September 29, 2018

MAGONJWA YA KUKU, TIBA NA KINGA

KIDERI

Ugonjwa huu huathiri kuku katika umri wowote na unapoingia kwenye kundi huweza kuua idadi kubwa ya kuku hao hadi kufikia asilimia tisini. Ndege wakubwa hustahimili kidogo kuliko wale wadogo kwasababu ya usugu mwilini (body immunity) uliojengeka kwa muda mrefu zaidi.


Ugonjwa huu husababishwa na kimelea cha kirusi kiitwacho Paramyxo viridae na huenezwa kwa njia ya hewa na kugusana.



Dalili zake:


Kukohoa na kuhema kwa shidaUte hutoka mdomoni na puaniKuku walioathirika hupata kizunguzungu.Kuharisha uharo wa kijani na njanoKuzubaa, kusinzia na mabawa kushukaBaada ya siku 2 kuku hupindisha shingoKuvimba machoKuzungukaKuku hutaga mayai hafifu.90% ya kuku huweza kufa

Tiba:

Ugonjwa huu hauna dawa.

Kinga

Kuchanja;

Chanja kuku wako kila baada ya miezi mitatu /na mara nne kwa mwaka.

Kuna chanjo aina mbili za ugonjwa huu, nazo ni;

Lasota: 

Inashauriwa kuku wanaopewa dawa hii wanyimwe maji ya kunywa siku moja kabla yake


Ni  vizuri kuwapa mchanganyiko maalum wa dawa wenye mchanganyiko wa  vitamin na dawa ya kuwaongezea kuku nguvu. Dawa hii itolewe saa moja au zaidi  baada ya kuwapa chanjo ya mdondo.


Thermostable I2 NCD vaccine:

Huwekwa katika chupa kimoja (vial) chenye dozi 400 za kukuChanjo hii inavumilia joto ikikaa bils nje ya jokofu kwa muda mrefu zaidi.Imetengenezwa katika mazingira ya nchi za joto.

Na inaweza kukaa kwa siku 14-15 ikiwa itatunzwa ipasavyo hata baada ya kutumia mara ya kwanza.

2)      Kuharisha Damu (Coccidiosis):


Ugonjwa huu husababishwa na kimelea cha protozoa cha jamii ya Eimeria (Eimeria tenela, Eimeria maxima, na Eimeria acervulina)


Kwa kawaida wadudu hawa hupenda kuishi kwenye mazingira machafu, kama vinyesi, vyakula vilivyooza na umaji maji (moist environments).


Dalili zake:

Kinyesi chake huchanganyika na damu


1)  Wakati mwingine kuku hunya damu


2)  Kuku hudhoofika sana


3)  Kuku huteremsha mabawa yake


4)  Hatimaye vifo hutokea

Kushusha mabawa.

 Kuharisha damu.

 Utumbo wenye damu

Tiba;


Ugonjwa huu hutibika kwa kutumia dawa za


(i) Kundi la suphur


Mfano: sulphonamides (ESB3) kwa siku 3-4


(ii) Amprolium


Dawa za ugonjwa huu hupatikana madukani hivyo ukipatwa na tatizo hilo fika kwenye maduka ya dawa aua muone mganga wa mifugo.


Kinga:


Zingatia usafi mara kwa mara


Kwakuwa ugonjwa huu huambatana na majimaji na uchafu wenye vimelea vya ugonjwa huu, ni  vizuri kuhakikisha banda la kuku linakuwa safi na kavu wakati wote.


Tenga kuku wagonjwa kutoka kwa walio wazima.Tumia dawa ya kinga ili kuepusha uwezekano wa kuku kuambukizwa ugonjwa huu


Dawa inayopendekezwa ni zile zinzoitwa (coccidiostat.


Tenga kuku wadogo (vifaranga) kutoka kwenye kundi la wakubwa.



3)      Homa ya Matumbo (fowl typhoid)


Husababishwa na vimelea vya wadudu wa bakteria wa jamii ya Salmonella.


Kimelea hicho cha bacteria huitwa Salmonella gallinarum.


Dalili zake:


Uharo mweupe au wa kijaniVifo hufikia kiasi cha 50%Rangi ya minofu hugeuka kuwa ya njanoViungo vya ndani kama maini , figo , bandama huvimbaMaini hung’aa kwenye mwanga mkali.


Tiba :Tumia dawa za antibiotiki kama vile furazolidone ili kutibu ugonjwa huu.


KINGA: Chanja kuku wako mara kwa mara .


Fanya usafi wa banda na vyombo vya kulishia na kunyweshea maji ipasavyo.



4)      Ugonjwa wa Mafua ya Ndege


Ugonjwa wa mafua ya ndege ni ugonjwa hatari sana kwa kuku na jamii nyingine za ndege.Pia ugonjwa huweza kuambukizwa na kusababisha vifo kwa binadamu.Ugonjwa huu husababishwa na kirusi kiitwacho OrthomyxovirusUgonjwa huu huenezwa kwa njia ya kugusana baina ya ndege na ndege  na baina ya ndege na binadamu.


Dalili zake


Dalili za ugonjwa huu huanza kuonekana katika kipindi cha siku 3-7 baada ya kuku kuambukizwa.


Dalili hutofautiana kutokana na umri wa ndege.


Baadhi ya dalili zake nihizi zifuatazo


Kuku /ndege hupumua kwa shida (dyspnoea).Kuzubaa.Kutokwa na machozi.Kukohoa na kupiga chafya.Kuharisha kinyesi chenye majimaji.Sehemu za kichwa zisizo na manyoya huvimba.uvimbe wenye majimaji huonekana kichwani na shingoni.Sehemu ya juu kichwani hubadilika na kuwa na rangi ya bluu iliyopauka.Kuku hutaga mayai yenye maganda laini.


Tiba:


Ugonjwa huu hauna tiba .


Kinga na kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu:


Toa taarifa kwa mganga (daktari wa mifugo aliye karibu ukiona dalili za ugonjwa huu.Tenga mabanda ya kuku wagonjwa na walio wazima.Fungia kuku wako wasitembee holela.Acha kununua kuku kutoka eneo linalohisiwa kuwa na ugonjwa huu.Acha kusafirisha mifugo /ndege bila idhini ya daktari.Zuia wageni kutembelea mabanda yako ya kuku.Acha kuhamisha mbolea ya kuku kwenda shambani kutoka kwenye banda la kuku wanaoumwa ugonjwa huu.Safisha mabanda na kuweka dawa chini ya usimamizi wa mtaalamu wa mifugo na kulipumzisha kwa siku 21kabla ya kuanza kufuga tena.Choma moto mkali au fukia chini mbolea kutoka kwenye banda la kuku wanaoumwa ugonjwa huu.Pata ushauri kutoka kwa mtaalamu wa mifugo aliye karibu nawe.



5)      Gumboro (infectious Bursal Disease)


Ugonjwa  huu husababishwa na kirusi


Dalili zake:


o   Hushambulia vifaranga


o   Uharo mweupe


o   Kuchafuka (dirting of anal area)


o   Kuvimba


o   Kiwango kikubwa cha vifo


o   Damu hutapakaa eneo la kutolea kinyesi


Kinga:


1)      Usafi


2)      lishe bora


3)      chanja vifaranga wakiwa na umri wa wiki tatu  kwa kutumia chanjo hai (live vaccine)



6)      Kifua Kikuu cha Ndege(Avian Tuberculosis-TB)


Husababishwa na kimelea aitwaye Mycobacterium avium.


Dalili zake:


o   Kukonda na Kupungua uzito


o   Vidonda  kwenye kishungi


o   Kupungua uzito/kukonda


o   Kuhara


Kinga:


Usafi:


Fanya usafi na vyombo , banda na mazingira .



7)      Magonjwa yatokanayo na Lishe (Nutritional and Metabolic Disorders)


Dalili za magonjwa haya hutegemea aina ya virutubisho vinavyokosekana mwilini


Kwa mfano:


o   Kupinda miguu (rickets) husababishwa na upungufu wa Vit.D, madini ya calcium na fosforasi.


o   Vidonda vyenye vyenye damu husababishwa na vit.K


o   Kichaa cha kuku na kusinyaa kwa misuli husababishwa na upungufu wa Vit.E


o   Magamba ya Mayai (egg shell)kuwa laini  ama umbo kuwa  bovu husababishwa na upungufu wa madini ya calcium na fosforasi.


o   Kudonoana kusababishwa kwa njia moja au nyingine na upungufu wa chakula na madini ya fosforasi na calcium


o   Kuvimba macho, upungufu wa damu huletwa na upungufu wa vit.A.


Kinga:


o   Kuwapa kuku mlo kamili


o   Kuelewa kwa kina aina za chakula kwa kila rika na aina ya kuku ; vifaranga , kuku wa mayai na wa nyama. (Poultry age and classes i.e chicks, layers and broilers)


o   Kufanya uchunguzi wa virutubisho vilivyomo katika aina ya chakula unachotumia.



8)       Minyoo (Helminthiasis)


Minyoo iko ya aina tatu kama vile minyoo kamba, minyoo bapa na minyoo ya mviringo


Dalili zake:


KudumaaKuwa manyoya hafifuKupungua uzitoKukondaMinyoo huonekana kwenye kinyesi



Kinga /kuzuia:


USAFI:


Fanya usafi wa vyombo, banda na mazingira.Tenga vifaranga kutoka kwa wale wakubwa.Badilisha matandazo kuondoa mazalia ya minyoo.Badilisha matandazo kila baada ya miezi mitatu.


Tiba:


Tumia dawa zinazopendekezwa na wataalamu hasa zile zinazoua minyoo ya aina zote (mfano: piperazine citrate).Hakikisha kila baada ya miezi mitatu unawapa kuku wako dawa za minyoo.



9)      Kupe, Utitiri, Chawa na Viroboto


kupe laini  waitwao Argus persicus,  chawa na viroboto wanaong’ata .


Dalili zake:


Kujikung’uta.Kupiga kelele.Kiasi cha damu hupungua mwilini.Utando wa ngozi ndani ya kope za macho hupauka.Utando wa ngozi ya juu mwilini huwa mnene.Magamba ya unga-unga hudondoka.


Kuzuia:


Tupa au choma masalia ya mayai yasiyoanguliwa na magamba ya mayai yaliyoanguliwa vifaranga.


Safisha banda mara kwa mara na kunyunyizia dawa; kuna dawa zinazopendekezwa na wataalamu za kunyunyizia kwenye banda la kuku. Mfano wa hizo dawa ni sevin , akheri powder n.k (Dawa hizi ni za unga).

September 22, 2018

KILIMO BORA NA RAHISI CHA EMBE

Embe ni tunda linalotokana na mti wa muembe, hupandwa kwa njia ya mbegu  kutoka kwenye tunda lilokwisha komaa au kuiva vizuri.



NAMNA YA KUANDAA MBEGU,

Mbegu nzuri huchaguliwa kutoka kwenye tunda lenyewe na kumenywa vizuri kwa ajili ya kuchukua kiini cha ndani, baada ya kutoa kokwa la nje, baaada ya hapo mbegu hufungwa vizuri kwenye tissue na kuachwa siku tatu (3) ikiwa ndani ya mfuko wenye unyevu kiasi, na siku ya 3 hutolewa na kupandwa kwenye kiriba, pia unaweza kuipanda moja kwa moja kwenye kiriba bila kuifunga kwenye tissue, faida za kuifunga kwenye tissue ni kuirahisisha kuota mapema.

NAMNA YA UPANDAJI WA MBEGU KWENYE VIRIBA.

kwanza viriba huandaliwa kwa kujazwa udongo mzuri wenye virutubisho vya kutosha, na upandaji wa mbegu hufuata, weka shimo kidogo ndani ya kiriba chako na weka mbegu kwenye hilo shimo,upande wa mgongo (chini) wa mbegu yako uwe juu na upande wa kiini uwe chini, baada ya hapo rudishia udongo wako taratibu na mwagilia maji kiasi.Pia wengine hupanda mbegu moja kwa moja shambani bila kukuzia kwanza miche kwenye kitalu. baada ya hapo miche huachwa na kukua baada ya miezi 3 huhamishiwa shambani.

Katika uzalishaji wa zao la miembe kuna njia mbili, 

 kuna ambayo; 

1.huchukua muda mrefu  kukua  

2. huchukua muda mfupi kukua hadi kufikia tunda, 

Inayochukua muda mrefu kukua ni ile ambayo hupanda moja kwa moja shambani na kuendelea kutunzwa hadi kufikia tunda, huchukua miaka 7 na zaidi hadi 15, 

muda mfupi ni ile inayofanyiwa kiunganishi (grafting) kutoka kwenye mche wenyewe (root stock) na kikonyo (scion) kutoka kwenye mti mkubwa ambayo tayari ulishatoa matunda, ya muda mfupi huchukua miaka 2.5 hadi 3 tayari kwa kuanza kutoa matunda.




FAIDA ZA KUUNGANISHA (GRAFTING) KWENYE MICHE YA EMBE.
hufanya mche uweze kukua kwa haraka na urahisi vizurihutoa nafasi ya kuchagua ni aina gani ya embe unahitaji kuzalisha kulingana na soko au upendeleo wako mwenyewehuvumilia kushambuliwa na magonjwa na waduduunaweza kuzalisha maembe kipindi ambacho sio msimu wake.aina za embe zinazotokana na kuunganisha au (grafting) ni Tommy, Kent, Red Indian, Alphonso,Keit, Dodo pamoja na borobo buyuni, yote hupendelewa sana sokoni nani matamu.

NAMNA YA UPANDAJI WA MICHE YA EMBE.

Kuchimba mashimo.

Miche ya embe hupandwa kwa nafasi ya mt  7-7 kati ya mche na mche na mt 7-7kati ya mstari na mstari shimo linatakiwa  liwe na kina cha ft-3 na upana kutegemea hali ya udongo. Waka wa kuchimba shimo udongo wa juu (wenye rutuba) na ule wa chini (usio na rutuba) lazima utenganishwe wa juu unaweza kuwekwa kulia na  wachini kushoto .

Kufukia mashimo.

Chukua samadi debe 1-2 changanya na udongo wa juu (ulioweka kulia) jaza mchanganyiko wa samadi na udongo ndani ya shimo hadi utengeneze mwinuko wa kitako cha 100 cm toka usawa wa ardhi,

Kupanda miche.

Kata mizizi inayotokeza nje ya mfuko, kabla ya kutoa, weka mche ndani ya shimo kisha chana hiyo nylon na kutoa taratibu hiyo nylon ili udongo usiachane na mizizi, ukishindilia kiasi, fukia shimo kwa udongo hadi kufikia sehemu inayotenganisha shina na mizizi ya mche. 





Namna ya kutunza miche baada ya kupanda.

Magugu huzuia miche kukua vizuri wakati ikiwa midogo au michanga, wakati wa kupalilia hakikisha hauharibu mizizi kwa kuikata.

Kilimo mseto.

Wakati miembe ikiwa michanga panda mazao ya muda mfupi katikati ya mstari kama vile kunde na maharage kwani mazao haya huzuia magugu kuota  na huongeza rutuba na thamani ya shamba.

Kuweka matandazo (mulching).

Nyasi  (mulching) husaidia kuhifadhi maji ardhini na hupunguza uotaji wa magugu na pia ya kioza huongeza rutuba ya udongo, hakikisha shina haligusani na matandazo ili kupunguza athari za mchwa na moto.

UMUHIMU WA KUPIMA UDONGO KABLA YA KULIMA

Udongo ni nini?
Udongo ni tabaka juu ya ardhi ambalo hufanya kazi kama chombo cha kukuzia mimea.
Udongo hujengwa kutokana na shughuli zinazoendelea za hali ya hewa kulingana na vipengele
kadhaa vya mazingira. Kwa sehemu kubwa kuundwa kwa udongo hutawaliwa na vipengele
vikuu vitano: hali ya nchi (k.m. mvua, joto na upepo), mwinuko wa eneo (mahali eneo lilipo),
viumbe hai (mimea na vijidudu), asili ya kitu kilichozalisha udongo (aina ya miamba na madini
ambayo udongo unatokananayo) na muda.
Udongo umetengenezwa na nini na unafanya nini?
Vitu vya msingi vinavyotengeneza udongo ni madini, mabaki ya viumbe hai, maji na hewa.
Udongo unaofaa (unaofaa kwa ajili ya kukuza mimea mingi) huundwa kwa asilimia takribani 45 ya madini, maji 25 %, hewa 25 %, na mabaki ya viumbe hai 5 %. Katika hali halisi, asilimia hizi hutofautiana sana kutegemea vipengele vingi kama vile hali ya nchi, upatikanaji wa maji, mbinu za kilimo na aina ya udongo. Hewa na maji kwenye udongo hupatikana katika nafasi za matundu kati ya punje za udongo. Uwiano kati ya nafasi ya tundu lililojaa hewa na tundu lillilojaa maji mara nyingi hubadilika kila msimu, wiki na hata kila siku, kutegemea maji yanayoongezeka kupitia mvua, mtiririko, maji ya ardhini na mafuriko. Ukubwa wa tundu lenyewe huweza kubadilika, kwa namna yoyote ile, kupitia michakato mbalimbali. Mabaki ya viumbe hai kwa kawaida huwa chini zaidi ya 5 % katika aina mbalimbali za udongo ambao hausimamiwi vyema.
*Sehemu ya Madini
Sehemu ya madini katika udongo imegawanywa katika aina tatu kulingana na ukubwa wa
punje: mchanga, mchangatope na mfinyanzi. Mchanga, mchangatope, na mfinyanzi kwa
pamoja hujulikana kama sehemu ya udongo yenye punje ndogo. Punje hizo zina kipenyo cha
chini ya mm 2. Punje kubwa za udongo hujulikana kama vipande vinavyotokana na miamba,
pia vina ukubwa tofauti (changarawe, mawe na jabali). Uwiano huu uliopo wa mchanga,
mchangatope na mfinyanzi hujulikana kama umbile asili la udongo. Umbile asili la udongo
lina jukumu muhimu katika mfumo wa matumizi ya virutubisho kwa sababu lina uwezo wa
kufanya virutubisho na maji kubaki au kutokubaki kwenye udongo. Kwa mfano, udongo
wenye umbile asilia laini una uwezo mkubwa wa kuhifadhi virutubisho vya udongo. Udongo
wenye umbile asilia laini huitwa udongo wa mfinyanzi, wakati udongo wenye umbile asilia
lenye chenga chenga huitwa mchanga. Hata hivyo, udongo ulio na mchanganyiko sawa wa
mchanga, mchangatope na ufinyanzi na kuonyesha tabia ya kila moja, huitwa udongo tifutifu
wenye rutuba.
*Muundo wa udongo
Muundo wa udongo unamaanisha mpangilio wa punje za udongo zinazounda matundu madogo na makubwa kati ya mabonge ya udongo. Muundo wa udongo ndio unaoshawishi jinsi maji yanavyopenya ndani ya udongo na kupitiliza, kiwango cha mzunguko wa hewa, uwezo wa udongo wa kuhimili mmomonyoko na jinsi mizizi ya mmea inavyokua kupitia tabaka za udongo. Matundu madogo ni mazuri katika kuhifadhi unyevu, wakati makubwa huruhusu upenyaji wa haraka wa maji ya mvua au umwagiliaji na kusaidia kuondoa maji kwenye udongo na hivyo kuhakikisha mzunguko wa hewa. Udongo hujikusanya pamoja na kugandishwa kwa njia mbalimbali. Katika baadhi za udongo ugandishaji wa punje huwa dhaifu sana, katika nyingine ni imara sana. Ukubwa wa mabonge katika baadhi ya udongo ni madogo madogo sana na laini, wakati katika aina nyingine mabonge ya udongo yana chembechembe na ni makubwa. Katika udongo wa aina nyingine, mabonge ni mazito na yana tundu chache, na katika nyingine mabonge yako wazi na yana matundu mengi. Katika udongo wenye muundo mzuri, chembechembe za madini na mboji ya kwenye udongo hutengeneza mabonge thabiti. Mchakato huu huchangiwa na viumbe hai kwenye udongo kama vile minyoo, bakteria na fangasi. Viumbe kwenye udongo hutoa taka mwilini ambazo hufanya kazi kama gundi na kugandisha chembechembe hizi pamoja. Fangasi zina aina ya nyuzi nyembamba zinazojulikana kama haife ambazo hupenya kwenye udongo na kugandisha chembechembe za udongo pamoja. Mboji hufanya kazi kama aina ya gundi, kusaidia chembechembe za udongo kushikamana. Hii inaonyesha wazi kwamba muundo wa udongo unaweza kuboreshwa kwa
Aina za udongo na sifa zake bainifu
Kuna aina tofauti za udongo. Aina zote ni mchanganyiko wa aina tatu za chembechembe za madini: kichanga, mchangatope na mfinyanzi. Kemikali zinazounda chanzo cha punje za udongo na jinsi punje hizi tatu zinavyounganishwa huamua aina ya udongo uliopo. Husaidia kujua sifa bainifu za msingi za udongo, iwapo udongo una asidi, alikali au hauna kitu chochote.
Aina tofauti za udongo ni kama ifuatavyo: Udongo wa kichanga, udongo wa mchangatope, na 1.udongo wa mfinyanzi.
Udongo wa kichanga
Udongo wa kichanga huundwa kutokana na kuvunjika vunjika na kumomonyoka kwa miamba kama vile mawe ya chokaa, matale, mawe meupe ya kungaa na mwambatope. Udongo wa kichanga una punje kubwa ambazo zinaonekana kwa macho, na kwa kawaida zina rangi za kungaa. Udongo wa kichanga huonekana kuwa na chenga ukiloweshwa au mkavu na hauminyiki unapouminya kwenye kiganja. Udongo wa kichanga hunyumbuka kwa urahisi na huruhusu unyevu kupenya kwa urahisi, lakini hauwezi kuuhodhi kwa muda mrefu. Huzoea haraka hali ya joto. Maji kupenya kwa urahisi huzuia matatizo ya kuoza mizizi. Udongo wa kichanga huruhusu maji kupitiliza zaidi ya kiasi kinachohitajika, ambayo husababisha mimea kukosa maji wakati wa kiangazi. Kwa hiyo iwapo mtu atapanda mimea katika udongo wa kichanga, itabidi kutegemea chanzo cha kudumu cha maji wakati wa kiangazi. Udongo wa kichanga una mboji kidogo sana na kwa kawaida una asili ya asidi. Kwa baadhi ya mazao kama peasi, ambayo huhitaji udongo wenye hali ya alikali ili uweze kutoa maua na kubeba matunda, kuna haja ya kuzimua hali ya asidi kwa kuongeza chokaa au kaboneti ya kalsiam kila mwaka ili kuendeleza hali inayofaa kwa kilimo. Udongo wa mchanga huathirika kwa urahisi na mmomonyoko hivyo inahitaji kukingwa dhidi ya upepo na mvua. Kupatikana kwa mboji mara kwa mara huboresha kwa kiwango kikubwa uwezo wake wa kuhifadhi maji na virutubisho, pia na uwezo wa kuzuia mmomonyoko. Matandazo pia husaidia udongo wa mchanga kuhodhi unyevu kupitia kupungua kwa mvukizo kutoka kwenye udongo.
2.Mchangatope
Mchangatope ni udongo wenye chenga ndogo zaidi kuliko udongo wa mchanga hivyo ni laini unapoushika. Udongo huu ukimwagiwa maji, unateleza kama sabuni. Unapoufi nyanga kati ya vidole vyako, unaacha uchafu kwenye ngozi. Mchangatope unapatikana katika maeneo asilia au kama tope katika tabaka kwenye maziwa, mito na bahari. Huundwa na madini kama vile mawe angavu ambayo yana madini aina ya kwatzi na punje ndogo ngodo za mabaki ya viumbe hai. Ni chengachenga kama udongo wa mchanga lakini unahodhi virutubisho vingi zaidi na unyevu. Unatengeneza gamba kwa urahisi juu ya udongo, ambalo huzuia maji kupenya na unaweza kuzuia mimea isichomoze. Katika hali ya unyevu, hupenyeza maji kwa urahisi na ni rahisi zaidi kulima. Kadri mabaki ya viumbe hai yanavyokuwa mengi, ndivyo inavyonyonya maji ya mvua vizuri zaidi na kuendeleza muundo wake hata baada ya mvua kubwa, hivyo kuzuia mmomonyoko.
3.Udongo mfinyanzi
Udongo mfinyanzi huundwa na chembe chembe ndogo sana ambazo zina sehemu ndogo sana ya kupitisha hewa. Udongo mfinyanzi huundwa baada ya miaka mingi ya miamba kumomonyoka na athari za hali ya hali ya hewa. Pia hutengenezwa kama mashapo yaliyotua baada ya mwamba kupasuliwa vipande vipande na hali ya hewa, kumomonyolewa na kusafi rishwa. Udongo mfinyanzi kutokana na mchakato wa uundwaji wake unakuwa na madini mengi sana. Udongo mfinyanzi unateleza na kunata unapokuwa mbichi lakini laini unapokauka. Udongo mfinyanzi huhodhi unyevu vizuri, lakini haupenyezi maji vizuri, hasa unapokuwa mkavu. Mara nyingi vidimbwi hutokea kwenye udongo mfi nyanzi na udongo hugandamizwa kwa urahisi. Kutokana na uwezo wake mdogo wa kupenyeza maji, hatari ya maji kutuama na ardhi kuwa ngumu, sio rahisi kufanya kazi na udongo mfinyanzi. Kuongeza mboji na jasi huboresha hali ya udongo na kuufanya kulimika kwa urahisi. Jasi na mboji hutenganisha chembe chembe za udongo mvinyanzi na hivyo kuruhusu maji kupenya na kuhodhiwa kwa usahihi. Kuongeza mabaki ya viumbe hai kwenye udongo hukuza kuongezeka kwa minyoo ya ardhini, ambayo husaidia kuinua ubora wa udongo.
4.Udongo tifutifu
Udongo tifutifu hutengenezwa na uwiano mzuri wa mchanga, mchangatope, mfi nyanzi
na mabaki ya viumbe hai. Huchukuliwa kama udongo unaofaa zaidi katika ardhi inayolimika. Udongo tifutifu una rangi nyeusi na unafanana na kushika unga mikononi. Umbile lake ni mchanga mchanga na huhodhi maji kirahisi sana, hata hivyo upenyezaji wake wa maji ni mzuri. Kuna aina nyingi za udongo tifutifu kuanzia wenye rutuba hadi ulio na tope zito na tabaka nene la juu. Hata hivyo kati ya aina zote hizi tofauti za udongo, udongo tifutifu ndio unaofaa zaidi kwa kilimo.
Rutuba ya udongo
Rutuba ya udongo ni nini?
Rutuba ya udongo inafafanuliwa kwa uwezo wake wa kutoa virutubisho vyote muhimu
kwa kiasi kinachotosheleza na katika urari sahihi kwa ajili ya ukuaji wa mimea, bila ya
kutegemea matumizi ya moja kwa moja ya virutubisho, wakati vipengele vingine vya ukuaji
kama vile mwanga, nyuzi joto na maji viko katika hali inayofaa. Uwezo huu hautegemei kwenye wingi wa virutubisho kwenye udongo peke yake, lakini pia kwenye ufanisi wa kubadilisha virutubisho ndani ya duara la virutubisho shambani.
Sifa za udongo wenye rutuba
Udongo wenye rutuba:
1.una virutubisho vingi muhimu kwa ajili ya lishe ya msingi ya mmea (ikiwemo naitrojeni,
fosfora, potasiam, kalsiam, magnesia na salfa);
2.una virutubisho vya kutosha vinavyohitajika kwa kiwango kidogo sana na mmea (ikiwemo boroni, kopa, chuma, zinki, manganizi, klorini na molibdenam);
3.una kiasi stahiki cha mabaki ya viumbe hai kwenye udongo;
4.una kipimo cha pH katika kiwango kinachofaa kwa ajili ya uzalishaji wa mazao (kati ya 6.0 na 6.8);
5.una muundo unaomengenyuka;
6.uko hai kibiolojia;
7.una uwezo mzuri wa kuhodhi maji na kutoa virutubisho.
Kiasi stahiki cha virutubisho vya mmea
Kuna aina 16 ya virutubisho muhimu ambavyo mimea huhitaji ili kukua vizuri. Kati ya elementi hizi 16 muhimu; haidrojeni, kaboni na oksijeni hupatikana kwa sehemu kubwa kutoka kwenye hewa na kwenye maji. Elementi nyingine muhimu hutoka ardhini na kwa ujumla husimamiwa na wakulima. Baadhi ya virutubisho hivi huhitajika kwa wingi katika tishu za mmea na huitwa virutubisho vikubwa. Virutubisho vingine vinahitajika kwa kiasi kidogo hivyo huitwa virutubisho vidogo. Virutubisho vikubwa vinajumuisha naitrojeni (N), fosfora (P) potasiam (K), kalsiam (Ca), magnezia (Mg) na salfa (S). Kati ya hizi N, P na K kwa kawaida huisha ardhini kwanza kwa sababu mimea inayahitaji kwa wingi kwa ajili ya ukuaji na maendeleo yao, hivyo hujulikana kama virutubisho vya msingi. Ni nadra kwa Ca, Mg na S kuwa kikwazo kwa ukuaji wa mmea, hivyo hujulikana kama virutubisho vya umuhimu wa pili. Pale ambapo udongo una asidi, chokaa mara nyingi huongezewa, ambayo ina kiasi kikubwa cha kalsiam na magnezia. Salfa kwa kawaida hupatikana katika mabaki yanayooza ya viumbe hai. Virutubisho vidogo ni: boroni (B), kopa (Cu), chuma (Fe), kloraidi (Cl), manganizi (Mn), molibdenam (Mo) na zinki (Zn). Kurejeshea mabaki ya viumbe hai kama vile mabaki ya mazao na majani ya miti ni njia bora ya kuipatia mimea inayokua virutubisho vidogo.
Mizizi ya mimea inahitaji mazingira ya aina fulani ili iweze kunyonya virutubisho kutoka kwenye udongo:
a) Kwanza, udongo lazima uwe na unyevu wa kutosha kuruhusu mizizi ichukue na kusafi risha virutubisho. Wakati mwingine kuipatia mimea maji kutaondoa dalili za upungufu wa virutubisho.
b) Pili, kipimo cha kupima uasidi cha pH ya udongo lazima kiwe katika kiwango fulani ili
virutubisho viweze kuachiwa kutoka kwenye punje za udongo.
c) Tatu, nyuzi joto ya udongo lazima iwe katika kiwango fulani ili unyonyaji wa virutubisho uweze kutokea.
d) Nne, virutubisho lazima viwepo karibu na eneo la mizizi ili mizizi iweze kuvifikia.
Kiwango cha nyuzi joto, pH na unyevu ni tofauti kwa spishi tofauti za mimea. Kwa hiyo kihalisia virutubisho vinaweza kuwepo kwenye udongo, lakini visiweze kunyonywa na mimea.
Ujuzi wa pH ya udongo, umbile asili na historia unaweza kuwa wa manufaa sana kwa kutabiri ni virutubisho gani vinaweza kuwa pungufu.

Udongo usio na asidi wala alikali (huru) kipimo huru cha pH
Kipimo cha udongo cha pH, ambacho huonyesha uasidi au ualikali, kinahusika zaidi katika jinsi virutubisho vinavyoweza kupatikana kwa urahisi kwenye udongo, ikijulikana kama uyeyushaji wa virutubisho. Mimea inatofautiana jinsi inavyoathiriwa na kiwango cha chini au juu cha pH. Mimea mingine huvumilia au hata kupendelea kiwango cha chini cha pH, mingine inapenda kiwango cha juu cha pH.
Udongo wenye pH chini ya 6.5 ambao huweza kurekebishwa na chokaa unaweza
kuchukuliwa kwamba ni udongo wenye asidi. Potasiam, kalsiam na Magnezia inapochuja kutoka kwenye udongo, udongo huwa na asidi. Hii inaweza kutokea kama kuna mvua nyingi (au maji ya umwagiliaji) ambayo huondoa virutubisho, au iwapo mbolea nyingi ya madini yenye naitrojeni itakapotumika.Katika udongo wenye asidi, mizizi ya mimea haikui kawaida kutokana na ayoni za sumu za haidrojeni. Fosforasi haiwezi kusafirishwa na upatikanaji wake hupungua. Shughuli nyingi za viumbe rafiki kama bakteria wa spishi za Azatobacter na bakteria wanaotengeneza nundu kwenye mikunde pia huathirika kadri asidi inavyoongezeka katika mazingira ya asidi, bakteria huambisha naitrojeni kidogo zaidi na kuozesha mabaki kidogo ya viumbe hai yenye kiwango kidogo cha sumu, hivyo hupelekea virutubisho vichache kupatikana.
Kuongeza chokaa au mboji yenye pH ya juu (8) kutasaidia kuzimua asidi na kuongeza pH, ili upatikanaji wa virutubisho uongezeke.
Udongo wenye alikali hutengenezwa kutokana na mkusanyiko wa sodiam inayoweza kutumika na mimea na pH ya juu. Udongo unaomwagiliwa ambao haupenyezi maji vizuri unaweza kusababisha udongo wenye alikali. Katika maeneo ya pwani, kama udongo una kaboneti, kuingia kwa maji ya bahari kunasababisha udongo wenye alikali inayotokana na kulundikana kwa sodiam kaboneti. pH ya udongo wenye alikali inaweza kurekebishwa kwa kutumia jasi
Kupima rutuba ya udongo
Uchambuzi wa udongo
Wakulima wanaweza wakagundua kwamba wakiweza kufanya uchambuzi wa udongo wao
katika maabara ni jambo la manufaa linalowawezesha kufahamu habari zaidi kuhusu rutuba
ya udongo wao.
Je udongo unapimwaje? Sampuli za udongo (soil samples) huchukuliwa kutoka kwenye shamba husika, kisha sampuli hizo hupelekwa maabara kwa ajili ya kupima udongo huo. Huchukua siku 7 hadi 14 kwa majibu ya udongo kuwa tayari.
Faida za kupima udongo
➢ Kupima udongo kunasaidia kujua aina ya zao linalofaa kwenye shamba lako
➢Kwa kupima udongo utajua virutubisho ambavyo viko kwenye udongo na kwa kiasi gani
➢ Kupima udongo kuna punguza gharama kwani utanunua mbolea kulingana na upungufu wa udongo wako, wakulima wengi wamekuwa wanatumia mbolea hata kwa mashamba ambayo virutubisho viko vya kutosha na pia kutasaidia kutunza mazingira kwasababu baazi ya virutubisho vikizidi kwenye udongo huweza kuharibu mazingira.
➢ Kupima udongo kutakusaidia kujua mahitaji kamali ya mbolea/ virutubisho
➢ Kupima udongo kutakusaidia kujua jinsi ya kuuboresha udongo kwa kuweka chokaa au jasi, hii ni baada ya kujua pH ya udongo.
➢ Kupima udongo kutakusaidia kujua zao gani upande
➢ Kupima udongo kutakusaidia kujua utumie mbolea gani na kwa kiasi gani.

MCHANGANUO WA KILIMO CHA MIWA

KILIMO BORA CHA MIWA : Kilimo cha miwa ni kilimo chenye tija kwa mkulima, kilimo hiki kinaweza kufanywa na mtu yeyote yule aidha awe ameajieiwa au laaa! Jambo la msingi ni kuhakikisha anajitoa kikamilifu katika kuhakikisha  unawekeza akili yake katika kulima kilimo hiki.

Kuna aina kuu 2 za miwa katika mbegu za miwa zilizo shamili sana ambazo ni:

  1. Bungala
  2. Miwa myekundu.

Unachotakiwa kufanya katika kulima kilimo hiki ni, Kwanza kabisa tafuta ekari moja ya shamba kisha anza maandalizi lakini zingatia kupuguza matumizi makubwa ya pesa kadri iwezakanavyo yaani kwa shughuli nyinginezo ambazo unaweza kuzifanya mwenyewe ni vyema ukazifanya ili kupunguza matumizi makubwa ya pesa mfano kulima, kupiga dawa, kupalia n.k

Tafuta mbegu ya miwa ya Bungala miwa hii ni laini sana na ni rahisi kuichana kwa kutumia meno, baada ya kupata miwa hii kata vipande vipande vya pingili tatu tatu. Kumbuka kwamba miwa ni rahisi sana kushambuliwa na mchwa pale tu inapokuwa imepandwa.

Ili kuzuia isiliwe na mchwa nenda katika maduka ya kilimo na ununue moja wapo ya madawa yafuatayo:-

  1. TAP 4% GR Tumia gram 100 za dawa kwa lita takribani 20 za maji kisha nyunyizia katika mashina ya miwa.
  2. Taniprid 25 WG. Tumia gram 100 za dawa kwa lita takribani 20 za maji au pia unaweza kuweka kijiko kimoja cha chai katika kila shina.
  3. Imida Gold Mls 20 kwa lita 20 za maji na unyunyizie shinani.
  4. Gammalin 20. Tumia gram 100 kwa lita takribani 20 za maji. Na unyunyizie katika vipande vya miwa au chovya vipande vya miwa katika maji hayo yaliyo na Gammalin 20 na ndipo uende ukavipande shambani kwako.
  5. Gladiator FT.
  6. Stom

 

Mambo yakufanya:

Zingatia kama utatumia aidha Gladiator au Gammalin au Stom, chukua ndoo ya maji ya lita 20 kisha uichanganye na dawa uliyoinunua kisha chukua kipande cha muwa na kukizamisha ndani ya maji hayo na baadae uende kuipanda shambani kwako, hivyo uewezekano wa miwa yako yote kuote utakuwa ni mkubwa sana maana shida kubwa ni mchwa na hapo tayari utakuwa umeidhibiti.

 

UPANDAJI WA MIWA

Hakikisha unapokuwa unapanda miwa yako acha nafasi ya mita moja (1m) kati ya mche na mche pia hakikisha una acha nafasi ya mita moja (1m) kati ya mstari na mstari. Kumbuka awali tulisema katakata muwa wako kupata vipande vilivyo na vipingili vitatu vitatu, hivyo sasa unapokuwa unapanda miwa hii hakikisha hizo pingili zote 3 zimezama ndani ya ardhi na kipande kidogo tu ndio kibakie juu ya uso wa ardhi na mche wako huo unapoutumbukiza kwenye ardhi uwe umelala wastani wa nyuzi 30.

Zile pingili katika muwa wako kumbuka ndipo sehemu hasa miwa inamokuwa inachipuka na kuota. Mantiki ya kuacha nafasi kubwa kati ya mche na mche ni kwa sababu hilo shina lako moja ulilolipanda linaweza likachipua vijimiwa vingine zaidi hata ya ishirini kama ukiliacha shina liendelee kuzaa tu kwa kadri linavyotaka na hatimaye shamba lako litakuwa msitu hata usiopitika.

Lakini kibaya zaidi ni kwamba miwa yako itakosa afya njema na mwisho wa siku miwa yako haitakuwa bora hata bei haitakuwa nzuri pindi utakapoamua au wakati wa kuuza utakapofika. Hivyo unashauriwa kuacha miwa kati ya tano mpaka kumi lakini mfano ukiacha miwa mitano katika shina moja ni dhairi hewa na mwanga vitakuwa vya kutosha shambani lakini hata chakula na virutubisho vingine kwa miwa hiyo vitakuwa lukuki na sio vya kung’ang’aniana hivyo mwisho wa siku utapata miwa mirefu na minene ambayo sokoni itakuwa na mvuto mkubwa kwa wateja.

Mfano chukulia kwamba umelima ploti ndogo tu ya upana mita 50 kwa urefu mita 70, kumbukumbu namna ya upandaji miwa kama tulivyozungumza hapo awali umbali wa mita moja moja kwa kila shina. Hivyo kwa ploti ya shamba hili utakuwa na miche au mashina uliyopanda kiasi cha 70×50=3500 (mashina elfu tatu na mia tano) sasa chukulia kwa hesabu rahisi kwamba kila shina umeruhusu miwa mitano tu ndio ikuwe pale maana yake kwa mashina 3500 utazidisha mara 5 ambapo itakuwa 3500×5= 17,500 hiyo ndio itakuwa jumla ya miwa itakayovunwa shambani.

Kwa tafiti zilizofanywa zinaonesha kama hautaki shida na unahitaji pesa ya haraka haraka sana huko huko shamba, basi unaweza ukajumlisha miwa yako kwa bei ya chini sana yaani tukadilie vile kwamba tunahitaji pesa ya haraka so tuuze muwa mmoja kwa bei ya jumla ya 300 hivyo jumla ya pesa utakayoipata itakuwa 17,500 × 300 = 5,250,000 (milioni tano laki mbili na nusu). Hiyo ni pesa ya haraka haraka huko huko shambani .

Ila kama ukiweza kusogea zaidi na kuuza kwa faida maana kama umeweza kupigana mpaka kuweza kuikuza ni dhairi kwamba unastahili kupata faida iliyo njema kwako hivyo ni muhimu kuangalia masoko yamekaaje pande zote za miji, ila kama utaweza kuifikisha Dar es Salaam ambako kiuhalisia soko lake ni kubwa sana .

Kama ukienda Kariakoo bei ya rejareja kwa muwa aina ya bungala wenye wastani wa urefu mita moja na robo bei yake ni 5,000 lakini ukienda mtaani kwa muwa huo huo aina ya bungala mfupi kidogo bei yake inakwenda mpaka 3,500 hivyo chukulia kwamba umeweza kufikisha Dar es Salaam huo mzigo wako wa miwa, hivyo mapato yako kama utaamua uuze kwa bei ya jumla ya 1,500 kwa kila muwa hivyo kiasi cha fedha utakachokipata kitakuwa ni sawa na idadi ya miwa yako zidisha bei ya kujumlishia yaani ingekuwa 17,500 × 1,500= 26,250,000 hii ni pesa utayoipata kwa halali kabisa wala haujamzulumu mtu.

Hapo umelima ploti ndogo tu, sasa chukua pengine umelima ekari moja na kwa shamba la miwa ekari moja kiwango cha chini kabisa cha wewe kuvuma miwa yako ni jumla ya miwa 24,500. Sasa chukulia kama umeweza kuipeleka Dar es Salaam maana yake utapata jumla ya 24,500 × 1,500= 36,750,000. Sasa mfano ndo ukalima ekari 4 hadi 5 hapo ni hakika unatoka katika kundi la uchumi wa chini na kuingia katika uchumi wa kati.

September 15, 2018

MWONGOZO WA UFUGAJI KUKU WA ASILI

Kuku wa Asili ni wale ambao wamekuwepo hapa nchini kwa miaka mingi na damu yao
haijachanganyika na ya kuku wa kigeni. Kuku hawa wana rangi na maumbo mbali mbali.
Idadi ya kuku wa Asili hapa Tanzania inakadiriwa kufikia milioni 56. Kati ya kaya milioni 3.8
zinazojishughulisha na kilimo nchini, kaya milioni 2.3 hujishughulisha na ufugaji wa kuku wa asili.
Kwa kawaida ufugaji wa kuku wa Asili hapa nchini kwetu Tanzania hufanywa na wafugaji wadogo
wadogo wanaoishi kando kando ya miji na wale wanaoishi vijijini. Kuku hawa hufugwa huria (freerange),
yaani hufungiwa ndani nyakati za usiku na hufunguliwa asubuhi ili wajitafutie chakula.
Kuku hawa hutoa mazao machache sana yaani nyama na mayai, kwa mfano kuku mmoja hutaga
kiasi cha mayai 40-60 kwa mwaka badala ya 100-150 iwapo atatunzwa vizuri. Pia uzito wa kuku
hai ni wa chini sana, wastani wa kilo 1.0–1.5 katika umri wa zaidi ya miezi 6 badala ya kilo 1.8–2.5
iwapo atatunzwa vizuri.

Sifa za Kuku wa Asili:
Wastahimilivu wa magonjwa, lakini ni muhimu wakikingwa na baadhi ya magonjwa ya kuku
kama mdondo, ndui ya kuku nk. ili kuweza kuwaendeleza.
Wana uwezo wa kujitafutia chakula ardhini, lakini ili kuwaendeleza ni lazima kuwapa chakula
bora cha ziada.
Wana uwezo wa kuatamia mayai, kutotoa, kulea vifaranga na ustahimilivu wa mazingira
magumu (ukame, baridi nk).
Nyama na mayai yake vina ladha nzuri kuliko kuku wa kisasa.
Kwa kiasi fulani wana uwezo wa kujilinda na maadui kama vile mwewe.
Pamoja na sifa hizi ni muhimu kuku hao wakapewa matunzo mazuri, wawekwe kwenye mabanda
mazuri na imara, pia wapewe maji na chakula cha kutosha.

Faida za Ufugaji wa Kuku wa Asili:
Chakula – nyama ya kuku na mayai hutumika kama chakula muhimu cha wanadamu, chenye
protini.
Chanzo cha kipato – mkulima hupata fedha akiuza kuku au mayai.
Chanzo cha ajira – ufugaji wa kuku hutoa ajira kwa jamii.
Kuku hutumika kwenye shughuli za ndoa kama vile kutoa mahari na pia ni kitoweo muhimu
katika sherehe hizo.
Gharama nafuu za kuanzisha na kuendesha mradi huu.
Ni kitoweo rahisi na chepesi kwa wageni kuliko wanyama wakubwa kama ng’ombe au mbuzi.
Ni kitoweo kisichohitaji hifadhi, hutumika mlo mmoja au miwili na kumalizika.
Kuku na mayai hutumika kwa tiba za asili.
Jogoo hutumika kama saa anapowika nyakati za alfajiri na majira mengine ya siku.
Hutuhabarisha iwapo kiumbe kigeni au cha hatari kwa mlio maalum wa kuashiria hatari.
Mbolea – kinyesi cha kuku kinaweza kutumika katika kurutubisha mashamba ya mazao na
mabwawa ya samaki.
Kuendeleza kizazi cha kuku wa asili hapa nchini.
Soko lipo la uhakika, ukilinganisha na kuku wa kisasa kwani nyama na mayai yake hupendwa
zaidi na walaji.
Manyoya ya kuku hutumika kama mapambo, pia huweza kutumiaka kutengenezea mito ya
kulalia na kukalia.
Shughuli za utafiti – kuku wanatumika katika tafiti nyingi za baiolojia, kama kutambua mambo ya
lishe.
Shughuli za viwandani:
Mayai yenye mbegu ya jogoo hutumika katika kutengeneza dawa za chanjo.
Magamba ya mayai yanaweza kutumika katika utengenezaji wa vyakula vya wanyama.
Kiini cha njano cha mayai kinaweza kutumika kutengeneza mafuta ya kuoshea nywele
(shampoo).
Mapungufu ya Kuku wa Asili:
Hutaga mayai madogo wastani wa gramu 47 ambapo kuku wa kisasa wastani wa gramu 55,
aidha hutaga mayai machache wastani wa mayai 60 kwa mwaka ambapo kuku wa kisasa
huweza kutaga hadi mayai 300 kwa mwaka.
Ukuaji taratibu – kuku wa asili hukua taratibu kutokana na lishe duni. Kutokana na hali hiyo kuku
huchukua muda mrefu (miezi sita) kufikia uzito wa kuchinjwa (kilo 1 – 1.5). Hali hii pia hufanya
faida ya ufugaji wa kuku wa asili kuchukua muda mrefu kupatikana.
Nyama yake ni ngumu (huchukua muda mrefu kuiva) ikilinganishwa na kuku wa kisasa.
Changamoto katika ufugaji kuku wa asili:
Mabanda: Ukosefu wa mabanda bora.
Wezi, wanyama na ndege hushambulia kuku.
Magonjwa: kama mdondo na ndui huathiri ufugaji wa kuku.
Tabia na miiko ya baadhi ya jamii. Baadhi ya jamii za makabila hapa nchini huona ufugaji wa
kuku kama ni kitu duni.
Upatikanaji haba wa chanjo za magonjwa kama vile, mdondo, ndui, homa ya matumbo.

September 14, 2018

ONGEZA KIPATO NA KILIMO CHA KAROTI

Karoti ni zao la mbogamboga ambalo ni zao mzizi, kwa kawaida hupatikana katika rangi ya machungwa,  nyekundu, njano. Karoti za sasa zimetokeza kutokana na karoti pori, Daucus carota. Karoti hutumika sana kwaajili ya kuongeza radha kama kiungo kwenye mboga au kwenye kachumbari na pia zinafaida kubwa katika mwili kwa kukupatia vitamin A na C pamoja na madini ya chuma hasa pale mtu atafunapo.

Hali ya hewa na udongo.
Karoti zinahitaji hali isiyokuwa na joto sana, wala baridi sana, kati ya nyuzi za degree 15 mpaka 27 za sentigredi. Kama ukanda wa pwani una joto kali, inatakiwa karoti zilimwa miezi ya majira ya baridi, karoti zinazotoka mazingira ya baridi huwa na radha nzuri pamoja na harufu nzuri. Udongo wa kichanga chepesi na tifutifu ndio unafaa katika kilimo cha karoti, udongo wa mfinyanzi na udongo mzito hudumaza mazao.

Utayarisha wa shamba.
Karoti zinahitaji Shamba la Karoti lilimwe kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45 kwenda chini ya ardhi. Mkulima anatakiwa kuandaa matuta yenye mwinuko wa kimo cha sentimita 28 – 40 kwenye shamba, na upana wa mita 1, pia mita 1.5 umbali wa tuta moja hadi lingine. Kwa maandalizi mazuri tengeneza mifereji midogo ya kusiha mbegu za karoti yenye umbali wa sentimita 15- 20, mifereji minne kwa tuta.

Mbegu
Jinsi ya kujua mbegu nzuri zenye uwezo wa kukua bila wasiwasi. Mbegu zenye uwezo wa kuota hutoa harufu kali unapozifikicha. Zilizopoteza uwezo wa kuota huwa hazitoi harufu yoyote. Ili mbegu ziote haraka ziloweke katika maji kwa muda wa saa 24. Baada ya hapo changanya mbegu hizo na mchanga, kwa kiasi kinacholingana ili kupata mtawanyiko mzuri wa mbegu wakati wa kupanda/kusia.

Upandaji.
Inahitajika uoteshe kwenye kitalu ndipo uhamishie shambani.
Weka mbegu katika chupa ya milimita 100 na toboa kidogo mfuniko, baada ya hapo Sia mbegu katika mifereji ya kupandia kwa kutikisa chupa yenye mbegu, ndipo, Funika mbegu kwa kutumia mboji au mchanga, ukimaliza Nyunyiza maji ya kutosha, Funika tuta na plastiki nyeusi, hatua nyingine Kandamiza plastiki kwa pembeni na kwa mabonge ya udongo ili isipeperushwe na upepo.

Mbegu huota baada ya siku 3-5 kutegemea na hali ya hewa. Inakupasa kukagua shamba mara tatu kwa siku. Baadaye Ondoa plastiki mara moja pindi utakapoona mbegu moja tu iliyoota. Usicheleweshe kuondoa plastiki husababisha miche inayoota kufa kwa kuunguzwa na joto lililo katika plastiki. Hapo tayari kwa kupanda shambani.

Upandaji wa moja kwa moja shambani katika matuta au sesa.
Kiasi cha kilo 8 za mbegu kinatosha kupandwa kwenye Hekta moja.

Mbolea
Weka mbolea aina za asili (samadi au mboji) mwanzoni, ila kama haukutumia mbolea ya samadi au mboji, weka mbolea ya S/A kilogramu 100 kwa hekta kama haukutumia mbolea za asili, kama ulitumia mbolea za asili basi weka kilogramu 50 kwa hekta. kisha tumia NPK wiki sita baada ya kupanda. Matumizi ya mbolea za maji yafanyike kila baada ya wiki mbili kutegemea na mahitaji

UPALILIAJI & UNYEVU
Ili kupata mavuno mengi palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu na nyasi kwa kung’olea kwa mkono, jembe na mangineyo, na kwenye udongo hakikisha kuna unyevu wa kutosha kama sio kipindi cha mvua inatakiwa umwagilie shamba lako kwa wiki mara mbili.

Magilonjwa na wadudu waharibifu wa zao hili.

Magonjwa ;

1. Madoajani (Leaf Spot):
Ugonjwa huu husababishwa na ukungu na hutokea wakati karoti zina urefu wa sentimita 13 mpaka 15. Hushambulia majani na kuyafanya yawe na madoa yenye rangi nyeusi iliyochanganyika na kijivu au kahawia. Sehemu zinazozunguka madoa haya hubadilika rangi na kuwa njano.
Ugonjwa ukizidi majani hukauka.

Zuia ugonjwa huu kwa kunyunyizia dawa za ukungu kama vile Dithane-M 45, Blitox, Copperhydroxide (Kocide), Copper Oxychloride, Cupric Hydroxide (Champion), Antrocol, Topsin M- 70% na Ridomil.

2. Kuoza Mizizi (Sclerotinia Rot).
Ugonjwa huu husababishwa na ukungu na hushambulia mizizi namajani. Dalili zake ni kuoza kwa mizizi na majani. Baadaye sehemu hizi hufunikwa na uyoga mweupe. Kwenye uyoga huu huota siklerotia kubwa zenye rangi nyeusi.

Zuia ugonjwa huu kwa kuzingatia yafuatayo:-

  • – Epuka kustawisha karoti kwenye maeneo yaliyoshambuliwa na ugonjwa huu.
  • – Nyunyuzia dawa za ukungu kama vile Dithane M- 45, Blitox, Topsin – M 70% na Ridomil.


3. Madoa Meusi (Black Leaf Spot):
Huu pia ni ugonjwa wa ukungu unaoshambulia majani na mizizi. Majani yaliyoshambuliwa huwa na rangi ya manjano ambayo baadaye hubadilika na kuwa kahawia. Mizizi huwa na madoa meusi yaliyodidimia. Ugonjwa huu unaweza kuzuiwa kwa kutumia mbegu zilizothibitishwa kitaalamu, kubadilisha mazao na kuepuka kujeruhi karoti wakati wa kupalilia, kuvuna au kusafirisha.

Wadudu waharibifu wa zao hili.

1. Minyoo Fundo:
Minyoo hii hushambulia mizizi na kuifanya iwe na vinundu. Hali hii husababisha mmea kudumaa na kupunguza mavuno. Minyoo fundo huweza kuzuiwa kwa kubalidilisha mazao. Baada ya kuvuna usipande mazao ya jamii ya karoti au mazao yanayoshambuliwa na wadudu hawa. Unaweza kupanda mazao ambayo hayashambuliwi na minyoo fundo kama vile mahindi. Pia hakikisha shamba ni safi wakati wote.

2. Imi wa Karoti:
Mashambulizi hufanywa na funza ambaye hutoboa mizizi. Ili kuzuia wadudu hawa tumia dawa kama vile Dichlorvos, Sapa Diazinon na Fenvalerate. Pia badilisha mazao na wakati wa kupalilia pandishia udongo kufunika mizizi.

3. Karoti Kuwa na Mizizi Mingi (Folking);
Hii hutokea kama karoti zimepandwa kwenye udongo wenye takataka nyingi na usiolainishwa vizuri. Vile vile utumiaji wa mbolea za asili zisizooza vizuri unaweza kusababisba karoti kuwa na mizizi mingi. Hali hii inaweza kuzuiwa kwa kulainisha udongo vizuri na kutumia mbolea za asili zilizooza vizuri.

Uvunaji.
Karoti hukomaa baada ya wiki 11 mpaka 13 kutoka mda ilipokuwa imepandwa kulingana na hali ya hewa ya eneo ilipolimwa, tani 15 hadi 25 za karoti huvuna katika hekta moja.

Soko
Karoti inatumika sana na watu mbalimbali, tafuta soko pale unapoona karoti zako zimekaribia kukomaa. Ulizia wanunuzi ni bei gani wataweza kuchukua pia kiasi gani watachukua.

HII NDIO FAIDA YA KILIMO CHA PAPAI




KILIMO BORA CHA PAPAYA
Papai ni moja ya tunda mashuhuli linatumika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Pia tunda hili linaweza kuwa na faida mbali na afya, katika kukuza uchumi wa mkulima wa zao hili. Pia linawezakuwa chanzo kikubwa cha pesa za kigeni kwa kuuza nje ya nchi.
Uzalishaji wa papai nchini Tanzania ni kwa kiasi kidogo ukilinganisha na mahitaji ya watumiaji, hivyo inahitajika nguvu zaidi katika uzalishaji wa zao hili.

Kijinsia mpapai umegawanyika katika aina tatu.
Mpapai wenye maua kiume tu. Mpapai wenye maua kike tu. Mpapai wenye maua ya jinsia zote (Hermaphrodite papaya). 
Katika uzalishaji kila aina ya mpapai unahitajika. Mpapai wenye maua ya kiume uhitajika katika urutubishaji wa mpapai wenye maua ya kike ili kupata matunda. Mpapai wenye maua ya jinsia zote hauhitaji mpapai wenye maua ya kiume maana uweza kujirutubisha wenyewe.
Kutokana na jinsia ya maua mpapai huweza kutengeneza matunda yenye maumbo tofauti. Matunda yanayotengenezwa kutoka katika mpapai wenye maua ya kike tu huwa na umbo la mviringo zaidi au yenye umbo la yai na matunda yanayotokana na mpapai wenye maua ya jinsia zote mbili huwa na umbo la refu zaidi au umbo la pear
.
UZALISHAJI WA ZAO LA PAPAI.
Miche ya mpapai Katika uzalishaji wa miche ya mpapai kuna aina mbili za mbegu ambazo huweza kutumika:
1. Mbegu za Kawaida (Local seeds).
Hizi ni mbegu ambazo huweza kukusanywa toka katika mipapai ya kienyeji. Aina hii ya mbegu ni vigumu kujua kati ya mbegu ni ipi dume, jike ama yenye jinsia zote.
Hivyo itakulazimu kung'oa baadhi ya mipapai dume pindi itakapo weka maua hivyo kuacha majike na yenye jinsia zote mbili. Mapapi yenye maua ya kiume uachwa kwa uwiano wa 1:50 ya mipapai yenye maua ya kike.
2. Mbegu chotara (Hybrid seeds)
Aina hii ya mbegu ni nzuri kwa sababu mbegu zote huwa ni ya mipapai nyenye maua ya kike na ya kiume pamaja (Hermaphrodite papaya)na pia hukua haraka na kutengeza miti mifupi yenye uzao mkubwa ukilinganisha na ile ya kienyeji. Mfano. Red royolen F1 au MALAIKA F1.
UPANDAJI.
Panda mbegu moja tu kwa kila kiriba chenye udongo uliochanganywa vizuri na kujazwa robo tatu. Kisha weka viriba vyako venye mbegu chini ya kivuri kisha mwagilia maji. Baada ya kumwagilia unaweza pulizia kiasi kidogo cha kiuwatilifu (fungicide & Insecticide) kwenye udongo wako ili kuzuia wadudu na fungasi wasiathili mmea wako.
Mbegu ya papai uweza chukua siku 8 hadi 15 kuchomoza toka kwenye udongo. Hivyo hakikisha unamwagilia maji kila siku kwa kiasi. Usimwagilie maji mengi sana. Mpapai huweza kuamishwa toka kwenye kitalu baada ya wiki sita hadi nane.
KITALU CHA MIPAPAI NA BAADHI YA SABABU MUHIMU ZINAWEZA ATHILI UKUAJI WA MIPAPAI.
Mpapai upendelea zaidi udongo unaopitisha maji na mzuko wa hewa kirahisi na wenye makadilio ya Ph 6.5. Inapowezekana zuia kupanda mimea yako kwenye udongo wa mfinyanzi na wenye magadi. Kiasi cha maji kilichopo kwenye udongo huweza kuonyesha ukubwa wa matunda.
Eneo lenye udongo wenye unyevunyevu mwingi huweza tengeneza matunda makubwa na yaliyoja maji maji na eneo lenye unyevunyeku kidogo hutengeneza matunda madogo na magumu. Mpapai hawezi kuvumilia upepo mkali, maji yaliotwama pamoja na ukame.
UANDAAJI WA SHAMBA.
Njia ya kuandaa shamba itategemea na eneo (topography), aina ya udongo, vifaa vinavyotumika kuhudumia shamba. Nafasi kati ya mmea na mmea ni mita 2 hadi 2.5 na kati ya mstari na mstari ni mita 2.5 hadi mita 3.
Andaa mashimo yenye upana na urefu wa sentimita 60. Tenga udongo wa chini na wa juu. Kisha changanya udongo wa juu na mbolea ya samadi. Katika kurushisha kwenye shimo tanguliza udongo ulochanganywa na mbolea ya samadi chini na juu malizia na udongo uloutoa chini wakati wa kuchimba shimo.
Kiasi cha mmea huwa kati ya 1000 hadi 2000 kwa hekta (400 hadi 800 kwa ekari) Kupanda mimea shambani Baada ya hizo wiki sita hadi nane hamishia mimea yako shambani. Kazi ya uhamishaji wa mimea ufanyika wakati wa asubuhi sana, jioni ama kukiwa na mawingu ili kuzuia madhara ya jua kwa mimea.
UWEKAJI WA MBOLEA. 
Zuia matumizi ya mbolea zenye chlorine maana mipapai uathiliwa na chlorine. Wiki moja baada ya kuhamisha miche yako weka mbolea gramu 28 kwa kila mche. Tumia mbolea yenye phosphate kwa kaisi kikubwa.
Mfano; - 12:24:12. (NPK) Baada ya hapo kila baada ya wiki mbili weka mbolea yenye Nitroni kwa kiasi kikubwa kiasi cha gramu 56 kwa mmea. Mfano. 20:10:10 (NPK) Potassium inahitajika kwa maua na kuweka matunda hivyo tumia mbolea yenye potassium kiasi kikubwa mara baada ya kuona mmea wako umeanza kuweka maua, kiasi cha gramu 114 cha mbolea huitajika, fanya hivyo kila baada ya mwezi. Mfano. 12:12:17 + 2 (NPK) . Weka mbolea ya majani yenye virutubisho vidogo vidogo ikiwemo boron kila mweze. Boron ni mbolea ya muhimu katika kupata matunda mazuri.
UMWAGILIAJI.
Maji ni sehemu ya muhimu sana katika maisha ya mmea kwa kipindi chote. Maji ni ya muhimu sana katika kuweka maua, matunda na ukuaji wa matunda. Katika ukuaji wa matunda hakikisha unaweka lita 23 kwa kila mmea kwa wiki.
Magugu Hakikisha unazuia magugu kipindi cha mwanzo ili kuzuia ushindani kati ya mimea na magugu kwa virutubisho na maji. Na pia kuzuia magugu kubeba vimelea na wadudu wanaoweza kuathili mazao yako.
HATUA ZA UKUAJI WA MPAPAI.
Kitalu - Wiki 1 - 6 -Hatua ya ukuwaji wa haraka baada ya kuamishiwa.Shamba - wiki 7 -16 -Maua na kuweka matunda.Wiki 17 - 21 -Kukua kwa matunda.Wiki 22 - 26 -Mavuno ya kwanza Wiki 37 -kuendelea Week 37 ni miezi tisa au kumi sio kwa hiyo kilimo cha mapapai huchukua miezi 10 kupata mavuno 
GHARAMA 
Kununua ekari moja inategemea na eneo ulipo na bei husika. Kununua mbegu tsh 50,000-100,000.Kumwagilizia kila siku -upandaji -kuhamisha kutoka kwenye vitalu hadi kwenye shamba -machine ya kumwagilizia 1,500,000/- Generator tsh lak 6 Mbolea tsh 100,000 kila mwez -na vibarua shambani -kulima kwa trekta 40,000 Gharama zote kama mil 3-4 hiv mpaka kuvuna.
MAVUNO NA FAIDA.
Kama umelima ekarI moja unaweza ukapata matunda 15- 35 kwa mvuno wa Kwanza tu twende kimahesabu EkarI ina miche 400-800 Tuseme tupate miche 600 kwa ekari, kila mche utoe matunda 20 chini kabisa 600×20=12,000.

Matunda Soko Kwa sasa unaweza ukauza kwa jumla jumla tsh 1500-3000 Tuuze kwa bei ya chini 1500 kwa kila papai 12000×1500=18,000,000/- Ukitoa Gharama za uendeshaji unaweza ukabaki na tsh 14,000,000 au toa 4,000,000 uweke kwenye dharura unaweza ukamake tsh 10 mil kwa ekar moja tu.

KILIMO CHA MIWA KINALIPA SANA

Kilimo cha miwa ni kilimo chenye tija kwa mkulima, kilimo hiki kinaweza kufanywa na mtu yeyote yule aidha awe ameajieiwa au laaa! Jambo la msingi ni kuhakikisha anajitoa kikamilifu katika kuhakikisha  unawekeza akili yake katika kulima kilimo hiki.

Kuna aina kuu 2 za miwa katika mbegu za miwa zilizo shamili sana ambazo ni:

  1. Bungala
  2. Miwa myekundu.

Unachotakiwa kufanya katika kulima kilimo hiki ni, Kwanza kabisa tafuta ekari moja ya shamba kisha anza maandalizi lakini zingatia kupuguza matumizi makubwa ya pesa kadri iwezakanavyo yaani kwa shughuli nyinginezo ambazo unaweza kuzifanya mwenyewe ni vyema ukazifanya ili kupunguza matumizi makubwa ya pesa mfano kulima, kupiga dawa, kupalia n.k

Tafuta mbegu ya miwa ya Bungala miwa hii ni laini sana na ni rahisi kuichana kwa kutumia meno, baada ya kupata miwa hii kata vipande vipande vya pingili tatu tatu .Kumbuka kwamba miwa ni rahisi sana kushambuliwa na mchwa pale tu inapokuwa imepandwa.

Ili kuzuia isiliwe na mchwa nenda katika maduka ya kilimo na ununue moja wapo ya madawa yafuatayo:-

  1. TAP 4% GR Tumia gram 100 za dawa kwa lita takribani 20 za maji kisha nyunyizia katika mashina ya miwa.
  2. Taniprid 25 WG. Tumia gram 100 za dawa kwa lita takribani 20 za maji au pia unaweza kuweka kijiko kimoja cha chai katika kila shina.
  3. Imida Gold Mls 20 kwa lita 20 za maji na unyunyizie shinani.
  4. Gammalin 20. Tumia gram 100 kwa lita takribani 20 za maji. Na unyunyizie katika vipande vya miwa au chovya vipande vya miwa katika maji hayo yaliyo na Gammalin 20 na ndipo uende ukavipande shambani kwako.
  5. Gladiator FT.
  6. Stom

Mambo yakufanya:

Zingatia kama utatumia aidha Gladiator au Gammalin au Stom, chukua ndoo ya maji ya lita 20 kisha uichanganye na dawa uliyoinunua kisha chukua kipande cha muwa na kukizamisha ndani ya maji hayo na baadae uende kuipanda shambani kwako, hivyo uewezekano wa miwa yako yote kuote utakuwa ni mkubwa sana maana shida kubwa ni mchwa na hapo tayari utakuwa umeidhibiti.

UPANDAJI WA MIWA

Hakikisha unapokuwa unapande miwa yako acha nafasi ya mita moja (1m) kati ya mche na mche pia hakikisha una acha nafasi ya mita moja (1m) kati ya mstari na mstari. Kumbuka awali tulisema katakata muwa wako kupata vipande vilivyo na vipingili vitatu vitatu, hivyo sasa unapokuwa unapande miwa hii hakikisha hizo pingili zote 3 zimezama ndani ya ardhi na kipande kidogo tu ndio kibakie juu ya uso wa ardhi na mche wako huo unapoutumbukiza kwenye ardhi uwe umelala wastani wa nyuzi 30.

Zile pingili katika muwa wako kumbuka ndipo sehemu hasa miwa inamokuwa inachipuka na kuota. Mantiki ya kuacha nafasi kubwa kati ya mche na mche ni kwa sababu hilo shina lako moja ulilolipanda linaweza likachipua vijimiwa vingine zaidi hata ya ishirini kama ukiliacha shina liendelee kuzaa tu kwa kadri linavyotaka na hatimaye shamba lako litakuwa msitu hata usiopitika.

Lakini kibaya zaidi ni kwamba miwa yako itakosa afya njema na mwisho wa siku miwa yako haitakuwa bora hata bei haitakuwa nzuri pindi utakapoamua au wakati wa kuuza utakapofika. Hivyo unashauriwa kuacha miwa kati ya tano mpaka kumi lakini mfano ukiacha miwa mitano katika shina moja ni dhairi hewa na mwanga vitakuwa vya kutosha shambani lakini hata chakula na virutubisho vingine kwa miwa hiyo vitakuwa lukuki na sio vya kung’ang’aniana hivyo mwisho wa siku utapata miwa mirefu na minene ambayo sokoni itakuwa na mvuto mkubwa kwa wateja.

Mfano chukulia kwamba umelima ploti ndogo tu ya upana mita 50 kwa urefu mita 70, kumbukumbu namna ya upandaji miwa kama tulivyozungumza hapo awali umbali wa mita moja moja kwa kila shina. Hivyo kwa ploti ya shamba hili utakuwa na miche au mashina uliyopanda kiasi cha 70×50=3500 (mashina elfu tatu na mia tano) sasa chukulia kwa hesabu rahisi kwamba kila shina umeruhusu miwa mitano tu ndio ikuwe pale maana yake kwa mashina 3500 utazidisha mara 5 ambapo itakuwa 3500×5= 17,500 hiyo ndio itakuwa jumla ya miwa itakayovunwa shambani.

Kwa tafiti zilizofanywa zinaonesha kama hautaki shida na unahitaji pesa ya haraka haraka sana huko huko shamba, basi unaweza ukajumlisha miwa yako kwa bei ya chini sana yaani tukadilie vile kwamba tunahitaji pesa ya haraka so tuuze muwa mmoja kwa bei ya jumla ya 300 hivyo jumla ya pesa utakayoipata itakuwa 17,500 × 300 = 5,250,000 (milioni tano laki mbili na nusu). Hiyo ni pesa ya haraka haraka huko huko shambani .

Ila kama ukiweza kusogea zaidi na kuuza kwa faida maana kama umeweza kupigana mpaka kuweza kuikuza ni dhairi kwamba unastahili kupata faida iliyo njema kwako hivyo ni muhimu kuangalia masoko yamekaaje pande zote za miji, ila kama utaweza kuifikisha Dar es Salaam ambako kiuhalisia soko lake ni kubwa sana .

Kama ukienda Kariakoo bei ya rejareja kwa muwa aina ya bungala wenye wastani wa urefu mita moja na robo bei yake ni 5,000 lakini ukienda mtaani kwa muwa huo huo aina ya bungala mfupi kidogo bei yake inakwenda mpaka 3,500 hivyo chukulia kwamba umeweza kufikisha Dar es Salaam huo mzigo wako wa miwa, hivyo mapato yako kama utaamua uuze kwa bei ya jumla ya 1,500 kwa kila muwa hivyo kiasi cha fedha utakachokipata kitakuwa ni sawa na idadi ya miwa yako zidisha bei ya kujumlishia yaani ingekuwa 17,500 × 1,500= 26,250,000 hii ni pesa utayoipata kwa halali kabisa wala haujamzulumu mtu.

Hapo umelima ploti ndogo tu, sasa chukua pengine umelima ekari moja na kwa shamba la miwa ekari moja kiwango cha chini kabisa cha wewe kuvuma miwa yako ni jumla ya miwa 24,500. Sasa chukulia kama umeweza kuipeleka Dar es Salaam maana yake utapata jumla ya 24,500 × 1,500= 36,750,000. Sasa mfano ndo ukalima ekari 4 hadi 5 hapo ni hakika unatoka katika kundi la uchumi wa chini na kuingia katika uchumi wa kati. Jamani bado hatujachelewa kungali bado fursa ziko kinachohitajika hapa ni kuthubutu tu, Mungu akubariki unapoyatafari haya lakini pia pindi ukifanikiwa usimsahau Mungu maana yeye ndiye nguzo ya mafanikio yako yote.

September 10, 2018

TENGENEZA MAFUTA YA VASSELINE PETROLIUM JELLY

Mahitaji:-

Parrafin oil vijiko 6 vya chakula

Petrolium jerry kikombe 1-2

Parrafin wax vijiko 2 vya chai

Lanolline kijiko 1 cha chakula

Fragrance  kijiko 1 cha chai

Vitamin E kijiko kimoja cha chakula

Chukua sufuria safi 

Weka jikoni kisha chukua parafine oil,parafine wax,petrolium jelly na lanoline kisha changanya kisha weka vit E na uchanganye vizr koshaipua koroga acha ipua na uweke fragrance kisha changanya na uache ipoe kbs 

Fungasha tayari  kwa matumizi

MKATE WA KUMIMINA

Vipimo


· 1 KIKOMBE CHA MCHELE  


· 1 KIKOMBE CHA NAZI YA UNGA 


·  1 KIKOMBE CHA SUKARI KUPUNGUA KIDOGO


· 1 KIKOMBE CHA MAJI AU MAZIWA VUGUVUGU


· 1 KIJIKO CHA CHAI CHA HAMIRA


· ILIKI KIASI UPENDAVYO


· UTE WA YAI MOJA 

Namna Ya Kutayarisha Na Kulpika

Osha na kuroweka mchele siku moja ndani ya maji ya baridi.Saga ndani ya blender, mchele, tui, maji au maziwa, iliki, na hamira mpaka  mchanganyiko uwe lani kabisa. Mimina ndani ya bakuli na ufinike. Weka mahali penye joto ili mchanganyiko uumuke(ufure).Mchanganyiko ukifura, washa oven moto wa 350°. Mimina sukari pamoja na ule ute wa yai ndani ya mchanganyiko na uchanganye vizuri. Ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.Chukua sufuria umimine mafuta kidogo. Washa jiko na uweke sufuria ipate moto kiasi. Mimina ule mchanganyiko ndani ya sufuria uuwache kama dakika 5 hivi kiasi mkate uanze kushikana.Funika sufuria na uvumbike(bake) ndani ya oven kama dakika 35-40 hivi, au mpaka mkate uive na uwe rangi ya hudhurungi juu yake.Epua na uwache upoe kabisa kabla ya kukata. Ni bora kuula siku ya pili yake.


 

VILEJA VYA TAMBI

MAHITAJI:

Siagi 1/4

Tambi nyembamba mifuko 2

Condensed milk/ maziwa mazito 1 kikopo 

Hiliki 1 tsp

Vanilla1tsp


UFANYAJI:

Chukuwa tambi zako zivunje lkn vizuri toboa ule mfuko kidogo hlf zivunje ndogo ndogo  mule mule hutoomia  mikono hlf teleka sufuria lako jikoni tia siagi yako ikishayayuka tia tambi zako anza kuzikaanga litigation kwa mwiko kidogo kidogo usieke moto mwingi mpk utaziona zimebadilika rangi lkn zisije zikaunguwa ziwe brown km hio picha hapo  zitakuwa tayari zima jiko ,funguwa yale maziwa yako yatie ile vanilla na hiliki hlf koroga then mimina kwenye zile tambi zako na ukoroge vizuri ili zichanganyike pamoja fanya upesi upesi ili visikauke chota kwa kijiko utie kwenye vikombe vya kahawa udidimize ,mie nimetia kwenye cup cake try ukimashadidiza kibirue kikombe juu chini ukikukute kitatoka wenyewe fanya hivo mpk umalize panga kwenye sahani serve kwa coffee or milk tea

September 01, 2018

KILIMO BORA NA RAHISI CHA STRAWBERRY

Utangulizi

strawberry (fukasidi) hustawi katika maeneo yenye joto la wastani, na hukua kwa haraka zaidi na uzalishaji kuongezeka linapolimwa kisasa zaidi, Hasa katika Green house. Zao hili hukua vizuri katika mwinuko wa mita 1500 na zaidi kutoka usawa wa bahari. Zao hili hata Tanzania hustawi zaidi katika mikoa mingi kama Morogoro,mbeya,iringa, Arusha, Kilimanjaro, na Pia hufanya vizuri katika mikoa ya Pwani endapo utalima kisasa zaidi na kufuata maelekezo ya kitaalamu(Under controlled condition)

Udongo


strawberry inaweza kustawi vizuri kwenye udongo tifutifu wenye rutuba. Zao hili haliwezi kustahimili ukuaji kwenye udongo wenye chachu nyingi, hasa chokaa kwani mizizi yake huoza kwa urahisi, Pia udongo unaotuamisha maji kama mfinyanzi sio mzuri sana kwa ustawishaji wa strawberry, Pima Udongo kabla ya kuanza kilimo sio kwa strawberry peke yake hata kwa mazao mengine 

Kupanda

Ili kuwa na mazao bora ambayo yatakuwezesha kupata soko la uhakika,  inashauriwa kuzalisha kwenye nyumba maalumu ya kuzalishia mazao (green house). 

1. Katika upandaji wa strawberry kwenye green house Utahitajika kuwa na Mabomba yenye matundu(Plastic Pipe)

  Matundu katika bomba hilo yawe na umbali wa inchi 1.
2.  Ni vyema matundu hayo yakawa zigzag, ili kuruhusu mimea utakayoipanda kukua vizuri bila kusongamana

        3. Tandika karatasi la nylon sakafuni ili kuwezesha maji utakayotumia kunyeshea kurudi kwenye bwawa au

sehemu ya kuhifadhia.

        4.Ning’iniza mabomba hayo kwa kutumia waya.

       5. Jaza kokote, yenye mapande makubwa kiasi.

       6 .Panda miche kwenye kila tundu kwa uangalifu ili mizizi isikatwe na kokoto zinazoshikilia mmea.

Kupanda Kwenye Shamba la Kawaida


Umwagiliaji


Mimea ya strawberry inahitaji maji kwa kiasi kikubwa sana. Hii inamaanisha kuwa unahitaji kuwa na mfumo mzuri

wa umwagiliaji kabla ya kuanza kilimo cha zao hili. Unapaswa kumwagilia mara nne kwa siku, kila baada ya saa nne unapaswa kumwagilia kwa robo saa. Hii itawezesha mimea yote kupata maji ya kutosha. Endapo stroberi haitapata maji ya kutosha, uzalishaji wake pia utakuwa ni hafifu sana, kwani maua hayatachanua ipasavyo na hata matunda kukomaa inakuwa ni shida.

Kuvuna

Zao la strawberry  huzaliana na kukomaa kwa haraka sana. Unaweza kuanza kuvuna stroberi baada ya mwezi mmoja tangu kupandwa. Kila wiki stroberi inakuwa na matunda mapya, na kila tunda likishatokeza huiva kwa haraka, hivyo uvunaji wake ni wa mfululizo ikshafikia hatua hiyo tegemea kuwa na wiki 2-3 za kuvuna mfululizo.

Kwa kuwa matunda ya stroberi ni laini, epuka kushika tunda wakati wa uvunaji ili lisiharibike. Shika kikonyo

cha tunda ili kuvuna kwa usalama. Usiache matunda yaliyoiva shambani kwa muda mrefu kwani yanaweza

kusababisha mimea kuoza. Pia yatapoteza ladha na virutubisho halisi vinavyotakiwai

Wadudu na magonjwa

Endapo strawberry inazalishwa kwenye nyumba maalumu ya mimea, hakuna magonjwa wala wadudu wanaoishambulia. Ikiwa mkulima anazalisha stroberi kwenye eneo la wazi, stroberi inaweza kushambuliwa na magonjwa ya ukungu, pamoja na magonjwa yanayosababishwa na virusi. Kama vile;

Wadudu Waharibifu wa Strawberry.

 Spider (two spotted) mite

a.  Cluster caterpillar

b.  Heliothis

c.  Looper

d.  Rutherglen bug

e.  Cutworm

f.  Aphids

g.  Queensland fruit fly

Magonjwa Lethal yellows

Mmea ulioathirika unaonyesha dalili zifuatazo;

   Majani yaliyokomaa yanakuwa na rangi ya dhambarau na yanajinyonganyonga kwa upande wa juu na kusababisha kuangua chini.

Majani chipukizi yanakuwa na rangi ya njano katika kingo za jani na kupelekea kudumaa kwa kikonyo cha jani. Huu ugonjwa unapunguza nafasi ya jani kushindwa kujitengenezea chakula chake na hivyo mmea kudumaa na kupelekea kufa kwa mmea.

Mnyauko fusari (fusarium wilt)

Huu ugonjwa huunezwa na mbegu zenye huu ugonjwa na husambazwa na vimelea vya fangasi ambavyo vipo kwenye udongo.

Ugonjwa huu hujitokeza Zaidi kwenye kipindi cha kiangazi na hushambulia sehemu za mirija yam mea ya kupitishia chakula hivyo mmea hukosa chakula na maji na hatimaye unyauka na kufa. Na shina la mmea ukipasua ndani unakuta lina rangi ya kahawia.

Kudhibiti

1.  Tumia mbegu safi na bora.

2.  Tumia dawa ya kuua wadudu na magonjwa ili kupata mazao mengi na yenye ubora.

3.  Choma masalia ya mazao ili kudhibiti uenezaji wa ugonjwa

4.  Chagua mbegu ambayo ina uwezo wa kuhimili magonjwa.

Matumizi ya strawberry


Matunda ya strawberry yana matumizi mbalimbali kulingana na uhitaji wa mtumiaji, jamii na maeneo.

Miongoni mwa matumizi hayo ni pamoja na  

  Kuliwa kama tunda  Kutia ladha katika aina mbalimbali za vyakula.  Kuweka rangi, harufu na nakshi katika vipodozi.  Kutengeneza marashi n.k.

strawberry inapooteshwa kwenye greenhouse hutoa mavuno mengi na yenye ubora. Wasiliana na wataalamu wa green agriculture kwa ajili ya ujenzi wa green house kwa ajili ya uzalishaji bora wastrawberry.


Visit website