Mkufunzi: Ombeni D. Haule.
1.JINA LA BIASHARA:
Duka la Nyama Safi.
2.WAZO LA BIASHARA:
Kununua mifugo au nyama kutoka kwa wauzaji/ machinjio yenye usalama, kisha kuuza nyama safi kwa wananchi, familia, migahawa na wafanyabiashara wa chakula.
3.BIDHAA MUHIMU:
Nyama ya ng'ombe
Nyama ya mbuzi/kondoo na kuku
Maini, ulimi na utumbo
Vipande maalumu kulingana na mahitaji ya mteja
4.WATEJA WALENGWA:
Familia, migahawa, mama/baba lishe, hoteli na wafanyabiashara wa vyakula.
5.MTAJI WA KUANZIA:
Takribani TSh 500,000–2,000,000, na zaidi kulingana na ukubwa wa biashara na vifaa vinavyohitajika Kwa matumizi.
6.VIFAA MUHIMU:
Mizani, visu, mashine/eneo la kukatia, meza, ndoo, vifaa vya usafi, friji au freezer na vifungashio.
7.MAHALI PA BIASHARA:
Eneo lenye watu wengi, karibu na soko, makazi, migahawa au kituo cha biashara, likiwa na mazingira yanayokidhi masharti ya usafi.
8.FAIDA:
Faida hupatikana kupitia tofauti kati ya gharama ya kununua nyama na bei ya kuuza, pamoja na kuuza bidhaa nyingine za buchani.
9.CHANGAMOTO:
Kuharibika kwa nyama, kupanda kwa bei ya mifugo/nyama, ushindani na gharama za umeme na vifaa vya kuhifadhi.
10.HITIMISHO:
Biashara ya nyama buchani inaweza kuwa chanzo kizuri cha kipato ikiwa nyama inanunuliwa kwa bei nzuri, inatunzwa kwa usafi na ubaridi unaofaa, na huduma nzuri inatolewa kwa wateja.
11.ZINGATIA:
Jali muda, lugha nzuri, usafi na kuwapa motisha wateja wako.

Maoni
Chapisha Maoni