1.1.1.ELIMU YA UJASIRIAMALI NA STADI ZA
BIASHARA
1.
Ujasiriamali katika sekta ya biashara (Entrepreneurship)
Ujasiriamali
ni kuanza na kuendesha na kumiliki biashara inayojitegemea.
1.1.2.Mjasiriamali ni nani?
Mtu
yeyote anayeamua kuchukua uamuzi hatarishi kwa kuwekeza mtaji katika kuanzisha
mradi ili kuingiza kipato na kupata faida.
1.1.3.Sifa za mjasiriamali
1.1.3.Mjasiriamali ana sifa kuu tatu:
1.Ni mwenye ufahamu.
2.Ni mwenye stadi.
3.Ni mwenye tabia za kijasiriamali.
·
Ni mwenye
ufahamu Mjasiriamali lazima awe
na ufahamu.. wa mambo yote yanayohusu kuanzisha na kuendesha miradi ya
kuongeza kipato/biashara. Ufahamu wa kujua nini maana ya biashara, kujua
kutathmini wazo la mradi, kutengeneza mchanganuo wa mradi na habari zote za
masoko.
·
Ni mwenye
stadi ..Mjasiriamali lazima awe
na ujuzi wa mradi anaoamua kuanzisha.
·
Ni mwenye
tabia za kiujasiriamali..Ujasiriamali
si tu kufanya biashara bali ni ile tabia unayoweza kuionyesha kwenye biashara
yako. Mjasiriamali ana tabia zifuatazo:
(a)
Ni mbunifu (Innovative)
M jasiriamali ni mbunifu katika biashara kwa
kuweka kitu kipya, mambo mapya, taratibu mpya, mipango mipya, kuweka huduma
tofauti na wenzake wenye biashara ileile.
(b) Ni
mwenye kuthubutu (Risk-taking)
Kuthubutu kwa mjasiriamali kuna kuja kwa njia nyingi
kama vile
Ø Kufanya uamuzi wa kuwekeza.
Ø Kufanya uamuzi wa kuanzisha mradi au
kufanya Biashara
No comments:
Post a Comment