October 31, 2018

MCHANGANUO WA KUFUGA KUKU WAKIENYEJI

*MAHITAJI*

1- Tetea 10 kwa jogoo 1

2- Banda bora

3- Vyombo vya chakula na maji

4- Chakula bora

5- Madawa na chanzo cha nishati joto na mwanga

6- Elimu na ujuzi wa malezi bora

7- Chombo au chumba cha kutunzia vifaranga

8- Mayai ya kuku wa kisasa/mayai mabovu(ambayo hayakuanguliwa)

9- Madaftari au kitabu cha kutunzia kumbukumbu


*KUKU 10*

1- Wakati wa kuanza mradi wako hakikisha una kuku 10 *(matetea)* wenye umri sawa na hawajawai kutaga hata mara moja.


2- Chagua kuku wenye rangi nzuri kutoka katika familia bora kutegemea malengo ya mradi wako.


3- Mfano kama lengo lako ni kuzalisha kuku wa kienyeji kwajili ya nyama basi chagua mbegu ambayo inakuwa haraka na yenye uzito mkubwa.


4- Au ikiwa lengo ni mayai basi ni vema kuchagua aina ya kuku yenye kukua haraka na kutaga mayai mengi.


5- Ili kupunguza gharama za manunuzi ya kuku na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji ni vema kununua kuku wadogo ambao wametoka tu kuachishwa kulelewa na mama zao.


6- Kuku hawa utawapata kwa bei ya chini, tena watafaa sana maana watakua na umri mmoja pia.


*JOGOO 01*

1- Jogoo mmoja tu anatosha kuwahudumia kuku matetea yote kumi.


2- Hakikisha katika uchaguzi wa jogoo bora lililochangamka, rangi mzuri, upanga umesimama, macho angavu, uzito wa kutosha, rangi nzuri na uwezo mkubwa wa kuzalisha.


3- Ni vema mfugaji akaelewa kwamba kuku wote watakaozalishwa watategemea ubora wa jogoo wake.


4- Uwezo wa kutaga kwa kuku na upatikanaji wa mayai pia hutegemea kwa karibu ubora wa jogoo aliyechaguliwa.


*BANDA BORA*

1- Miongoni mwa mambo mhimu naya kwanza kuzingatiwa katika ufugaji wa kuku wa kienyeji kama mradi ni maandalizi ya banda bora.


2- Kuku huhitaji banda bora ili wasiathirike na madhara mbalimbali.


3- Mfugaji anatakiwa kuandaa banda lenye ukubwa wa mita 10 kwa mita 04.


4- Yani urefu uwe mita 10 na upana upana wa mita 04. Kisha kata vyumba vya mita 2 urefu na upana mita 4 kutoka katika banda lako hivyo utakuwa na jumla ya vyumba vitano vyenye ukubwa unaolingana.


5- Ujenzi uzingatie malighafi na vifaa vinavyopatikana kwa urahisi katika mazingira husika.


 Mfano katika maeneo ambayo fito zinapatikana kwa urahisi banda linaweza kuandaliwa kwa miti na kukandikwa kwa udongo.


6- Au sehemu ambayo mabanzi hupatikana kwa urahisi basi banda laweza kujengwa kwa kutumia mabanzi.


7- Vifaa vya kujengea banda vizingatie pia gharama na upatikanaji wake katika eneo husika.


*Baadhi ya vifaa hivyo ni kama ifuatavyo:-*

1- *Sakafu*

√Saruji

√udongo

√mbao

√mianzi/fito


*Kuta*

√Fito/mabanzi mbao,

√nguzo mianzi

√udongo,

√matofali,

√mawe

√mabati

√wavu


*Paa*

√Nyasi

√makuti

√majani ya migomba

√mabati/vigae.


*Wigo*

√Matofali

√mbao

√fito/nguzo

√mabanzi/mianzi

√matete, wavu na mabati


*Banda bora la kuku linatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-*


*Imara*

1-/Lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na pia dhidi ya hali ya hewa hatarishi kwa mfano jua kali, upepo, baridi na mvua pamoja na wanyama hatari.


2- Lenye mwanga, hewa na nafasi ya kutosha inayoruhusu usafi kufanyika kwa urahisi.


3- Lijengwe sehemu yenye mwinuko isiyotuama maji, isiyo na upepo mkali na iwe mbali kidogo na nyumba ya kuishi watu.


4- Liwe na vichanja kwa ajili ya kuku kupumzika na kulala


5- .Liwe na sehemu ya kuwekea chakula, maji, kutagia, kuatamia na sehemu ya kulelea vifaranga.


6- Liwe na nafasi ya kutosha kulingana na idadi ya kuku na kuweka vyombo vya chakula na maji.


7- Kwenye mazingira ya joto banda liwe la ukuta mfupi na sehemu kubwa wazi yenye wavu hadi kufikia kwenye paa.


8- Kwenye mazingira ya baridi banda liwe na ukuta mrefu unaokaribia paa na sehemu ndogo tu iwe wazi yenye wavu ili kupitisha hewa na mwanga.


*JINSI YA KUFANYA*

1- Wakuze kuku wako hadi watakapofikia muda wa kutaga.


2- Wakianza kutetea ni kiashiria kwamba wakati wa kutaga umekaribia hivyo andaa viota kwajili ya kutagia.


3- Viota vinapaswa viwe na ukubwa stahiki ili kumwezesha kuku kuyafunika mayai yote vizuri wakati wa kuatamia, viota viwe vinavyozuia mayai kutawanyika, viwe mahali pakavu na safi.


4- Hakikisha kuku wote wanataga katika viota tofauti.


5- Kuku anapotaga mayai matatu unapashwa kuchukua mayai mawili na kumwachia yai moja ili kumfanya aendelee kutaga zaidi.


6- Kuku akifikia yai la kumi na mbili anza kumwachia mayai matatu ili kumwandaa kwa kazi ya kuetamia.


7- Kwa kufanya hivi, kuku atataga mayai 15 au zaidi na ikiwa atataga mayai 15 au chini ya hapo nakushauri utafute mayai mengine ujazilizie ili kufikisha mayai 20 kwa kila kuku.


 *Zingatia kwamba mayai unayoyatoa kwa kila kuku, yanatunzwa sehemu salama, mahali pakavu, pasafi na penye joto la wastani*


8- Kuku wote wanapaswa kuanza kuatamia kwa siku moja. Ili kufanikisha hili inapasa uwe karibu na kuku wako.


9- Kuku mmoja akianza kuatamia mwekee mayai ya kuku wa kisasa au mayai mabovu ya kuku wa kienyeji.


10- Utafanya hivi hadi kuku wako wote watakapoanza kuatamia mayai.


11- Kuweka mayai mabovu au mayai ya kuku yaliyotumika humfanya kuku aendelee kuatamia akijua ni mayai yake.


12- Baada ya kuona kwamba kuku wako wote wapo tayari kwa kuatamia mayai, waandalie banda maalumu kwajili ya kuatamia yani chumba kimoja katika lile banda letu.


13- Ninashauri kwamba chumba kwajili ya kuatamia kiwe chumba cha kwanza au cha mwisho katika mfuatano wa vyumba vya banda lako. Andaa viota bora vya kuatamia, weka mayai 20 kwa kila kiota, ikiwa hayajatimia unaweza kununua kwa wafugaji wengine ili kuifikia idadi yako.


14- Waamishe kuku kutoka wanapotagia na kuwaweka katika chumba ulichokiandaa kwajili ya kuatamia.


15- Ili ufanikiwe katika zoezi hili inafaa lifanyike wakati wa usiku na unafanya katika giza.


16- Mweke kuku katika kila kiota na asubuhi wajikute kila mmoja katika kiota chake.


17- Wahudumie kwa chakula na maji ya kutosha. Wakati wa usiku waongezee joto la ziada kwa kuweka jiko au ndoo ya chuma yenye chengachenga za mkaa au kama una umeme weka taa za joto.


28- Baada ya siku 21-25 kuku wako wataanza kuangua vifaranga.


29- Huu ndio wakati unaotakiwa kuwa karibu sana na kuku wako kuliko wakati wote.


30- Watenge vifaranga mara tu baada ya kuanguliwa; waweke katika chumba chao maalumu mbali na kuku.


31- Kama chumba cha kuatamia kilikuwa cha kwanza basi vifaranga wawe chumba cha mwisho n.k


32- Ukishawatenga vifaranga mbali na matetea wako, wawekee tena mayai mengine 20 kila tetea, mayai ambayo utayanunua kwa wafigaji wenzako.


33- Hakikisha kuku waliotaga hayo mayai ni wazuri, hawana magonjwa na wanauzito/ukubwa unaofaa.


34- Mayai yote yakaguliwe vizuri ili kujua kwamba yameharibika, yana nyufa au mabovu. Kabla ya kuweka mayai mengine hakikisha chumba chako ni kisafi na viota vimesafishwa, havina wadudu na uchafu wowote.


35- Kuku wako bila kujijua wataanza kuetamia upya mayai uliowawekea.


36- Ukiwawekea mayai rudia mzunguko kama nilivyokwambia awali.


37- Baada ya siku 21 hadi 25 tena utapata vifaranga wako wengine tena. Fuata kila hatua kama nilivyokwambia hapo awali. Lakini kwa awamu hii nashauri waache matetea wako wapumzike wala usiwapatie mayai mengine tena.


*JINSI YA KULEA VIFARANGA*

1- Ikikaribia siku ya 20 tangu ulipowawekea matetea wako mayai katika chumba cha kuetamia, andaa chumba kwa ajili ya kulea vifaranga


2- Safisha kwa kuondoa uchafu na wadudu wote.


3- Washa taa ya joto au weka chombo cha kutoa joto katika chumba cha vifaranga nusu saa kabla huja anza kuingiza vifaranga wako. Weka pia chakula na maji ya kutosha katika vyombo vyenye umbile na ukubwa utakaowawezesha vifaranga kuvitumia


4- Tandaza magazeti, maboksi, makaratasi n.k katika sakafu ya chumba hicho. Hakikisha vifaranga wako hawajikusanyi sehemu moja maana wakifanya hivyo wengi wao watakufa ili ufanikiwe katika jambo hili, banda lako liwe la mduara katika kona zake.


5- Weka joto la kutosha. Joto la kutosha ni lile linalowafanya vifaranga watawanyike chini ya chanzo cha joto wakati kama joto limezidi vifaranga kukimbia mbali na chanzo cha joto na ikiwa joto halitoshi vifaranga hujukusanya chini ya chanzo cha joto.


6- Baada ya siku 3 utawapatia chanjo ya Gumboro na siku 7 wapatie chanjo ya New Castle, utarudia tena kuwapa chanjo hii baada ya mwezi mmoja kisha utafanya hivi kila baada ya miezi mitatu mitatu.


*MAPATO YA MRADI WAKO*

1- Katika uzazi wa kwanza utapata vifaranga 150 kwa wastani wa vifaranga 15 kwa kila kuku. Tuseme haujazingatia kanuni za ufugaji za makala hii ukapata vifaranga 100 yani wastani wa vifaranga 10 kwa kila kuku. Kisha baadaye wakakua wakafa kuku 50 yani watano kwa kila kuku utakuwa na jumla ya kuku 50.


2- Baada ya wiki 3 utapata tena kuku tufanye kwa mahesabu kama hayo hapo juu kwa hasara utakuwa na kuku wengine 50, na kufanya jumla ya kuku 100. Ikiwa kuku wako baada ya uzao wa pili uliwapumzisha kwa miezi miwili basi mwezi wa 3 utapata tena kuku vifaranga 100 na wiki 3 baadaye utapata wengine 100. Kwa mahesabu kama hayo awali wakikuwa utakuwa na kuku wengine 100 ambao watakuwa.


3- Baada ya miezi 6 utakuwa na kuku wakubwa wa uzao wa kwanza 50, uzao wa pili kuku 50 na utakuwa na kuku wenye umri wa miezi mitatu 50 wa uzao wa 3 na kuku wengine 50 wa uzao wa 4.


4- Katika kuku 100 wa uzao wa kwanza na pili, tufanye kuku 50 wawe matetea ukijumlisha na kuku 10 ulioanza nao mradi utakuwa na matetea 60. Ikiwa kila tetea atatotoa vifaranga 10 na vikakua vitano tu, mwishoni utakuwa na kuku 300 na baada ya miezi mitatu kuku wengine 900 toka katika kutoka kwa uzao wa kwanza, wapili na watatu.


5- Hivyo mwaka wa pili utafunga na kuku si chini ya 1,200/= wanaotaga mayai.


6- Ukiuza majogoo yote 1,200/= kwa bei ya 8,000/= ili upate pesa ya kujenga miundombinu bora maana sasa utakuwa na kuku wengi wanaoendelea kuzaliana kwa kasi utapata pesa kiasi cha *TZS 7,200,000/=*


Sasa ongeza kuku wako wa kutaga hadi wafikie kuku 4,000 maana sasa utakuwa na pesa za kutosha kuendesha mradi wako.


7- Sasa ukiwa na kuku *4000* wa kienyeji wa kutaga mayai, ikiwa kuku *3000* tu watataga ukauza yai moja kwa bei ya haraka haraka ya *TZS 250* tu, utapata *TZS 750,000/=* kwa siku ambayo sawa na TZS *22,500,000/=* kwa mwezi na *TZS 270,000,000/=* kwa mwaka sawa sawa na *128,572 USD*. Kumbuka mwamba makadilio haya niya chini sana. Ukifata kanuni zote kwa makini na maombi huku ukimtanguliza Mungu utafikia hata TZS *500,000,000/=* kwa mwaka.


8- Kumbuka unapofanikiwa kupata mapato ya kila aina, umtolee *Mungu zaka(x10%)* ya mapato yako, pia ukatoe sadaka ambayo ni kubwa kuliko zaka na uwasaidie masikini na wahitaji.


9- Tunza kumbukumbu zako zote za fedha katika daftari maalumu kuhusu mapato na matumizi ya mradi wako. Pia hali ya kuku wako kuhusu tarehe za chanjo ya mwisho, siku walipoanza kuatamia, magonjwa yanayowasumbua mara kwa mara.

October 26, 2018

Kutuhusu ebusol

MILK SHAKE YA EMBE

MAHITAJI

1-  Maembe makubwa 3

2- 1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa hiriki 

3- Cardamom powder (weka kidogo kidogo kulingana na ladha)

4- Sukari *vijiko 2* vya chakula

5- *240 gram* ya maziwa ya maji

6- Vipande vya barafu

*(Ice cubes)*

7- Kijiko 1 cha chakula cha vanilla ice cream

*Unaweza tumia maembe yaliyogandishwa katika friji*


Menya maembe kisha weka katika Brenda


Weka maziwa ya maji na cardamom powder. Washa blenda yako kwa kasi ndogo ili kusaidia isage pole pole ukipata mapovu toa kwa kijiko.


Kisha weka barafu na endelea kusaga ipondeke kabisa na barafu.


Kisha ongeza sukari na jitaidi kulamba/kuonja uweze pata ladha unayoitaka.


Baada ya hapo kinywaji kitakuwa tayari kwaajili ya kunywa/kuuza pia unaweza weka ice cream wakati wa matumizi

October 25, 2018

JINSI YA KUTENGENEZA EGG CHOPS ZA NYAMA NA UNGA WA MCHELE

Mahitaji

1- Mayai 8 makubwa au 10 madogo

2- Nusu kilo ya nyama =na gm 500 na nyama hii iwe ya kusaga

3- Kitunguu1cha wastani

4- Kijiko 1 cha chakula cha  kitunguu saumu na tangawizi

5- Binzari manjao kijiko 1 cha chai au nusu inatokana na inavyokolea maana manjano nyingine huwa Kali sana hivyo unahitajika kuwa mwangalifu.

6- Kijiko 1 cha chai garam masala powder

7- Robo *(¼)* kikombe majani ya kotimiri/ giligilani

8- Chumvi kwa kuonja

9- Nusu *(½)* kikombe unga wa mchele

10- Mafuta ya kukaangia


*Maelekezo*

Weka mayai kwenye sufuria ukiwa umeyaosha vizuri na ubandike jikoni jiko likiwa na moto wa wastani chemsha mayai yaive kama unavyopenda. 


Wakati mayai yanachemka, andaa viungo vingine; katakata majani ya kotimiri na kitunguu vipande vodogovidogo sana


Katika bakuli kubwa; weka nyama, kitunguu, majani ya kotimiri, kitunguu saumu na tangawizi, bizari ya manjano, pilipili ya unga na garam masala. 


Vunja yai moja uongeze kwenye mchanganyiko. 


Changanya vizuri, weka na chumvi kwa kuonja


Gawanya mchanganyiko kwenye madonge 6 hadi 8 yaliyolingana (inategemea na ukubwa wa mayai). Menya na mayai, weka pembeni


Funika kila yai na donge moja ya nyama. Hakikisha yai linakuwa katikati na limefunikwa vizuri na nyama.


Sawazisha vizuri kwa juu kisha paka unga wa mchele kwenye madonge ya nyama kwa juu, hakikisha kila sehemu imefunikwa vizuri


Chemsha mafuta kwenye kikaangio katika moto wa wastani. 


Wakati mafuta yanachemka, piga yai moja lililobakia. 


Chovya kila egg chop kwenye yai, tingisha kidogo ili yai lililozidi litoke kabla ya kuweka kwenye mafuta


Kaanga mpaka ziwe na rangi ya kahawia


Hamishia egg chops zilizoiva kwenye sahani iliyowekwa tissues za jikoni au chujio la bati ili mafuta yote yachuje kishaa Itakuwa tayari kwa biashara

October 23, 2018

JINSI YA KUPIKA WALI WA RANGI TATU

MAHITAJI

WALI WA MANJANO

1- Mchele wa basmati kikombe 1 cha chai

2- Mafuta ya kupikia kijiko1 ½ 

Nyanya 2 zilizomenywa na kukatwakatwa

3- Karoti 3 zilizochemshwa na kuiva

4- Unga wa binzari 1/4 kijiko

Chumvi kiasi 

5- Kwa wali wa mweupe

6- Mchele wa basmati kikombe 1 cha chai

7- Mafuta ya kupikia kijiko1 ½ 

8- Tui la nazi kikombe 1

9- Unga wa hiliki Kijiko 11/2 chachai


*WALI WA KIJANI*

*MAHITAJI*

1- Mchele wa basmati kikombe 1 cha chai

2- Mafuta ya kupikia kijiko 1 ½ 

3- Chumvi kiasi

4- Vitunguu maji 2

5- Kitunguu saumu kilichopondwa 1

6- Tangawizi iliyopondwa 1

7- Nazi iliyosagwa vijiko 2

8- Majani 8 hadi 10 ya mnanaa

9- Majani ya giligilani kikombe kimoja

10- Pilipili manga kijiko 1

11- Garam masala kijiko 1 cha chai

12- Namna ya kuandaa

13- Unatakiwa kupika wali walo katika sufuria tatu tofauti. Kwa 


*WALI MWEUPE*

1- Wali mweupe unatakiwa kupika kama ilivyozoeleka huku ukiongeza hiliki kama kiungo chako.


2- Unachotakiwa kufanya ni kuosha mchele wako.


3- Kisha injika tui jikoni weka chumvi na baadaye hiliki.


4- Hakikisha maji uliyoinjika yana uwezo wa kuivisha wali wako.


5- Baada ya kuiva palia na weka pembeni.


*KWA WALI WA RANGI YA CHUNGWA*

1- Anza kwa kupika wali wa mafuta. Kwa kuosha mchele na kuuchemsha kwa kiwango cha maji ya kutosha kuivisha.


2- Hakikisha unaweka chumvi ili kuufanya wali wako kuwa na ladha.


3- Chukua karoti na nyanya saga pamoja.


4- Kisha kaanga binzari na changanya na mchanganyiko wa nyanya na karoti.


5- Chukua wali wako uliokwishawiva na changanya katika mchanganyiko wako huo.


6- Wali wote utakuwa wa rangi ya chungwa.


*WALI WA KIJANI*

1- Kwa wali wa kijani , anza kwa kupika wali wenyewe kama nilivyoelekeza hapo juu.Kisha chukua kitunguu maji, saumu, tangawizi nazi , majani ya mnanaa,majani ya giligilani,hoho, pilipili manga na kisha saga kwenye machine ya kusagia.


2- Chukua mafuta ya kupikia weka jikoni, na kaanga garam masala na baadaye weka mchangayiko wako wa kijani kwenye sufuria hiyo iliyoko jikoni.


3- Endelea kukaanga hadi viive kabisa.


4- Ipua na changanya na wali wako. Utapata wali wa kijani.

Baada ya hapo pakua. Na weka kwenye bakuli lenye muundo unaopendelea.


5- Anza kwa kuweka rangi yeyote kati ya hizo ulizopika. Panga vizuri kwa kufuata mpangilio maalum unaweza kuanza na rangi ya machungwa, nyeupe na kijani ikaja mwisho au kinyume chake.


6- Pamba wali wako kwa kuweka jani dogo la giligilani na kipande cha karoti.

Chakula choko kipo tayari kwa kuliwa

UTENGENEZAJI WA TAMBI ZA DENGU

MAHITAJI

1.    Unga wa dengu ½ kilo


2.    Binzari nyembamba ½ kijiko cha mezani


3.    Unga wa pilipili manga kijiko 1 cha chai


4.    Unga wa mchele ¼ kilo


5.    Chumvi kiasi


6.    Mafuta ya alizeti ½ lita


7.    Baking powder


*JINSI YA KUTENGENEZA*

1- Changanya unga wa mchele pamoja na ule wa dengu. Kisha chukua nyunyuzia baking powder na baadaye chumvi


2- Weka unga wa binzari nyembamba na pilipili manga.


3- Changaya vizuri na kisha weka maji kidogo kidogo huku ukukanda hadi liwe donge gumu kama unavyofanya kwenye maandazi.


4- Baada ya hapo weka donge lako pembeni na funika. Acha likae kwa muda wa nusu saa hadi saa moja.


5- Baada ya hapo chukua karai la mafuta weka jikoni acha hadi mafuta yapate moto kabisa. Kisha chukua mashine ya kupikia tambi na weka donge lako. Kandamiza taratibu huku ukiruhusu minyororo ya tambi kuingia kwenye mafuta yaliyo jikoni.


6- Weka kiasi kiasi huku ukikaanga. Acha mpaka zitakapokuwa zimeiva na kukauka vizuri. Ipua na weka pembeni.


7- Weka kwenye sahani safi na kavu.Tambi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.


8- Tafuta fingushio vizuri funga kisha peleka sokoni 

October 22, 2018

JINSI YAKUTENGENEZA MAANDAZI YA MAYAI NA MAZIWA

Mahitaji

1- Unga wa ngano ½ kilo

2- Sukari 200g (kikombe kimoja cha chai)

3- Chumvi ½ kijiko kidogo (cha chai )

4- Hamira kijiko 1 kidogo

5- Yai 1

6- Maziwa ya unga vijiko 2 vikubwa

7- Butter kijiko 1 kikubwa

8- Iliki kijiko1 kidogo

9- Maji ya uvuguvugu ya kukandia

10- Mafuta ya kuchomea lita 1

11- Kibao cha kusukumia unga wa ngano

12- Sinia au ubao ulionyooka


*Maelekezo*

1- Weka unga kwenye bakuli kisha ongeza sukari, chumvi, yai, maziwa ya unga, butter na hiliki. 

2- Changanya viambato mpaka mchanganyiko uwe sawia.

3- Ongeza maji ya uvuguvugu kiasi kwenye mchanganyiko na uanze kukanda. 

4- Ni vizuri kukanda mchanyiko huu kwa muda wa dakika 15 ili kuhakikisha donge lote la unga limelainika vizuri.

5- Gawanya unga uliokwandwa katika madonge manne (4) tofauti.

6- Weka unga wa ngano kidogo katika kibao cha kusukumia na uanze kusukuma donge moja katika shape ya chapati. 

7- Katika kusukuma, hakikisha unga wako uko wa wastani – siyo mwembamba sana wala mnene.

8- Ukimaliza kusukuma kata unga kutokana na umbo upendalo kupika maandazi na uyatandaze katika ubao au sinia lililonyooka. 

9- Hakikisha sinia au ubao umenyunyuziwa unga wa ngano ili kuzuia unga utakaoweka usingandie.

10- Rudia hiyo hatua kwa madonge yote yaliyobakia.

11- Ukimaliza kuandaa maandazi yako, weka maandazi yako katika sehemu iliyokuwa na joto ili yaweze kuumuka. 

12- Hii inaweza kuchukua hadi masaa 3 ili hamira kuumua vizuri unga wako.

13- Unga ukishaumuka, bandika sufuria, au kikaangio pamoja na mafuta jikoni

14 Hakikisha mafuta ni mengi ili kuwezesha maandazi kuiva vizuri.

15- Mafuta yakishachemka tumbukiza mandazi. 

16- Acha maandazi kwenye mafuta mpaka yabadilike rangi na kuwa ya brown.

17- Maandazi yakishaiva, ipua na weka kwenye chujio ili kukausha mafuta. Rudia hatua hizi kwa maandazi yote yaliyobaki.

18- Subiri yapoe na yako tayari kuliwa/kuuza

UTENGENEZAJI WA BAJIA/BAGIA ZA DENGU

Malighafi

1- Unga wa dengu kikombe kimoja

2- Vitunguu maji 2 (Katakata vipande vidogo vidogo)

3- Vitunguu saumu vilivyo sagwa kijiko cha chai 1

4- Baking Powder kijiko cha chai 1

5- Maji Kiasi

6- Chumvi

7- Mafuta ya kukaangia

8- Pilipili , Kotmiri ukipenda


Matayarisho

1- Chukua bakuli kubwa changanya unga wa dengu na vitunguu maji na vikisha changanyika weka vitunguu saumu, kotmiri iliyokatwa katwa na baking powder. Weka chumvi kiasi kidogo.


2- Weka maji kidogo kidogo hadi mchanganyiko wako uwe mzito kisha uache kwa muda.


3- Bandika kikaango jikoni na weka mafuta, yakishachemka chota mchanganyiko wako kwa kijiko na kuweka kwenye mafuta. 


4- Angalia usiweke mara nyingi sana ili bagia zisijeshikana.


5- Zikiiva na kuanza kubadilika rangi epua na uweke mahali zitoke mafuta.


6- Hakikisha moto sio mkali sana ili ziive na sio kubabuka.


7- Andaa tayari kwa biashara/kula na kinywaji chochote.

JINSI YA KUTENGENEZA BISKUTI ZA MAZIWA

HITAJI/MALIGHAFI

1- Vikombe vinne vya unga wa ngano uliochekechwa vizuri.

2- Maziwa kikombe cha chai 1½.

3- Baking powder vijiko vinne vya chai.

4- Mafuta/blueband vijiko sita vya chai.

5- Chumvi kijiko kimoja cha chai.


*HATUA ZA UTENGENEZAJI*

• Chukua unga uliokwisha pimwa tayali, changanya na baking powder na chumvi kijiko kimoja cha chai.


• Chukua mafuta kwa mkono uchanganye pamoja na mchanganyiko wa ungaWeka maziwa na uchanganye mpaka uji uwe mzitoAcha kwa *dakika 30*


• Kata muundo/umbo unalotaka (model) unapotaka kuitengeneza.


• Weka katika Pre- heated oveni, joto *175ºC* kwa dakika *10 hadi 15* kama unapenda zikauke zaidi.


• Toa biskuti na kuziacha kwa muda ili zipoe,


• Tia kwenye vifungashio tayari Kwa chakula au biashara.

October 21, 2018

JINSI YA KUTENGENEZA JAMU YA EMBE NA KARAKARA (passion)

Hii ni aina ya jamu ya asili ambayo inaweza kutumiwa kwa kula na mkate au aina nyinginezo za vitafunwa, au mtumiaji anavyopendelea kuitumia. 


- Jamu hii inatengenezwa kutokana na mchanganyiko wa aina mbili za matunda, embe na karakara


- Namna ya kusindika jamu ya embe na karakara

Dondoo: Kiwango cha mahitaji yatakayoainishwa hapo chini na maelezo yake ni kwa ajili ya, kutengeneza na kupata kiasi cha chupa 15 za nusu (½) lita.


*Mahitaji*

• Maembe 50 makubwa yaliyoiva vizuri


• Karakara ½ kilo


• Sukari nyeupe kilo 3


• Juisi ya limao lita ⅛



*Namna ya kuandaa*

• Osha maembe vizuri kwa maji safi


• Menya kwa uangalifu

• Katakata vipande vidogo vidogo


• Unaweza kusaga maembe hayo endapo si laini


• Osha karakara (passion fruits) vizuzi kwa maji safi


• Kata na utoe sehemu ya ndani (chakula)


• Changanya na maembe uliyokwisha kuandaa


• Weka sukari nyeupe kilo tatu kwenye mchanganyiko huo


• Weka lita 1 ya juisi ya limao


• Bandika jikoni


• Koroga taratibu kwa muda wa nusu saa


• Epua na ufungashe


*Ufungashaji*

• Wakati mchanganyiko ukiendelea kuiva jikoni, hakikisha unaandaa vifungashio/chupa


• Ni muhimu kuhakikisha kuwa chupa hizo zimeoshwa vizuri na kuwekwa kwenye chombo maalumu cha kuulia vimelea (Sterilizer)


• Weka jamu yako kwenye vifungashio kulingana na ujazo unaohitaji ikiwa bado ya moto

• Funga chupa/kifungashio kiasi


• Rudisha kwenye chombo maalumu cha kuulia vimelea


• Acha humo kwa muda wa dakika tano


• Ondoa na ufunge vizuri


• Pindua chupa/kifungashio mfuniko ukae chini. Hii itasaidia mfuniko kufunga vizuri


• Weka nembo tayari kwa mauzo


TENGENEZA BAGIA ZA KUNDE

MAHITAJI

1- Vikombe 2 kunde

2- Kitunguu 1 kikubwa

3- Pilipili kichaa 2 (nyekundu na kijani ukipenda)

4- Vijiko 3 vya chakula maji ya limao (ukipenda)

5- Kijiko 1 cha chai baking powder

6- Vijiko 1½ vya chai tangawizi

7- ¼ kikombe majani ya giligilani

8- Chumvi kwa kuonja

9- Mafuta ya kukaangia


*MAELEKEZO*

1- Osha na kuloweka kunde kwenye maji ya moto siyo chini ya masaa 8, au usiku mzima


2- Katakata kitunguu, pilipili, majani ya giligilani; twanga tangawizi. Weka pembeni


3- Chuja kunde maji


4- Weka kunde, maji ya limao na pilipili kwenye mashine ya kusagia chakula au blender ila isilainike sana. 


5- Unaweza pia kutumia mashine ya mkono ukipenda au kutwanga kwenye kinu. (hakikisha mashine yako ina nguvu ya kutosha kusaga kunde)


6- Ikilainika, ongeza kitunguu na majani ya giligilani kwenye mchanganyiko, saga kwa sekunde kama 20. 


7- Hakikisha vitunguu na majani ya giligilani hayasagiki kabisa.

8- Weka mchanganyiko kwenye bakuli kubwa.


9- Ongeza chumvi na bakingo powder, changanya vizuri


10- Chemsha mafuta kwenye kikaango katika moto wa wastani. 


11- Yakichemka, tumia vijiko 2 au mikono kutengeneza umbo kama la yai au umbo la bagia


12- Weka kwenye mafuta. Kaanga mpaka ziwe na rangi ya kahawia


13- Toa bhajiya zilizoiva kwenye mafuta. 


14- Hamishia kwenye sahani/bakuli iliyowekewa tissues, au tumia chujio la bati ili mafuta yachuje


15- Pakua za moto na inapendeza kula na  chachandu ya machicha ya nazi na mtindi

JINSI YA KUTENGENEZA SOSI YA UKWAJU

Mahitaji

1-Ukwaju - 2 Paketi

2-Chumvi - kiasi

3-Tende - ¼ kikombe

4-Pilipili mbichi - 1

5-Bizari ya jiyrah (Cummin powder) - ¼ kijiko


*Namna ya kutayarisha*

1-Toa kokwa ukwaju, kisha roweka kwenye maji ya moto. 

2-Chambua tende utoe kokwa weka kando.

3-Tia vitu vyote katika mashine, saga hadi vitu visagike vyote.

3-Mimina katika bakuli ukiwa tayari kutolewa na aina nyingi ya vyakula upendavyo.


*Kidokezo:-*

Ikiwa huna tende tumia sukari vijiko 2 viwili vya supu.


Inaweza kuliwa na aina nyingi ya vyakula kama; dehii baree, biriani, nyama/kuku wa kuchoma, mishkaki, sambusa, kachori, katlesi viazi vya duara (chops), kababu na vinginevyo vingi.

October 20, 2018

JINSI YA KUTENGENEZA UBUYU

MAHITAJI

1- Sukari vikombe 2

2- Maji vikombe 2

3- Nusu kikombe unga wa ubuyu 

4- Vikombe 4 ubuyu wenyewe 

5- 1/4 tsp pili pili ya unga 

6- 1/4 tsp chumvi

7- 1/4 tsp iliki ya unga

8- Rangi nyekundu au yeyote  utakavyopenda.


*JINSI YA KUTENGENEZA*

- Katika sufuria,weka maji na sukari na chumvi na pili pili ya unga na Rangi na iliki.  Moto uwe juu kiasi na changanya vyote hivyo vipike vizuri. 


2- Wakati vitu vinaanza kujipika utakuta rojo linatoa mapovu. Endelea tu kukoroga acha rojo lipikike vizuri. Baada ya hapo mapovu yakianza kutulia inamaanisha kua rojo limeanza kua zito.

Sasa hapo chota kidogo katika mwiko na test kwa vidole kama rojo linanata ua halinati. Rojo linatakiwa linate ndio linakua limeiva. Lisinate Sana kiasi tu. 


- Kisha mimina ubuyu wa kokwa na changanya vizuri kabisa katika rojo. Endelea kupika vizuri kama dakika 2 hivi. Kisha mimina unga wa ubuyu na changanya vizuri tena.  


- Endelea kupika mpaka unaona sukari inaanza kuganda na kung'aa na kushika vizuri katika ubuyu. 


- Hapo sasa zima jiko na mimina ubuyu katika sinia kubwa na acha ubuyu upoe.


- Ukishapoa ubuyu tayari kwa biashara au kuliwa.

USINDIKAJI WA MAZAO YOTE YA NAFAKA

1- Ili kuongeza matumizi ya mazao hayo na kudumisha ubora wake ni muhimu teknolojia za

kusindika nafaka zitumike. Usindikaji pia huongeza thamani ya zao.


2- Punje za mahindi hutumika kupika makande na husindikwa kupata unga unaotumika katika

matumizi mbalimbali.Vile vile bidhaa nyingine zinazotokana na mahindi ni mafuta na wanga.


KUSINDIKA MAHINDI KUPATA UNGA

- Kuna aina mbili za unga wa mahindi:-

1- Unga wa mahindi yasiyokobolewa *(Dona)* 


2- Unga wamahindi yaliyokobolewa *(Sembe)*


KUSINDIKA MAHINDI KUPATA UNGA WA DONA


Vifaa

• Mashine ya kukoboa

• Mashine ya kusaga

• Ungo

• Debe

• Mifuko

• Chekeche ya nafaka


JINSI YA KUSINDIKA

1- Pepeta na pembua mahindi ili kuondoa vumbi na takataka nyingine kwa kutumia chekeche,

ungo au sinia.


2- Osha kwa mahindi yako kwa maji safi na salama


3- Anika kwenye chekeche safi ili yakauke


4- Saga mahindi kupata unga


5- Fungasha kwenye mifuko safi na kavu ya pamba, plastiki/nailoni, makaratasi yasiyopitisha

unyevu kisha hifadhi katika sehemu safi na kavu


6- Kumbuka kuwa Kusaga mahindi bila kukoboa hudumisha virutubishi vilivyomo kwenye mahindi na

kupunguza upotevu wa chakula.


UNGA WA MAHINDI YALIYOKOBOLEWA


JINSI YA KUSINDIKA

1- Pepeta na pembua mahindi ili kuondoa vumbi na takataka nyingine kwa kutumia chekeche,

ungo au sinia


2- Koboa na saga


3- Fungasha kwenye mifuko safi na kavu ya pamba, plastiki/nailoni na ya karatasi isiyopitisha

unyevu.


4- Hifadhi kwenye sehemu safi na kavu


5- Kumbuka Kusaga mahindi yaliyokobolewa hupunguza virutubishi na wingi wa chakula kwa kiasi

cha asilimia *17 hadi 33*


6- Matumizi ya unga wa mahindi


7- Hutumika kutengeneza vyakula mbalimbali kama vile ugali, uji, togwa na vyakula vya watoto.


8- Pia huchanganywa na shayiri na kutengeneza vinywaji kama vile bia.


KUSINDIKA MPUNGA

1- Mpunga husindikwa kupata mchele ambao pia husindikwa kupata unga.


2- Kusindika mpunga kupata mchele


Vifaa

• Mashine ya kukoboa

• Madebe

• Ungo

• Chekeche

• Vifungashio


JINSI YA KUSINDIKA

1- Anika mpunga juani kwa muda wa siku moja kisha uache upoe kwa usiku mmoja ndipo ukoboe.


2- Pepeta na pembua kutoa takataka kabla ya kukoboa


3- Koboa kwa kutumia mashine.


KUFUNGASHA

1- Baada ya kupanga madaraja fungasha kwenye mifuko isiyopitisha unyevu na hifadhi katika

sehemu kavu na safi.


MATUMIZI YA MCHELE

1- Mchele hutumika kutengeneza vyakula mbalimbali kama vile wali, uji, biriani, mseto, pilau, bisi,

tambi na vitafunwa. Chenga za mchele hutmika kwa kutengeneza chakula cha mifugo.


KUSINDIKA MCHELE KUPATA UNGA


*Vifaa*

• Mashine ya kusaga

• Vifungashio


*JINSI YA KUTENGENEZA*

1- Saga mchele safi kupata unga


2- Fungasha kwenye mifuko safi na kavu isiyopitisha unyevu


3- Hifadhi katika sehemu safi na kavu.


4- Matumizi ya unga wa mchele

Hutumika kupika ugali, uji na vitafunwa.


*KUSINDIKA MTAMA/ AUWELE*

1- Punje za mtama na uwele hupikwa makande na husagwa kupata unga.


*KUSAGA MTAMA/ UWELE KUPATA UNGA*


*Vifaa*

• Mashine ya kusaga

• Ungo

• Chekeche ya nafaka

• Kichanja

• Turubai

• Vifungashio safi


*JINSI YA KUSAGA*

1- Pepeta na kupembua mtama/ uwele ili kuondoa mavumbi na takataka nyingine.


2- Tumia chekeche au ungo kupepeta na kupambeua


3- Osha kwa maji safi kisha anika juani kwenye kichanja au turubai


4- Saga kupata unga wa mtama/uwele


5- Fungasha kwenye mifuko ya nailoni/ plastiki


6- Hifadhi katika sehemu safi na kavu


7- Matumizi ya unga wa mtama/uwele


8- Hupikwa ugali, uji na togwa. Vile vile hutumika katika kutengeneza vyakula vya watoto


*KUSINDIKA NGANO*

1- Ngano husagwa ili kupata unga


*Vifaa*

• Vifungashio

• Mashine ya kusaga


*JINSI YA KUSAGA*

1- Nyunyuzia maji kwenye ngano


2- Koboa na saga ili kupata unga


3- Weka kwenye vifungashio safi na visivyopitisha maji


*MATUMIZI*

1- Unga wa ngano hutengeneza vitafunwa kama vile mikate, chapati, maandazi, tambi na

keki.

October 19, 2018

JINSI YA KUANDAA MAZIWA YA SOYA

FAIDA ZA SOYA YA CHAI

- Soya huwafaa sana wenye matatizo ya shinikizo la damu


- Kama mtu ana shinikizo la damu ni vema akatumia soya kama kinywaji maana huweka mapigo ya moyo katika hali ya msawazo.


- Wakati mtu mwenye mapigo ya moyo ya kupanda hashauriwi kabisa kutumia majani ya chai au kahawa, hivyo kinywaji cha soya ni suluhisho kwake na mbadala sahihi.


- Kwa mtu mwenye shinikizo la damu la kushuka anapaswa kutumia soya maana itaweka mapigo ya moyo katika hali ya kawaida.


- Kunywa majani ya chai au kahawa kunapandisha mapigo ya moyo na ikiwa ataendelea kutumia vinywaji hivi basi moyo huzoea; na siku mapigo ya moyo yakishuka anapata shida na kuingia gharama kubwa kununua madawa ya ghali sana ili kupandisha mapigo ya moyo.


- Hivyo namshauri kwamba atumie kinywaji cha soya ili siku mapigo ya moyo yakishuka anaweza akatumia sasa majani ya chai au kahawa kama dawa tu ili kupandisha mapigo ya moyo.


*Matatizo ya vidonda vya tumbo*

- Matumizi ya soya ya chai ni rafiki kwa mazingira ya tumbo kutokana na kufanya kazi vema katika mazingira ya tindikali ya tumbo.


*Gharama ndogo*

- Maandalizi ya soya ya chai ni rahisi na hugharimu kiasi kidogo tu cha fedha huku yakikuhakikishia manufaa mengi sana kiafya.


- Soya robo kilo (250mg) inakupatia pia soya ya chai robo kilo (250mg) pia, hivyo hakuna kinachopotea na waweza kuitumia kwa muda mrefu sana.


*JINSI YA KUANDAA MAZIWA YA SOYA*

1- Anza kwa kuchambua soya yako 2KG (Kilo 2) ili kuondoa mawe, nafaka zisizohitajika na soya zilizoharibika.


2- Kisha osha na loweka soya yako kwa masaa 24 yani kwa mfano umeloweka leo saa 1 asubuhi, iache hadi kesho saa 1 asubuhi.


3- Baada ya saa 24 kupita toa maganda na kutwanga soya yako kwa kutumia kinu au saga kwa kutumia blenda mpaka itakapolainika vizuri.


4- Hakikisha chombo unachotwangia ni kisafi kabisa ili maziwa yasichafuke na kupunguza thamani yake.


5- Kisha changanya soya ulizozitwanga na maji safi na salama lakini zingatia kutochanganya maji mengi sana hata maziwa yako yakawa mepesi sana.


*Maziwa Yakiwa Tayari Kwa Kuchujwa*

6- Baada ya kuchanganya maji na soya uliyoitwanga, chuja kwa kutumia kitambaa cheupe kisafi chenye nafasi ndogo sana ili kuzuia chembechembe za soya kupenya.


7- Hapo utakuwa umepata maziwa ya soya.


8- Mabaki ya soya uliyokamua yanaweza kutumika kutengeneza bagia kwa kuyachanganya na viungo na unga wa ngano kidogo kwajili ya kushikiza bagia zako.


9- Au unaweza kutumia kama chakula cha ziada kwa kuku kama mbadala wa dagaa au uduvi


10- Kisha chemsha maziwa yako hadi yaive kabisa. Ikumbukwe kwamba maziwa ya soya yana tabia sawa na maziwa mengine ya wanyama katika utaratibu wa kuyaandaa.


11- Hivyo katika kuchemsha maziwa ya soya, weka chombo chini ya sufuria au chungu chako ili kuepuka kuganda kwa maziwa katika sufuria au chungu na kufulumia kwa maziwa.


12- Yakisha chemka na kuiva vizuri unaweza kuyatumia kwa chakula au kwa kitafunwa chochote.


Unaweza kuongeza soya ya chai kama unataka upate chai ya maziwa.


13- Ili unufaike sana na maziwa haya basi tumia asali badala ya sukari.


*FAIDA YA MAZIWA YA SOYA*

1- Maandalizi rahisi kwa unafuu mkubwa sana


2- Matumizi ya maziwa ya soya yanakulahisishia gharama za kupata maziwa mengi kwaajili ya nyumbani maana kwa 2kg za soya  ukapata maziwa zaidi ya lita 10.


3- Utajiri wa virutubisho vya chakula.


4- Maziwa ya soya yana mchango mkubwa kwa mtumiaji kwani yamesheeni virutubisho vyote vilivyopo hata katika maziwa ya wanyama lakini faida yake kubwa zaidi ya maziwa ya wanyama, maziwa ya soya hayana mafuta ya lehemu yanayoganda na kudhuru mwili wa mtumiaji.


5- Maziwa ya soya hayana pia vimelea vya magonjwa mbalimbali vilivyomo ndani ya maziwa ya wanyama.


6- Kwa watoto wadogo Maziwa ya soya yana mchango mkubwa katika ukuaji wa watoto wadogo bila kujali umri wa mtoto na Kwa wale watoto ambao wameachishwa ziwa la mama kwa sababu mbalimbali kama kifo, magonjwa, kutengana n.k wanaweza wakakua vizuri kwa kutukia maziwa ya soya kuliko aina yoyote ile ya maziwa.


7- Maziwa ya soya ni mdabala na jibu sahihi kwa mahitaji yako ya maziwa

8- Yanaweza yakaganda na kuwa mtindi.

9- Ikiwa mtumiaji atataka apate mtindi basi atayachukua maziwa ya soya baada ya kuchemshwa, kuiva vizuri na kupoa katika chombo cha kugandishia maziwa nayo yataganda kwa utaratibu uleule kama yagandishwavyo maziwa ya wanyama.

10- Kisha waweza kuyatumia kwa chakula chochote

October 07, 2018

MADAWA YA ASILI KUTIBU KUKU

Madawa ya asili ya kutibu magonjwa ya kuku ni mazuri kutumia kwa kuwa na faida zifuatazo;-


1.Hupatikana kwa urahisi. 2.Rahisi kutumia,

3. Gharama nafuu,

4. Zinatibu vizuri na HAZINA MADHARA.


Pia unaweza ukatengeneza unga wa mimea hiyo na kuchanganya kwenye pumba za Kuku.


SHUBIRI MWITU(Aloe vera). 

Chukua majani 3-5 makubwa, katakata na loweka ndani ya maji lita 10 kwa masaa 12 hadi 16 Wape kuku kwa siku 5 - 7 Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine baada ya masaa 12 Mchanganyiko huu unaweza kutibu:

1. Kideri/Mdondo (Mdonde/Chikwemba/Kitoga/Chinoya/Sotoka) - inyweshwe kabla ya kinga. 

2. Homa ya matumbo (Typhoid).

3. Mafua (Coryza). 

4. Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera).


MLONGE

Mlonge una vitamin A na C. Chukua majani ujazo wa mikono miwili. Kisha yapondeponde na kuyaweka katika lita 10 za maji na iache kwa masaa 12-16, chuja na wape kuku. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine. Mlonge hutibu:

1. Mafua.

2. Kideri - inyweshwe kabla kwa kukinga

3. Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera). 

4. Homa ya matumbo.


PILI PILI.

Ponda ponda, kisha changanya na maji na wawekee kuku wawe wanakunywa kwa muda wao. Inasemekana inasaidia kutibu mdondo (lakini mapema kabla maradhi kuingia). Dawa ya kutibu Kuku Kuharisha namna yoyote.


MPAPAI 

Kuandaa: Kata jani moja bichi la Mpapai na uliponde ponde lilainike kiasi. Kisha changanya na maji kiasi cha lita mbili na nusu. Kutumia (kwa tiba) - Kuku wapewe maji hayo wanywe,wasipewe maji mengine kwa ajili ya kunywa kwa siku angalau nne au zaidi, Inafaa zaidi kila siku kuwaandalia dawa mpya ili dawa isiharibike. Kutumia (kwa kinga) - Kupambana na magonjwa ya kuku


Jinsi ya kutibu na kuchanja - Hata kama kuku hawaharishi, wakizoeshwa kunywa maji yenye majani ya mpapai yaliyopondwa angalau mara tatu kwa wiki watakingwa magonjwa mengi. Njia nyingine ya kutumia Mpapai: Chukua majani ya Mpapai uyatwange upate kisamvu chake kiasi cha lita 1. Changanya kisamvu hicho na pumba 2kg. Waweza kuongezea maji kidogo na kuwapatia kuku wanaoumwa watumie chakula hicho hadi wapone. Kama kuku ni wachache, andaa chakula wa nacho kumaliza kwa siku moja ili kisibakie na kuharibika kabla hawajakimaliza.

October 06, 2018

KILIMO BORA NA RAHISI CHA MIHOGO

Mihogo ni zao muhimu sana kwa chakula kwa nchi nyingi za Afrika na Amerika ya kusini. Kwa mara ya kwanza zao hili lililetwa na wareno, hapa Afrika. Zao hili hulimwa nchi zaidi ya 34 za Afrika kwenye hekari zaidi ya ekari milioni 200. Kilimo cha mihogo huhitaji ujuzi kidogo sana na ni rahisi kulima. Zao hili hustahimili ukame na huweza kubakia ardhini kwa muda mrefu kuepukana na baa la njaa. Upatikanaji wa mavuno ni wa uhakika kuliko mazao ya nafaka. Mizizi ya mihogo ndio tegemeo kubwa la wakulima. Mihogo huwa na kiasi kikubwa sana cha VITAMINI ‘A’ na kiasi kidogo cha protini. Ulaji wa mihogo huwasaidia walaji kuepukana na ugonjwa wa ukavu macho. Pia majani ya mihogo huweza kutumika kama mboga za majani (KISAMVU). Kuna kemikali iitwayo CYNOGENIC GLUCOSIDE ambayo inaweza kuwa sumu kama mihogo isipoandaliwa vizuri. Mihogo mitamu ina kiasi kidogo sana cha kemikali hii na huweza kuliwa hata Mibichi.


HALI YA HEWA, UDONGO NA MAHITAJI YA MAJI



Kwenye ukanda wa Ikweta zao hili hulimwa hadi mita 1500 kutoka usawa wa bahari. Halijoto ya 20-30° hufaa kwa kilimo cha mihogo. Zao hili halistahimili maji yaliyotuama na hupendelea zaidi jua la kutosha. Mihogo huzaa vizuri kwenye udongo tifutifu-kichanga wenye rutuba ya kutosha. Pia huweza kuzalishwa kwenye sehemu iliyoathirika na mmomonyoko wa udongo ambapo mazao mengine hayasitawi. Rutuba ikizidi sana ardhini mihogo huwa na majani mengi sana na mizizi kidogo.


UPANDAJI WA MIHOGO


Kupanda mihogo kwa kutumia mihogo iliyohifadhiwa haiwezekani kwa sababu mizizi haina vichipukizi. Mihogo inapandwa kwa kutumia pingili za shina lake zenye urefu wa sm 20-30 na upana wa sm 2-2.5. Vipingili vizuri ni vile vitokanavyo na sehemu ya shina iliyokomaa vizuri. Mimea kwa ajili ya mbegu inatakiwa iwe na umri wa miezi 8-14. Kadiri mimea inavyokuwa na umri mkubwa ubora wake wa kuzalisha mbegu huongezeka. Pia pingili ndefu ni nzuri kuliko pingili fupi. Mimea yenye afya nzuri tuu itumike kwa ajili ya pingili. Kama zimeathirika kidogo zinaweza kutibiwa kwa kuzizamisha kwenye maji yenye joto la 50° kwa dakika 15 kabla ya kupanda.

Baada ya kukatwa vipingili visikae muda mrefu zaidi ya siku mbili. Huweza kupandwa kwa kusimamishwa, kuinamishwa kidogo ama kwa mlalo. Wakati wa kupanda EPUKA kugeuza vipingili juu chini kwani mihogo itazaa kidogo sana.


NAFASI ZA UPANDAJI


Kama mimea inapandwa peke yake nafasi huwa si sawa endapo ikipandwa pamoja na mazao mengine. Kama mihogo ikipandwa peke yake nafasi kutoka mmea hadi mmea ni mita 1. Kwahiyo kwa eka, vipingili 4000 vinatosha. Sehemu nzuri ya kupanda mihogo ni sehemu yenye muinuko kiasi isiyotuamisha maji. Sehemu inayotuamisha maji mihogo hushindwa kutoa mizizi yenye afya.


UTUNZAJI WA SHAMBA


Shamba lilpaliliwe kila baada ya wiki 3-4 mpaka zifikie muda wa miezi 2-3 tangu kupanda. Baada ya hapo mimea inaweza kufunika na kuzuiya magugu yenyewe kwahiyo kupalilia sio muhimu sana. Kama shamba halina rutuba ya kutosha, mbolea ya samadi inafaa na mkulima anashauriwa kuongeza majivu kama ukuaji si mzuri, majani kuwa ya giza na vialama vya kahawia kwenye majani. Kutandazia shamba ni muhimu sana.


MZUNGUKO/MCHANGANYO WA MAZAO


Mazao ya mikunde kama karanga, kunde, hufaa sana kupanda pamoja na mihogo kwani huongeza rutuba ya udongo. Pia kuchanganya mihogo na mimea mingine husaidia kuthibiti mmomonyoko wa udongo.


MAGONJWA YA MIHOGO



African Cassava Mosaic Disease (ACMD)

 


Ugojwa huu ni ugonjwa hatari zaidi wa mihogo hapa barani Afrika na umeenea sehemu zote zizolima mihogo Africa. Husababishwa na kupanda vipingili vilivyoathirika na waduduweupe wa mihogo. Husababisha hasara ya zaidi ya asilimia 90%.


DALILI ZA UGONJWA


Dalili za awali za ugonjwa huu ni muonekano wa michirizi meupe hasahasa kwenye majani.


NINI CHA KUFANYA

Tumia vipandikizi visivyo na ugojwa huu. Inashauriwa kutumia vipingili kutoka kwenye matawi ya mihogo na siyo kwenye shina kubwa kwani uwezekano wa kuwa na ugunjwa huuu ni mkubwa kwenye shina kuliko matawi.

Tumia aina za mihogo inayostahimili ugonjwa huu kama ( SS 4, TMS 60142, TMS 30337 and TMS 30572).

CASSAVA BACTERIAL BLIGHT (Xanthomonas campestris Pv. Manihotis)



(MNYAUKO BACTERIA)



Ugonjwa huu ni kizuizi kikubwa cha kuzalisha mihogo hapa Afrika.



DALILI

Mwanzoni ugonjwa huu huonekana kwenye majani, ambapo huonekana kama yameloweshwa na maji. Ugonjwa ukishamiri majani huanza kudondoka. Wakati wa unyevu unyevu bacteria hutoa uchafu kama gundi chini ya majani.Ugonjwa huu huenezwa sana kwa kutumia vapandikizi vilivyoathirika na pia matone ya mvua. Wadudu kama panzi hueneza ugojwa huu pia. Mkulima pia huweza kueneza huu ugojwa akipita shambani wakati ama baada tuu ya mvua.

NINI CH A KUFANYA

Tumia vipandikizi salama visivyo na ugojwa huu.

Inashauriwa kuchanganya mihogo na mahindi ama tikiti maji ili kupunguza ugojwa huu.

Fanya mzunguko wa mazao na ikiwezekana pumzisha ardhi.

Ondoa na choma mimea yote na magugu shambani ama kwatua na kuyafukia chini ya ardhi



BROWN LEAF SPOT (Cercosporidium henningsii) UGONJWA MADOA YA MAJANI.



Majani yaliyokomaa tuu ndio yanayoonyesha dalili za ugojwa huu. Majani huonekana na madoa ya kahawia, baada ya muda huwa njano na mwisho kudondoka


CASSAVA BROWN STREAK VIRUS DISEASE (Potyvirus - Potyviridae)

Ugonjwa huu ni hatari zaidi ukanda wa pwani na Zanzibar na huenezwa na wadudu weupe wa mihogo na pia kwa kupanda vipingili vilivyo na ugonjwa huu. Majani huonekana ya njano ila wakati mwingine majani huweza kuonekana yana afya nzuri wakati mizizi imeshaoza sana.