WAZO LA BIASHARA: UTENGENEZAJI WA ICE-CREAM


Mkufunzi: Ombeni D. Haule

1. WAZO LA BIASHARA:
Kununua au kutengeneza ice cream kwa gharama nafuu na kuuza katika maeneo yenye watu wengi kama shule, masoko, vituo vya daladala na maeneo ya burudani.

2. MTAJI WA KUANZIA:
Takribani TSh 50,000–100,000, kulingana na vifaa na kiasi cha bidhaa.

3. VIFAA MUHIMU:
Ice cream/stock ya kuanzia
Cooler box au chombo cha kuhifadhia baridi
Vijiko na vikopo
Maboksi/packaging
Barafu au mfumo wa kugandisha

4. WATEJA:
Watoto, vijana, familia na watu wanaopenda vinywaji/vyakula vya baridi.

5. FAIDA:
Nunua kwa bei ya jumla, uza kwa bei ya rejareja na ongeza aina/flavour zinazopendwa zaidi. Kwa mtaji mdogo, unaweza kuanza na bidhaa chache na kuongeza biashara kadri faida inavyopatikana.

6. SIRI YA MAFANIKIO:
Chagua eneo lenye wateja wengi, zingatia usafi, hifadhi ice cream katika baridi inayofaa, na tumia bei rafiki.

7.HITIMISHO:
Biashara ya ice cream ni biashara inayoweza kuanza kwa mtaji mdogo na kukua hatua kwa hatua ikiwa eneo, usafi na bei vitasimamiwa vizuri.

Maoni