July 29, 2018

Jifunze kutumia mitandao ya kijamii kwa faida

Watu wengi tumejikita katika kutumia mitandao ya kijamii pasipo kupata faida yeyote. Wengi wetu tunatumia kama kiburudisho cha nafsi. Wengi tunapenda sana kitu ambacho kinaitwa ‘likes, followers’ na habari mbalimbali ambazo hazina msaada wowote katika maisha yetu.
Pia taarifa ambazo tumekiwa tunazipata katika mitandao hiyo, ni taarifa za aina moja, na ndio maana taarifa moja ambayo itakuwa ni kuyashangaza kila mtu atatamani sana na yeye aweze kuipost katika akaunti zake za mitandao ya kijamii. Tabia hii napenda kuita ni ulevi wa mitandao.
Ulevi huu wa mitandao umetufanya wengi wetu kuwa na fani ya uandishi pasipo kusomea. Unakuta mtu kapata taarifa fulani katika mitandao ya kijamii naye pasipo kujua chanzo cha habari hiyo, na yeye anapost katika mitandao ambayo anamiliki.
Lakini ukweli ni kwamba kama upo makini na maisha yako, ni vyema pia ukawa makini na mitandao ya kijamii pia. Unaweza ukawa bado unajiuliza leo Afisa mipango anazungumzia nini? Wala usikwame mahala popote nipo kwa ajili ya kukueleza ukweli japo ukweli huu hautaupenda, hata usipoupenda nataka lengo langu ubadili

Mitandao ya kijamii imeuwa ikieleza bayana, jinsi watu na tabia zao jinsi zilivyo. Siku hizi ukitaka kujua tabia ya mtu jaribu kuingia katika mitandao yake ya jamii halafu chunguza kwa umakini kilichomo ndani ya mitandao hiyo ya jamii utajua tabia ya mtu huyo pasina kumuuliza mtu yeyote. "Mitandao ya kijamii ni kioo cha tabia" kwani kinatupa picha kamili ya jinsi mtu alivyo.
Upo usemi usemao mtu akinyanyua kinywa chake kuzungumza, anaeleza yeye ni mtu wa aina gani, kwa usemi huo huo nami naongezea mitandao ya kijamii ndiyo sehemu ambayo inatoa picha kamili kwa watu ya kwamba wewe ni mtu wa aina gani?
Hivyo kila wakati nakusihi kama kweli unajiheshimu na unapenda kuongeza mtandao mkubwa wa marafiki ili kupata mafanikio makubwa, unatakiwa kuanza kuitumia kitandao ya kijamii kwa faida kama ifuatavyo;-
1. Hakikisha marafiki ulionao katika mitandao yako ya kijamii ni marafiki wa faida kwako. Kwani wengi wetu katika mitandao ya kijamii tuna marafiki wengi ila marafiki wa faida ni wachache. Mwingine ataniuliza sasa nitajuje kama huyu niliyenaye ni rafiki wa faida? Jibu lipo wazi fuatilia vitu ambavyo anafanya na kupost utapata majibu kwamba ni rafiki wa faida au laaah!
2. Hakikisha unaposti vitu ambavyo vinakuelezea wewe kwa ujumla kwa watu wengine. kama ni biashara basi tangaza mara kwa mara huduma au bidhaa ambazo unauza. Lengo la kufanya hivi si kupata wataja pekee, bali kutakufanya uweze kuongeza mtandao wa watu mbalimbali ambao watakuwa wanafanya mambo ambayo na wewe unayafanya, hivyo itakuwa mwanzo mpya wa kubadilishana mawazo.
3. Hakikisha unasoma kila siku vitu vipya katika eneo ambalo litakujenga. Ondoka mara moja katika lile kundi la watu ambao wanapata taarifa za aina moja. Hivyo jijengee utaratibu mpya wa kupata taarifa ambazo ni za kipekee (unique information). Kama wewe ni mwimbaji wa muziki, hakikisha unapata taarifa ambazo zitakujenga katika eneo hilo zaidi.
Kama niilivyosema hapo awali ya kwamba mitandao ya kijamii huwapa watu taarifa ya kwamba wewe ni mtu wa aina gani, hivyo jijengee utaratibu ambao utawafanya watu wapate picha kamaili kuhusu wewe, pia kuhusu  mambo mbalimbali ambayo unayafanya.
Mwisho nimalize kwa kusema ya kwamba, jifunze kutumia mitandao ya kijamii kwa faida, kwani ndio msingi mkubwa wa mafanikio yako.

No comments:

Post a Comment