March 31, 2017

UTOFAUTI KATI YA VICOBA NA SACCOS



Kuna tofauti gani kati ya VICOBA na SACCOS?
VICOBA na SACCOS ni vikundi vya kiuchumi vyote vina malengo sawa isipokuwa mfumo wa uendeshaji.
1.         Katika VICOBA wanachama uweka kiwango cha hisa na mara nyingi huanzia Sh.1000 na kuendelea, kiwango hicho ni kidogo ukilinganisha na kiwango cha hisa katika SACCOS.
2.       WanaVICOBA umaliza mzunguko wao baada ya miezi kumi na mbili (12) na kufanya tathmini ikiwemo kugawana makusanyo na faida.
3.      Riba ya mkopo katika VICOBA ni ndogo (mara nyingi haizidi 10%)
4.     Kikundi cha VICOBA kinaundwa na wanachama 15-30, wanaoishi eneo moja au wanaofanya kazi pamoja.
5.       Gharama za uendeshaji wa VICOBA ni ndogo kwani hakuna ofisi (wanachama huchagua mahali pa kukutana kwa muda usiozidi saa moja), vile vile viongozi wa VICOBA hawaajiriwi (wanafanya kazi za kujitolea)

March 30, 2017

UFUAJI WA KUKU WATANO WAKIENYEJI UPATE KUKU 200 KWA MIEZI 6 TU ,,,10,000/= MARA 200= 2000,000/=


Hebu anza na kuku Watano (5) tu Majike wenye Rika/Umri mmoja (au wanaokaribiana). Watunze vizuri kwa kuwapatia chakula kilicho na mchanganyiko kamili wa viini lishe vinavyotakiwa katika mwili wa kuku, yaani; wanga, protini, calcium, chumvichumvi, madini joto nk (kama nilivyoeleza hapa chini). Wawekee na Jogoo mmoja mzuri wa kienyeji/kizungu/chotara (kama nilivyoeleza hapa chini juu ya uchaguzi wa majogoo).

Wanapoanza kutaga watayarishie mahali pazuri/Kiota kizuri cha kutagia na kuatamia kwa kuwajengea viota ndani ya banda. Hakikisha mahali hapo hapavuji wala hapapati unyevunyevu wala joto kali sana. Hakikisha mahali hapo pana usalama wa kutosha (mahali wanyama hatari kama vicheche, pakashume, nyoka nk hawawezi kufika).

Kuku wakiendelea kutaga na sasa ukaona wanakaribia kuatamia,Anza kuchagua aina ya mayai unayotaka kuku wako walalie. Hii inamaanisha kuwa; ukichagua mayai makubwamakubwa hayo yanakuwa na vifaranga majogoo na mayai madogomadogo mara nyingi huwa ni ya vifaranga majike. Acha kuwawekea mayai ya mviringo kama mpira!

Hakikisha kuku wote wanasubiriana ili walalie/waatamie kwa pamoja.

Weka mayai 12 hadi 15 kwa kila kiota cha kuku 1 kulingana na umbo la kuku wako. Kuku anaweza kutaga hadi mayai 30 kwa kila msimu wa kutaga unapofika. Unaweza kutumia mayai machache kati ya 30 kwa kumuatamishia kuku wako huku mayai mengine yakisubiri awamu ya pili ya kuatamiwa.Kwa mfano ukiwawekea kuku wako hao watano, Kuku 5 x Mayai 12 = Mayai 60.

Kwa kawaida kuku huatamia/hulalia mayai kwa siku 19 hadi 21/24 tu hadi anapototoa vifaranga. Hakikisha unawawekea kuku walioatamia chakula chenye viini lishe vya kutosha na maji mengi karibu na viota vyao ili wakitoka kwenye viota vyao wale chakula mara moja na kunywa maji kisha warudi haraka kwenye mayai yao. Hii itasaidia kuangua mayai yote 12/15 bila kuharibu yai hata moja. Au hata yakiharikbika basi hayataharibika mengi kama ukiacha kuwawekea chakula waende kufukuzana na panzi na vyakula majalalani huko nje na kuchelewa kurudi kwenye mayai yao.

Wakati ukisubiria siku hizo 21/24 anza kujenga kibanda kidogo ndani ya banda kubwa ulilojenga awali au jikoni au andaa boksi kubwa na gumu kwaajili ya kutunzia vifaranga watakaoanguliwa ndani ya siku 21/24 zijazo.

Baada ya kuku hao 5
kuangua vifaranga wako 60 hapo ndipo kazi kubwa ya kulea vifaranga inapoanza. Elewa kuwa ili upate mafanikio haraka hakikisha kuwa kazi ya kulea vifaranga inakuwa yako na siyo ya kuku! Kwanza, Unatakiwa kuondoa na kuchoma moto/kufukia mabaki yote ya mayai na kuboresha usafi wa banda lote ili kuepusha magonjwa kama vile kuharisha, viroboto, papasi nk. Hapo unaweza kuwatoa vifaranga wako wote 60 mmojammoja kadri wanavyoanguliwa hadi kufikia kifaranga wa mwisho, yaani Yule wa 60 na kuwaweka katika kibanda kidogo/boksi ulichokijenga na kuwawekea mayai mengine mama zao (yale 15/18 kati ya 30 uliyoyabakiza) ili waatamie tena kwa siku 21 hadi 24 zingine. Unapotoa kifaranga kutoka kwa kuku aliyeatamia humfanya kuku Yule ashindwe kutoka kwenye mayai maana hana mtoto wa kulea.

Akimaliza kuangua mayai yote na ukamuwekea mengine ni rahisi kwake kuendelea kuatamia maana atasubiri kupata vifaranga na ndipo atajikuta amelalia kwa siku 21 zingine bila wasiwasi. Kwa kufanya hivyo utakuwa tayari umejipatia vifaranga/kuku zaidi ya 100 ndani ya wiki 7 tu! Sasa Unatakiwa kuwajali sana kuku hawa wanaolalia kwa mara ya pili kwa kuwapa chakula cha kutosha, maji, majani ya makongwe, mchicha, mchunga nk ili wapate vitamini na madini mengine muhimu kwa afya zao. Fanya hivyo hata watakapokuwa wametotoa na ukawanyang'anya vifaranga. Hii itawasaidia ili wasinyonyoke sana manyoya maana kuku wengi hunyonyoka manyoya wanapoatamia. Kwa kufanya hivi, kuku wako watakaa kwa wiki 2 hadi 3 bila vifaranga na kisha wataanza kutaga tena na kuatamia kama mwanzo.
Vifaranga wako hakikisha unawatengenezea chumba chao kido ndani ya banda kubwa/jikoni, kisha wawekee chanzo chochote cha joto kama vile; taa ya chemli/jiko la mkaa/vizinga vya moto nk ili wasiathiriwe na baridi hasa wakati wa usiku. Umakini mkubwa sana unatakiwa hapa! Hakikisha unakuwa makini wakati wa usiku ili kuongeza na kupunguza joto ndani ya kibanda cha vifaranga maana wakati huu maranyingi joto hupungua na ubaridi huongezeka na hivyo unaweza kuua vifaranga wako.

NAMNA YA KULEA VIFARANGA.
Katika ulezi wa vifaranga kama kuku utawanyang'anya vifaranga vyao utatakiwa kuwajengea banda dogo (ndani ya banda kubwa/uzio) ili uwawekee chanzo cha joto kama taa/jiko la mkaa (kama ni sehemu/majira ya baridi). Kama utatumia jiko la mkaa unatakiwa kuacha kwanza hadi mkaa mweusi uwake wote ndipo uweke bandani maana mkaa ukitoa moshi unaweza kuathiri vifaranga vyako. Angalia namna ya kuweka jiko lako la mkaa juu kidogo ili vifaranga wasiungue. Hakikisha taa yako haitoi moshi sana na haivujishi mafuta. Pia uwe na akiba ya mafuta ya taa ya kutosha. Usiweke mafuta mengi kwenye taa maana inaweza kulipuka ikakuletea hasara. Vifaranga wasizidi 50 kwa boksi 1. Hakikisha umewasha taa/jiko lako ndani ya boksi saa tatu au zaidi kabla ya kuwaweka vifaranga ili chumba/boksi lipate joto kabla ya vifaranga kuwasili. Njia hizi zinahitaji uangalifu wa hali ya juu sana kwani kuhatarisha/kuua vifaranga ni kuhatarisha maendeleo yako. Kama utaamua kutumia umeme pia ni vizuri zaidi maana inapunguza hatari zaidi.





KUTABU CHA UFUGAJI KUKU WATANO KINAPATIKANA KWA PDF 
WASILIANA NASI 0659144660/0758069046

KILIMO CHA BUSTANI HUTEGEMEA UDONGO YENYE RUTUBA










KUCHAGUA ENEO
1.kuandaa shamba- Katika uchaguzi wa eneo kwa ajili ya bustani zingatia yafuatayo:
  • Mwinuko- Eneo lisiwe kwenye mwinuko mkali kwa sababu sehemu kama hizo zinaweza kusababisha mmomonyoko wa udongo. Endapo sehemu itakuwa ya mwinuko tengeneza matungazi (terrace) ili kuzuia mmomonyoko.
  • Udongo- Udongo unaofaa ni wenye rutuba, mboji nyingi na unaopitisha maji kwa kirahisi. Vilevile usiwe na historia ya magonjwa na wadudu waharibifu.
  • Chanzo cha Maji -Eneo la bustani liwe karibu na maji ya kudumu. Maji yasiwe na chumvi nyingi kwani huathiri ukuaji wa mimea.
  • Kitalu -Kitalu kisiwekwe mahali palipo na kivuli kingi kwa kuwa husababisha mimea kuwa dhaifu.
  • Kuzuia Upepo Mkali-Eneo la bustani lipandwe miti mipakani ili kuzuia upepo mkali. Upepo mkali huharibu mimea kwa kuvunja vunja majani na matawi na husafirisha vimelea vya magonjwa na wadudu. Pia hufanya udongo wa juu kukauka haraka na kuleta mmomonyoko.
A.KUTAYARISHA MATUTA-Ni muhimu udongo utifuliwe vizuri. Mabonge makubwa yavunjwe vunjwe ili Kurahisisha upitaji wa maji na hewa katika udongo. Matuta huinuliwa kidogo toka usawa wa ardhi ili kuzuia maji yasituame. Matuta haya yasitumike wakati wa kiangazi. Wakati wa kiangazi tengeneza matuta yaliyodidimia kidogo.

B.KUMWAGILIA MAJI- Hakikisha udongo una unyevu wa kutosha kwa kumwagilia siku moja kabla ya kuotesha mbegu. Pia baada ya kupanda mwagilia kitalu au shamba maji ya kutosha. Maji mengi husababisha mbegu au miche kuoza.

C.KUPANDA-Kina cha kupanda kitategemea ukubwa wa mbegu. Mbegu ndogo hupandwa katika kina kifupi zaidi kuliko mbegu kubwa. Upandaji wa baadhi ya mbegu unaweza kufanyika kila wiki ili kuweza kupata mboga mfululizo.

D.KUOTESHA MBEGU KWENYE KITALU-Baadhi ya mbegu za mboga huoteshwa kwanza kwenye kitalu na baadaye miche huhamishiwa shambani. Mbegu hizini kama vile za bilinganya, kabichi, nyanya, pilipili hoho na vitunguu. Kitalu kwa ajili ya kuotesha mbegu hakina budi kitayarishwe wiki moj a kabla ya kusia mbegu. Wakati wa kutayarisha kitalu, ardhi ikatuliwe katika kina cha kutosha sentimita 30 kwenda chini. Ili kuongeza mtuba ya udongo mbolea za asili kama vile samadi, takataka na mbolea vunde zilizooza vizuri ziwekwe kabla ya kusia mbegu.
  E.KUTUMIA MBEGU BORA-Tumia mbegu bora zilizohifadhiwa kwenye dawa. Mbegu bora ni zile ambazo zimekomaa na kukauka vizuri, hazikushambuliwa na wadudu wala magonjwa na ambazo zina uwezo wa kuota vizuri. Inashauriwa kutumia mbegu zilizothibitishwa kitaalamu.

F.KUWEKA KIVULI NA MATANDAZO-Utandazaji wa majani makavu na uwekaj i wa kivuli ni muhimu ili kuzuia jua linaloweza kunyausha miche. Matandazo pia husaidia kuhifadhi unyevu, joto la udongo na hupunguza palizi ya mara kwa mara. Kivuli kiruhusu mwanga wa kutosha na kiondolewe kidogo kidogo kadiri mimea inavyokua.
Uwekaji wa kivuli ni muhimu ili kuzuia jua kali

G.KUITAYARISHA MICHE KABLA YA KUPANDIKIZA:-Wiki mbili kabla ya kuihamisha miche toka kitaluni, unashauriwa kupunguza kumwagilia ili kuizoesha iweze kustahimili hali ya sehemu inapohamishiwa. Mwagilia kitalu siku moja kabla ya kung'oa miche ili kurahisisha ung'oaji na kuepuka kuikata mizizi. Pia shamba kwa ajili ya kuhamishia miche limwagiliwe siku moja kabla ya kupandikiza ili kuloanisha udongo.

MATUMIZI YA MBOLEA
  1. Mboji, Samadi na Mbolea Vunde
    Mboga hustawi, vizuri sana katika udongo wenye mbolea hizo. Hivyo ni vema mbolea hizo ziwekwe shambani kabla ya kupanda au kupandikiza. Kiasi kinachotakiwa ni ndoo moja kwa tuta lenye upana na urefu wa mita moja.
  2. Mbolea za Viwandani
    Mbolea za viwandani zimegawanyika katika makundi makuu matatu, nayo ni mbolea za chumvichumvi, chokaa na kijivu,
(a) Mbolea za Chumvichumvi
Mbolea hizi hujulikana kama mbolea za kukuzia na huwekwa shambani baada ya mimea kuota. Zina virutubisho vingi vya Naitrojeni ambavyo huifanya mimea kukua haraka.Pia zinahusika na utengenezaji wa kijani kibichi kwenye mmea.

Nchini Tanzania mbolea za chumvichumvi zinazotumika zaidi ni:-

- Sulphate ofAmmonia (S/A) 21% N
- Calcium Ammonium Nitrate (CAN) 26 % N
- Urea 46% N.
- Mbolea ya mchanganyiko N.P.K. 25.5.5 na 20.10.10

(b) Mbolea za Chokaa-Hizi ni mbolea zinazotumika kupandia mbegu au miche. Husaidia uotaji mzuri wa mimea, huimarisha mizizi, na hutumika katika utengenezaji wa chakula na mbegu kwenye tunda. Vilevile huhusika na usafirishaji wa nguvu kwenye mmea na hufanya mazao kukomaa haraka. Mbolea hizi huwekwa shambani wakati wa kupanda.

Aina ya mbolea za chokaa zinazotumika hapa nchini ni Triple Super Phosphate (TSP) 46% P2O5. Vilevile unaweza kutumia N.P.K 6.20.18 kwa kupandia.

(c) Mboleaza Kijivu (Potashi)-Potashi ni kirutubisho kinachosaidia mimea katika utengenezaji wa protini na wanga. Kadhalika huhusika na utumiaji wa madini muhimu kwa maisha ya mimea. Mbolea hii pia huwezesha matunda kukomaaa, kuiva haraka, na kutengeneza mbegu bora. Vilevile husaidia ongezeko la maji kwenye mmea na kuufanya ustahimili magonjwa, ukame, baridi na hali ya udongo wenye alkalini nyingi.

Mbolea za Potashi zinazotumika ni:-
- Muriate of Potash 48 - 60% K2O
- Sulphate of Potash 48 - 50% K2O

H.KUBADILISHA MAZAO SHAMBANI-Kubadilisha mazao shambani ni utaratibu wa kuachs kupanda mfululizo aina ileile ya zao katika eneo hilo hilo. Iwapo eneo ni kubwa, bustani igawanywe katika sehemn tatu au nne ili kuepuka kupanda mfolulizo aina ileile ya zao. Katika kila sehemu panda aina nyingine ya mazao na ya familia tofauti kila baada ya kuvuna.

Baada ya kuvuna; mazao ya sehemu ya kwanza yapandwe katika sehemu ya pili, ya pili katika sehemu ya tatu na ya tatu yapandwe katika sehemu ya nne na yale ya nne yapandwe katika sehemu ya kwanza.
Kubadilisha mazao shambani huzuia ongezeko la wadudu na magonjwa yanayoshambulia jamii moja ya zao. Vilevile huhifadhi rutuba ya udongo na huzuia uotaji wa magugu. Utaratibu huu pia humwezesha mkulima kuweka kiasi cha mbolea kinachotakiwa shambani. Ufuatao ni mfano wa kubadilisha mazao.

MFANO WA KUBADILISKA MAZAO
Jamii ya Nyanya
  • Bilinganya
  • Nyanya
  • Pilipili
  • Viazi Mviringo
Jamii ya Matango
  • Matango
  • Maboga
  • Matikiti Maji
Mimea ya Mizizi
  • Karoti
  • Vitunguu
I.MATUMIZI YA MADAWA-Ni muhimu kutumia madawa ili kukinga mimea kutokana na athari za wadudu na magonjwa. Hata hivyo madawa yatumike pale inapobidi kwani ni ghali na yana madhara kwa mazingira na watu.
Mambo yafuatayo yanatakiwa kuzingatiwa wakati wa kutumia madawa. Hakikisha unatumia dawa inayoshauriwa na wataalamu.
  1. Soma kwa uangalifu maelezo yanayoambatana na dawa toka kwa watengenezaji, kabla ya kutumia na yasikiukwe. Hii itakusaidia kujua vifaa, kiasi na jinsi ya kutumia. Madawa ni hatari kwa binadamu na wanyama kama yatatumika isivyopasa.
  2. Wakati wa kuchanganya na kunyunyizia dawa, vaa nguonavifaavyakinga. Vifaa hivi ni kofia, glovus, viatu (gumboots), kitambaa cha kufunika mdomo na pua, miwani na ovaroli.
  3. Tumia maji safi kuchanganya dawa.
  4. Epuka kuvuta hewa yenye dawa. Wakati wa kunyunyizia dawa usielekee upepo unakotoka bali elekea upepo unakoenda.
  5. Usile wala kuvuta wakati wa kuchanganya au kunyunyizia dawa.
  6. Baada ya kunyunyizia dawa osha mwili kwa sabuni na maji mengi na safi.
  7. Maji yanayotumika kusafishia bomba yasimwagwe katika maji yaliyotuama au yanayotembea kwani yanaweza kuleta madhara sehemu nyingine. Maji yamwagwe kwenye shimo na kufukiwa.
  8. Nguo na vifaa vingine vilivyotumika zifuliwe mara moja kwa sabuni na maji safi.
  9. Osha vizuri mikono kwa sabuni kabla ya kula, kunywa chochote au kuvuta sigara.
  10. Makopo au chupa zilizokuwa na dawa zisitumike bali ziharibiwe na kufukiwa.
  11. Hifadhi madawa mahali salama na pasipofikiwa na watoto kwa urahisi. Dawa ziachwe katika makasha., chupa au makopo yake zilimokuwemo. Hata siku moja madawa ya mimea yasitumike kwa kutibu binadamu.
  12. Endapo kutakuwepo na matatizo yeyote katika matumizi muone Mtaalamu kwa ushauri.
  13. Iwapo sehemu ya kutolea dawa itaziba, tumia nyasi au kijiti kuzibua. Kamwe usizibue kwa mdomo.
J.UTUMIAJI WA MBOGA BAADA YA KUNYUNYIZIA DAWA-Mboga zisitumike mara baada ya kunyunyizia dawa. Kila dawa ina siku zake za salama, lakini kwa madawa yaliyo mengi ni siku 14 toka kunyunyizia. Hivyo ni muhimu kusoma maelezo yanayoambatana na dawa. Ikiwa mboga zitatumika kabla ya muda huo huleta madhara kwa mlaji kama vile magonjwa ya kansa. Vilevile mbegu zilizowekwa dawa zisitumike kwa kula.

K.MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU-Ni muhimu kukinga mimea dhidi ya wadudu na magonjwa ili kupata mazao mengi na bora. Zifuatazo ni njia mbalimbali zinazoweza kutumika katika kuzuia magonjwa na wadudu waharibifu.

K.UTHIBITI SANGO
Njia hii hutumia mbinu zifuatazo
  • Kupanda mbegu bora;
  • Usafi wa bustani ambao ni pamoja na kuchoma takataka na kuondoa magugu yanayoweza kutunza wadudu na magonjwa.
  • Kuchanganya mazao
  • Kutumia samadi na mboji
  • Kupanda kwa nafasi
  • Kutumia aina ya mbegu zinazovumilia au kustahimili mashambulizi ya magonjwa na wadudu
L.UDHIBITI WA KITEKNOLOJIA
Kutumia aina mbalimbali za madawa
  • Kutumia mimea inayoua wadudu, kama vile muarobaini, pilipili kali, aina fulani ya maua, marejea, tumbaku, wadudu kama vile walawangi, manyigu na mbawakau.

2.VIFAA VYA BUSTANI
Ili kuboresha kilimo cha mboga ni muhimu kuwa na

1.       jembe,

2.      kamba,

3.      reki,

4.     uma wa bustani

5.      ndoo ya kumwagilia maji,

6.     bomba la kunyunyizia dawa,

7.      toroli, panga,

8.      kwanja, sepetu,

9.     beleshi karai

10.  gan buti nk

 KITABU CHA KILIMO CHA BUSTANI KINAPATIKANA KWA PDF WASILIANA NASI 0659144660/0758069046

MJASIRIAMALI ANASIFA ZAKIJASIRIAMALI



1.1.1.ELIMU YA UJASIRIAMALI NA STADI ZA BIASHARA
1. Ujasiriamali katika sekta ya biashara (Entrepreneurship)
Ujasiriamali ni kuanza na kuendesha na kumiliki biashara inayojitegemea.
1.1.2.Mjasiriamali ni nani?
Mtu yeyote anayeamua kuchukua uamuzi hatarishi kwa kuwekeza mtaji katika kuanzisha mradi ili kuingiza kipato na kupata faida.
1.1.3.Sifa za mjasiriamali
1.1.3.Mjasiriamali ana sifa kuu tatu:
          1.Ni mwenye ufahamu.
          2.Ni mwenye stadi.
          3.Ni mwenye tabia za kijasiriamali.
·        Ni mwenye ufahamu Mjasiriamali lazima awe na ufahamu.. wa mambo yote yanayohusu kuanzisha na kuendesha miradi ya kuongeza kipato/biashara. Ufahamu wa kujua nini maana ya biashara, kujua kutathmini wazo la mradi, kutengeneza mchanganuo wa mradi na habari zote za masoko.
·        Ni mwenye stadi ..Mjasiriamali lazima awe na ujuzi wa mradi anaoamua kuanzisha.
·        Ni mwenye tabia za kiujasiriamali..Ujasiriamali si tu kufanya biashara bali ni ile tabia unayoweza kuionyesha kwenye biashara yako. Mjasiriamali ana tabia zifuatazo:
(a)  Ni mbunifu (Innovative)
 M jasiriamali ni mbunifu katika biashara kwa kuweka kitu kipya, mambo mapya, taratibu mpya, mipango mipya, kuweka huduma tofauti na wenzake wenye biashara ileile.
 (b)  Ni mwenye kuthubutu (Risk-taking)
Kuthubutu kwa mjasiriamali kuna kuja kwa njia nyingi kama vile
Ø Kufanya uamuzi wa kuwekeza.
Ø Kufanya uamuzi wa kuanzisha mradi au kufanya Biashara