Mkufunzi: Ombeni D.Haule.
1.JINA LA BIASHARA:
Utengenezaji na Uuzaji wa Mkaa Mbadala.
2.MAELEZO YA BIASHARA:
Biashara ya kutengeneza mkaa mbadala kwa kutumia mabaki ya mimea kama vile mabua, maganda ya nafaka, maranda ya mbao na taka nyingine zinazoweza kuwaka. Malighafi husindikwa, kuchanganywa na kifungamanishi, kukandamizwa na kukaushwa ili kupata mkaa unaotumika kupikia.
3.WALENGWA WA BIASHARA:
- Familia na wapishi wa nyumbani
- Mama ntilie na migahawa
- Hoteli na shule
- Wauzaji wa mkaa
4.VIVAA MUHIMU:
Mashine/forma ya kukandamiza, ndoo, beseni, mizani, sehemu ya kukaushia na vifaa vya kufungashia.
5.MTAJI WA KUANZIA:
Unaweza kuanza kwa mtaji mdogo wa takribani TSh 100,000–500,000, kulingana na vifaa na kiwango cha uzalishaji.
6.FAIDA:
Malighafi nyingi hupatikana kwa gharama ndogo, hivyo biashara inaweza kuleta faida inapopata wateja wa kudumu. Pia hutoa matumizi ya mabaki ya kilimo na kupunguza utegemezi wa mkaa wa kuni.
7.NJIA ZA MASOKO:
Uza kwa maduka, masoko, migahawa, mama ntilie na moja kwa moja kwa familia. Tumia na mitandao ya kijamii kutangaza bidhaa.
8.HITIMISHO:
Utengenezaji wa mkaa mbadala ni wazo la biashara linaloweza kuanzishwa kwa kiwango kidogo na kukua hatua kwa hatua kadri soko na uzalishaji vinavyoongezeka.
9.ZINGATIA:
Jali muda, lugha nzuri, Usafi na motisha Kwa wateja.

Maoni
Chapisha Maoni