Mahitaji :
Unga – Mug 1
Sukari 1/3 kikombe ( mug )
Mayai 5
Siagi - 4 Vijiko vya kulia
Hamira 1 Kijiko kulia
Baking Powder - 1 Kijiko cha chai
Vanilla - 1 Kijiko cha chai
Hiliki zilizosagwa - 1 Kijiko cha chai
Sukari ya laini ya unga (icing sugar) mug 1
Maelezo :
Kwenye bakuli pana vunjia mayai, unatia sukari, hamira, baking powder, vanilla na hiliki ikisha unapiga kwa kutumia mchapo wa kupigia keki ama mwiko kwa nguvu. Unapiga mchanganyiko kwa muda wa dakika tano. Weka siagi kwenye sufuria na yeyusha na kuipasha moto mpaka iwe moto ikisha unaimimina kwenye mchanganyiko na unapiga tena kwa dakika mbili tu. Weka unga kwenye sinia au bakuli kubwa ikisha unamimina ule mchanganyiko kwenye unga na unaukanda kutumia mkono, mpaka ulainike.Ukiona unga mwingi basi ongeza maziwa kidogo mpaka uwe sawa, na ukiona unga mwepesi sana basi unaweza kuongeza unga kidogo pia mpaka ukae sawa mfano wa unga wa maandazi.Sukuma na ukate madonge kama unavyoyaona hapo juu. Tumia kifuniko cha chupa kwa kukatia kiduara kidogo katikakati ya madonge. Ukimaliza kukata madonge yote, yaweke kidogo yaumuke halafu teleka mafuta na uyakaange.
Ukitoa kwenye mafuta yachuje mafuta na kabla ya kupoa yawe moto moto yachovye kwenye icing sugar na uhakikishe yote yameenea sukari juu. Ukimaliza tia kwenye sahani acha zipowe na zitakuwa tayari kwa kuliwa.
BY MAPISHI RAHISI NA FASTA FASTA.
No comments:
Post a Comment