isiyopitisha unyevu
3- Hifadhi katika sehemu safi na kavu.
4- Matumizi ya unga wa mchele
Hutumika kupika ugali, uji na vitafunwa.
*KUSINDIKA MTAMA/ AUWELE*
1- Punje za mtama na uwele hupikwa makande na husagwa kupata unga.
*KUSAGA MTAMA/ UWELE KUPATA UNGA*
*Vifaa*
• Mashine ya kusaga
• Ungo
• Chekeche ya nafaka
• Kichanja
• Turubai
• Vifungashio safi
*JINSI YA KUSAGA*
1- Pepeta na kupembua mtama/ uwele ili kuondoa mavumbi na takataka nyingine.
2- Tumia chekeche au ungo kupepeta na kupambeua
3- Osha kwa maji safi kisha anika juani kwenye kichanja au turubai
4- Saga kupata unga wa mtama/uwele
5- Fungasha kwenye mifuko ya nailoni/ plastiki
6- Hifadhi katika sehemu safi na kavu
7- Matumizi ya unga wa mtama/uwele
8- Hupikwa ugali, uji na togwa. Vile vile hutumika katika kutengeneza vyakula vya watoto
*KUSINDIKA NGANO*
1- Ngano husagwa ili kupata unga
*Vifaa*
• Vifungashio
• Mashine ya kusaga
*JINSI YA KUSAGA*
1- Nyunyuzia maji kwenye ngano
2- Koboa na saga ili kupata unga
3- Weka kwenye vifungashio safi na visivyopitisha maji
*MATUMIZI*
1- Unga wa ngano hutengeneza vitafunwa kama vile mikate, chapati, maandazi, tambi na
keki.
shukrani kwa elimu na naomba unifunze jinsi ya kusindika dengu .asante
ReplyDelete