WAZO LA BIASHARA YA KUUZA MICHE

Mkufunzi: Ombeni D. Haule.

1.JINA LA BIASHARA:
Kitalu cha Miche Bora

2.AINA YA BIASHARA:
Kuzalisha na kuuza miche ya matunda, mboga na miti mbalimbali.

3.BIDHAA ZITAKAZOUZWA:
-Miche ya papai, embe, parachichi na chungwa

-Miche ya nyanya, pilipili na kabichi
Miche ya miti ya mbao na kivuli

-Miche ya maua na mapambo

4.WATEJA WANAOLENGWA:
Wakulima, wafugaji, taasisi, shule, kaya, wafanyabiashara na watu wanaopenda bustani.

5.MTAJI WA KUANZIA:
Tsh 100,000–300,000, kulingana na ukubwa wa kitalu.

6.VIFAA VYA MUHIMU:
Mbegu, vifuko vya miche, udongo, samadi, maji, vifaa vya kumwagilia na eneo la kitalu.

7.NAMNA YA KUPATA FAIDA :
Nunua au zalisha mbegu kwa gharama ndogo, zitunze vizuri hadi miche ikue, kisha iuze kwa bei yenye faida. Uzalishaji wa miche mingi huongeza mapato.

8.MASOKO:
Uza moja kwa moja kwenye kitalu, masoko ya wakulima, mitandao ya kijamii na kwa kuwaandalia wateja oda za miche.

9.FAIDA KUU:
Biashara hii inaweza kuanzishwa kwa mtaji mdogo, ina soko kwa wakulima na inaweza kupanuliwa hatua kwa hatua.

10.HITIMISHO:
Biashara ya kuuza miche mbalimbali ni fursa nzuri ya kujiajiri. Kwa usimamizi mzuri, ubora wa miche na masoko mazuri, inaweza kuleta kipato na kukua kuwa kitalu kikubwa cha kibiashara.

10.ZINGATIA
Jali muda, lugha nzuri, usafi na kutoa motisha Kwa mteja.

Maoni