1.JINA LA BIASHARA:
ebusol Kuni Bora.
2.AINA YA BIASHARA:
Kukata, Kununua, kukusanya na kuuza kuni kwa familia, migahawa, mama ntilie na biashara zinazotumia kuni kupikia.
3.MTAJI ANZIA:
TSh 100,000 – 500,000, kulingana na kiasi cha kuni, usafiri nk.
4.MAHITAJI MUHIMU:
- Kuni
- Shoka,panga
- Kamba
- Usafiri kama Gari,guta,baiskeli au mkokoteni.
- Eneo la kuhifadhia kuni.
5.WATEJA:
Familia, mama ntilie, migahawa, shule na wafanyabiashara wanaotumia kuni.
6.MAHARI PA KUFANYIA BIASHARA:
Karibu na maeneo ya makazi, masoko, migahawa au maeneo yenye mahitaji makubwa ya kuni.
7.NAMNA YAKUPATA FAIDA:
Kata,nunua/kusanya kuni kwa bei nafuu, zipange vizuri na kuziuza kwa vipimo au mafungu yenye bei yenye faida.
8.FAIDA LENGWA:
Kwa usimamizi mzuri, biashara inaweza kutoa faida ya takribani TSh 20,000–50,000 kwa siku, kutegemea mtaji, eneo na wingi wa wateja.
9.CHANGAMOTO:
Usafirishaji, uhifadhi wakati wa mvua, ushindani na upatikanaji wa kuni kwa bei nafuu.
10.HITIMISHO:
Biashara ya kuuza kuni inaweza kuanzishwa kwa mtaji mdogo na kukua taratibu. Mafanikio yanategemea kupata chanzo cha kuni cha uhakika, eneo zuri la biashara na wateja wa kudumu.
11.ZINGATIA:
Lugha nzuri ya biashara, uhakika wa Kuni Kwa wateja wako, toa motisha nk.

Maoni
Chapisha Maoni