Mkufunzi: Ombeni D. Haule
1.JINA LA BIASHARA:
ebusol mbogamboga na matunda.
2.MAELEZO YA BIASHARA:
Biashara hii inahusisha kulima, kununua mboga mbichi kama mchicha, matembele, kisamvu, kabichi, sukuma wiki, nyanya, vitunguu,karoti nk kutoka kwa wakulima au sokoni, kisha kuziuza kwa wateja katika eneo lenye mahitaji madogo na makubwa.
3.LENGO LA BIASHARA:
Kutoa mboga safi na zenye ubora kwa bei nafuu huku kupata faida na kujenga chanzo cha kudumu cha mapato.
4.WATEJA WANAOLENGWA:
Familia, wafanyakazi, mama lishe, migahawa, hoteli na wauzaji wengine wa chakula.
5.MTAJI WA KUANZIA:
Biashara inaweza kuanza kwa mtaji mdogo, kwa mfano TSh 50,000–100,000, kulingana na ukubwa wa biashara.
6.MAHITAJI YA MUHIMU:
Elimu,mtaji, meza au kibanda, vikapu, mifuko, beseni, mizani.
7.ENEO LA BIASHARA:
Soko, karibu na maeneo ya makazi, stendi, shule, ofisi au sehemu yenye watu wengi.
8.FAIDA:
Mboga ni bidhaa zinazotumika kila siku, hivyo zina soko la kudumu. Faida inaweza kuongezeka kwa kununua moja kwa moja kwa wakulima na kuuza kwa bei nzuri.
9.CHANGAMOTO:
Mboga huharibika haraka. Mfanyabiashara anatakiwa kununua kiasi kinacholingana na mahitaji, kuhifadhi vizuri na kuuza kwa wakati.
10.HITIMISHO:
Biashara ya kuuza mboga mbogamboga ni wazo rahisi kuanza kwa mtaji mdogo na linaweza kukua hatua kwa hatua kwa kuongeza aina za mboga na wateja.
ZINGATIA:
Jali muda, kuwa na lugha nzuri, usafi, motisha nk.

Maoni
Chapisha Maoni