July 28, 2018

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA HAUJAINGIA KATIKA KILIMO CHA BIASHARA

KILIMO ELIMU

Kabla haujaamua kuingia katika Kilimo cha kibiashara inakupasa kwanza ufahamu mambo muhimu ambayo yatakusaidia katika shughuri yako ya Kilimo husika.

Kwani inakupasa kutambua kila kazi ya kuingiza kipato ina changamoto zake na Kilimo ni moja ya kazi yenye changamoto nyingi ambazo yakupasa nyingine ujipange jinsi ya kukabiliana nazo kabla ya kuingia katika kilimo husika.


Mambo hayo muhimu ni.

1.Utayari kuingia katika Kilimo.

Inakupasa kabla hujajiingiza katika Kilimo uwe tayari wewe mwenyewe kuamua kuanza kufanya Kilimo husika, kwa maana nyingine namaanisha maamuzi yako ya kuingia katika Kilimo yatokane na uchaguzi wako mwenyewe baada ya kuangaliaya na kuona Kilimo ni moja ya jambo litakaroboresha kipato chako.

Hivyo utayari wako utakusaidia kuongeza ari na juhudi zaidi katika kazi yako na kukupunguzia kukata tamaa njiani.


2. Uchanguzi wa Kilimo kinachokufaa .

Kabla ya kuingia katika Kilimo lazima kwanza ufanye uchaguzi wa kilimo gani ambacho utafanya.

Katika uchaguzi lazima uchague kitu ambacho utakuwa tayari kukifanya bila kupata pingamizi la utayari wa kufanya  kilimo hicho.

Hapa katika uchaguzi ukichagua Kilimo ambacho si sahihi kwako ndipo ambapo husababisha changamoto nyingi katika kilimo chako hapo baadaye.


3. Utafiti na ushauri wa gharama juu ya kilimo ulichokichagua.

Baada ya kufanya uchaguzi wako inakupasa ufanye utafiti wa gharama utakazoweza kuzimudu katika Kilimo chako.

Hili litaendana na ushauri wa jinsi gani ya kuweza kufanya Kilimo chako kwa gharama nafuu zaidi ili kama ikitokea hasara uwe na uwezo wa kuikabili vizuri.


4. Panga bajeti yako kabla hujaanza Kilimo.

Yakupasa upange bajeti yako kabla hujaanza Kilimo kwa kuangalia utafiti na ushauri wa gharama juu ya Kilimo ulichokichagua.


5. Usimamizi mzuri.

Wakulima tunasema uchungu wa Kilimo aujuaye mkulima, msemo huu unamaanisha uangalizi wako kwa ukaribu katika Kilimo chako unahitajika zaidi kuliko kuwa mtu wa kuagiza tuu bila kufuatilia maendeleo ya Kilimo chako wakati kinafanyika.


6. Tafuta ushauri wa utaalam wa Kilimo ulichokichagua.

Kabla hujaanza usisite kutafuata ushauri Wa kitaalam Wa Kilimo ulichokichagua.ili uwe karibu na kugundua tatizo katika Kilimo athari ya tatizo husika na pia hili litakusaidia kufanya Kilimo chako kwa uhakika zaidi.


7. Anza Kilimo chako kwa uhakika.

Mwisho baada ya kupitia hatua hizo juu anza kufanya Kilimo chako kwa uhakika zaidi na pia huku unatambua Kilimo nacho ni biashara kama zilivyo biashara nyingine hivyo uwe makini katika Kilimo chako ili kujiepusha na changamoto zitakazojitokeza katika Kilimo chako na changamoto hizo zisiwe kikwazo katika kukuzuia kuendelea na Kilimo chako

ebuso.blogspot.com

No comments:

Post a Comment