UFUGAJI BORA NA
RAHISI WA SUNGURA
Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa
na una muda wa kuwahudumia wanyama waha, ufugaji wao si rahisi kama vile
ukifuga paka au mbwa, sungura wanahitaji uangalizi na hassa kwenye usafi kwa
sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu
MABANDA
Kuna aina mbili za
mabanda ya kufugia kwanza ni yale ya kuwafungia ndani muda wote bila kutoka nje
na ya pili ni ile ya pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na mabanda na wanaweza kutoka
nje kwenye ua maalum, katika aina zote mbili ni muhimu kuhakikisha hakuna
upenyo wa kuruhusu panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa sungura.
UFUGAJI WA NDANI
1 - Usitumie banda la
kioo (aquarium) kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha
2 - Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha
hakuna sehemu zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakumia ni
mpaka wapone wenyewe au umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic sungura
hana uwezo wa kuzimeng'enya na kuisha mwilini mwake, siku ukimchinja atabakia
na dawa na hata ukinusa nyama yake utahisi harufu ya dawa
3 - Ukubwa wa banda usipungue mita 4 * 2 kwa kila sungura
mmoja, likiwa kubwa zaidi ni vizuri
4 - Chini kuwekewe matandazio kama nyasi kavu au maranda ya
mbao, lakini maranda yatokanbayo na miti yenye mafuta kama mi-pine na
mikaratusi hayafai, wawekee kipande cha blanket au taulo la zamani kwa ajili ya
kulalia na kujifungulia hasa kwa wazazi
5 - Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara wanapohisi hatari,
unaweza kutumia mbao, box gumu au plastiki
UFUGAJI WA NJE
- Sehemu yote
izungushiwe wavu wa kuku kuzuia panya kuingia na wanyama wengine kama paka,
mbwa, mwewe nk
2 - Upande mmoja uwe na mabanda, sehemu ya chakula na maji
pamoja na kivuli kwa ajili ya sungura kupumzika
- Futi moja chini ya
udongo kuwe na zege kuzuia sungura kuchimba na kwenda mbali
4 - Eneo la wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa
za kuulia wadudu au mbolea, pia majani yaliyoota yasiwe ni yale yenye sumu
(waone wataalamu wakushauri au ng'oa yote)
MAJI
Tumia mabakuli ya kigae, usiweke vya plastiki maana
huvitafuna na kuwaathiri au jengea kwa saruji, maji yabadilishwe kila siku na
vyombo visafishwe kila siku
CHAKULA
Wapewe majani makavu kwani muhimu sana kwa ajili ya mfumo wa
kumeng'enya chakula, mabaki ya mboga za jikoni baada ya kuchambuliwa, pia
unaweza kuwawekea pumba au chakula cha kuku (growers mash) kwenye vyombo maalum
kama chakula chenye virutubisho (concentrates) Kiasi cha protini wanachohitaji ni 17%
USAFI
Kila siku jaribu kuondoa uchafu kama vyakula vilivyo
mwagika, na kinyesi kilichoganda kwenya matandazio, fagia na kubadili
matandazio angalau mara moja kwa wiki, manyoya ya sungura mzazi yasiondolewe
hii huonyesha kwamba anakaribia kujifungua watoto
MENO
Wakati mwingine meno ya mbele hukua sana na kumsababishia
usumbufu wakati wa kula, waone wataalam ukiona ni marefu zaidi na yanahitaji
kupunguzwa, dalili kuu ni sungura kushindwa kula kwa zaidi ya masaa 12
MIGUU
Miguu ya sungura si kama ya wanyama wengine, nyayo zake
zimefunikwa kwa manyoya, angalia ukiona yananyonyoka kuna tatizo chunguza,
kucha zake zinahitaji kupunguzwa zikikua sana waone maofisa ugani wa mifugo
wakusaidie kwa hili
UBEBAJI
Usimbebe kwa kutumia masiki yake huwa wanaumia sana, shika
ngozi nyuma ya shingo kama paka ukitaka kumbeba na pia weka mkono mmoja kwa
chini ili kusapoti uzito
DAWA
Wapewe dawa ya minyoo kama piperazine kila baada ya miezi
mitatu, dawa za wadudu kama akheri powdeer zinyunyuziwe kwenya mabanda yao
kuzuia viroboto, usiwape dawa nyingine bila ushauri wa kitaalamu, antibiotics
ndio usijaribu kabisa kama nilivyosema mwanzo
VITABU VYA MIFUGO VINAPATIKANA, PIGA 0659 144 660
No comments:
Post a Comment