July 29, 2018

Elimu kwa vikundi vya vicoba na maendeleo: Sehemu ya kwanza

By Ombeni haule

1.0 UANZISHAJI WA VIKUNDI 

1.1 Maana ya kikundi 

Kikundi ni muungano/umoja wa hiari kati ya watu wenye nia na 

madhumuni/malengo yanayofanana kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za 

kimaendeleo kwa manufaa yao ya kifamilia au jamii kwa ujumla. 

Malengo yanaweza kuwa ya kiuchumi au ya kijamii wakati shughuli zaweza kuwa; 

shughuli za kiuchumi (kama vile kilimo,ufugaji, viwanda vya usindikaji n.k.) 

shughuli za kijamii (kama vile ujenzi wa miundo mbinu na mazingira, kituo cha 

kulea watoto na wazee n.k). 

1.2 Lengo la kuanzisha kikundi 

Kwa nini tunaanzisha vikundi? 

Uzoefu unaonyesha kuwa wakulima wanaanzisha vikundi kutokana na sababu 

zifuatazo: 

• Kukusanya nguvu (rasilimali) ya pamoja ili kuweza kufikia malengo ya 

kiuchumi kiurahisi kuliko ukiwa mtu mmoja. Mfano; 1. nguvu kazi (rasilimali 

watu) katika kufanya kazi 2. Nguvu ya pesa (rasilimali pesa) kwa ajili ya 

mtaji wa kuendeshea shughuli iliyobuniwa na kikundi. 

• Kurahisisha mawasiliano na kazi kwa watoa huduma. Mfano Bw/Bi shamba 

ni rahisi kuhudumia kikundi kuliko mtu mmoja. 

• Kulenga soko la pamoja.Mfano kukusanya mazao na kuuza kwa pamoja 

hasa katika masoko ya kisasa yanayohitaji bidhaa kwa wingi kwa vipindi 

maalumu. 

• Kubadilishana mawazo ujuzi pamoja na uzoefu baina ya wanachama 

wenyewe. Kuwa na sauti ya pamoja katika kujitetea mambo 

yanayowahusu. 

Kimsingi sababu zilizotajwa ni sahihi kutokana na mahitaji ya wanakikundi na jamii 

kwa ujumla. Hatahivyo, haishauriwi kuanzisha vikundi kwa lengo la utegemezi wa 

rasilimali kutokana sehemu nyingine. Tukifanya hivi, vikundi vitakuwa sio endelevu 

kwani ili kikundi kiwe endelevu kinatakiwa kianzishwe katika misingi ya kwamba 

lengo litatekelezeka kupitia nguvu na rasilimali za wanachama wenyewe. 

1.3 Aina ya vikundi 

Kuna aina kuu mbili za vikundi vya wakulima navyo ni.

[7/29, 10:52 AM] Omben ebusol: 1.3.1 Vikundi vya kiuchumi 

Hivi ni vikundi vinavyojishughulisha na shughuli za uzalishaji mali. 

Mfano wa aina hii ya vikundi, ni kikundi cha “Sululu” kilichopo kata ya Bungu 

wilaya ya Rufiji. Hiki ni kikundi ambacho shughuli yake kuu ni kuzalisha muhogo, 

kusindika na kupata “Chipsi” na unga wa muhogo kisha kufungasha, kusafirisha 

na kuuza kwa mnunuzi ambaye ni Power Foods Ltd. 

1.3.2 Vikundi vya kijamii 

Hivi ni vikundi vinavyojishughulisha na utatuzi wa kero za kijamii kama vile 

utunzaji wa mazingira, ujenzi wa miundo mbinu (mfano mifereji, 

barabara,majengo ya shule na hospitali), kuhudumia watoto yatima, wazee na 

shughuli za kufa na kuzikana. 

Mfano wa aina hii ya vikundi ni kikundi cha “Chapakazi” katika kijiji cha Tundu, 

kata ya Bupu wilaya ya Mkuranga. Kikundi hiki kilianzishwa kwa lengo la kufanya 

ujenzi wa miundo mbinu kijijini kwao ikiwemo ukarabati wa barabara iliyokuwa 

kikwazo katika kusafirisha mazao ya kilimo na mifugo kutoka kijijini kwao kwenda 

sokoni. 

1.4 Mambo ya muhimu ya kuzingatia wakati wa kuanzisha vikundi 

1.4.1 Sifa za wanachama ndani ya vikundi 

• Awe tayari kulipa ada 

• Ahudhurie mikutano yote na vikao na mafunzo 

• Awe mbunifu 

• Awe anajitolea kufanya kazi za kikundi kwa bidii 

• Auamini uongozi na kueleza bayana yaliyo mazuri na mabaya juu ya uongozi 

na kikundi kwa ujumla. 

• Akubaliane na maamuzi yanayofanywa na wanachama 

• Asaidie wenzake wakati wa shida na raha 

• Awe tayari kukitetea kikundi hata nje kwa watu wengine 

• Awe mchangiaji wa mawazo katika kikundi 

• Asaidie kutunza mali za kikundi

Inaendelea

No comments:

Post a Comment