December 31, 2018

TENGENEZA DONAT YA ICING SUGAR

Mahitaji :


Unga – Mug 1

Sukari 1/3 kikombe ( mug ) 

Mayai  5

Siagi - 4 Vijiko vya kulia

Hamira  1 Kijiko kulia

Baking Powder - 1 Kijiko cha chai

Vanilla - 1 Kijiko cha chai

Hiliki zilizosagwa -  1 Kijiko cha chai

Sukari ya laini ya unga (icing sugar) mug 1


Maelezo : 


Kwenye bakuli pana vunjia mayai, unatia sukari, hamira, baking powder, vanilla na hiliki ikisha unapiga kwa kutumia mchapo wa kupigia keki ama mwiko kwa nguvu. Unapiga mchanganyiko kwa muda wa dakika tano. Weka siagi kwenye sufuria na yeyusha na kuipasha moto mpaka iwe moto ikisha unaimimina kwenye mchanganyiko  na unapiga tena kwa dakika mbili tu. Weka unga kwenye sinia au bakuli kubwa ikisha unamimina ule mchanganyiko kwenye unga na unaukanda kutumia mkono, mpaka ulainike.Ukiona unga mwingi basi ongeza maziwa kidogo mpaka uwe sawa, na ukiona unga mwepesi sana basi unaweza kuongeza unga kidogo pia mpaka ukae sawa mfano wa unga wa maandazi.Sukuma na ukate madonge kama unavyoyaona hapo juu. Tumia kifuniko cha chupa kwa kukatia kiduara kidogo katikakati ya madonge. Ukimaliza kukata madonge yote, yaweke kidogo yaumuke halafu teleka mafuta na uyakaange.

Ukitoa kwenye mafuta yachuje mafuta na kabla ya kupoa yawe moto moto yachovye kwenye icing sugar na uhakikishe yote yameenea sukari juu. Ukimaliza tia kwenye sahani acha zipowe na zitakuwa tayari kwa kuliwa.


BY MAPISHI RAHISI NA FASTA FASTA.

TENGENEZA KATLESS HIZI HAPA (KACHORI)

 KACHORI  HUTUMIKA KAMA KITAFUNWA KWAJILI YA PICNIC, CHAI YA ASUBUHI AU SAA 10 JIONI HUPENDWA SANA NA WATU WA LIKA ZOTE. KACHOLI HII NI MAALUMU KWA WALE WENYE MATATIZO WASIOTUMIA UNGA WA NGANO.

MAHITAJI

300 gram nyama ya kusaga

1 kilo ya viazi ulaya (5-6)

1 kijiko cha chakula Mafuta ya kupikia

½ kijiko kidogo cha chai Cumin seeds (Jeera) 

1 ½ kijiko kidogo cha chai Coriander powder (Dhaniya) 

2 pili pili mbuzi au ndefu za kijani 

1 ½ Tangawizi mbichi

¼ Kijiko cha chai Garam Masala

4 kijiko kikubwa cha chakula maji ya limao au ndimu

 ½ chumvi

10 gram kitunguu swaumu

5 mayai ya kuku

Mafuta kwajili ya kukaangia

JINSI YA KUTENGENEZA

Chemsha viazi kwenye pressure cooker au sufuria vikiwa na maganda yake.

Chemsha nyama ya kusaga na maji 50 gram, kitunguu swaumu 10 gram na vijiko 4 vya mai ya limao mpka iive kisha weka pembeni.

Kisha menya viazi ulivyochemsha kisha kata katika vipande vidogo. Pasha mafuta ya kupikia kijiko kimoja kwenye kikaango.

Kisha weka mbegu za cumin kwenye kikaango. Mbegu za cumin zikishapasuka, ongeza coriander powder, pili pili mbuzi, Tangawizi, Kisha weka chumvi na viazi. Kaanga kwa dakika 2-3 itakua imeiva vizuri.

Kisha ponda mchanganyiko wako mpaka uwe laini kabisa

Kisha chukua mchanganyiko huo laini wa viazi na tengeneza maumbo madogo ya mviringo ukubwa kama limao kisha bonyeza kwa kutumia kidole kati kati ya umbo hilo utapata nafasi ya kuweka kijiko kimoja cha chai nyama ya kusaga iliyoiva kisha funika kwa kutumia viazi na jitaidi kuviringisha tena kwa kutumia mikono yako miwili ili upate umbo zuri.

aada ya kumaliza kuandaa maumbo safi kabisa ya duara na yenye nyama ya kusaga kwa ndani, piga mayai pembeni kwenye bakuli na chovya umbo moja moja na weka kwenye kikaango chenye mafuta ya moto kaanga ukishapata rangi tu ya kahawia toa maana viazi na nyama vimeshaiva unachotafuta ni kau kau na rangi safi ya kahawia pande zote.

MPATIE MLAJI KACHORI HII IKIWA YAMOTO PIA UNAWEZA USIWEKE PILI PILI NA TANGAWIZI HASA KWA WALE WANOSUMBULIWA NA VIDONDA VYA TUMBO AU MATATZIZO YA GESI TUMBONI NA BADO KACHORI YAKO IKAWA SAFI SANA. UNAWEZA KULA NA TOMATO SAUCE, MAYONAISE, CHACHANDU AU ACHALI.

*From Alhidaaya*

TENGENEZA HII KEKI SIMPLE SANA

Hakuna kitu chochote kitamu chenye harufu na radha nzuri kama keki uliyoipika kwa mikono yako. Upishi wa keki ni mwepesi sana endapo mpishi atazingatia vitu muhimu vinavyohitajika pamoja na hatua zake. 


*MAHITAJI*

*unga vikombe2

*maziwa kikombe1

*sukari kikombe1

*siagi kikombe1

*baking powder vijiko vidogo 2

*mayai 6 yakienyeji

*vanilla matone mawili au limao 1 Zingatia Limao au vanilla hutumika kwaajili ya kupunguza harufu ya mayai kwenye keki.kwahiyo ukikosa vanilla pia waweza kutumia maganda ya limao au maganda ya chungwa. 


Pia andaa jiko lako la mkaa mapema ili lipate joto pamoja na sufuria iliyopakwa siagi ndani ili kuzuia keki kuganda.


*HATUA*

*Andaa bakuli lako la udongo na mwiko ambao utatumia kuchanganya mchanganyiko wako


*chukua kikombe kimoja cha siagi na utie katika bakuli pamoja na kikombe kimoja cha sukari.


*koroga mchanganyiko wa sukari na siagi mpaka pale utakapolainika na chembe chembe za sukari kupotea kabisa


*Weka yai moja baada ya jingine huku ukiendelea kuukoroga mchanganyiko wako bila kupumzisha mkono


*Weka matone mawili ya vanilla au maganda ya limao huku ukiendelea kuchanganya.


*Weka unga vikombe viwili uliochanganywa na baking powder kwenye mchanganyiko wako na endelea kuukoroga taratibu


*Baada yahapo tia maziwa kikombe kimoja nauchanganye taratibu


*Mimina taratibu mchanganyiko wako kwenye sufuria maalumu yakupikia iliyopakwa siagi. 


Zingatia Iwapo utapenda keki yako iwe na rangi unaweza ukaweka kokoa kwenye mchanganyiko wako.


*Weka sufuria ya mchanganyiko katika jiko lenye joto la wastani kwa muda wa nusu saa

Yani makaa juu na chini


*Baada ya hapo toa keki yako tayari kwakuliwa.

December 30, 2018

*JINSI YAKUTUMIA MBEGU ZA MABOGA, FAIDA ZAKE,NA JINSI GANI UNAWEZA KUTUMIA MBEGU ZA MABOGA KAMA DAWA*

*MAGONJWA HATARI 10 YANAYOTIBIKA KWA KUTUMIA MBEGU ZA MABOGA*


*UTANGULIZI*

- Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya muhimu zaidi mwilini kama madini ya zinki, kopa, maginizia, manganizi na chuma, mbegu za maboga ni tamu na zinaweza kutafunwa nyakati zozote na mahali popote.


- Tafiti mbalimbali zimethibitisha pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida nyingi kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10 yafuatayo:


*1- UGONJWA WA MOYO*

- Kiasi kingi cha madini ya magnesium katika mbegu za maboga yanazifanya mbegu hizi kuwa mhimu sana kwa watu wenye magonjwa mbalimabli ya moyo.


- Madini ya magnesium ni mhimu kwa ajili ya kuimarisha msukumo wa damu kwenye moyo na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hatimaye kutibu na kuzuia magonjwa ya moyo.


- Mbegu hizi pia zina mafuta mengine mhimu zaidi kwa watu wenye ugonjwa wa moyo yenye *OMEGA 3*


*2- HUIMARISHA KINGA YA MWILI*

- Mbegu za maboga zimebarikiwa kuwa na kiasi cha kutosha cha madini ya zinki (zinc). Kazi kubwa ya madini ya zink ni kuimarisha kinga ya mwili.


- Upungufu wa madini ya zink unaweza kupelekea matatizo kadhaa mwilini ikiwemo kuzaa watoto njiti, kuishiwa nguvu za kiume, matatizo ya homoni, chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo shuleni kimasomo na matatizo mengine kadhaa ya kimwili na kiakili.


*3- HUONGEZA UWEZO WA MACHO KUONA*

- Mbegu za maboga zina Vitamini E, vitamini A, lutein, beta-carotene na zeaxanthin, vitu hivi vinavyopatikana katika mbegu za maboga ni mhimu kwa ajili ya nuru ya macho. Vitamini A na madini ya zinki ni mhimu kwa ajili ya uzalishaji wa ‘melanin’ kimeng’enya mhimu ambacho hutengenezwa kwa asili na miili yetu kwa ajili ya ulinzi wa afya ya macho.


*4- KINGA YA KISUKARI*

- Kisukari ni moja ya ugonjwa unaoendelea kwa kasi na kuwasumbua watu wengi kila pembe ya dunia.


- Mbegu za maboga zina vitu vitatu mhimu zaidi ambavyo ni *Nicotinic acid’,* *‘Trigonelline’* na *D-chiro-inositol’* ambavyo husaidia kushusha damu sukari mwilini na kudhibiti kazi za *insulini* hivyo kuwa kinga na kuleta ahueni kubwa kwa watu wenye kisukari.


- Kama unasumbuliwa na kisukari fanya mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku.


*5- DAWA BORA YA USINGIZI*

- Mbegu hizi zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha homoni za usingizi.


- Kwenye mbegu za maboga kuna vimeng’enya viwili mhimu zaidi ambavyo huhusika na usingizi na afya ya akili moja kwa moja navyo ni *‘L-tryptophan’ na ‘tryptophan’.* Gramu 100 tu za mbegu za maboga zina kiasi cha kutosha cha *tryptophan’* mpaka mg 576. Tryptophan ndiyo inahusika kuleta usingizi wenye utulivu pia huondoa msongo wa mawazo au stress mwilini.


- Kwa kuongezea mbegu za maboga zina kiasi kingi cha vitamini za kundi B. Muda mchache kabla ya kwenda kulala tafuna mbegu za maboga na utapata usingizi mtulivu kabisa mpaka asubuhi.


- Kwahiyo kama una tatizo la kukosa usingizi jaribu kutumia mbegu za maboga


- Kumbuka kukosa usingizi mara nyingi huwa ni matokeo ya msongo wa mawazo na kama ulivyoona mbegu hizi zinaondoa pia stress!


*6- DAWA BORA YA UVIMBE*

- Mbegu za maboga zinao uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini sambamba na uvimbe *(inflammation).* Kama ujuavyo sehemu kubwa ya vivimbe mwilini ni matokeo ya sumu kadhaa mwilini.


-  Mbegu za maboga zitakuondolea uvimbe mwilini bila kukuachia madhara yoyote mabaya hapo baadaye.


- Kama unasumbuliwa na uvimbe popote jaribu kutumia mbegu za maboga


- Mbegu za maboga pia ni dawa nzuri kwa aina nyingi za kansa mwilini.


*7- HUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAYENYONYESHA*

- Mbegu za maboga zina protini nyingi bora itokanayo na mimea isiyo na madhara kama ile ya kwenye wanyama.


- Pia zina *OMEGA 3* Mama mjamzito hata unayenyonyesha tumia mbegu za maboga na utakuwa na uhakika wa kutoa maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto.


*8- DAWA NZURI KWA MATATIZO YA TEZI DUME*

- Wataalamu wengi wa lishe wanapendekeza mbegu za maboga zitumike kwa wanaume wa rika zote yaani vijana hadi wazee kwani zimethibitika kuwa msaada mkubwa kwa afya ya tezi dume.


- Tafiti nyingi zinasema mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya Zinki madini ambayo ni mhimu *SANA* kwa afya ya tezi dume na husaidia uponyaji wa tatizo la tezi dume moja kuwa kubwa kuliko nyingine tatizo lijukanalo kwa kitaalamu kama *benign prostatic* *hyperplasia’.*.


*9.- ZINAONGEZA NGUVU ZA KIUME*

- Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado.


- Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo/stress kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, lakini pia zinashusha lehemu *(cholesterol),* zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), zinashusha kisukari, zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya zaidi ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili na Zina madini ya chuma pia


- Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote, ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ukiwa ofisini unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako. Sambamba na hilo kama tulivyoona pale juu kwamba zinaongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha kwa upande wa wanaume zinaongeza pia uwingi wa mbegu za kiume *(sperm count)* ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utapata kuona matokeo mazuri.


*10- ZINAONDOA PIA MSONGO WA MAWAZO (STRESS)*

- Msongo wa mawazo au stress kama mlivyozoea wengi ni tatizo linaloendelea kuwasumbua watu wengi miaka ya sasa. Mbaya zaidi wengi huwa hawaelewi nini madhara ya hizo stress wanazojipa. Yaani stress au msongo wa mawazo unaweza kukuletea magonjwa mengine mwilini zaidi ya 50, hivyo utaona ni jinsi gani ilivyo mhimu kwako kuweka chini stress zako na uendelee na maisha kwani kuendelea kuwa na stress ni hatari zaidi kwa afya yako.


- Moja ya sababu kuu ya watu wengi kuwa na stress ni usawa usio sawa wa homoni zao *(hormonal imbalance)*


- Hivyo kama una tatizo la homoni kwenye mwili hebu weka mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na hutakawia kuona tofauti.


-  Mbegu za maboga zina kimeng’enya mhimu sana kwa kutuliza mawazo kiitwacho *‘tryptophan’* na asidi amino zingine mhimu zinazohusika kutengenezwa kwa homoni nyingine ijulikanayo kama *‘serotonin’*.


- Kama ulikuwa hujuwi ni kuwa *serotonin* ni homoni inayohusika na kazi mhimu sana ya kurekebisha matendo ya kitabia na kutoa matokeo chanya kwa mambo yanayohusu usingizi, hali ya mawazo kwa ujumla na mambo yanayohusu njaa.


- Mbegu za maboga ni msaada mkubwa kwa kina mama waliofikia ukomo wa siku zao na huondoa matatizo ya kiafya yatokanayo na kukoma kwa hedhi.


- Ni msaada kwa watu wenye saratani mbalimbali, huimarisha ukuaji na ustawi wa mifupa na meno, huondoa harufu mbaya ya kinywa na husaidia pia wenye tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara.

*NAMNA NZURI YA KULA MBEGU ZA MABOGA*


- Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa wengi wanapenda zilizo kaangwa



- ukikaanga isizidi dk15 - 20 hivi na huwa nazichanganya na maji ya chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.


- Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga kwa siku ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kwa siku.

JINSI YA KUANZISHA BUSTANI NDOGO NYUMBANI.

*ebusol cdf*

Uanzishaji wa bustani nyumbani ni jambo ambalo huwaweza kulifanya kwa kiasi ambacho kinaweza kukuletea faida kemkem, Kwa kutumia malighafi unazo ziona nyumbani waweza fanikisha zoezi hili, iwe ni mifuko ya nailoni. Makopo, gunia, au kiji pande kidogo cha ardhi na ukaweza kukitunza.

Mboga ambazo unaweza kuzizalisha nyumbani ni kama mchicha, nyanya, kitunguu, sukuma wiki, kabichi, chinizi, majani ya maboga na pilipili (kali au hoho).

Mboga zilizo nyingi hutumia muda wa miezi mitatu hadi kufikia muda wake wa kuvunwa, Hivyo hakiwezi kukuchosha na mazao kama mchicha huchukua wiki karibuni 2 mpaka 3 na unaweza kutumia/kuvuna.

Faida za mbogamboga hizi ni nyingi ikwemo kiafya kwani husaidia kuongeza damu mwilini, kutupatia nguvu na hata kutusaidia uwezo wa kuona vizuri kama mchicha na karroti. Pamoja na hata kiuchumi kama uzalishaji wako hapo nyumbani utakidhi na ziada waweza fanya biashara.


FAIDA ZA BUSTANI HIZI ZA NYUMBANI.

- Ni rahisi sana kufanya.

- Ni chanzo kizuri cha mboga nyumbani.

- Inasaidia watoto kupenda kula mboga za majani, kwani uweza kuziona jinsi zinavyozalishwa na kupenda zaidi uzalishaji.

- Ungalizi wake ni wa karibu na hata udhibit wa magonjwa ni mkubwa.


AINA ZA BUSTANI AMBAZO NI RAHISI SANA KUANZISHA UKIWA NYUMBANI.

- Kwa kutumia makopo au makasha ya mbao.

- Kwa kutumia gunia.

- Kwa kuandaa kitalu.


BUSTANI YA MAKOPO/NDOO NA MAGUNIA

Bustani ya makopo hiutaji vitu vifuatavyo,

- Kopo/ndoo.

- Udongo.

Udongo huwezesha mmea kujishikiza pia kuupatia mmea virutubisho muhimu.

- Mbolea za samadi.

Kwaajili ya kuupatia mmea viini lishe.

- Pumba za mpunga/mchanga

Pumba husaidia kuupatia mmea kupitisha maji, pia kupitisha mizizi.


HATUA MUHIMU ZA KUFUATA.

1. Changanya udongo wako na mchanga/pumba za mpunga na mbolea kwa uwiano wa udongo 5:2:1

2. Toboa chombo utakachotumia iwe ni gunia au kopo.

3. Weka mchanganyiko wote katika chombo ulicho nacho kisha weka mche au mbegu.


BUSTANI ZA KWENYE KITALU/VITALU

Endapo hautatumia kopo au gunia tengeneza kitalu chako kwa kuchanganya udongo na mbolea pekee.

Kisha panda mbegu/miche yako kwa nafasi.


UANGALIZI.

Kila zao lina aina yake ya uangalizi japo nyingi hifanana sana kwa zao kama nyanya hutaitajika kuweka miti maalumu kwa ajili kuipatia sapoti, kuepuka kuanguka chini na hata kupelekea kufa kwa mmea.


MAMBO YA KUZINGATIA.

- Mwagilia mboga yako mala baada tu ya kupanda na kuendelea ikitegemeana ni aina gani ya mboga.

- Unapoona wadudu au dalili yeyote ya magonjwa fuata taratibu zote za utumiaji viatilifu kuzuia kusambaa kwa wadudu au magonjwa hayo.

- Mboga kama sukuma wiki, nyanya, pilipili, waweza vuna mara kwa mara, kazi yako ni kumwagilia tu.

- Usiweke bustani yako katika kivuli na bali iwekwe katika sehemu ambayo mwanga wa jua itaifkia mimea, kwa kuiweka katika kivuli itapelekea mmea kudumaa, hivyo inapaswa ikae katika mwanga.

- Endapo hutatumia makopo au gunia unatakiwa kubadilisha udongo wako kwa muda, Baada ya mavuno ya misimu ili kuakikisha mboga zako zina pata virutubisho ya kutosha.


CHANGAMOTO ZA BUSTANI HIZI ZA MBOGAMBOGA.

Kwa watu wengi hupatikanaji wa maji ya uhakika inaweza kuwa ni shida sana.

Kuna baadhi ya mbinu unaweza tumia na ukatumia maji uliyo nayo kwa ufanisi wa hali ya juu.

- Kwa kutumia makopo ya maji makubwa, weka maji na kisha toboa tundu dogo kwa chini kisha funga kifuniko chako vyema kutorusu hewa kuingia, kwa kufanya hivyo utawezesha matone madogo ya maji kuufikia mmea, nah ii itakuwezesha kutotumia maji na maji megi na bali maji yataakayo tumika yatatumika kwa ufasaha sana.

- Tumia kilimo cha matone, kwa kutengeneze mfumo mdogo tu wa mirija hata kwa wale watakao tumia kitalu. Weka kiifadhia maji kwa juu na kisha unganisha kwa kutengeneza mirija midogo/mipira midogo na itoboe kulingana na nafasi ya miche yako.

- Weka matandazo kuzunguka mmea yanaweza kuwa ya nyasi kavu au Maranda ya mbao, hii itasaidia kuhifadhi unyenyevu uliopo kuendelea kuwepo kwa kupunguza upotevu wa maji kwa jua kali

CHANGAMOTO ZA UTENGENEZAJI WA CHAKULA CHA KUKU.

Gharama za ufugaji wa kuku zikiwa asilimia 100. basi 80 huwa ni chakula na 20 ndo mambo mengine kama dawa.


Watu wengi tumekuwa tukijaribu kutengeneza chakula ili tushushe chini gharama za kufuga kuku. Hakuna anaye pe nda kuguga kwa gharama za juu.


NIN CHANGAMOTO ZAKE?

1. Upatikanaji wa malighafi

Unaweza kuwa na nia ya kutengeneza kweli chakula lakini.unaweza zunguka na usipate baadhi ya malighafi.


2. Malighafi kutofautiana ubora

Moja ya chalange kubwa hasa kwa utengenezaji wa chakula cha kuku sa kisasa kamaBroiler na layers ni ubora wa Malighafi

Je mahindi unayo tumia yana ubora? Soya je? Dagaa au samaki je?

Hivi vitu saa zingibe vyenyewr hutofautiana ubora na unaweza kuta kabisa kabisa DCP iliyoko kwenye mahindi yanayo limwa Songea ikawa tofauti kabisa na yanayo limwa Dodoma.

Unaweza kuta soya ikawa na DCP tofauti tofauti.

Unaweza kuta Dagaa wa Baharini wakawa na DCP tofauti na dagaa wa ziwani kama Victoria au Tanganyika.

Hii hiwa ni changamoto namba 1.


3. Gharama za kutafuta Malighafi.

Unaweza jikuta badala ya kupunguza gharama ukajikuta umeongeza gharama mara 2 zaidi.

Unaweza toka nyumbani kwenda kununua malighafi. Ukafika ukakuta Hilo Duka soya hakuna inabidi uwashe gari au upande Daladala uende kwingine. unafika na huko unakuta hakuna inabidi uende kwingine tena.

Ukijumlisha hizo gharama za usafiri unajikuta umetumia gharama kubwa sana.


Je huwa unapiga hizo gharama za mizunguko?

4.Formula ya kutengeneza vyakula.

Hii ni changamoto kubwa sana na kuna jambo watu huwa hatujui kuhusu hizi formula.


- Formula inabadilika unavyo taka, 

- Kuna Formula nyingi sana hata wewe unaweza unda Formula yako na ikawa bora zaidi.

- Watu hutengeneza formula kutokana na mambo kama haya:

A. Climatic condition- Baridi au joto

B. Aina ya breed, Wazalishaji wa breed mara nyingi huwa na formula zao kwa ajili ya breeds zao na unakuta wamefanyia majaribio na kuamua hivyo.

C. Upatikanaji wa malighafi na ubora wake pia. Kama nilivyo sema nafaka moja inaweza kuwa na ubora tofauti.

- Formula inategemeana wewe una nini mkononi.


5. Kukosa vyombo vya kupimia DCP, hii sasa  ndo huwa kikwazo kikubwa kabisa kabisa.

Huwezi pima DCP kwa macho, kama kiutalamu DCP ya vifaranga ni asilimia 19 hadi 23 je utaijuaje? utajuaje sasa hiki chakula kina DCP ya 23%? ni ngumu sana.


NINI CHA KUFANYA?


1. Malighafi zinunuliwe kwa wakati mmoja hasa kipindi cha mavuno na zihifadhiwe, kufanya hivyo kutakupunguzia usumbufu wa kuzitafuta.


2. Kwenye Malighafi ya aina moja kiwa na ubora tofauti ni changamoto kubwa sana ambayo sasa hapo lazima uwe na vipimo vya kupimia DCP kujua ni kiwango gani, pia kununua sehemu moja, kama ni dagaa basi tumia wa Ziwani siku zote au wa Baharini siku zote na sio leo wa baharini kesho wa ziwani.


3.FORMULA

Formula sio tatizi kabisa kwenye kutengeneza vyakula, unaweza tengeneza formula yako wewe mwenyewe na kuifanyia majaribio. 


4. Tafuta sehemu zenye vyombo vya kupimia DCP ili iwe inapelekea sampo kwa ajili ya kupima na kujua chakula chako kina DCP kiwango gani.


UTENGENEZAJI WA CHAKULA KWA KUKU WA KISASA HASA BROILER NA LAYER


Hapa ndo challange ilipo na hii ni kutokana kwamba hawa ni exotic breeds.


Unapo anza kutengeneza anza na kidogo sana na tenga kuku wachache wa kuwafanyia majaribio.

Ndani ya banda unaweza kata na kutenga Broiler hata10 na wafanyia majaribio kwa chakula chako, na kila siku waangalie na wapime uszito kujua utofauti wake na ambao wanakula cha Dukani. 


Usikurupuke kutengeneza chakula kingi make mwisho wa siku utakitupa tu na utakuwa umeingia hasara.fanya try and erro.

Unaweza tengeneza hata  kwa formula tatu tofauti na kuwafanyia majaribio kuku tofauti.


DCP= Digestive Crude Protein. Hiki ndo kipimo cha kupima ubora wa chakula cha kuku.

ebusol cdf

JINSI YA KUTENGENEZA MINYOO KWAAJILI YA KUKU

ebusol cdf

Kutengeneza minyoo ya chakula (red worms planning) Red worms planning ni utaratibu wa kuzalisha minyoo kwa ajili ya kuku na Samaki, Zipo hybrid Red Worms ambazo mara nyingi hununua sample kutoka nje ya nchi Kama Kenya,China au hapa Tanzania fuata hatua zifuatazo kuzalisha Red worms asilia. 1.Chukua mavi ya ngombe mapya au ngombe aliyechinjwa mavi ya tumboni 2.Kusanya Damu damu, ngozi, utumbo, magoroto, nyamanyama nk

3.Pakia kwenye kiloba au gunia kati ya chaguo A au B hapo juu

4.Chimba shimo la wastani kisha mwagia maji ndoo kubwa 4

5: Fukia hilo gunia na mwaga maji ndo 2 mara 1/2 kwa siku kwa muda wa siku 8/12

6: Baada Ya siku hizo kupita fukua na chepe utakuta minyoo mitupu ya kutosha kwa ajili ya chakula cha kuku au samaki na siku zinavyozidi kwenda ndo wanazidi kuzaliana na kuwa wakubwa.


JINSI YA KUTENGENEZA FUNZA KWA CHAKULA CHA KUKU .

Moja ya virutubisho muhimu kwa kuku ni protini ambayo unaweza ukawapa kupitia vyakula mbalimbali. Funza ni wadudu walio na protini nyingi ambayo inahitajika sana kwa ajili ya ukuaji wa kuku. Zipo njia mbalimbali ambazo zinatumika kutengeneza funza na hivyo kukupunguzia gharama za vyakula vya kuku. Jinsi ya Kutengeneza funza. Tafuta kinyesi cha kuku au mavi ya ngo'mbe ambayo unaweza pata machinjioni au kuku wako mwenyewe. Chukua kinyesi weka kwenye kidumu kilichokatwa kisha weka pumba za mahindi kwa juu. Halafu weka maji kidogo ili kuvutia nzi waweze taga mayai hapo. Utaendelea kuweka maji kwa siku mbili na kisha uache siku tatu. Siku ya nne au ya tano funza wataanza kutokea, wakusanye, waoshe na kisha wape kuku wale.


KANUNI AU HATUA ZAKUFUATA KUTENGENEZA MCHWA

1. Andaa mahitaji muhimu yanatakiwa -kinyesi kikavu cha ngombe au mbuzi -majani makavu,au mabua ya mahindi,maharage hata maranda unaweza tumia mojawapo au ukachanganya -chungu,au sufuria au box 2. Changanya vitu tajwa hapo juu vyote vizuri

3. Nyunyizia maji kila kilichomo kilowane kiasi 4. Weka mchanganyo wako kwenye chombo ulichokiandaa,chungu,sufuria au box

5. Chukua chombo hicho kakiweke sehemu ambayo unahisi mchwa wanaweza kupatika mfano,kichuguu, kwenye njia mchwa, sehemu nyingi ya ardhi kavu mchwa wanapatika

6. Acha chombo chako hapa kwa masaa 24, ila chombo umekiweka kwa kukifunika upande mmoja uwe umenyanyuka kidogo kuruhusu hewa kuingia kwenye mchanganyiko

7. Baada ya huo muda mchwa wengi watakuwa wamezalishwa ndani ya chombo chako

8. Chukua chombo kwa upesi kwa kukigeuza ili mchwa usirudi aridhini kisha kawape kuku wako, zoezi hili ni jipesi sana halihitaji wewe kutumia muda mwingi fanya kila siku ili vifaranga na kuku wako wastawi vizuri.