Hii ni aina ya jamu ya asili ambayo inaweza kutumiwa kwa kula na mkate au aina nyinginezo za vitafunwa, au mtumiaji anavyopendelea kuitumia.
- Jamu hii inatengenezwa kutokana na mchanganyiko wa aina mbili za matunda, embe na karakara
- Namna ya kusindika jamu ya embe na karakara
Dondoo: Kiwango cha mahitaji yatakayoainishwa hapo chini na maelezo yake ni kwa ajili ya, kutengeneza na kupata kiasi cha chupa 15 za nusu (½) lita.
*Mahitaji*
• Maembe 50 makubwa yaliyoiva vizuri
• Karakara ½ kilo
• Sukari nyeupe kilo 3
• Juisi ya limao lita ⅛
*Namna ya kuandaa*
• Osha maembe vizuri kwa maji safi
• Menya kwa uangalifu
• Katakata vipande vidogo vidogo
• Unaweza kusaga maembe hayo endapo si laini
• Osha karakara (passion fruits) vizuzi kwa maji safi
• Kata na utoe sehemu ya ndani (chakula)
• Changanya na maembe uliyokwisha kuandaa
• Weka sukari nyeupe kilo tatu kwenye mchanganyiko huo
• Weka lita 1 ya juisi ya limao
• Bandika jikoni
• Koroga taratibu kwa muda wa nusu saa
• Epua na ufungashe
*Ufungashaji*
• Wakati mchanganyiko ukiendelea kuiva jikoni, hakikisha unaandaa vifungashio/chupa
• Ni muhimu kuhakikisha kuwa chupa hizo zimeoshwa vizuri na kuwekwa kwenye chombo maalumu cha kuulia vimelea (Sterilizer)
• Weka jamu yako kwenye vifungashio kulingana na ujazo unaohitaji ikiwa bado ya moto
• Funga chupa/kifungashio kiasi
• Rudisha kwenye chombo maalumu cha kuulia vimelea
• Acha humo kwa muda wa dakika tano
• Ondoa na ufunge vizuri
• Pindua chupa/kifungashio mfuniko ukae chini. Hii itasaidia mfuniko kufunga vizuri
• Weka nembo tayari kwa mauzo
No comments:
Post a Comment