ENTRE-BUSINESS
SOLUTION CO LTD
TUNAWAFIKIA KWA: Elimu ya ujasiriamali
na stadi bora za biashara, Fursa mbalimbali za biashara Tanzania, Uhamasishaji,
uundaji na uboreshaji wa vikundi vya maendeleo na Simu; 0659 144 660 / 0758 069
046 / imfo.ebusol@gmail.com / ebusol.blogspot.com
Ilala DCC Karume Dar es salaam
1. ELIMU YA UJASIRIAMALI NA STADI
BORA ZA BIASHARA
Ujasiriamali
ni kuanza na kuendesha na kumiliki biashara inayojitegemea.
2. Mjasiriamali
ni nani?
Mtu yeyote
anayeamua kuchukua uamuzi hatarishi kwa kuwekeza mtaji katika kuanzisha mradi
ili kuingiza kipato na kupata faida.
3. Sifa
za mjasiriamali
Mjasiriamali
ana sifa kuu tatu:-
1. Ni mwenye ufahamu.
2. Ni mwenye stadi.
3. Ni mwenye tabia za kijasiriamali.
(i) Ni
mwenye ufahamu
Mjasiriamali
lazima awe na ufahamu wa mambo yote yanayohusu kuanzisha na kuendesha miradi ya
kuongeza kipato/biashara. Ufahamu wa kujua nini maana ya biashara, kujua
kutathmini wazo la mradi, kutengeneza mchanganuo wa mradi na
habari zote za
masoko.
(ii) Ni
mwenye stadi
Mjasiriamali
lazima awe na ujuzi wa mradi anaoamua kuanzisha.
(iii) Ni
mwenye tabia za kiujasiriamali
Ujasiriamali
si tu kufanya biashara bali ni ile tabia unayoweza kuionyesha kwenye biashara
yako. Mjasiriamali ana tabia zifuatazo:-
(a) Ni mbunifu (Innovative)
M jasiriamali ni mbunifu katika biashara kwa
kuweka kitu kipya, mambo mapya, taratibu mpya, mipango mipya, kuweka huduma
tofauti na wenzake wenye biashara ileile.
(b) Ni mwenye kuthubutu (Risk-taking)
Kuthubutu kwa mjasiriamali kuna kuja kwa njia
nyingi kama vile:
1.Kufanya
uamuzi wa kuwekeza.
2.Kufanya
uamuzi wa kuanzisha mradi au kufanya Biashara.
M jasiriamali huwa hajutii uamuzi na ushauri
alioufanyia kazi pale anapoanguka kibiashara au kupata hasara, hukaa chini na
kutafakari na kurekebisha makosa na kuendelea na biashara.
(c) Ni mwepesi wa kuona fursa (Opportunistic).
M jasiriamali ni mwepesi wa kuona fursa na
kuitumia, anazitafuta fursa, anaziendeleza, na anapata maendeleo.
(d) Ni
mwenye kuwa na malengo [achievement oriented]
M jasiriamali huweka malengo ya shughuli
anazozifanya, huwa haridhiki, anajitahidi kupanua kila wakati biashara yake,
anaiendeleza na kuikuza na baadaye malengo yake yanakuwa
makubwa.Wafanyabiashara walioridhika siyo wajasiriamali.
(e) Ni mwenye bidii (Hard working).
M jasiriamali ni mwenye bidii ya kufanya kazi
na hakati tamaa kirahisi.
(f) Anayejitegemea (Independent).
N i mwenye kushughulikia matatizo yake kwanza
mwenyewe, anatafuta ni jinsi gani ya kujikwamua mwenyewe, anafikiria kwanza
mwenyewe kabla ya kutafuta msaada.
(g) Ni mwenye kujenga uhusiano (Networking).
M jasiriamali anajitahidi kufahamiana na watu
wengine wengi, anapojenga uhusiano na watu mbalimbali inamsaidia kuondoa
matatizo mengi ya kibiashara.
(h) Ni
mwenye kuona mbali (Future oriented).
M jasiriamali anaangalia mbali katika
biashara. Hata akifa biashara yake inaendelea kuwepo.
(i) Ni mwenye kutunza kumbukumbu.
M jasiriamali ni mtunzaji wa kumbukumbu
zinazomsaidia kukumbuka, kuona kama anapata faida au hasara na inamsaidia kujua
mambo muhimu yanayohusu biashara zake kwa ajili ya maboresho.
4. Changamoto zinazowakabili wajasiriamali
(i) Miradi mingi ya kuongeza kipato inayoendeshwa
haina sifa ya kujiendesha kwa faida.
(ii) Wajasiriamali wengi hufanya biashara zao kwa
kubahatisha bila kujua wanatarajia nini na kwa kipindi gani.
(iii) Wajasiriamali wengi hawawezi kukopesheka kwa
sababu hawana cha kumshawishi mtoa mkopo ili aone kama fedha yake itarudi kwa
kukosa mpango biashara.
(iv) Wajasiriamali wengi wameshindwa kujua gharama
halisi za biashara yao kwa kukosa mpango wa biashara.
(v) Wajasiriamali wengi hawajui washindani wao na
mbinu za washindani wao, hivyo kushindwa kuweka mkakati wa kukabiliana na
washindani.
(vi) B iashara nyingi hukwama kufikia matarajio ya
mjasiriamali kwa kukosa kuzifahamu shughuli za masoko kwa undani.
(vii) U pangaji wa bei unachangia kuua biashara
nyingi ndogondogo kwa sababu kazi nyingi wanazozifanya wajasiriamali wanadhani
hazina gharama kwa kuwa wanatekeleza wao. Na hivyo huendelea kupunguza uwezo wa
biashara kidogo na hatiamaye hufa.
(viii) Wajasiriamali wengi wasiokuwa na stadi za
ujasiriamali na stadi za biashara huwa wanakimbilia sana kwa waganga wa
kienyeji wakati biashara zao zinayumba bila kufanya tathimini ya kina.
(ix) Biashara nyingi zinazoendeshwa na
wajasiriamali wadogo zinakabiliwa na tatizo kubwa la kutokutunza kumbukumbu kwa
usahihi kwa kutokujua umuhimu na faida zake. Biashara za namna hii mara nyingi
haziwezi kujibu maswali kama vile kipindi hiki faida katika biashara ni
shilingi ngapi. Ni marekebisho gani yanatakiwa kufanyika katika biashara ili
kuongeza ufanisi na tija, mjasiriamali amejipangia mshahara kiasi gani, kiasi
gani kimetumika kutoka kwenye biashara kwa matumizi binafsi.
By Ombeni haule
No comments:
Post a Comment