August 27, 2018

TOFAUTI KATI YA MJASIRIAMALI NA MFANYA BIASHARA

SIFA ZA MJASIRIAMALI

Kama wewe ni mjasiriamali basi lazima utakuwa na sifa moja wapo ama sifa zote kati ya hizi zifuatazo

  • Lazima utakuwa mtatuzi wa matatizo mbalimbali yanayoikumba jamii
  • Lazima utakuwa mbunifu na jasiri katika mazingira yoyote aliyopo
  • Lengo lako kuu litakuwa sio kutengeneza fedha bali fedha itakuwa ni matokeo ya kutatua changamoto Fulani
  • Nguzo yako kuu itakuwa ni uvumilivu na kutokata tamaa
  • Lazima utakuwa unatengeneza kiasi kikubwa cha fedha kwa kutumia nguvu kidogo na kwa muda mfupi
  • Hutatafuta wala kubembeleza wateja bali wateja watakutafuta na kukubembeleza wewe uwapatie huduma au bidhaa unayoitoa
  • Mwisho kabisa lazima utakuwa mdadisi na mwenye kupenda kujifunza kitu kipya kila siku.

SIFA ZA MFANYABIASHARA

Kama wewe lengo lako ni kuwa mfanyabiashara na si mjarisiamali basi lazima       utakuwa na sifa moja wapo kati ya hizi au sifa zote hizi lazima utakuwa nazo.

  • Lengo lako kuu litakuwa ni kutengeneza fedha na si kuwa mtatuzi wa matatizo katika jamii
  • Mara nyingi utakuwa unatangaza sana bidhaa au huduma unayoitoa kuliko elimu juu ya huduma au bidhaa unayoitoa
  • Utakuwa unapata wateja kwa msimu kulingana na biashara unayoifanya na sio wateja wa kudumu
  • Lazima utakuwa unabembeleza wateja ili uwape huduma au bidhaa badala ya wao kukubembeleza wewe
  • Ushindani huwa ni mkubwa sana kwa wafanyabiashara kuliko kwa wajasiriamali
  • Ni rahisi sana kwa mfanyabiashara kukata tamaa kwa kile anachokifanya kuliko mtu ambaye ni mjasiriamali
  • Wafanyabiashara wengi biashara zao hazidumu hufa ndani ya muda mfupi baada ya kuanzishwa .
  • Mara nyingi hutengeneza fedha kiasi kidogo kwa nguvu nyingi na kwa muda mrefu zaidi n.k

TENGENEZA TOMATO SAUCE

Malighafi zinazotumika

  1. Nyanya kilo 1.
  2. Vitunguu maji viwili.
  3. Vinegar vijiko 3 vya chai.
  4. Sukari vijiko 2 vya chai.
  5. Chumvi kijiko Kimoja cha chai
  6. Maji ya moto Kikombe Kimoja cha chai.
  7. Mafuta ya Kula vijiko 7 ya vyakula.

 

Haya Ndiyo mahitaji ya kutaka kutengeneza nyanya souce, Hata hivyo Kama Unataka kutengeneza Zaidi Ya Hapo unatakiwa kuongeza uwiano wa mahitaji Hayo.

 

JINSI YA KUTENGENEZA nyanya SOURCE.

 

HATUA YA KWANZA.

  1. a) Menya Nyanya Rangi vitunguu kisha vikate vipande vidogo vidogo.

 

  1. b) Tumia Brenda Kusaga mchanganyiko Wako.

 

  1. c) Anza kuweka malighafi namba 1 Hadi namba 4 katika brenda Yako kutokana Rangi uwiano (uwiano) uliopewa Hapo Juu. Saga to dakika Kadhaa Hadi Uone imetokea rojo Laini.

 

HATUA YA PILI.

  1. a) Tumia sufuria yenye Nafasi kupika Mseto Huu.

 

  1. b) Weka sufuria Yako jikoni tia mafuta ya Kula acha yachemke kisha mwagia Mseto Wako Rangi kisha uanze kukoroga to dakika 30 kuelekea Upande Mmoja huku ukichemka.

 

  1. c) Baada ya Hapo epua Mseto Huo utakuwa Tayari imeshakuwa nyanya funga Vizuri Rangi kisha Peleka Sokoni.

KILIMO CHA KAROTI

UTANGULIZI
Karoti ni aina ya mboga yenye vyanzo vingi vya calcium, iron na wingi wa vitamin B. Kwa jina la kisayansi inajulikana kama Daucus carotana hustawi sana kwenye udongo wa tifutifu wenye pH ya 6-6.5 na joto (temperature) la 18-24
karoti inalimwa maeneo mengi sana nchini ikiwa pamoja na mbeya, morogoro( maeneo ya uluguru na mgeta), iringa pamoja na kilimanjaro.


aina za caroti
Nanteshi inapatikana maeneo mengi na inalimwa sana hapa Tanzania. inakuwa kwa haraka na nitamu sana.Chantenay. hii pia ina ladha nzuri nainataka kufanana na Nantes lakini mizizi yake ni dhaifu ukilinganisha na Nantes.

UANDAAJI WA SHAMBA.
shamba linatakiwa liandaliwe vizuri kuondoa magugu yote na udongo unatakiwa kutifuliwa vizuri kurahisisha mizizi kupenya vizuri kwenye udongo  na maji kupenya vizuri. na pia matuta yake yawe yameinuka kuzuia maji kutuama kwenye tuta, kwani maji kutuama husababisha mizizi kuoza na mmea kutokukua vizuri.

 

UOTESHAJI.
karoti hupandwa kwa kutumia mbegu moja kwa moja shambani (direct sown), kiasi cha mbegu kinachotumika kupanda (seed rate) ni3.5-4 kg per ha. na mara nyingi hairuhusiwi kuhamisha miche (no transplanting) kwa sababu mizizi yake ni dhaifu ambayo haitastahimili kukua baada ya kuhamishwa.
baada ya wiki ya nne kutoka kupandwa hufuatia kungolea miche iliyorundikana kuipa nafasi kwaajili ya kufanya miche iwe na afya nzuri(thinning).
mbegu za karoti ni ndogo sana ambazo zinatakiwa kupandwa kwenye urefu wa ( 1.9 -2.5) cm.

UMWAGILIAJI
Hakikisha udongo una unyevu wa kutosha hasa siku za mwanzo. Karoti zilizokosa maji kwa muda mrefu huzaa mizizi midogomidogo. Pia udongo mkavu ukipata maji mengi ghafla husababisha karoti kupasuka. Hivyo mwagilia shamba mara kwa mara kuhakikisha udongo una unyevu wa kutosha wakati wote, kama hali ya hewa m yajua kali.

UTUNZAJI.
mmea unatakiwa umwagiliwe kwa siku asubuhi na jioni kuupa mmea maji ya kutosha ili uweze kukua vizuri.kungolea magugu ili kuzuia ushindani kati ya mmea na magugu kwa ajili ya kuupa mmea afya nzurikupunguza mirundikana ya miche ili kupatia mimea afya nzurikuweka mbolea kwa kukuzia  mmea

KUPUNGUZA MCHE 

Mimea ya karoti inahitaji kupunguzwa mara mbili. Mara ya kwanza hupunguzwa ikiwa na majani matatu mpaka manne au wiki mbili tangu kupandwa na kuachwa katika nafasi ya sentimita tano mpaka saba. Mara ya pili hupunguzwa ikiwa na urefu wa sentimita 10 mpaka 13, na kuachwa katika nafasi ya sentimita 10 mpaka 15. Karoti zilizopunguzwa zinaweza kutumika kwa chakula.
 

MAGONJWA YA KAROTI.
magonjwa ya bacteria (bacterial disease). ambayo husababisha kusinyaa kwa mimea (wilting), na kufanya mmea usikue (stunted growth) na shina kuoza (stem rot) pamoja na kuoza kwa karoti.

magonjwa ya fangasi. (fungal disease).  kama kata kiuno (damping off) huu ugonjwa hushambulia sana miche hufanya miche ishindwe kukua vizuri na mara nyingi hupelekea mche kufa.

NAMNA YA KUZUIA MAGONJWA SHAMBANI.
tumia mbegu safi wakati wa kupanda, zuia magugu shambani, zuia wadudu wote, na hakikisha shamba  linakuwa safi, (field sanitation) ili kuzuia magonjwa ya mmea nakufanya mmea ukue vizuri.

UVUNAJI.
karoti huvunwa baada ya miezi mitatu na huvunwa kwa kuvuta (uprooting) baada ya miezi mitatu pia inaweza kuvunwa siku 20 kabla ya kuvunwa. karoti hutoa tani (tonne) 30-50 per ha.

SOKO LA KAROTI. 
karoti ni zao  muhimu sana ambalo hutumika kama mboga. 
huuzwa kwa mafungu au moja moja ambayo kwa moja huanzia kwa  200 shilingi za Kitanzania. soko lake hupatikana sana karibu mikoa yote Tanzania kutokana na faida za karoti katika lishe.

TENGENEZA JUICE ZA MCHANGANYIKO WA MATUNDA MBALIMBALI

1. Juice ya ukwaju mix na custard


2. Juice ya carrot na ndimu hii taste inakua kama fanta orange


3. Juice ukwaju cucumber na zile pipi za kifua 


4. Jiuce ya passion na milk


5. Juice ya karkadee na mdalisini


6. Chukua ukwaju roeka then chuja halaf kando chukua custard na maji mix bandika kwenye jiko pika mpk iwe nzito then mix na ukwaju na maji kiasi chako ongeza sukari weka kwa fridge ipate baridi


7. passion,embe na beetroot


8. Beetroot na mbirimbi za kizungu


9. Watermelon and yellow passion  👍


10. Guava na cucumber


11. Orange juice kisha weka embe bivu na u blend, ajab sana ladha yake


12. Boiled carrots + milk+ condensed milk


13. Pineapple and mint


14. Ukwaju na tangawizi mbichi.


15. Beetroot ginger carrot and passion


16. Pineapple + mangoe


17. Tree tomatoes with beetroot


18. Pineapple+Ginger+Mango+passion+Carrot+Passion+Ginger


19. beet root, ginger, carrot, mango is bae


20. Pink Mapera+milk


21. Beetroot mint leaves n black pepper


22. Avocado banana and milk


23. Lime and mint.


24. Beetroot, treetomatoes and passion.


25. Watermelon and strawberries


26. Avocado +cucumber+ndim kdg.Embe +passion+Ubuyu juice


27. 2 ripe mangoes, 1 banina and drops of vanilla essence.  😋


28. Watermelon na black current soda ajab blend water melon na maji bt juice Uwe nzitto then freeze wakat wakuserve unamix soda na hio juice


29. Avocado, milk and bananas


30. Mangoes and bananas  😋


31. Melon and lemon juice


32. Carrots,passion na mango


33. Hibiscus leaves+mint+iliki (just soaked)


34. ukwaju, quencher ya strawberry rose sherbet


35. Three dates, vanilla ice cream scoup, two cups cold milk. Blend with some ice cubes.  😋.


36. Papaya and milk


37. Caricadee na oranges


38. Ovacado,papayu,embe and banana wablend namaziwa


39. Beetroots , passion carrots very tastry And Good for blood


40. Or ananas And mint Good for joint pains


41. Mango,carrot and pineapple.


42. Ginger, mint And lemon very tasty


43. Avocado +milk


44. Passion +carrots na sugar wacha thu


45. beetroot + carrots+ watermelon ( a lot since it has lots of water)+little bit of lemon/ ginger


46. Ukwaju+ cardamon


47. Lemon na watermelon serve with mint leaves on top ajab.


48. mango+iliki+maziwa+ice cream vanilla+a bit of sugar...Ajjab!!


49. Beetroot na Ukwaju...Tamuuuu


50. Passion na unga wa mabuyu


51. Avacado na mix na maembe nikipata passion pia naeka so sweet

52. Cucumber n lemon

53. Pineapple na coconut milk ajabb

54. Mangoes mix ripe and unripe ones ,milk and some sugar then blend together very tasty  :-)

55. Sweet melon + Pineapple + passion

56. Watermelon + Strawberry + lemon 

57. Mango + Passion + Tree Tomato

58. Pawpaw + Oranges 

59. Pineapple + Mint

60. Watermelon+mango+lemon juice blend them na sugar then chuja..tamuu

61. Maembe mabichi+ginger and cardamon

62. Water melon plus ukwaju

63. Mango+passion+orange

64. Watermelon + ukwaju + strawberry flavor

65. Ripe mangoes + Maziwa + mint leaves blend with ice cubes

66. Karkadee + strawberry flavor

67. Raw mango, ripe mango, ginger plus milk

68. Mabungo ..lakini chemsha kdg na sukari...ikipoa saga ..ueke sukari n barafu ..very nice

August 18, 2018

Kutuhusu ebusol

Ujasiriamali na stadi Bora za biashara

JINSI YA KUOTESHA MBEGU YA PAPAI

MWONGOZO.

Ili mbegu zilizo kavu za papai zipasuke na hatimae kuota zinahitaji vitu zifuatavyo.


Mwanga wa jua wa kutosha

hali joto

unyevunyevu.


hatua za kuotesha.

1. Fungua pakti yako ya mbegu.

2. Weka maji kwenye chombo  chochote na uloweke mbegu kwa muda wa siku 3 (saa 72). hakikisha unamwaga maji na kuweka mengine kila baada ya saa 24.

3. Baada ya saa 72 kupita, chukua kitamba na weka mbegu zako zote kwenye kitamba na kuzifunika vizuri.

4. Chimba shimo dogo kwenye sehemu ya mwanga wa jua wa kutosha, kisha weka mbegu ulizofunika kwenye kitamba na kuzifukia.

5. Mwagilia maji kila siku sehemu ya juu uliyofukia mbegu. itachukua siku 8 mpaka 12 mbegu kupasuka kutegemea na halijoto.

6. Mbegu zikipasuka unazihamishia kwenye kitalu au tray ya kupandia mbegu au kwenye viriba (polythene tube). katika hatua hii tumia kijiti au kitu chenye ncha kali katika kupanda mbegu. Hii inasaidia kuepuka kuvunja maotea ya mbegu.

7. Hakikisha unaweka mbegu si kwa kufukia sana. weka mbegu juu juu na fukia kwa kiasi kidogo sana udongo. Mara nyingi mbegu za papai hazina nguvu sana za kusukuma udongo kama utazifukia sana.

8. Baada ya kuweka mbegu, chukua mfuko wa sandarusi (jute bags) na  funika juu ya kitalu tafadhari usitumie majani makavu katika hatua hii.

9. Mwagilia maji kwa siku mara moja juu ya mifuko ya sandarusi kwa muda wa siku 3-5 mbegu zitaanza kutoa majani ya awali.

10. Baada ya siku 6-7 ondoa mifuko ya sandarusi.

11. Mbegu zikifikia sm 8-10 unaweza kuhamishia kwenye mashimo na kwenda kuotesha shambani.

August 17, 2018

JINSI YA KUTAFUTA MASOKO

UTANGULIZI 

Kuwafundisha washiriki kufikiri ki- masoko na kuelewa baadhi ya mbinu za masoko kitu ambacho kitawafanya waelewwe maana ya maneno “soko na masoko” pia utafiti wa soko na kuyafanyia kazi  katika biashara/miradi yao. 


Soko ni nini? 

Soko ni utaratibu au mtindo  uliowekwa kwa mujibu wa kanuni /sheria  kumwezesha mfanya biashara kuuza bidhaa zake kwa wateja/walaji. Husaidia kupanga nini uuze,nani umuuzie au jinsi gani watu wanavyoweza kujuakitu gani unauza,hivyo kukuwezesha kuzalisha kile ambacho kinahitajika  katika soko sahihi. 


Mafanikio katika biashara hutokana na mwonekano wa kipekee  wa bidhaa au bidhaa unayozalisha kukidhi matakwa ya walaji au wateja pia, kuweza kutambua  aina fulani ya watu ambao wangependa kununua bidhaa yako na kuweza kueleza  bayana ni kitu gani, watu wategemee kunufaika kwa kunua bidhaa zako kati ya kundi hili la walengwa. 


Kwa kifupi soko ni MTEJA Wa bidhaa na huduma uayozalisha 


Soko lako ni; 


Wateja wako ulionao kwasasa 

Wateja uaotarajia kuwapata baadae 

Wateja uliopoteza na untarajia watakurudia tena 


Masoko ni nini? 

Masoko ni shughuli yoyote ile anayofanya mfanyabiashara ili kuimarisha biashara yake. 


Haitoshelezi tu kukaa kungojea oda. 


Mfano wa shughuli hizo ni; 


Kuelewa matakwa ya wateja wa bidhaa yako 

Kupanga bei ambayo wateja  watakuwa tayari kulipa na itakupa faida 

Usambazaji wa bidhaa au huduma kwa wateja wako 

Kuwavutia wateja wanaume bidhaa au huduma yako 


UTAFITI WA SOKO 

1. Kwa nini tujifunze kuhusu soko? 

a)  Mahitaji (demand) 


Waswahili husema ‘unaweza kumlazimisha punda aende mtoni lakini huwezi kumlazimisha anywe maji’inamaana bidhaa zako kuwa wakati soko halihitaji bidhaa zako huwezi kulazimisha bidhaa yako inunuliwe 


b)  Bidhaa sahihi – usijaribu kumuuzia kitana mtu mwenye kipara bali muuzie kofia 


c)  Kufuata mkumbo-ni vema kutofautisha bidhaa za kuuza kwa wateja 


2. Unahitaji kufahamu nini kutokana na soko lako? 

Maswali yafuatayo ndio yakusaidia kufanya utafiti wa soko lako 


Wateja wako ni akina nani? 


Wako wapi 

Mahitaji yao ni nini? 

Wanapendelea nini kutokana na bidhaa zako 

Ni mara ngapi na kiasi gani a wanacho nunua? 

Wana nunua wakati gani? 

Ni kiasi gani cha pesa wako tayari kutoa? 

Ni jinsi gani bidhaa zitawafikia wateja 

Washindani wako ni wapi? 

Ubora wa bidhaa zao na bei zao vikoje 


NB; kutafuta majibu ya maswali haya kunaitwa utafiti wa masoko 


3. Jinsi ya kufanya utafiti a soko 

Mbinu zifuatazo zinaeza kutumika kufanya utafiti wa soko la bidhaa au huduma unazozalisha:- 


Kupitia Kwa wateja (kusikiliza maoni yao, kuachunguza na kuwauliza maswali). 

Kuwauliza maswali watumiaji mbali mbali wa bidhaa zako ( nini wanachohitaji na wasicho kihitaji, mapendekezo na nini kiongezwe) 

Kwa marafiki na ndugu 

Kusoma kwenye vitabu, magazeti, kusikiliza radio na kuangalia televisheni 

Kupeleka bidhaa zako katika maonesho ya biashara 

Kuangalia biashara za washindani wako: bei, ubora, tofauti za bidhaa,, kuonesha bidhaa, na huduma zinazoambatana na bidhaa zako 

Onesha sampuli ya bidhaaa au tembezasampuli ya bidhaa na waulize watu maoni juu ya bidhaa zako 


4. Jumuisho la masuala ya masoko 


B-Nne  katika masoko 

Bidhaa 

Bei 

Banda 

Bango 


a)  BIDHAA- Bidhaa ni kitu chochote kinachozalishwa kwa ajili ya kuuza au kutumia. 


Sifa za bidhaa 

Bidhaa nzuri ni ile inayoridhisha na inakidhi matakwa ya soko. Kwa mfano:- 


Ubora(muda, malighafi nzuri, iliyotengenezwa vizuri) 

Yenye kuvutia ( rangi,mapambo,usafi, utengenezaji mzuri) 

Mtindo (umbile zuri, inahusiana na thamani,saizi) 

Ya kisasa (Inayoendana matumizi ya mtindo uliopo- fassion) 

Tofauti na bidhaa za ashindani 


b) BEI- Bei nithamani ya bidhaa au huduma ambayo mteja yuko tayari kumudu au kulipia. Kwa hiyo bei hujumuisha Gharama zote na faida au Bei huiumuisha gharama za ununuzi, gharama za uendeshaji na faida. 


Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kupanga bei. 

Ghrama zote ka jumla (gharama halisi)

Bei za wapinzani 

Mahali ulipo 9 kiasi ambacho wwateja wwako radhi kulipia kwa kutegemea uezo wao kifedha) 

Msimu (kwa mfano bei kubwa za vinyago msimu wa watalii au bei ndogo za feniture wakati wa mvua ) 

Kupata faida ya kutosha kuendesha shughuli bila matatizo 


c) Banda au mahali pa kufanyia biashara 

Banda ni mahali muhimu sana  katika kuuza bidhaa au huduma. Mahali pa kufanyia biashara  panatakiwa pae na sifa zifuatazo:- 


Rahisi kufikiwa na wateja 

Usalama, usafi 

Sehemu ya maegesho 

Kuwa karibu na huduma nyingine muhimu kama vile usafiri wa daladala, sehemu za vinywaji, vyakula,umeme n.k 

Yenye mwanga wa kutosha 

Rahisi kuonekana 

Huduma hutolewa saa zote 


5. Upangaji mzuri wa bidhaa mahali pa biashara. 


Bidhaa zipangwe kwa seti 

Mahali pa wazi panapoonekana kiurahisi 

Weka bidhaa chache katika makundi madogo madogo 

Weka bidhaa za aina mbalimbali 

Panga sehemu yenye mwanga wa kutosha 

Sehemu safi 

Tumia picha au katalogi 


6. BANGO AU UVUMISHAJI 

Uvumishaji unajumuisha shughuli kadhaa  ikiwa ni pamoja na uvumishaji  wa mauzo,utangazaji,uhusiano wa jumuia na mbinu za kuuza. Shughuli hizo zinasaidia kuwavitia wateja, lakini hasahasa zinawapa wateja imani na bidhaa zako kuhakikisha kuwa hawanunui kwa mtu mwingine.Jambo muhimu la kuzingatia katika uvumishaji wa bidhaa ni lazima uwe mchangamfu na kuwa macho kuvutia wateja. 


Kuvumisha mauzo (sales promotion) 

Punguza bei yako kidogo ili wateja waone kuwa ni ndogo. Mfano:-  shs 999.00 badala ya 1000.00 

Weka bei maalum wakati wa sikukuu mbalimbali 

Panga bidhaa madirishani ilizionekane kwa nje (display) 

Uza bidhaa zinazoendana. Mfano muuza maandazi anaweza kuuza chai au muuza sukari anaweza kuuza majani ya chai 

Utangazaji 


Radio, magazeti,tv,sinema,mabango,kadi za biashara za mwenye biashara9business card)na sifa zinazotolewa kwa njia yam domo na watu watu waliokwisha kutumia bidhaa hizo. 


Mahusiano 

Kuchangia huduma za jamii Kama vile elimu, afya mazingira n.k 


Mbinu za uuzaji 


Jinsi ya kutambulisha bidhaa, eleza faida za bidhaa na ubora ake 

Kumthamini mteja 

Eleza faida ya bidhaa yako kabla hujataja bei 

Jaribu kuuliza juu ya mahitaji ya mteja ili uweze kumwelekeza kwenye bidhaa itakayomfaa. 

Kama mteja akiuliza bidhaa ambayo huuzi , unamwekeza zinapoatikana. 


MKAKATI WA MASOKO 


Kuwa na mkakati wa soko utakusaidia kufiki malengo yako kupitia kuweka lengo kuu/kubuni bidhaa/huduma mchanganyiko na kuchukua SWOT ANALYSIS(maeneo tunayofanya vizuri,maeneo ambayo hatufanyi vizuri,fursa tulizonazo, na changamoto zinazotukabili) katika bidhaa /huduma.


MAELEZO YA MALENGO YAKO 

Maelezo ya malengo ni nini? Ni maelezo ya jumla  juu ya kila unachotarajia kufikia,au lengo kuu la shirika. Hujulikana pia kama dira ya shirika . hivyo ni vema kuwa na wazo ambalo unaweza kuliweka kama kitovu cha kukuwezesha kuona unapoelekea  kibiashara. Kulingana na kukua kwa biashara yako waweza kuendeleza malengo yako kuipa nguvu dira yako 


Lengo lako lazima liwe dhahiri / bayana 

Ni nini unataka kutimiza? 

Kwa nini/ sababu gani ya kutimiza? 

Nani atafanya nini? 

Ni wapi utafanyia kile unachotarajia? 

Kipi kinatakiwa kufikia lengo lako? 

Malengo yako lazima yaweze kupimika. 


Kwa kiasi gani? 

Vingapi? 

Malengo yako lazimayawe ya kufikiwa.

Ya juu Sana kisi cha kushindwa kufikia malengo yako? 

Ya chini Sana kisi kwamba malengo yako hayaleti maana? 

Ni muhimu kuweka malengo yanayokubalika lakini yenye kutamanisha. 

Malengo yako yawe na uhusiano na kile unachotaka kufanya 


Tuzo nitakayoipata baada ya kufikia malengo itazidi gharama (faida) 

Tuzo nitakaipata baada ya kufikia malengo itafikia maezo ya malengo yako ya awaliKufikiwa kwa malengo yako kutakusaidia  kufikia mipango yako? 


Malengo yako lazima yaende na wakati 


Ni lini litaanza? 

Itachua muda gani kufikia malengo yako?Naweza kufanya nini kila juma,Mwezi juu ya bidhaa nyingine iliyopo ambayo ina matumizi sawa na ile anayohitaji, mteja..

August 10, 2018

MCHANGANUO WA KILIMO CHA MATIKITI

Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. 


Zao hili lina wapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. 


Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama kama matango,maboga na maskwash. 


Zao la tikiti maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi. 




Katika shamba la ukubwa wa shamba la ekali moja(1.acre) lililoandaliwa vizuri, kupandwa na kuhudumiwa vizuri mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi cha TANI 15-36, ambacho kitamsaidia kupata fedha zitakazo msaidia katika mahitaji yake mbalimbali na kuondokana na Umasikini.


Tikiti maji ni moja ya mazao ya matunda ambayo yamejipatia umaarufu mkubwa kote ulimwenguni. Zao ili ni moja ya mazao ambayo ni rahisi sana kuzalisha na lisilohitaji gharama kubwa. Gharama ya kulima ni kuweza kufahamu mazingira yanayofaa kwa ajili ya tikiti maji, uchaguzi sahihi wa mbegu, upandaji, matunzo na mambo mengine machache yasiyokuwa na gharama kwa mkulima.



Faida ni kubwa kwa mkulima, kwa kuwa zao hili huuzwa kwa kilo na ukubwa hutegemeana na matunzo shambani. Mkuu wangu kilimo cha bustani ni changamoto! Faida ipo tena nzuri ya kuridhisha kabisa. Binafsi nina uzoefu wa kutosha juu ya kilimo cha tikiti maji.


Mathalani unataka kulima ekari1 ya tikiti, huu ni mchanganuo mfupi kabisa;kawaida ekari1=sqm4000 Kwa spacing ya 1m shimo hadi shimo na 2m mstari kwa mstari na kila shimo huwa naacha miche 2 na kuruhusu matunda3. Na kama utapata mbegu ya hybrid itakuwa vizuri zaidi maana MATUNDA yake yanajiuza yenyewe, shambani ni sh1500. 

So ukishusha hesabu hapo juu: 

Jumla ya mashina ktk ekari1 ni 

Sqm4000÷(1m×2m)×2=4000 

Idadi ya MATUNDA =(4000×3)=12000 

Mauzo shambani ni 12000×1500=Tshs18,000,000/= 

Tatizo ni usimamizi, ila kilimo hiki kinalipa sana!anza kulima zao hili ili uweze kujiongezea kipato na kuondokana na umaskini wa kujitakia. Amka sasa.



AINA ZA MATIKITI MAJI

Kuna aina kuu mbili za matikiti maji, ambazo ndani yake zimegawanyika kulingana na aina ya mbegu, ilipofanyiwa utafiti na kuzalishwa. Aina hizo ni;

Matikiti yenye rangi ya kijani. Aina hii ni ya duara na huwa na umbo kubwa.

Matikiti yenye rangi ya mabaka mabaka. Aina hii ni ndefu na huwa na umbo la wastani.


Uzalishaji

Kwa kawaida ekari moja huchukua miche elfu mbili na mia tano (2,500) ya matikiti maji. Gharama ya uzalishaji wa zao hili ni ndogo sana ukilinganisha na aina nyinginezo za mazao. Tunda la tikiti maji huwa na uzito wa kati ya kilo mbili mpaka kilo kumi na tano. Kilo moja huuzwa kati ya shilingi za kitanzania 350-1000. 


Zao hili husaidia katika udhibiti wa magugu shambani, pamoja na utunzaji wa udongo kwa kuwa hutambaa na kufunika udongo.kangetakilimo



MATAYARISHO YA SHAMBA NA UPANDAJI

Baada ya kuchagua aina ya mbegu unayohitaji kupanda, inashauriwa kulima shamba na kuacha kwa muda wa kipindi kitakachoruhusu nyasi na magugu mengine kuoza kabla ya kupanda.Hii inasaidia majani na magugu kutoota upesi pindi ukipanda miche yako ya matikiti.kangetakilimo 


Hakikasha kuwa shamba lako limelimwa vizuri na udongo kulainika, udongo uwe umechimbuliwa kiasi cha inchi 8-10 kwenda chini.kangetakilimo




 Hakikisha kuwa shamba lako lina nafasi ya kutosha kwa kuwa matikiti huhitaji nafasi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kupata mwanga wa jua wa kutosha. Katika shamba la ukubwa wa hecta moja kiasi cha kilo 3-4 cha mbegu kinaweza kutumika.kangetakilimo


 Panda mbegu 2 au 3 moja kwa moja katika kila shimo. Usipande katika kitalu kwasababu miche ya mitikiti huwa ni dhaifu sana wakati wa upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 - 2 kutoka mstari hadi mstari. kangetakilimo


Zingatia kutokutumia mbegu za tikiti uliloninua kwasababu linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi na ubora wa matikiti yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)kangetakilimo


Kila shimo hakikisha umeweka mbegu tatu na uzipande kwa utaratibu wa pembe tatu au kwa lugha rahisi mafiga.

Zikishaanza kutoa matunda hakikisha kila shina unaacha matunda matatu mengine kata ili kuruhusu ukuaji mzuri wa tunda kwani yakiwa mengi yatakuwa yanagawana chakula hivyo tunda kuwa dogo ambalo ukipeleka sokoni unapata pesa kidogo.

August 04, 2018

MKOJO WA NG'OMBE NI MBOLEA SAFI SANA KWA KILIMO


habari kwa ufupi.

wiki hii tunajifunza juu ya mbolea za asili na jinsi ya kutumia shambani lengo kubwa ni kuzalisha vyakula hai.

Leo tutajifunza kitu ambacho huwenda ukuwai kufikiria kuhusu Mkojo wa Ng'ombe.

Utangulizi.

Mbolea ya mkojo wa Ng'ombe husaidia katika kilimo cha mazao mbalimbali, Vinavyopatikana katika Mkojo wa Ng'ombe Maji (Chumvichumvi), Madini kama vile Phosphorus, Potasiamu na Nitrojeni. Pia katika vidonda inasaidia kidogo kama ( Antimicrobial Agent).


UTENGENEZAJI WA MBOLEA YA MKOJO WA NG'OMBE.


Mbolea hii hupatikana kwa kukusanya mkojo wa mnyama na kuhifadhiwa katika chombo kama vile ndoo, dumu, pipa n'k hadi uoze kwa wastani wa siku 15 zinatosha kuozeasha mkojo huo.


JINSI KUWEKA MKOJO WA NG'OMBE SHAMBANI.


Mkojo wa Ng'ombe unaweza kutumia kwa uwiano wa lita 1 ya mkojo kwa lita 10 za maji kwa mimea midogo na kwa mimea mikubwa unaweza kutumia uwiano wa lita 1 mkojo kwa lita 5 za maji.


MATUMIZI YAKE SHAMBANI

-Kwa kupulizia katika majani- lowesha mmea wako kuanzia katika majani hadi shinani.


NB. Mkojo wa Ng'ombe ukitumia kwa mfululizo shambani unapunguza kabisa matumizi ya mbolea za viwandani.


FAIDA ZA KUTUMIA.

-Mimea huwa na rangi ya kijani zaidi.

-Inasaidia kuboresha hali nzuri ya udongo ( inaboresha soil texture)

- Inaondoa rangi ya unjano katika majani.

- Inafanya kazi kama kichocheo cha ukuaji wa mmea (growth promoters)

- Udongo uliowekwa mkojo wa ng'ombe haupati tatizo la upungufu wa madini yasio makuu(micronutrients), hivyo mbolea hii huongeza madini ya ziada katika udongo.

-Inatengeneza mazingira mazuri ya ukuaji wa minyoo (earthworm) hivyo kutengeneza mazingira mazuri ya minyoo kuozesha majani ya mimea n'k na pia kuruhusu mfumo mzuri wa hewa katika udongo.


Zingatia 

Matumizi ya mkojo wa Ng'ombe kila baada ya siku 10 hadi 14 unafanya kazi kama kiua wadudu kana aphidi na wengineo.


MAGONJWA YA KUKU NA TIBA ZAKE

Kuku hushambuliwa na magonjwa mbalimbali ambayo mengine yanatibika kwa dawa na mengine hayana tiba bali kuku hupewa chanjo maalumu ambayo

huzuia magonjwa hayo.Leo nitawaeleza baadhi ya magonjwa ambayo hushambulia kuku mara

kwa mara na ambayo ni chanzo cha kuwakatisha tamaa wafugaji wa kuku.

A.) MAGONJWA YANAYOHITAJI CHANJO

1> GUMBORO

Ugonjwa huu husababishwa na virusi.

DALILI ZA UGONJWA

-Kuku kuzubaa na kulundikana, pamoja na

kusinzia

-Kuku kuharisha

-Kuwa na vifo vingi kwa kuku

TIBA

Ugonjwa huu hauna tiba,,Kuku wakipewa Dawa

za oxytetracycline hupunguza vifo.

KINGA

wakinge kuku wapo kwa kuwapa chanjo ya

gumboro (Gumboro vaccine)

*2> MAHEPE (Marecks)*

Ugonjwa huu husababishwa na virusi*

*DALILI*

-Kuku hupata ulemavu na vifo vya mara kwa

mara.

*TIBA*

Ugonjwa huu hauna tiba

KINGA

Chanjo hutolewa kwa vifaranga wenye umri wa

siku moja,vifaranga hupewa chanjo ya mahepe

(Marecks vaccine)

3>NDUI YA KUKU (Fowl Pox)

Ugonjwa huu husababishwa na virusi.

*DALILI*

-Kuku hupatwa na vidonda kichwani.

-Kuku hupata uvimbe mweupe kwenye

mdomo na kushindwa kula.

TIBA

Ugonjwa huu hauna tiba.

KINGA

Chanja kuku wako wa siku 60-90 kwa chanjo ya

Ndui ya kuku (Fowl pox vaccine).

*4>MDONDO (New castle)*

Ugonjwa huu husababishwa na virusi

*DALILI*

-Ugonjwa huu hutokea kwa ghafla na kuenea

kwa haraka

-Vifo vya kuku huwa vingi

-kuku hupumua kwa shida

-Kuku hupooza na kulemaa miguu

-Kuku hupinda shingo yake

-Kuku hupunguza kutaga mayai

-kuku huarisha

-Kuku Kuzunguka zunguka na kutembea

kinyume nyume.

TIBA

Hauna tiba

*KINGA*

Chanja vifaranga wako na kuku wako kwa

chanjo ya Mdondo (New Castlef vaccine) na

urudie chanjo hii kila baada ya miezi mitatu.

*B.)MAGONJWA* YANAYOTIBIKA KWA DAWA

1>KUHARA DAMU (coccidiosis)(Koksidiosisi

Ugonjwa huu husababishwa na virusi.

*DALILI*

-Kuku huzubaa na kujikunyata

-Kuku kuharisha LinkedI chenye damu au

kinyesi cha kahawi

-Kuku hudhoofika,manyoya huvurugika na

kulegea mabawa na kuonekana kama wawevaa

koti

-Kuku hupungukiwa homa ya kula

-Vifo huwa vingi kwa vifaranga

*TIBA*

Wape kuku wako dawa kama Esb 3, Amprolium,

au Basulfa.

KINGA

Zingatia usafi wa banda la kuku na usiruhusu

unyevuunyevu katika banda la kuku,

*2>HOMA YA MATUMBO(Fowl typhoid)*

Husababishwa na bakteria

DALILI

-Kuku hupata homa kali

-Kuku huarisha kinyesi cha kijani au njano

-Vifo huwa vingi hasa kwa vifaranga wenye

wiki 1-2

-Kuku huzubaa,kuvimba viungo vya

miguu,kuchechemea,kukosa hamu ya kula

-Kuku wanaotaga hupunguza utagaji,hutaga

mayai yenye ganda laini na hupata vifo vya

ghafla

*TIBA*

Dawa za oxytetracycline kama

Furamax,Typhoprim hutibu ugonjwa huu.

KINGA

Hakikisha usafi wa banda na vyombo vya

chakula na maji kwa kuku.

Tenganisha kuku wagonjwa na wazima

C)MINYOO

Hushambulia kuku wote wakubwa na vifaranga

DALILI

-Kuku hukonda

-Kuku huarisha

-Kuku hukohoa

-Kuku hupunguza utagaji

-Kuku hudumaa katika ukuaji/hawakui vizuri

-Kuku hupungua uzito

*TIBA*

Tumia dawa za minyoo kama piperazine

KINGA

Wapewe dawa za minyoo mara kwa mara kila

baada ya miezi mitatu

D)VIROBOTO/CHAWA/UTITIRI

Hushambulia sana vifaranga na hutokea vifo

kwa wingi kwa vifaranga Kwa kuku wakubwa

tatizo halionekani kwa sana lakini nao

huathiriwa sana.

*DALILI*

-Kuku kutochangamka

-Ukuaji mdogo wa kuku

-Kuku kutotaga na kuhatamia vizuri kutokana

na kusumbuliwa na chawa,utitiri au viroboto

-Viroboto huonekana kuganda machoni

wakinyonya damu

TIBA

Tumia dawa za unga kama sevin dust

5% ,Malathion ,akheri powder kwa kuku wote na

mabanda yao.

KINGA

Boresha usafi wa mabanda ya kuku.

E)UKOSEFU WA VITAMINI A

huathiri sana kuku wadogo.

*DALILI*

-Kuku huvimba macho na kutoa uchafu mzito

kama sabuni ya kipande iliyolowana.

-Mara nyingi ugonjwa hujitokeza baada ya

kipindi kirefu cha kiangazi

TIBA

wape kuku wote dawa za vitamini za kuku

zinazouzwa dukani.

*KINGA*

Wape kuku wako mchicha na majani mabichi

mara kwa mara.

*ZINGATIO*

Fuata ushauri wa matumizi sahihi kwa kila

dawa pindi ununuapo katika duka la dawa..

August 03, 2018

KILIMO CHA MTAMA KINAFAIDA

Mtama unaweza kutumika kwa kuchemshwa na    kuliwa kama ulivyo, kusagwa na kutumika kwa uji, kutengenezea vinywaji kama vile bia, kuoka mikate, na aina nyinginezo za vitafunwa. Mmea wa mtama pia hutumika kwa ajili ya malisho ya mifugo kama vile hay  na sileji. Mtama unastawis vizuri kwenye mazingira yenye wastani wa milimita 400 – 700 za mvua kwa mwaka. Pia mtama unavumilia sehemu zinazotuhamisha maji, na unaweza kulimwa sehemu zenye mvua nyingi.


         Mtaama unafaa pia kwa sehemu kame zenye wastani wa joto la chini kiasi cha nyuzi joto 18°C, ili kuweza kuota vizuri, na kiasi cha nyuzi joto 25-30°C ili kukua vizuri. Mtama hauwezi kuvumilia barafu. Mtama unaweza kukua kwenye aina zote za udongo. Kwa kiasi kikubwa unafaa zaidi kwenye udongo wa mfinyanzi, lakini pia kwenye udongo ambao una kiasi kidogo cha mchanganyiko wa kichanga. Mtama unaweza kuvumilia uchachu kwenye udongo kuanzia pH 5.0-8.5, na inavumilia udongo wenye chumvi kuliko yalivyo mahindi.


*Aina za mtama*

        Kwa jumla kuna aina zaidi ya 30 za mtama zinazolimwa kama chakula. Mtama hustawi vizuri kwenye joto ikivumilia pia ukame. Hivyo ni nafaka muhimi kwenye maeneo yabisi za Afrika. Katika miaka ya nyuma kilimo chake kiliachwa mara nyingi kwa ajili ya mahindi kwa sababu mahindi huleta mazao makubwa zaidi kwa ekari. Lakini wakati wa ukame mahindi ni hasara na watu hurudi-rudi kwenye kilimo cha mtama.


         Aina za mtama zinatofautiana kulingana na rangi      zake, kuna nyeupe, nyekundu, na kahawia. Mbegu za asili huwa zinachavushwa kwa urahisi zaidi lakini mavuno yake huwa ni hafifu ukilinganisha na mbegu za kisasa. Hata hivyo, aina za kisasa zinazalishwa kwa gharama nafuu zaidi zinapopandwa kwa kufuata kanuni za kilimo bora.


*Serena:*  Ina punje za kahawia. Aina hii hustawi kwenye eneo lenye mvua za wastani na hukomaa katika kipindi cha siku 110. Aina hii huwa na shina na mizizi imara, ambapo huweza kuzalisha kiasi cha kilo 3,000 kwa hekari moja. Ambapo zinahitajika kilo 5 za mbegu kwa hekari moja. Aina hii ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa milia, kutu, na madoa ya kahawia kwenye majani.


*Seredo:*  Hii ni aina nyingine yenye punje za kahawia, na inapendekezwa Kulimwa kwenye eneo lenye mwinuko wa mita 1,500 kutoka usawa wa bahari. Aina hii huchanua baada ya siku 71 na hukomaa katika kipindi cha siku 120. Aina hii huwa ni ndefu, na ina uwezo wa kuzalisha kilo 5000 kwa hekari moja. Ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa wa milia, kutu, mabaka kwenye majani, na madoa ya kahawia kwenye majani.


*Gadam:* Inafanya vizuri katika sehemu ambazo si kame sana. Katika nchi nyingi mfano Kenya, aina hii ya mtama hutumika kutengenezea bia na pia kwa chakula. Aina hii huvumilia bungo na ugonjwa wa majani.


*Hakika na Wahi:*  Hizi ni aina mbili za mtama ambazo zimezalishwa na kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga kwa ajili ya kuoteshwa kwenye mashamba yalioathiriwa na viduha. Mbegu hizi zina rangi ya manjano iliyopauka. Unga wa aina zote mbili zinafaa sana kwa kupika ugali.


Aina Nyingine za Mtama zinazolimwa kwa Wingi ni: _*Pato, Tegemea, Sandala, Malawi, Mesia, Swale na Uwele*_, Hasa kwa Kanda ya Kati.


      ✍🏼Utayarishaji wa shamba na kupanda

Kwa kawaida mtama hupandwa kwa kutumia mbegu. Mbegu hupandwa shambani moja kwa moja baada ya shamba kuandaliwa, lakini pia zinaweza kurushwa shambani, kasha zikavurugwa pamoja na udongo. Unapaswa kutayarisha shamba la kupanda mtama, iwe ni kwa ajili ya malisho au chakula kabla mvua za msimu hazijaanza. Zao hili hufanya vizuri zaidi kwenye udongo ulio laini. Linaweza pia kupandwa kwenye udongo ambao haukulimwa vizuri na bado ukaota vizuri.


Nafasi:  Mtama unaopandwa kwa ajili ya malisho, unaweza kupandwa kwa nafasi ya sentimita 75×10. Aina za mtama ambazo zinalengwa kwa ajili ya lishe kwa binadamu na wanyama, zinahitaji nafasi kiasi cha sentimita 60×20. Nafasi hutoa mwanya wa kuwa na kiwango kikubwa cha malisho. 

         Mkulima anaweza kupanda mbegu za mtama kiasi cha kilo 2.4-3.3 kwa hekari moja. Ni mara chache sana mbegu hupandwa kwenye vitalu na kuhamishiwa shambani baadaye.


*Kupanda:* Mtama hupandwa mvua zinapoanza kunyesha. Mbegu ni lazima zifukiwe ardhini usawa wa sentimita 3 kwenda chini, hii itasaidia kuepuka kuota wakati ambao si msimu kamili wa mvua.  

          Pia zinaweza kufukiwa kiasi cha sentimita 2 wakati ardhi inapokuwa na unyevu. Mtama unahitaji rutuba ya hali ya juu wakati wa kupanda na wakati wa kuota. Ni vizuri kutumia samadi au mboji iliyooza vizuri wakati wa kuandaa shamba.


*Mseto*:  Unaweza kupanda mtama mseto na mazao jamii ya mikunde, na kuongeza mboji shambani mwako. Hii inaweza kuwa njia nzuri zaidi ya kupata virutubisho vinavyohitajika. Mseto wa mazao jamii ya mikunde inashauriwa iwe ni kama vile maharagwe, kunde, n.k


*Uangalizi na utunzaji*

       Ni lazima kung’oa baadhi ya mimea inapokuwa na urefu wa sentimita 30, au siku 30 baada ya kupanda, ili kuwa na uhakika wa nafasi ya sentimita 10 kati ya mstari na mstari kwa mtama unaokusudiwa kwa ajili ya malisho, na nafasi ya sentimita 20 kati ya mstari kwa mtama uliokusudiwa kwa ajili ya chakula na lishe ya mifugo.


          Palizi ya mkono ifanyike walau mara mbili. Shamba la mtama ni lazima liwekwe katika hali ya usafi na kutokuruhusu magugu wakati wote hasa katika kipindi cha mwanzoni.

*Mavuno*

       Mavuno huanzia Tani 12-35 kwa Hekta kutegemea Aina ya Mtama na Matunzo ya Shamba husika

UIMARISHAJI WA KIKUNDI

JIFUNZE KUPIKA SAMBUSA

Mahitaji

1. Unga wa ngano kilo 1

2. Nyama iliyosagwa kilo 1

3. Vitunguu maji nusu sado

4. Vitunguu saum vilivyosagwa kijiko 1 cha chakula 

5. Tangawizikijiko 1 cha chakula 

6. Chumvi kidogo

Hatua; Jinsi ya kutengeneza

1. Chukua nyama iliyosagwa injika jikoni pamoja na vitunguu saumu,tangawizi na chumvi 

kisha kanga hadi viwe rangi moja

2. Ipua halafu tia vitunguu maji kabla haijapoa na uchanganye vizuri

3. Chukua ngano na ukande manda,kisha katakata na uandae vichapati kwa ajiri ya 

kutengeneza vibahasha vya sambusa.kaanga hizo bahasha bila mafuta kisha kunja na 

tia mchanganyiko wako

4. Fungasha kwenye vibahasha vyako na ukaange sambusa zako kwenye mafuta yenye 

moto hafifu

ZIFAHAMU MBEGU BORA ZA MAHINDI

1.Mahindi WE4106

Aina hii ni mahindi chotara.

Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa

Bahari.

·Inakomaa Kwa wastani wa siku 106.

·Ina ukinzani wa magonjwa ya milia yamahindi (maize streak), bakajani kijivu wa   mahindi (grey leaf spot) na kutu yamajani (leaf rust).

·Inakoboleka vizuri (good poundability).

·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.8 kwa hekta.

·Inastahimili ukame.kangetakilimo


Ø Mahindi WE4102

·Aina hii ni mahindi chotara.

·Inastawi katika ukanda wa chini na katiwa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa

bahari.

·Inakomaa kwa wastani wa siku 105.

·Ina ukinzani wa magonjwa ya milia yamahindi (maize streak), bakajani kijivu

wa mahindi (grey leaf spot) na kutu yamajani (leaf rust).

·Inakoboleka vizuri (good poundability).

·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.7kwa hekta.

·Inastahimili ukame.kangetakilimo


Ø Mahindi WE4110

·Aina hii ni mahindi chotara.

·Inastawi katika ukanda wa chini na katiwa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa

bahari.

·Inakomaa kwa wastani wa siku 101 hadi 111.

·Ina ukinzani wa magonjwa ya milia yamahindi (maize streak), bakajani kijivu wa       majani (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).

·Inakoboleka vizuri (good poundability)kangetakilimo

·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.6 kwa hekta.

·Inastahimili ukame.


Ø Mahindi WE4114

·Aina hii ni mahindi chotara.

·Inastawi katika ukanda wa chini na katiwa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa

  bahari.

·Inakomaa kwa wastani wa siku 102.

·Ina ukinzani wa magonjwa ya milia yamahindi (maize streak), bakajani kijivu wa    mahindi (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).

·Inakoboleka vizuri (good poundability).

·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5.9 kwa hekta.

·Inastahimili ukame.


Ø Mahindi WE4115

·Aina hii ni mahindi chotara.

·Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa

   bahari.

·Inakomaa kwa wastani wa siku 104 hadi 112.

·Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), bakajani kijivu wa   mahindi (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).

·Inakoboleka vizuri (good poundability).

·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.4,kwa hekta.

·Inastahimili ukame.


Ø Mahindi WE4112

 ·Aina hii ni mahindi chotara.

·Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa

   bahari.

·Inakomaa kwa wastani wa siku 103.

·Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), Ukungu kijivu

  wa mahindi (grey Leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).

·Inakoboleka vizuri (good poundability)

·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.5 kwa hekta.

·Inastahimili ukame.


2. Kituo cha Utafiti Selian

Ø Mahindi  Selian H215

·Aina hii ni mahindi chotara.

·Inastawi katika mwinuko wa mita 800 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.

·Inakomaa kati ya siku 105 hadi 148.

·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5 kwa hekta.

·Inastahimili ugonjwa wa bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) hususan

katika maeneo ya kanda ya kaskazini


3. Kituo cha Utafiti Tumbi

Ø Mahindi T104

·Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV)

·Inastawi katika ukanda wa kati katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,500.

·Inakomaa kwa wastani wa siku 104 hadi 128.

·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 4.5 kwa hekta.


Ø Mahindi T105

·Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV)

·Inastawi katika ukanda wa kati katika mwinuko wa mita 600 hadi 1500.

·Inakomaa kwa wastani wa siku 103 hadi 129.

·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5.4 kwa hekta.


4. Aminata Quality Seeds & Consultancy Ltd


Ø Mahindi NATA H401

·Aina hii ni mahindi chotara.

·Inastawi katika ukanda wa chini na kati katika mwinuko wa mita 400 hadi 1,500.

·Inakomaa kwa wastani wa siku 120 hadi 130.

·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 7 kwa hekta.

·Inastahimili ugonjwa wa bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot), baka jani   (leaf blight) na kutu ya majani (leaf rust).

·Inakoboleka vizuri (good poundability).


Ø Mahindi NATA K 8

·Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV).

·Inastawi katika ukanda wa chini na kati katika mwinuko wa mita 0 hadi 1,600.

·Inakomaa kwa wastani wa siku 110 hadi 120.

·Inastahimili magonjwa ya bakajani wa mahindi (grey leaf spot), milia ( maize

streak virus) na ‘Turcicum blight’.

·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 4.9 kwa hekta.


5. Krishna Seed Company Ltd

Ø Mahindi Krishna Hybrid-1

·Aina hii ni mahindi chotara.

·Inastawi katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.

·Inakomaa kwa muda wa siku 128.

·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.9 kwa hekta.

·Inastahimili magonjwa ya majani wa ukungu kijivu wa mahindi (grey leafspot)  milia ya mahindi (maize streak virus).


Ø Mahindi Krishna Hybrid-2

·Aina hii ni mahindi chotara.

·Inastawi katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.

·Inakomaa kwa muda wa siku 134.

·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 7.6 kwa hekta.

·Inastahimili magonjwa ya ukungu kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na milia ya mahindi (maize streak virus).


6. Meru Agro-Tours & Consultancy Co. Ltd

Ø Mahindi MERU LISHE 503

·Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV).

·Aina ya mahindi lishe yaliyo na kiwango kikubwa cha viini muhimu vya protini.

·Hustawi katika mwinuko wa mita 800-1,200 kutoka usawa wa bahari.

·Inakomaa mapema kwa wastani wa siku99.

·Ina stahimili magonjwa ya bakajani kijivu wa mahindi(grey leaf spot)na milia ya mahindi ( maize streak virus).

·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 4.3kwa hekta.

·Inakoboleka kirahisi.


Ø Mahindi LISHE 511

·Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV).

·Aina ya mahindi lishe yaliyo na kiwango kikubwa cha viini muhimu vya protini.

·Hustawi katika mwinuko wa mita 800-1,200 kutoka usawa wa bahari.

·Inakomaa kwa muda wa wastani wa siku 98.

· Ina ukinzani wa magonjwa ya bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na

milia ya mahindi ( maize streak virus).

·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5.2 kwa hekta.

·Inakoboleka kirahisi.


6. IFFA Seed Company Ltd

Ø Mahindi Kaspidi hybrid

·Aina hii ni mahindi chotara.

·Hustawi katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.

·Inakomaa kwa muda wa siku 150 hadi siku 155.

·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.1 kwa hekta.

·Inastahimili magonjwa wa bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na milia ya mahindi (maize streak virus).


Ø Mahindi Kisongo hybrid

·Aina hii ni mahindi chotara.

·Hustawi katika ukanda wa mwinuko wa mita 600 had 1,200 kutoka usawa wa

bahari.

·Inakomaa katika siku 138.

·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.8 kwa hekta.

·Inastahimili magonjwa ya bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na milia ya   mahindi (maize streak virus).


Ushauri wa matumizi ya mbegu zilizoboreshwa unatofautiana kutoka eneo moja na lingine kwa sababu ya

v  Mwinuko kutoka usawa wa bahari

v  Kiasi cha mvua katika eneo husika

v  Muda unaotumia mbegu

v  hadi kukomaa


August 01, 2018

IFAHAMU HISTORIA YA VICOBA

 1. VICOBAmaana yake ninini? maana yake ninini? maana yake ninini? 

Jibu. VICOBA maana yake ni Village Community Bank na iki Jibu wa na maana ya Kiswahili 

ya Benki ya jamii vijijini. Mfumo huu unatekelezwa kwa kuanzishwa kikundi kutokana na 

watu au wanajamii wanaoishi eneo moja na kama siyo mtaa mmoja basi kijiji kimoja na 

hii husaidia sana uendeshaji wa kikundi husika. 

2. Mfumo wa Mfumo wa VICOBAulianza lini Tanzania na athiri yake ni wapi? ulianza lini Tanzania na athiri yake ni wapi? ulianza lini Tanzania na athiri yake ni wapi? 

Jibu. Mfumo wa VICOBA kwa mara ya kwanza ulianzishwa mwaka Jibu. 2002 mwezi wa 

kumi. Mfumo huu ulianzishwa na shirika la kidini lijulikanalo kwa sasa kwa jina la IRCPT 

na kwa kipindi hicho lilikuwa linajulikana kwa jina la WCRP. WCRP walianzisha mfumo 

huu baada ya kwenda kujifunza Zanzibar ambako CARE International walikuwa 

wanatekeleza mradi wa Jozani saving and credity association (JOSACA). Watendaji 

wa WCRP baada ya kujifunza mfumo wa JOSACA kwa kina na kutokana na uzoefu 

wao wa uendeshaji wa shughuli za kifedha wakaamua kubadilisha jina na kuita mfumo 

wa VICOBA. 

Mfumo huu kwa mara ya kwanza ulianzishwa eneo la Ukonga na kisarawe ambapo 

vikundi kumi vilianzishwa na ndivyo vikundi vikongwe kuliko vikundi vyovyote hapa 

Tanzania na kwa bahati nzuri vikundi hivi bado vipo hai. Mfumo huu baada ya 

kuonyesha mafanikio makubwa Ukonga na Kisarawe serikali na mashirika mbalimbali 

ya kimaendeleo yaliweza kutembelea Ukonga na kujifunza na kila aliyejifunza aliamua 

kwenda kuanzisha vikundi katika maeneo ya mradi wake. 

Asili ya Mfumo wa VICOBA ni mfumo wa MMD ambao kwa mara ya kwanza 

ulianzishwa nchini Niger na kwa jina la Mata Masu Dubara (MMD). MMD ni jina la 

kihausa na kwa Kiswahili inamaanisha ni akina ma akina ma akina mama katika harakati za maendeleo ma katika harakati za maendeleo ma katika harakati za maendeleo. 

Mfumo huu umekuwa na majina mengi kwa kila nchi kuamua kuita majina kutokana na 

miradi ya kimaendeleo wanayoitekeleza. Mfano mfumo huu Uganda unajulikana kwa 

jina la JENGA, Msumbiji unajulikana kama OVAPHERA na zimbambwe KI. Hata hivyo 

kila nchi ambako mfumo huu unatekelezwa kuna mamboresho mbalimbali yamefanyika

[8/1, 11:16 PM] Omben ebusol: na hapa ndipo unapo kuja kuona mfumo wa VICOBA unatofauti ya kiutekelezaji na 

uendeshaji wake na mfumo wa JOSACA, VSLA, SILC, VITOVU na mifumo mingine. 

Mfumo wa VICOBA wenyewe katika utekelezaji wake nao umetofautiana baina ya 

wadau mbalimbali ambao wapo katika mfumo huu na hii ni changamoto kwa wadau 

wote wa VICOBA ambao wanahitajika kukaa pamoja na kujadili jambo hilo.