Ubuyu wa Nazi,Sukari/Pilipili
Njia hii inatumika sana kwa biashara ndogondogo na matumizi ya nyumbani.
-MAHITAJI MUHIMU (VIFAA)
1.Ubuyu mbichi (tamarind)
2.Sukari
3.Pilipili ya unga
4.Chumvi kidogo
5.Maji safi
6.Rangi ya chakula (hiari)
7.Karai/sufuria
8.Kijiko cha mbao
9.Sahani/trei ya kukaushia
10.Mifuko ya kufungashia
-HATUA ZA UTENGENEZAJI
1.usafisha Ubuyu
2.Chambua maganda ya nje
3.Ondoa mbegu
4.Safisha ubuyu kwa maji safi
-KUCHEMSHA:
1.Weka ubuyu kwenye sufuria
2.Ongeza maji kiasi kidogo
3.Chemsha dakika 10–15 mpaka ulainike
4.Mimina maji, bakiza ubuyu
-KUANDAA MCHANGANYIKO:
1.Ongeza sukari kulingana na kiasi cha ubuyu
2.Ongeza pilipili ya unga
3.Ongeza chumvi kidogo
(Hiari)
4.Ongeza rangi ya chakula
5.Koroga vizuri
-KUPIKA MPAKA KUKAUKA
1.Pika kwa moto wa wastani
2.Endelea kukoroga hadi mchanganyiko uwe mzito na ushikamane
3Hakikisha hauungui
-KUKAUSHWA
1.Mimina ubuyu kwenye trei/sahani
2.Tandaza vizuri
3.Weka juani au sehemu yenye hewa
4.Kaushwa kwa masaa 24–48
-KUKATA NA KUFUNGASHA
1.Kata vipande vidogo
2.Fungasha kwenye mifuko safi
3.Tayari kwa matumizi au kuuza
VIDOKEZO VYA BIASHARA
1.Tumia gloves kwa usafi
2.Pima ladha (sukari & pilipili) ili kuwavutia wateja
3.Tumia vifungashio vyenye mvuto
4.Andika tarehe ya kutengenezwa
FAIDA (MAKADIRIO)
1.Mtaji mdogo
2.Paketi 1 = TSh 200–500
3.Faida nzuri hasa shule NK
TUNAWAFIKIA POPOTE MLIPO KWA ELIMU YA UJASIRIAMALI STADI BORA ZA BIASHARA FURSA MBALIMBALI NA UWEKEZAJI
ebusol.blogspot.com
0760-240-456/0780-750-772
ebusol.blogspot.com
No comments:
Post a Comment