Mkufunzi: Ombeni D. Haule
1. Jina la Biashara:
Kilimo na Uuzaji wa Uyoga.
2. Wazo la Biashara:
Kuanzisha uzalishaji wa uyoga aina ya Oyster kwa kutumia mabaki ya mazao kama majani, pumba na mabaki ya mimea. Kilimo hiki kinaweza kufanyika kwenye chumba au banda dogo na hakihitaji shamba kubwa.
3. Mahitaji Muhimu:
- Banda/chumba cha uyoga
- Mbegu (spawn) bora za uyoga
- Mifuko ya plastiki
- Malighafi ya kuzalishia uyoga
- Meza/racks za kuweka mifuko
- Maji na vifaa vya usafi
4. Mtaji:
Unaweza kuanza kwa mtaji mdogo kulingana na idadi ya mifuko utakayotumia. Ni vizuri kuanza kidogo, kujifunza uzalishaji na kuongeza uzalishaji hatua kwa hatua.
5. Uzalishaji:
Andaa na pasteurize malighafi, weka kwenye mifuko, panda spawn, hifadhi kwenye mazingira yanayofaa na simamia unyevunyevu pamoja na usafi hadi uyoga uanze kuota. Uzalishaji unaweza kufanyika mwaka mzima.
6. Soko:
Uyoga unaweza kuuzwa kwa familia, migahawa, hoteli, maduka, supermarkets na wafanyabiashara wa vyakula. Unaweza pia kuukausha na kuufungasha ili kuongeza muda wa kuhifadhi.
7. Faida:
Biashara inaweza kutoa kipato kwa kutumia eneo dogo, na mabaki ya kilimo yanaweza kutumika kama malighafi. Pia uyoga una soko la chakula na unaweza kuongezwa thamani kwa kukaushwa na kufungashwa.
8. Ushauri:
Anza na kiwango kidogo, pata mafunzo ya vitendo, tumia spawn bora, zingatia usafi na tafuta wanunuzi kabla ya kuongeza uzalishaji.

Maoni
Chapisha Maoni