FAIDA ZA SOYA YA CHAI
- Soya huwafaa sana wenye matatizo ya shinikizo la damu
- Kama mtu ana shinikizo la damu ni vema akatumia soya kama kinywaji maana huweka mapigo ya moyo katika hali ya msawazo.
- Wakati mtu mwenye mapigo ya moyo ya kupanda hashauriwi kabisa kutumia majani ya chai au kahawa, hivyo kinywaji cha soya ni suluhisho kwake na mbadala sahihi.
- Kwa mtu mwenye shinikizo la damu la kushuka anapaswa kutumia soya maana itaweka mapigo ya moyo katika hali ya kawaida.
- Kunywa majani ya chai au kahawa kunapandisha mapigo ya moyo na ikiwa ataendelea kutumia vinywaji hivi basi moyo huzoea; na siku mapigo ya moyo yakishuka anapata shida na kuingia gharama kubwa kununua madawa ya ghali sana ili kupandisha mapigo ya moyo.
- Hivyo namshauri kwamba atumie kinywaji cha soya ili siku mapigo ya moyo yakishuka anaweza akatumia sasa majani ya chai au kahawa kama dawa tu ili kupandisha mapigo ya moyo.
*Matatizo ya vidonda vya tumbo*
- Matumizi ya soya ya chai ni rafiki kwa mazingira ya tumbo kutokana na kufanya kazi vema katika mazingira ya tindikali ya tumbo.
*Gharama ndogo*
- Maandalizi ya soya ya chai ni rahisi na hugharimu kiasi kidogo tu cha fedha huku yakikuhakikishia manufaa mengi sana kiafya.
- Soya robo kilo (250mg) inakupatia pia soya ya chai robo kilo (250mg) pia, hivyo hakuna kinachopotea na waweza kuitumia kwa muda mrefu sana.
*JINSI YA KUANDAA MAZIWA YA SOYA*
1- Anza kwa kuchambua soya yako 2KG (Kilo 2) ili kuondoa mawe, nafaka zisizohitajika na soya zilizoharibika.
2- Kisha osha na loweka soya yako kwa masaa 24 yani kwa mfano umeloweka leo saa 1 asubuhi, iache hadi kesho saa 1 asubuhi.
3- Baada ya saa 24 kupita toa maganda na kutwanga soya yako kwa kutumia kinu au saga kwa kutumia blenda mpaka itakapolainika vizuri.
4- Hakikisha chombo unachotwangia ni kisafi kabisa ili maziwa yasichafuke na kupunguza thamani yake.
5- Kisha changanya soya ulizozitwanga na maji safi na salama lakini zingatia kutochanganya maji mengi sana hata maziwa yako yakawa mepesi sana.
*Maziwa Yakiwa Tayari Kwa Kuchujwa*
6- Baada ya kuchanganya maji na soya uliyoitwanga, chuja kwa kutumia kitambaa cheupe kisafi chenye nafasi ndogo sana ili kuzuia chembechembe za soya kupenya.
7- Hapo utakuwa umepata maziwa ya soya.
8- Mabaki ya soya uliyokamua yanaweza kutumika kutengeneza bagia kwa kuyachanganya na viungo na unga wa ngano kidogo kwajili ya kushikiza bagia zako.
9- Au unaweza kutumia kama chakula cha ziada kwa kuku kama mbadala wa dagaa au uduvi
10- Kisha chemsha maziwa yako hadi yaive kabisa. Ikumbukwe kwamba maziwa ya soya yana tabia sawa na maziwa mengine ya wanyama katika utaratibu wa kuyaandaa.
11- Hivyo katika kuchemsha maziwa ya soya, weka chombo chini ya sufuria au chungu chako ili kuepuka kuganda kwa maziwa katika sufuria au chungu na kufulumia kwa maziwa.
12- Yakisha chemka na kuiva vizuri unaweza kuyatumia kwa chakula au kwa kitafunwa chochote.
Unaweza kuongeza soya ya chai kama unataka upate chai ya maziwa.
13- Ili unufaike sana na maziwa haya basi tumia asali badala ya sukari.
*FAIDA YA MAZIWA YA SOYA*
1- Maandalizi rahisi kwa unafuu mkubwa sana
2- Matumizi ya maziwa ya soya yanakulahisishia gharama za kupata maziwa mengi kwaajili ya nyumbani maana kwa 2kg za soya ukapata maziwa zaidi ya lita 10.
3- Utajiri wa virutubisho vya chakula.
4- Maziwa ya soya yana mchango mkubwa kwa mtumiaji kwani yamesheeni virutubisho vyote vilivyopo hata katika maziwa ya wanyama lakini faida yake kubwa zaidi ya maziwa ya wanyama, maziwa ya soya hayana mafuta ya lehemu yanayoganda na kudhuru mwili wa mtumiaji.
5- Maziwa ya soya hayana pia vimelea vya magonjwa mbalimbali vilivyomo ndani ya maziwa ya wanyama.
6- Kwa watoto wadogo Maziwa ya soya yana mchango mkubwa katika ukuaji wa watoto wadogo bila kujali umri wa mtoto na Kwa wale watoto ambao wameachishwa ziwa la mama kwa sababu mbalimbali kama kifo, magonjwa, kutengana n.k wanaweza wakakua vizuri kwa kutukia maziwa ya soya kuliko aina yoyote ile ya maziwa.
7- Maziwa ya soya ni mdabala na jibu sahihi kwa mahitaji yako ya maziwa
8- Yanaweza yakaganda na kuwa mtindi.
9- Ikiwa mtumiaji atataka apate mtindi basi atayachukua maziwa ya soya baada ya kuchemshwa, kuiva vizuri na kupoa katika chombo cha kugandishia maziwa nayo yataganda kwa utaratibu uleule kama yagandishwavyo maziwa ya wanyama.
10- Kisha waweza kuyatumia kwa chakula chochote
This comment has been removed by the author.
ReplyDelete