Mkufunzi: Ombeni D. Haule
WAZO LA BIASHARA: KUUZA VIFAA VYA SIMU
1.JINA LA BIASHARA:
Duka la Vifaa vya Simu
2.WAZO LA BIASHARA:
Kununua na kuuza vifaa mbalimbali vya simu kama chaja, earphones, USB cables, power bank, screen protector, cover, memory card na betri.
3.WATEJA LENGWA:
Wanafunzi, wafanyakazi, wafanyabiashara na watumiaji wote wa simu.
4.MTAJI WA KUANZIA:
Unaweza kuanza na takribani TSh 100,000–300,000, kulingana na aina na wingi wa bidhaa.
5.MAHALI PAKUFANYIA BIASHARA:
Sokoni, kituo cha daladala, karibu na shule/chuo, maeneo ya biashara au kupitia WhatsApp na mitandao ya kijamii.
6.MFANO WA MGAWANYO WA MTAJI:
Covers: TSh 50,000
Chaja: TSh 50,000
USB cables: TSh 30,000
Earphones: TSh 30,000
Screen protectors: TSh 20,000
Usafiri/ufungashaji: TSh 20,000
7.FAIDA:
Bidhaa nyingi zinaweza kununuliwa kwa bei ya jumla na kuuzwa kwa bei ya rejareja, hivyo kupata faida kwenye kila bidhaa.
8.MKAKATI WA MAFANIKIO:
Nunua bidhaa zinazotumika sana, linganisha bei za wauzaji mbalimbali, epuka bidhaa zenye ubora duni, weka bei zinazoshindana na tumia WhatsApp/Facebook/TikTok kutangaza.
9.HITIMISHO:
Biashara ya vifaa vya simu inaweza kuanzishwa kwa mtaji mdogo na kukua hatua kwa hatua kwa kuongeza aina na idadi ya bidhaa kulingana na mahitaji ya wateja.
10.HITIMISHO:
Jali muda, lugha nzuri, usafi na kuwapa motisha wateja wako.

Maoni
Chapisha Maoni