January 06, 2019

8.WAZO LA BIASHARA: UVUNAJI NA UUZAJI WA MKOJO WA SUNGURA

Ufugaji wa Sungura umekuwa ukiendelea kushamiri sehemu Mbali Mbali za Dunia kutokana na kuwa na bidhaa nyingi zitokanazo na ufugaji huo

Bidhaa hizo in kama

(a) Nyama

(b)Mkojo

(c)Ngozi

(d)Samadi

Licha ya kutumika Kama mapambo na baadhi ya nchi, Sungura aina ya Angola wamekuwa wakitumika kama chanzo cha Sufi kutokana na manyoya yao kuwa mengine

Mradi wa ufugaji Sungura umekuwa ni mradi pekee ambao unawekeza Leo na kuanza kuvuna Leo,leo (Mkojo na samadi)

Licha ya kuwa wafugaji wengi wamekuwa wakifuga kwaajili ya nyama, zao la Mkojo wa Sungura kwa faida yake pengine no kubwa kuliko mazao mengine yote.


Matumizi ya Mkojo wa Sungura kama mbolea;-

Kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha madini ya nitrogen phosphorus na potassium mbolea ya Mkojo wa Sungura imekua mbadala wa mbolea za NPK na CAN ambazo kwa kiasi kikubwa zimekua zikichangia ongezeko la soil acidity

Ikitumika katika ratio ya lita moja ya Mkojo wa Sungura kwa lita 5 za maji kunyunyuzia katika majani au ardhi wakati wa asubui au jioni kipindi ambapo stomata zipo wazi itakupa matokeo mazuri katika viazi,maharage,

miche ya matunda, mbogamboga, mahindi na mazao mengine

Lakini pia Kama kimiminika cha asili chenye uwezo wa kurudisha rutuba iliyopotea ardhini

Matumizi ya Mkojo wa Sungura Kama kiuatirifu (insecticides)

Mkojo wa Sungura una,kiasi kikubwa cha Ammonia ambayo ndio makali yake halisi ambayo Uharibu kabisa mazingira rafiki ya uzalianaji wa bacteria na fangasi katika mmea

Mkojo wa Sungura ukitumika kwa kiasi cha lita 1 katika Lita 2 za maji kunyunyuzia katika majani ambayo yameshambuliwa na wadudu kila siku,huua wadudu na kurejesha afya ya mmea

Mkojo wa Sungura huua wadudu kama aphids,fungus, mites ,leaf miners nk

Katika mmea ambao haujashambuliwa, ukinyunyuzia kwa wiki Mara,moja inatosha kuupatia mmea afya bora,ustahimilivu wa magonjwa ya bacteria na fangasi pia kukupatia mavuno mengi.

January 03, 2019

NAMNA YA KUJENGA BUSTANI YA GUNIA



UTUNZAJI WA KITALU CHA BUSTANI

Na Ombeni Haule cdf

Baada ya kuandaa kitalu hakikisha unakitunza vizuri ili kuweza kupata miche bora ya kupandikiza shambani. Matunzo ya kitalu hujumuisha mambo yafuatayo;

Kujengea kichanja/Kivuli (Shading)

Umwagiliaji

Kupiga dawa za wadudu na magonjwa

Kupunguzia miche na

Kuitayarishaji miche kabla ya kuipandikiza.

(a) Kujengea kichanja / Kivuli

Mbegu zitakapoota ondoa matandazo na tengeneza kichanja chenye kimo cha mita 1 kutoka ardhini kilichotandazwa nyasi au makuti kufunika kitalu. Kichanja hiki hutengenezwa ili kuipa kivuli miche ambayo bado ni michanga isije kuungua na mionzi ya jua na kushindwa kukua vizuri. Vilevile kichanja husaidia kupunguza kasi ya matone ya mvua kubwa ili miche isijeruhiwe.

(b) Umwagiliaji

Mwagilia maji kitaluni kila siku asubuhi na jioni hadi wakati wa kutayarisha miche. Ni vyema kuzingatia uwezo wa udongo kutunza maji ili kuepuka kuzidi kwa kiwango cha maji kunakoweza kupelekea kudumaa kwa miche kitaluni na kuchelewesha upandikizaji.

(c) Kupunguzia miche

Punguza miche kitaluni ili kuondoa msongamano wa miche na kubaki na miche itakayoweza kukua vizuri kwa nafasi. Hili ni muhimu hasa kwa miche yenye majani mapana kama vile miche ya nyanya na kabichi. Miche ya kabichi hupunguziwa siku nne hadi wiki moja tangu mbegu kuota wakati miche ya jamii ya nyanya hupunguziwa baada ya wiki moja tangu kuota kwa mbegu. Miche iliyopunguzwa katika tuta moja inaweza kuhamishiwa katika tuta lingine.

(d) Kupiga dawa za Wadudu na Magonjwa

Unaweza kuanza kunyunyizia dawa za ukungu na kuua wadudu wiki moja hadi mbili tangu miche kuota. Chagua dawa kulingana na wadudu waharibifu na magonjwa yanayo shambulia zao husika. Hakikisha unafuata maelekezo ya dawa husika.

(e) Kuitayarisha miche (Acclimatization)

Miche hutayarishwa ili isipate tabu kuzoea hali ngumu ya shambani na hivyo kupona haraka inapopandikizwa. Utayarishaji wa miche hufanywa kwa kupunguza matandazo ya nyasi katika kichanja polepole kuanzia wiki mbili kabla ya kupandikiza. Ondoa kivuli chote na punguza kiwango cha maji ya kumwagilia wiki moja kabla ya kupandikiza ili kuiwezesha miche kuzoea hali ya ukame.

Zingatia: Usichelewe kupandikiza miche kwa sababu miche mikubwa ni vigumu kuihamisha na mizizi yake ni mirefu hivyo inaweza kukatika kwa urahisi. Pandikiza miche ikiwa na mizizi iliyozungukwa na udongngo

December 31, 2018

TENGENEZA DONAT YA ICING SUGAR

Mahitaji :


Unga – Mug 1

Sukari 1/3 kikombe ( mug ) 

Mayai  5

Siagi - 4 Vijiko vya kulia

Hamira  1 Kijiko kulia

Baking Powder - 1 Kijiko cha chai

Vanilla - 1 Kijiko cha chai

Hiliki zilizosagwa -  1 Kijiko cha chai

Sukari ya laini ya unga (icing sugar) mug 1


Maelezo : 


Kwenye bakuli pana vunjia mayai, unatia sukari, hamira, baking powder, vanilla na hiliki ikisha unapiga kwa kutumia mchapo wa kupigia keki ama mwiko kwa nguvu. Unapiga mchanganyiko kwa muda wa dakika tano. Weka siagi kwenye sufuria na yeyusha na kuipasha moto mpaka iwe moto ikisha unaimimina kwenye mchanganyiko  na unapiga tena kwa dakika mbili tu. Weka unga kwenye sinia au bakuli kubwa ikisha unamimina ule mchanganyiko kwenye unga na unaukanda kutumia mkono, mpaka ulainike.Ukiona unga mwingi basi ongeza maziwa kidogo mpaka uwe sawa, na ukiona unga mwepesi sana basi unaweza kuongeza unga kidogo pia mpaka ukae sawa mfano wa unga wa maandazi.Sukuma na ukate madonge kama unavyoyaona hapo juu. Tumia kifuniko cha chupa kwa kukatia kiduara kidogo katikakati ya madonge. Ukimaliza kukata madonge yote, yaweke kidogo yaumuke halafu teleka mafuta na uyakaange.

Ukitoa kwenye mafuta yachuje mafuta na kabla ya kupoa yawe moto moto yachovye kwenye icing sugar na uhakikishe yote yameenea sukari juu. Ukimaliza tia kwenye sahani acha zipowe na zitakuwa tayari kwa kuliwa.


BY MAPISHI RAHISI NA FASTA FASTA.

10.WAZO LA BIASHARA: UTENGENEZAJI WA KATLESS

 KACHORI  HUTUMIKA KAMA KITAFUNWA KWAJILI YA PICNIC, CHAI YA ASUBUHI AU SAA 10 JIONI HUPENDWA SANA NA WATU WA LIKA ZOTE. KACHOLI HII NI MAALUMU KWA WALE WENYE MATATIZO WASIOTUMIA UNGA WA NGANO.

MAHITAJI

300 gram nyama ya kusaga

1 kilo ya viazi ulaya (5-6)

1 kijiko cha chakula Mafuta ya kupikia

½ kijiko kidogo cha chai Cumin seeds (Jeera) 

1 ½ kijiko kidogo cha chai Coriander powder (Dhaniya) 

2 pili pili mbuzi au ndefu za kijani 

1 ½ Tangawizi mbichi

¼ Kijiko cha chai Garam Masala

4 kijiko kikubwa cha chakula maji ya limao au ndimu

 ½ chumvi

10 gram kitunguu swaumu

5 mayai ya kuku

Mafuta kwajili ya kukaangia

JINSI YA KUTENGENEZA

Chemsha viazi kwenye pressure cooker au sufuria vikiwa na maganda yake.

Chemsha nyama ya kusaga na maji 50 gram, kitunguu swaumu 10 gram na vijiko 4 vya mai ya limao mpka iive kisha weka pembeni.

Kisha menya viazi ulivyochemsha kisha kata katika vipande vidogo. Pasha mafuta ya kupikia kijiko kimoja kwenye kikaango.

Kisha weka mbegu za cumin kwenye kikaango. Mbegu za cumin zikishapasuka, ongeza coriander powder, pili pili mbuzi, Tangawizi, Kisha weka chumvi na viazi. Kaanga kwa dakika 2-3 itakua imeiva vizuri.

Kisha ponda mchanganyiko wako mpaka uwe laini kabisa

Kisha chukua mchanganyiko huo laini wa viazi na tengeneza maumbo madogo ya mviringo ukubwa kama limao kisha bonyeza kwa kutumia kidole kati kati ya umbo hilo utapata nafasi ya kuweka kijiko kimoja cha chai nyama ya kusaga iliyoiva kisha funika kwa kutumia viazi na jitaidi kuviringisha tena kwa kutumia mikono yako miwili ili upate umbo zuri.

aada ya kumaliza kuandaa maumbo safi kabisa ya duara na yenye nyama ya kusaga kwa ndani, piga mayai pembeni kwenye bakuli na chovya umbo moja moja na weka kwenye kikaango chenye mafuta ya moto kaanga ukishapata rangi tu ya kahawia toa maana viazi na nyama vimeshaiva unachotafuta ni kau kau na rangi safi ya kahawia pande zote.

MPATIE MLAJI KACHORI HII IKIWA YAMOTO PIA UNAWEZA USIWEKE PILI PILI NA TANGAWIZI HASA KWA WALE WANOSUMBULIWA NA VIDONDA VYA TUMBO AU MATATZIZO YA GESI TUMBONI NA BADO KACHORI YAKO IKAWA SAFI SANA. UNAWEZA KULA NA TOMATO SAUCE, MAYONAISE, CHACHANDU AU ACHALI.

*From Alhidaaya*

10. WAZO LA BIASHARA: UTENGENEZAJI WA KEKI

Hakuna kitu chochote kitamu chenye harufu na radha nzuri kama keki uliyoipika kwa mikono yako. Upishi wa keki ni mwepesi sana endapo mpishi atazingatia vitu muhimu vinavyohitajika pamoja na hatua zake. 


*MAHITAJI*

*unga vikombe2

*maziwa kikombe1

*sukari kikombe1

*siagi kikombe1

*baking powder vijiko vidogo 2

*mayai 6 yakienyeji

*vanilla matone mawili au limao 1 Zingatia Limao au vanilla hutumika kwaajili ya kupunguza harufu ya mayai kwenye keki.kwahiyo ukikosa vanilla pia waweza kutumia maganda ya limao au maganda ya chungwa. 


Pia andaa jiko lako la mkaa mapema ili lipate joto pamoja na sufuria iliyopakwa siagi ndani ili kuzuia keki kuganda.


*HATUA*

*Andaa bakuli lako la udongo na mwiko ambao utatumia kuchanganya mchanganyiko wako


*chukua kikombe kimoja cha siagi na utie katika bakuli pamoja na kikombe kimoja cha sukari.


*koroga mchanganyiko wa sukari na siagi mpaka pale utakapolainika na chembe chembe za sukari kupotea kabisa


*Weka yai moja baada ya jingine huku ukiendelea kuukoroga mchanganyiko wako bila kupumzisha mkono


*Weka matone mawili ya vanilla au maganda ya limao huku ukiendelea kuchanganya.


*Weka unga vikombe viwili uliochanganywa na baking powder kwenye mchanganyiko wako na endelea kuukoroga taratibu


*Baada yahapo tia maziwa kikombe kimoja nauchanganye taratibu


*Mimina taratibu mchanganyiko wako kwenye sufuria maalumu yakupikia iliyopakwa siagi. 


Zingatia Iwapo utapenda keki yako iwe na rangi unaweza ukaweka kokoa kwenye mchanganyiko wako.


*Weka sufuria ya mchanganyiko katika jiko lenye joto la wastani kwa muda wa nusu saa

Yani makaa juu na chini


*Baada ya hapo toa keki yako tayari kwakuliwa.

December 30, 2018

*JINSI YAKUTUMIA MBEGU ZA MABOGA, FAIDA ZAKE,NA JINSI GANI UNAWEZA KUTUMIA MBEGU ZA MABOGA KAMA DAWA*

*MAGONJWA HATARI 10 YANAYOTIBIKA KWA KUTUMIA MBEGU ZA MABOGA*


*UTANGULIZI*

- Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya muhimu zaidi mwilini kama madini ya zinki, kopa, maginizia, manganizi na chuma, mbegu za maboga ni tamu na zinaweza kutafunwa nyakati zozote na mahali popote.


- Tafiti mbalimbali zimethibitisha pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida nyingi kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10 yafuatayo:


*1- UGONJWA WA MOYO*

- Kiasi kingi cha madini ya magnesium katika mbegu za maboga yanazifanya mbegu hizi kuwa mhimu sana kwa watu wenye magonjwa mbalimabli ya moyo.


- Madini ya magnesium ni mhimu kwa ajili ya kuimarisha msukumo wa damu kwenye moyo na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hatimaye kutibu na kuzuia magonjwa ya moyo.


- Mbegu hizi pia zina mafuta mengine mhimu zaidi kwa watu wenye ugonjwa wa moyo yenye *OMEGA 3*


*2- HUIMARISHA KINGA YA MWILI*

- Mbegu za maboga zimebarikiwa kuwa na kiasi cha kutosha cha madini ya zinki (zinc). Kazi kubwa ya madini ya zink ni kuimarisha kinga ya mwili.


- Upungufu wa madini ya zink unaweza kupelekea matatizo kadhaa mwilini ikiwemo kuzaa watoto njiti, kuishiwa nguvu za kiume, matatizo ya homoni, chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo shuleni kimasomo na matatizo mengine kadhaa ya kimwili na kiakili.


*3- HUONGEZA UWEZO WA MACHO KUONA*

- Mbegu za maboga zina Vitamini E, vitamini A, lutein, beta-carotene na zeaxanthin, vitu hivi vinavyopatikana katika mbegu za maboga ni mhimu kwa ajili ya nuru ya macho. Vitamini A na madini ya zinki ni mhimu kwa ajili ya uzalishaji wa ‘melanin’ kimeng’enya mhimu ambacho hutengenezwa kwa asili na miili yetu kwa ajili ya ulinzi wa afya ya macho.


*4- KINGA YA KISUKARI*

- Kisukari ni moja ya ugonjwa unaoendelea kwa kasi na kuwasumbua watu wengi kila pembe ya dunia.


- Mbegu za maboga zina vitu vitatu mhimu zaidi ambavyo ni *Nicotinic acid’,* *‘Trigonelline’* na *D-chiro-inositol’* ambavyo husaidia kushusha damu sukari mwilini na kudhibiti kazi za *insulini* hivyo kuwa kinga na kuleta ahueni kubwa kwa watu wenye kisukari.


- Kama unasumbuliwa na kisukari fanya mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku.


*5- DAWA BORA YA USINGIZI*

- Mbegu hizi zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha homoni za usingizi.


- Kwenye mbegu za maboga kuna vimeng’enya viwili mhimu zaidi ambavyo huhusika na usingizi na afya ya akili moja kwa moja navyo ni *‘L-tryptophan’ na ‘tryptophan’.* Gramu 100 tu za mbegu za maboga zina kiasi cha kutosha cha *tryptophan’* mpaka mg 576. Tryptophan ndiyo inahusika kuleta usingizi wenye utulivu pia huondoa msongo wa mawazo au stress mwilini.


- Kwa kuongezea mbegu za maboga zina kiasi kingi cha vitamini za kundi B. Muda mchache kabla ya kwenda kulala tafuna mbegu za maboga na utapata usingizi mtulivu kabisa mpaka asubuhi.


- Kwahiyo kama una tatizo la kukosa usingizi jaribu kutumia mbegu za maboga


- Kumbuka kukosa usingizi mara nyingi huwa ni matokeo ya msongo wa mawazo na kama ulivyoona mbegu hizi zinaondoa pia stress!


*6- DAWA BORA YA UVIMBE*

- Mbegu za maboga zinao uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini sambamba na uvimbe *(inflammation).* Kama ujuavyo sehemu kubwa ya vivimbe mwilini ni matokeo ya sumu kadhaa mwilini.


-  Mbegu za maboga zitakuondolea uvimbe mwilini bila kukuachia madhara yoyote mabaya hapo baadaye.


- Kama unasumbuliwa na uvimbe popote jaribu kutumia mbegu za maboga


- Mbegu za maboga pia ni dawa nzuri kwa aina nyingi za kansa mwilini.


*7- HUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAYENYONYESHA*

- Mbegu za maboga zina protini nyingi bora itokanayo na mimea isiyo na madhara kama ile ya kwenye wanyama.


- Pia zina *OMEGA 3* Mama mjamzito hata unayenyonyesha tumia mbegu za maboga na utakuwa na uhakika wa kutoa maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto.


*8- DAWA NZURI KWA MATATIZO YA TEZI DUME*

- Wataalamu wengi wa lishe wanapendekeza mbegu za maboga zitumike kwa wanaume wa rika zote yaani vijana hadi wazee kwani zimethibitika kuwa msaada mkubwa kwa afya ya tezi dume.


- Tafiti nyingi zinasema mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya Zinki madini ambayo ni mhimu *SANA* kwa afya ya tezi dume na husaidia uponyaji wa tatizo la tezi dume moja kuwa kubwa kuliko nyingine tatizo lijukanalo kwa kitaalamu kama *benign prostatic* *hyperplasia’.*.


*9.- ZINAONGEZA NGUVU ZA KIUME*

- Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado.


- Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo/stress kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, lakini pia zinashusha lehemu *(cholesterol),* zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), zinashusha kisukari, zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya zaidi ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili na Zina madini ya chuma pia


- Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote, ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ukiwa ofisini unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako. Sambamba na hilo kama tulivyoona pale juu kwamba zinaongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha kwa upande wa wanaume zinaongeza pia uwingi wa mbegu za kiume *(sperm count)* ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utapata kuona matokeo mazuri.


*10- ZINAONDOA PIA MSONGO WA MAWAZO (STRESS)*

- Msongo wa mawazo au stress kama mlivyozoea wengi ni tatizo linaloendelea kuwasumbua watu wengi miaka ya sasa. Mbaya zaidi wengi huwa hawaelewi nini madhara ya hizo stress wanazojipa. Yaani stress au msongo wa mawazo unaweza kukuletea magonjwa mengine mwilini zaidi ya 50, hivyo utaona ni jinsi gani ilivyo mhimu kwako kuweka chini stress zako na uendelee na maisha kwani kuendelea kuwa na stress ni hatari zaidi kwa afya yako.


- Moja ya sababu kuu ya watu wengi kuwa na stress ni usawa usio sawa wa homoni zao *(hormonal imbalance)*


- Hivyo kama una tatizo la homoni kwenye mwili hebu weka mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na hutakawia kuona tofauti.


-  Mbegu za maboga zina kimeng’enya mhimu sana kwa kutuliza mawazo kiitwacho *‘tryptophan’* na asidi amino zingine mhimu zinazohusika kutengenezwa kwa homoni nyingine ijulikanayo kama *‘serotonin’*.


- Kama ulikuwa hujuwi ni kuwa *serotonin* ni homoni inayohusika na kazi mhimu sana ya kurekebisha matendo ya kitabia na kutoa matokeo chanya kwa mambo yanayohusu usingizi, hali ya mawazo kwa ujumla na mambo yanayohusu njaa.


- Mbegu za maboga ni msaada mkubwa kwa kina mama waliofikia ukomo wa siku zao na huondoa matatizo ya kiafya yatokanayo na kukoma kwa hedhi.


- Ni msaada kwa watu wenye saratani mbalimbali, huimarisha ukuaji na ustawi wa mifupa na meno, huondoa harufu mbaya ya kinywa na husaidia pia wenye tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara.

*NAMNA NZURI YA KULA MBEGU ZA MABOGA*


- Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa wengi wanapenda zilizo kaangwa



- ukikaanga isizidi dk15 - 20 hivi na huwa nazichanganya na maji ya chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.


- Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga kwa siku ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kwa siku.