October 18, 2019

ZIFAHAMU HIZI AINA ZA MBOLEA



Mbolea yenye kuweza kufyonzwa na majani ya mimea 
Mbole ya kisasa na wakati ujao 
Inafaa kwa kila aina ya mimea.

D.I.GROW. 
Ni mbolea ogani kimiminiko yenye asili ya magugu ya baharini aina ya Acadia ambayo imeundwa kwa kutumia teknolojia ya Marekani. 
Imesheheni: N (Naitrojeni), P (Fosforasi), Ca (Kalisi) Mg Magnesi), S (Salfa), Fe (Chuma), Zn (Zinki), Cu (Shaba), Mo (Molebdenamu), B (Boroni), Auxini, Cytokinin, Giberellini, asidi ya mboji, magugu ya baharini, vyote hivi husababisha ukuaji wenye afya, na ustawishaji na uzalishaji.

Kuna aina mbili za  Organic Plus Fertilizer.

D.I.GROW (Growth Booster) (KIJANI) 
HUtumika wakati mmea unakuwa ukiwa mche, baada ya mavuno, na wakati afya ya mmea inapozorota 
- huchochea ukuaji mizizi, majani, na mazao haraka 
-huongeza kasi ya usanidinuru kwenye majani 
-huchochea ufyonzaji virutubisho kwenye mmea 
huendeleza upinzani dhidi ya maradhi na kinga maradhi 
-huhakikisha ukuaji na kupevuka 
-hurudisha afya kwa mmea baada ya kuvunwa.

D.I.GROW (Fruits & Flowers Enhancer) (NYEKUNDU) 
hutumika wakati mmea unachanua na kutoa matunda 
-huharakisha, kuchanua na uzalishaji wa matunda 

-hupunguza kupukutika kwa maua na matunda kabla ya wakati 
-huongeza ubora wa maua na matunda
-huzaa matunda makubwa, kwa wingi na huwa matamu zaidi 
-huongeza ukusanyaji wa usanidinuru kwa hiyo hutoa matunda,kiazi,kitunguu, mzizi 
huongeza muda ambao tunda linaweza kuhifadhiwa kwenye ghala kabla ya kuanza kuharibika.

KAMILIFU NA YENYE URARI WA VIRUTUBISHO VYA MIMEA HUONGEZA NISHATI YA MIMEA 
Imetengenezwa ili iweze kuchanganywa na viuavidudu au viuakuvu. 
Itumike mapema asubuhi au jioni.

*JIFUNZE JIAJIRI UMASKINI HAUKUBALIKI*

January 06, 2019

8.WAZO LA BIASHARA: UVUNAJI NA UUZAJI WA MKOJO WA SUNGURA

Ufugaji wa Sungura umekuwa ukiendelea kushamiri sehemu Mbali Mbali za Dunia kutokana na kuwa na bidhaa nyingi zitokanazo na ufugaji huo

Bidhaa hizo in kama

(a) Nyama

(b)Mkojo

(c)Ngozi

(d)Samadi

Licha ya kutumika Kama mapambo na baadhi ya nchi, Sungura aina ya Angola wamekuwa wakitumika kama chanzo cha Sufi kutokana na manyoya yao kuwa mengine

Mradi wa ufugaji Sungura umekuwa ni mradi pekee ambao unawekeza Leo na kuanza kuvuna Leo,leo (Mkojo na samadi)

Licha ya kuwa wafugaji wengi wamekuwa wakifuga kwaajili ya nyama, zao la Mkojo wa Sungura kwa faida yake pengine no kubwa kuliko mazao mengine yote.


Matumizi ya Mkojo wa Sungura kama mbolea;-

Kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha madini ya nitrogen phosphorus na potassium mbolea ya Mkojo wa Sungura imekua mbadala wa mbolea za NPK na CAN ambazo kwa kiasi kikubwa zimekua zikichangia ongezeko la soil acidity

Ikitumika katika ratio ya lita moja ya Mkojo wa Sungura kwa lita 5 za maji kunyunyuzia katika majani au ardhi wakati wa asubui au jioni kipindi ambapo stomata zipo wazi itakupa matokeo mazuri katika viazi,maharage,

miche ya matunda, mbogamboga, mahindi na mazao mengine

Lakini pia Kama kimiminika cha asili chenye uwezo wa kurudisha rutuba iliyopotea ardhini

Matumizi ya Mkojo wa Sungura Kama kiuatirifu (insecticides)

Mkojo wa Sungura una,kiasi kikubwa cha Ammonia ambayo ndio makali yake halisi ambayo Uharibu kabisa mazingira rafiki ya uzalianaji wa bacteria na fangasi katika mmea

Mkojo wa Sungura ukitumika kwa kiasi cha lita 1 katika Lita 2 za maji kunyunyuzia katika majani ambayo yameshambuliwa na wadudu kila siku,huua wadudu na kurejesha afya ya mmea

Mkojo wa Sungura huua wadudu kama aphids,fungus, mites ,leaf miners nk

Katika mmea ambao haujashambuliwa, ukinyunyuzia kwa wiki Mara,moja inatosha kuupatia mmea afya bora,ustahimilivu wa magonjwa ya bacteria na fangasi pia kukupatia mavuno mengi.

January 03, 2019

NAMNA YA KUJENGA BUSTANI YA GUNIA



UTUNZAJI WA KITALU CHA BUSTANI

Na Ombeni Haule cdf

Baada ya kuandaa kitalu hakikisha unakitunza vizuri ili kuweza kupata miche bora ya kupandikiza shambani. Matunzo ya kitalu hujumuisha mambo yafuatayo;

Kujengea kichanja/Kivuli (Shading)

Umwagiliaji

Kupiga dawa za wadudu na magonjwa

Kupunguzia miche na

Kuitayarishaji miche kabla ya kuipandikiza.

(a) Kujengea kichanja / Kivuli

Mbegu zitakapoota ondoa matandazo na tengeneza kichanja chenye kimo cha mita 1 kutoka ardhini kilichotandazwa nyasi au makuti kufunika kitalu. Kichanja hiki hutengenezwa ili kuipa kivuli miche ambayo bado ni michanga isije kuungua na mionzi ya jua na kushindwa kukua vizuri. Vilevile kichanja husaidia kupunguza kasi ya matone ya mvua kubwa ili miche isijeruhiwe.

(b) Umwagiliaji

Mwagilia maji kitaluni kila siku asubuhi na jioni hadi wakati wa kutayarisha miche. Ni vyema kuzingatia uwezo wa udongo kutunza maji ili kuepuka kuzidi kwa kiwango cha maji kunakoweza kupelekea kudumaa kwa miche kitaluni na kuchelewesha upandikizaji.

(c) Kupunguzia miche

Punguza miche kitaluni ili kuondoa msongamano wa miche na kubaki na miche itakayoweza kukua vizuri kwa nafasi. Hili ni muhimu hasa kwa miche yenye majani mapana kama vile miche ya nyanya na kabichi. Miche ya kabichi hupunguziwa siku nne hadi wiki moja tangu mbegu kuota wakati miche ya jamii ya nyanya hupunguziwa baada ya wiki moja tangu kuota kwa mbegu. Miche iliyopunguzwa katika tuta moja inaweza kuhamishiwa katika tuta lingine.

(d) Kupiga dawa za Wadudu na Magonjwa

Unaweza kuanza kunyunyizia dawa za ukungu na kuua wadudu wiki moja hadi mbili tangu miche kuota. Chagua dawa kulingana na wadudu waharibifu na magonjwa yanayo shambulia zao husika. Hakikisha unafuata maelekezo ya dawa husika.

(e) Kuitayarisha miche (Acclimatization)

Miche hutayarishwa ili isipate tabu kuzoea hali ngumu ya shambani na hivyo kupona haraka inapopandikizwa. Utayarishaji wa miche hufanywa kwa kupunguza matandazo ya nyasi katika kichanja polepole kuanzia wiki mbili kabla ya kupandikiza. Ondoa kivuli chote na punguza kiwango cha maji ya kumwagilia wiki moja kabla ya kupandikiza ili kuiwezesha miche kuzoea hali ya ukame.

Zingatia: Usichelewe kupandikiza miche kwa sababu miche mikubwa ni vigumu kuihamisha na mizizi yake ni mirefu hivyo inaweza kukatika kwa urahisi. Pandikiza miche ikiwa na mizizi iliyozungukwa na udongngo